ENDELEA KUPOKEA ADVENTIST WORLD KISWAHILI

Tunawathamini na kuwatambua wote waliojisajili na tuna taarifa mpya na za kusisimua kuhusu jinsi mnaweza kuendelea kusoma na kupata Adventist World.

KULIPATA KWENYE WHATSAPP

Kwa sababu ya umaarufu wa kulipata jarida hilo kwenye WhatsApp, tunahamia kwenye mfumo mpya wa kutangaza ambao utatuwezesha kuwasiliana nanyi mara kwa mara. Bonyeza kiungo kilicho hapo chini kujiunga na chaneli ya WhatsApp Broadcast ambapo tutakujulisha toleo jipya linapokuwepo.

KULIPATA KWENYE TOVUTI

Lipate jarida hilo kwenye tovuti yetu, kwa kukibonyeza kiungo kilicho hapo chini:

Tovuti hiyo vilevile inabeba Adventist World kwa lugha anuwai.

KULIPATA KWENYE FACEBOOK

Kiungo cha toleo la hivi karibuni la Adventist World huwekwa kwenye Ukurasa wa Facebook wa Adventist World-Kiswahili kila mwezi. Kwa “Liking” ukurasa huu utapokea taarifa zetu mpya na kuweza kututumia jumbe ukiwa na majibu yoyote.

HIFADHI MAKTABA YA JARIDA LA KISWAHILI KWENYE SIMU YAKO AU KOMPYUTA

Tumetengeneza maktaba ya kidijitali ya majarida yote ya Adventist World. Ili kulipata kusanyo hili kwa urahisi kwenye simu yako, fuata hatua zilizo hapo chini:

 

Bonyeza kiungo kilicho hapo chini ili kuipata maktaba.

Fuata maagizo hayo kuiweka maktaba hiyo kwenye simu yako au kompyuta.

 

AU

Fuata maagizo hayo kuiweka maktaba hiyo kwenye simu yako au kompyuta.

 


Kwa maoni yoyote au majibu, tafadhali jiskie huru kututumia barua pepe kwenye kwambokaj@ecd.adventist.org. Tunapenda kusikia kutoka kwako na tunatazamia uhusiano mzuri na wasomaji wetu wa Adventist World-Kiswahili.

Asante sana na Mungu awabariki,
Timu ya Adventist World-Kiswahili

Tunaamini katika nguvu ya maombi, na tunakaribisha hitaji la maombi ambayo tutashiriki katika ibada ya watendakazi kila Jumatano asubuhi. Tuma maombi yako kwa kwambokaj@ecd.adventist.org, na utuombee tunapofanya kazi pamoja kuendeleza ufalme wa Mungu.

Picha ya jalada: Drew Murphy / Baurzhan Ibrashev / iStock / Getty Images Plus / Getty Images

Baraka za Ukuu Halisi 

Na John Peckham

Wengi huwafikiria matajiri na wenye mamlaka kama walio wakuu ulimwenguni, walio juu ya wote na waliobarikiwa na Bwana. Na wengi hutumia maisha yao kujitahidi kuwa miongoni mwao. Katika ufalme wa Mungu, hata hivyo, si wale wanaokaa viti vya mbele walio wakuu, bali ni wale wafuatao kielelezo cha Kristo cha utumishi. Kwani “hakuja kutumikiwa, bali kutumika” (Mt. 20:28).

 

Ukuu ni nini, basi?

 

Ulimwengu una viwango vingi unavyopimia ukuu: mafanikio ya kitaaluma, uongozi wa kisiasa na kijeshi, mavumbuzi ya kisayansi na kitabibu, utajiri na madaraka, uwezo katika riadha, tamthilia, uandishi na muziki. Yesu, kwa upande mwingine, alijibu hoja za wanafunzi Wake kuhusiana na yule ambaye angekuwa mkubwa kabisa kwa maneno haya, “Yeyote atakayempokea mtoto huyu kwa jina langu anipokea mimi; na yeyote atakayenipokea mimi ampokea Yeye aliyenituma. Kwa kuwa aliye mdogo miongoni mwenu nyote, huyo ndiye aliye mkubwa” (Luka 9:48; tazama pia Mathayo 20:16). Ni wale wamfuatao Kristo katika kuwatumikia wengine walio wakuu halisi na waitwao wenye heri.

 

Ulimwengu unasema, walio wa muhimu wanaostahili kuheshimiwa ni matajiri na watu maarufu. Yesu anasema, “Heri walio maskini wa roho, maana ufalme wa mbinguni ni wao” (Mathayo 5:3).

 

Ulimwengu unasema, heri wanaoshangilia mafanikio waliyopata. Yesu anasema, “Heri wenye huzuni, maana hao watafarijika” (Mathayo 5:4).

 

Ulimwengu unasema, heri wenye ujasiri na wenye fahari, walio na uwezo wa kupata kile watakacho (kwa hakika wengi wanaonea fahari sana madaraka). Yesu anasema, “Heri wenye upole, maana hao watairithi nchi” (Mathayo 5:5).

 

Ulimwengu unasema, heri wanaoishi maisha ya anasa(starehe), wakipata vyakula, vinywaji na huduma bora kabisa chini ya jua. Yesu anasema, “Heri wenye njaa na kiu ya haki; maana hao watashibishwa.  Heri wenye rehema, maana hao watapata rehema. Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu” (Mathayo 5:6-8).

 

Ulimwengu unasema, heri washindi. Yesu anasema, “Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu. “Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu ” (Mathayo 5:9-11).

 

Wakristo na taasisi za Kikristo, basi wasitafute ukubwa na madaraka mbele za ulimwengu bali njia za ukuu wa halisi zilizofundishwa na kudhihirishwa na Kristo. Kama unataka kuwa mkuu na mwenye heri machoni pa Mungu, tenda kama alivyotenda Kristo—jihusishe na utafute kuwahudumia wale ambao mara nyingi ulimwengu hauwatilii maanani. Chukua msalaba wako na umfuate Yesu katika eneo lako la mvuto. Toa huduma kama alivyohudumu Yesu na uishi maisha ambayo yanaakisi ukuu Wake–ukuu halisi wa upendo na rehema.

Picha: Adventist Record

Zaidi ya washiriki wa kanisa 900 walikusanyika kwa ajili ya kongamano la maombi la North New South Wales katika Hifadhi ya Likizo na Maburudisho ya Yarra huko Stuarts Point, Australia. Kongamano hilo la maombi lilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na lilihudhuriwa na watu 120, na limekuwa likikua kila mwaka. 

“Kila mara jambo hili limekuwa na litaendelea kuwa lenye mguso mioyoni mwetu kusaidia watu walio katika uhitaji mkubwa na kuwawezesha kuwa na tumaini jema la maisha mapya yaliyo bora kupitia matibabu; huu ndio uelewa wetu kuhusu kusudi letu kama kanisa la Waadventista wa Sabato."

—Bernd Quoss, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Waldfriede, iliyopo Berlin, Ujerumani, kuhusu ushirikiano kati ya Hospitali maalumu ya ugonjwa wa Fistula Gynocare iliyopo Eldoret, Kenya. Tarehe 29 Januari Stella Mokaya Orina, balozi wa Kenya, alitembelea Waldfriede na kuelezea furaha yake juu ya ushirikiano huo. Madaktari kutoka Waldfriede wamefanya safari mara kadhaa kwenda Kenya miaka ya hivi karibuni ili kumfanyia upasuaji mwanamke aliyeathirika na ugonjwa wa fistula na kuwafundisha watumishi wa mahali hapo kuhusu matibabu na jinsi ya kufanya upasuaji.

Zaidi ya 900

Idadi ya walimu wa Shule ya Sabato, viongozi wa huduma na wanafunzi wa Biblia waliokutana kupitia matangazo ya moja kwa moja yaliyoratibiwa na Divisheni ya Amerika Kaskazini kwa ajili ya kongamano la Shule ya Sabato la Do It Together mwezi Februali 7-8. Tukio hili lililenga kujadili kuhusu njia mpya na bunifu za kuunganisha masomo ya Shule ya Sabato huku wakiwashirikisha wanafunzi wa kila umri. Wakati tukio hilo likiendelea waliohudhuria walipata nafasi ya kuhudhuria mojawapo ya warsha 15 na wakufunzi walitoa kitini kwa walimu kwa ajili ya masomo yajayo.

Je, kanisa linajali kwa kiasi gani?

Waumini kote ulimwenguni waliulizwa ikiwa wanahisi kwamba kanisa lao mahalia linawajali au la. 

“Tunamshukuru Mungu kwa kujitoa kwa Idara ya Vijana, ambayo ilishirikiana na Idara za Huduma za Jamii na Shule ya Sabato katika kanisa la Zion ili kufanikisha mradi huu. Kujitolea kwao ni kielelezo cha huduma ya Yesu.”

Guno B. Emanuelson, mwenyekiti wa Misheni ya Suriname, kuhusu waumini wachanga wa kanisa la Waadventista walioungana na viongozi wa kanisa ili kusaidia idadi kubwa ya watu wasio na makazi nchini kwao. Zaidi ya watu 40 walikutana katika mji mkuu wa Paramaribo, kushiriki tumaini, kuleta furaha na kukutana na mahitaji muhimu ya jamii yao. Watu wapatao 100 walipewa huduma, mavazi, chakula kizuri, vinywaji na nakala za magazeti ya Waadventista mahalia.

“Kila mwaka wainjilisti wetu wa vitabu wanasambaza machapisho yaliyo na ukweli katika makazi ya watu, shuleni na katika maktaba zote huko Pasifiki, watu wengi wamekuwa wakibadili mitazamo ya maisha yao kwa kumfuata Kristo kwa njia ya ubatizo na kubadilisha mfumo wa maisha yao kama matokeo ya kusoma machapisho hayo. Umilele pekee ndio utafunua matokeo ya kweli ya kazi yao ya uaminifu.”

—Tony Wall, Mkurugenzi msaidizi wa huduma ya machapisho katika Kisiwa cha Pasifiki, kuhusu kazi ya wainjilisti wa vitabu katika Kisiwa cha Pasifiki. Hivi karibuni Papua New Guinea na Fiji walifanya mikutano ya wainjilisti wa vitabu iliyotoa mafunzo kuhusu vifaa vya kisasa vya mawasiliano na mikakati ya uuzaji. 

Zaidi ya 1,500

Idadi ya wanafunzi waliopokea jozi ya viatu na soksi. Kwa mwaka wa pili mfululizo AdventHealth Ottawa huko Kansas, Marekani, na AdventHealth Ottawa Foundation walishirikiana na shirika lisilo la faida la taifa la Shoe That Fit ili kutoa jozi mpya za viatu vipya vya michezo na jozi mbili za soksi kwa kila mwanafunzi katika shule saba za msingi katika wilaya ya Franklin. Nchini Marekani mmoja kati ya watoto watatu anaishi katika familia yenye kipato cha chini na moja kati ya dalili zinazoonyesha umaskini ni kutokuwa na viatu. 

“Tukiwa na idadi ya makanisa karibu 270 yanayojihusisha, hii ni fursa ya kuungana na jamii. Tunayatia moyo makanisa kufanya programu kama za kujifunza Biblia, matukio ya afya na mfululizo wa matukio ya uinjilisti wakati eneo lao litakapofikiwa.” 

Terry Johnson, Mwenyekiti wa Unioni Konferensi ya Australia, kuhusu mpango mpya wa uinjilisti unaoangazia Bubsie, Citroen 5CV iliyorejeshwa, akiendesha kupitia Australia. Kikosi hicho kitafanya zoezi la kwanza la kuzunguka nchi nzima ambalo lilikamilishwa na mwinjilisti wa vitabu wa Waadventista Nevill Westwood mwaka 1925. Mradi huu utampeleka Bubsie katika miji na jamii mbali mbali, akishiriki kisa cha Westwood na kugawa machapisho ya Waadventista na masomo ya Biblia bure.

Wanafunzi, familia, viongozi wa kanisa na wa shule washerehekea tukio muhimu la kihistoria.

Ana Júlia Alem, Divisheni ya Amerika Kusini na Adventist World

Chuo Kikuu cha Waadventista Brazil (UNASP) kilifikia hatua muhimu ya kihistoria tarehe 23 Februari wakati wanafunzi, familia na viongozi wa shule na kanisa walipokusanyika katika kampasi yake iliyopo Hortolândia kwa ajili ya uzinduzi wa darasa la shahada mpya iliyoidhinishwa ya utabibu. Tukio lilijumuisha utambulisho rasmi wa muundo na mtaala wa programu hiyo na sherehe ya kuvaa makoti meupe ili kukutana na wagonjwa.

 

Tukio lililofanyika Februali 23 liliwaleta pamoja viongozi mbali mbali, akiwemo mwakilishi wa matabibu wa mkoa na watumishi wengine wa umma kama vile José Zezé Gomes, meya wa mji wa Hortolândia. Liliakisi pia muonekano wa pekee kwa uwepo wa mwenyekiti wa Divisheni ya Amerika Kusini, Stanley Arco, pamoja na michezo mbali mbali ya muziki. 

 

Mkurugenzi wa Konferensi Kuu wa Idara ya Elimu Lisa Beardsley-Hardy alituma maoni yake binafsi kwa viongozi wa kanda huko Amerika Kusini. “Kwa furaha na shangwe tunawapongeza washiriki wote wa kikosi chenu kwa maono yenu, jitihada, kujitoa na uvumilivu kwa kuifanyia kazi fursa ambayo Mungu amewapatia kwa kuanzisha [programu ya] shule ya utabibu,” Beardsley-Hardy aliandika ujumbe huu kwa njia ya barua pepe na kuituma kwa mkurugenzi wa UNASP Martin Kuhn. “Niliwaahidi kwamba Idara ya Huduma za Afya ya GC itaendelea kuwa mshirika mwenye shauku katika uzinduzi wenu wenye mafanikio na maendeleo ya siku zijazo.”

 

Viongozi wa Huduma za Afya wa GC pia walituma barua ya pongezi wakisherehekea tukio hilo la kihistoria. “Tulishuhudia uongozi wa Mungu na juhudi kubwa na kazi ngumu ambazo zimeufanya mradi huu kufanikiwa,” barua hii ilisainiwa na mkurugenzi wa idara Zeno Charles-Marcel na kusomwa na mkurugenzi msaidizi Milton Mesa. “Tunawatakia mafanikio mema katika jitihada hizi.”

 

 

MABWENI MAPYA YA WANAFUNZI 

Viongozi pia walizindua mabweni ya wanafunzi katika kampasi ya Hortolândia. Mabweni mapya yana vyumba vyenye viyoyozi na uthibiti wa bayometriki. Wakazi wanaweza kupata chakula katika mkahawa wa shule na kupata msaada binafsi na shughuli za michezo chuoni. 

 

Henrique Romaneli, mkurugenzi mkuu kampasi ya Hortolândia, alieleza kuwa mabweni mapya yanajumuisha maeneo ya kuishi, bwawa la kuogelea na eneo kubwa lenye nyasi. Alisema, “Tumeyafurahia sana mabweni haya mapya.”

 

 

KUFUNGUA DARASA 

Programu hiyo pia iliangazia darasa lililofundishwa na Ricardo Costa, daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na ambaye sasa ni mkuu wa Shule ya Sayansi ya Tiba. Costa alikazia misukumo iliyomtia moyo katika kazi yake na jinsi alivyopata ushauri wa kukabiliana na matatizo katika kitabu cha Mithali. Kisha akaongoza katika darasa la anatomia ya moyo na mada nyingine muhimu za afya, akiwapa wanafunzi sura ya kwanza ya utata na umuhimu wa ujuzi wa matibabu.

 

Costa aliwapa wanafunzi ushauri. “Tafuteni maarifa na hekima. Msichague yasiyo muhimu. Huku ni kumheshimu Mungu na wazazi wenu, waliowekeza katika kazi zenu,” alisema.

 

 

MUITIKIO WA WANAFUNZI

Kuingia katika shule ya utabibu imekuwa uzoefu wa kutia moyo kwa wanafunzi. Kwa mwanafunzi Fabrizio Ferrari, uamuzi wa kusomea udaktari ulitokana na shauku ya kufuata kazi ambayo imekuwepo siku zote. “Baba yangu alikuwa daktari, kwa hivyo nilikuwa karibu sana na taaluma hiyo kila wakati. Leo nina fursa ya kufuata ndoto yangu,” alisema.

 

Aline Alves, mwenye umri wa miaka 22, daima alikuwa na ndoto ya kusoma udaktari. Akivutiwa na baba yake, muuguzi na mfadhili wake mkuu, Alves alieleza sherehe ya kuvaa koti jeupe kama wakati muhimu sana. “Ni ahadi tunafanya kwa kuwajibika kwa ajili ya maisha ya watu,” alisema.

Sherehe za hivi karibuni za kitamaduni zasababisha ubatizo katika jamii hiyo ya kitamaduni.

Johana Garcia na Habari za Divisheni ya Amerika – Kati

Kwa mara ya kwanza katika historia Tamasha la Muziki na Uinjilisti la China, lililofanyika Februari 13-15, lilizindua vuguvugu la imani ambalo viongozi wa kanisa mahalia wanasema linalenga kubadilisha maisha ya kiroho ya jamii ya Wachina nchini Panama.

 

Sherehe hizo ziliratibiwa na Divisheni ya Amerika – Kati (AID), Unioni ya Panama na Konferensi ya Metropolitan Panama, sherehe hiyo iliwaunganisha pamoja watu zaidi ya 50 wenye asili ya Kichina, iliweka kumbukumbu ya mkutano wa kwanza wa Waadventista katika jamii hii nchini Panama.

 

Tukio hili lilijumuisha vitu vya kitamaduni na muziki wa Magharibi wakiwa na lengo la kukuza uhusiano unaositawi uliopo kati ya tamaduni za Kichina na Kanisa la Waadventista.

 

Likifanyika katikati mwa mji wa kibiashara wa Wachina nchini Panama, tukio hili lilitoa zaidi ya burudani za kitamaduni. Viongozi walitambua kwamba ilisawiri hatua muhimu kuelekea katika ujenzi wa kituo cha mvuto chenye lengo la kuhamasisha ujifunzaji wa lugha ya Kimandari huku wakitoa matibabu ya kiafya na kukuza uhusiano wa kiroho miongoni mwa watu walioshiriki. 

 

Viongozi wa kanisa walisema, tukio hili liliimarisha mahusiano ya tamaduni na lilikuwa na athari ya kiroho ya moja kwa moja. Kama matokeo ya sherehe hiyo, Wachina saba walibatizwa, wakati wengine 13 wakimkubali Yesu na kuweka alama ya mwanzo mpya wa imani kwa jamii ya Wachina nchini Panama.

 

Moja ya ushuhuda unaogusa hisia ulitolewa na Yami Zhou Yinying. Siku fulani iliyopita, alipokuwa akitembea akipita katika mahali pa mkutano, aliona tangazo lililohusu utoaji wa huduma za matibabu ya kiafya bure na ujumbe kutoka kwa Kanisa la Waadventista. Akiwa anahitaji kuelewa kuhusu utoaji wa huduma hii ya bure, aliamua kufuatilia.

 

Yinying, aliyekuwa akitafuta msaada kwa muda mrefu baada ya mume wake kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi, aliona huduma hii kama fursa ya kumsaidia. Alistaajabishwa na ukarimu, wema na kutokuwa na ubinafsi kwa huduma hii. Aliyashukuru matibabu yale kwani hali ya mume wake iliimarika mno. Wakati masomo ya Biblia yalipotolewa, alivutiwa zaidi kujifunza kuhusu ujumbe wa Kristo.

 

Kwa kushukuru kwa msaada aliopewa, Yinying aliamua kuyatoa maisha yake kwa Yesu kwa njia ya ubatizo wakati wa sherehe. Wakati alikuwa akipanda kutoka ndani ya kisima cha ubatizo, alisema kuwa hata mvua ambayo ilikuwa inaanza kunyesha, ilikuwa ni mbaraka kutoka mbinguni. Yinying anatumika kama mtafsiri wa wahubiri, katika Union ya China ambayo mwenyekiti wake ni Daniel Jiao. Katika siku ya kwanza ya mkutano, hakuna mtu hata mmoja aliyekuwa na ujasiri wa kutafsiri kutoka lugha ya Kichina kwenda katika lugha ya Kihispania. Hata hivyo, Jiao alimkaribia Yinying na kumuomba ajaribu kutafsiri. Alikubali na kwa ujasiri alitafsiri katika kipindi chote cha sherehe hiyo.

 

Kituo cha mvuto kitaendeleza utume wake kwa vikundi vya masomo ya Biblia vinavyokutana siku za Jumamosi na wakati huo huo wakitangaza ufundishaji wa lugha ya Kimandari na kutoa huduma za kitamaduni zinazozingatia afya.

 

 

MUSTAKABALI WA KANISA LA WAADVENTISTA LA WACHINA NCHINI PANAMA

Wakati wasimamizi walikuwa wakifurahishwa na matokeo ya papo kwa hapo ya tukio hili, walikuwa pia na mipango mikubwa waliyokuwa wakiisisitiza. Tunashukuru kwa ajili ya uwezeshaji unaoendelea kutoka IAD na Union ya Panama, viongozi wanaamini kuwa kanisa lililopo katika jamii ya Wachina litaendelea kukua.

 

“Tukio hili hakika limekuwa mbaraka,” alisema Mwenyekiti wa Konferensi ya Metropolitan Panama Javier Espinosa. “Zaidi ya vile ambavyo ilikuwa mwanzo, kaka zetu na dada zetu wa Kichina wanahisi kama wamepata makazi ya kiroho, mahali ambapo wanaweza kukua pamoja.” 

Ofisi mbili mpya za tawi na vituo viwili vipya vya nyenzo vimefunguliwa katika vyuo vikuu.

Emeraude Victorin, Utafiti wa Taasisi ya Geoscience na Adventist Review

Utafiti wa Taasisi ya Geoscience (GRI) umeonyesha umuhimu wa tukio la kihistoria kwa kuyapa kibali matawi mawili mapya na vituo vipya viwili vya rasilimali katika kamati zake tendaji nchini Loma Linda, California, Marekani, tarehe 26 Februari. Ofisi na vituo hivi vipya vya DRI vimeimarisha dhamira ya Kanisa la Waadventista wa Sabato ya kushiriki katika imani na katika uwanja wa sayansi ulimwenguni.

 

Matawi haya mapya ya ofisi na vituo vya rasilimali ni matokeo ya mkakati wa ubia kati ya GRI na Taasisi za Elimu za Waadventista. Wakati vikao vya kamati tendaji vilipokuwa vinakaa mikataba minne ya ufahamu iliidhinishwa kati ya GRI na mashirika husika. Ofisi za tawi la Divisheni ya Ulaya – Asia (ESD) zimewekwa katika Chuo Kikuu cha Zaoksky, Zaoksky, Urusi. Ofisi itakuwa chini ya uongozi wa Aleksei Popov, mfizikia wa nyuklia. Tawi la ofisi za Afrika Magharibi – Kati (AWD) liko katika Chuo Kikuu cha Babcock, Ilishan-Remo, Nigeria; Oluwole Oyedeji, mtaalamu wa jiolojia, ndiye mkurugenzi wa ofisi hii.

 

Sharti mojawapo la tawi la ofisi ni kwamba linatakiwa kuongozwa na mkurugenzi aliyehitimu elimu ya Ph.D. katika fani inayoendana na mambo ya sayansi. Uwezo wa kitaaluma wa mkurugenzi unawasaidia kuratibu tafiti na elimu kuhusu asili na mada za uumbaji na kuwaruhusu waweze kuanzisha kazi za uumbaji zinazowiana na shughuli zinazofanywa katika maeneo ya kampasi ya chuo husika, katika Mazingira yao yanayowazunguka na kote katika eneo la divisheni ambako wanahudumu.

 

Moja kati ya vituo vya rasilimali viliyochaguliwa kipo katika eneo la Chuo Kikuu cha Chile, Chillan, Chile. Kituo hiki kinaongozwa na Cesar Arriagada Campos, ambaye ni mtaalamu wa mambo ya makumbusho. Kituo kingine cha rasilimali kipo katika kampasi ya Chuo Kikuu cha Waadventista Engenheiro Coelho Brazili kilichopo katika jimbo la São Paulo. Tiago Souza, mwana baiolojia ndiye kiongozi wa kituo hiki.

 

Kabla ya kuongezeka huku, GRI ilisimamia matawi ya ofisi nne. Matawi hayo yapo katika maeneo mbalimbali ulimwenguni katika Divisheni ya Ulaya – Kati, Amerika – Kati, Kaskazini mwa Asia – Pasifiki na Divisheni ya Amerika ya Kusini. Mbali na matawi ya ofisi, kuna vituo hai 11 ulimwenguni katika maeneo mbali mbali ya taasisi za elimu ya Waadventista.

 

Rony Nalin mkurugenzi wa GRI anasema, “Uanzishwaji wa matawi mapya ya ofisi za GRI na vituo vya rasilimali ni hatua ya thamani na ya kimkakati katika kuongeza namna ya kufikisha ujumbe wetu kuhusu uumbaji na historia ya dunia.” “Tumefurahi sana kushiriki katika kazi pamoja na viongozi wa ESD na WAD pamoja na wawakilishi kutoka katika vyuo viwili ambao wamezifanya ndoto zao kuwa halisi. Lengo kuu ni kuimarisha weledi wa mitandao yetu, kuunganisha utaalamu mkubwa wa kitaaluma, kutayarisha walimu bora na kuweka msisitizo wa rasilimali katika kipengele hiki muhinu cha ujumbe wa Waadventista.”

 

Mwanzo mpya wa ofisi hizi ni matokeo ya uhitaji wa shughuli ya makusudi katika imani na sayansi, pamoja na mipango ya masafa marefu. Mtandao ulioimarishwa utazidisha uwezo wa GRI wa kutoa rasilimali, mafunzo na fursa za utafiti kwa wanazuoni, wanafunzi na washiriki wa kanisa kote ulimwenguni.

 

Kama Robert Osei Bonsu, mwenyekiti wa WAD, alivyosema: “Vituo hivi vitaakisi dhamira ya Kanisa la Waadventista wa Sabato ya kuuinua ukweli wa Biblia huku wakijihusisha katika uchunguzi wa wasomi ambao unaimarisha imani zetu na ushuhuda katika kipindi hiki cha maendeleo ya kisayansi.”

Viongozi wamejifunza programu mpya ili kuzipa tumaini jipya fursa za utume katika maeneo yao yote. 

Libna Stevens. Habari kutoka Divisheni ya Amerika – Kati

Divisheni ya Amerika-Kati (IAD) ilichukua hatua ya kwanza ya kuzipa tumaini jipya fursa za utume kote katika maeneo yake ya divisheni inayoundwa na mikoa 25 wakati wa mafunzo yaliyokuwa yanafanyika huko Miami, Florida Marekani. Kikao cha mafunzo kilichofanyika kwa muda wa siku mbili kiliwaleta pamoja viongozi watendaji wa union na wafanyakazi wote ili kusisitiza juu ya kuongeza fursa za utume kwa kutumia mpango wa kanisa unaofanywa mtandaoni wa kuandikisha washiriki uitwao VividFaith.

 

VividFaith ni kifaa cha kimtandao kilichotengenezwa ili kuwaunganisha wamishonari na fursa za kazi ya utume ulimwenguni. VividFaith ni sehemu muhimu ya mpango mpya wa utume wa Konferensi Kuu, ambao unahitaji kupanga upya vipaumbele vya kanisa na utume kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa washiriki wake wanaobadilika na jamii kwa ujumla.

 

Hii ni mara ya kwanza IAD kushirikiana na VividFaith katika kipimo hicho kikubwa wakati wa tukio lililoitwa “Kazi ya Uandikishaji” alisema Samuel Telemaque, mkurugenzi wa Shule ya Sabato na Utume wa Kiadventista wa IAD. Kama mkurugenzi, matokeo ya mafunzo haya ni mipangilio 158 ya utume iliyowekwa kwenye programu ya VividFaith, ikiwa na mwitikio mkubwa na wa haraka.

 

“Kukiwa na mafunzo kutakuwa na uwezeshaji,” alisema Telemaque, aliyekuwa kiongozi mkuu wa tukio hilo. “Viongozi wapya wa kikosi chetu cha VividFaith watasaidia kukuza utume wa IAD na tunatarajia kuwakaribisha na kuwaandaa wamishonari kwa ajili ya fildi nyingi za utume ndani ya divisheni yetu.”

 

 

MBINU STAHIKI ZA UTUME ULIMWENGUNI

Maandalizi kwa ajili ya mafunzo yalianza mwishoni mwa mwaka 2024 na yalihusisha uratibu wa kina. Kwa mujibu wa Fylvia Fowler Kline, Meneja wa VividFaith, mafanikio ya tukio hili yalitokana na mpangilio makini. Viongozi waliainisha fursa za utume ambazo zinahitaji wataalamu maalum na kuandaliwa maelezo ya kazi kwa kina na kuhakikisha uwezeshaji mzuri wa kifedha unaandaliwa kwa kila nafasi kabla ya siku ya tukio. Kline alieleza kuwa, “Jambo la tofauti kuhusu VividFaith ni uwezo wake wa kutoa huduma ambazo zinaendana na mahitaji ya jumuiya na sera zake na kuandikisha wanaojitolea, waajiriwa, wafanyakazi wa mbali, wafanyakazi wanaofanya kazi mahali kwa wakati mmoja na wegine wengi.”

 

 

KUPANUA MAWANDA YA KAZI YA UTUME 

Tukio la mafunzo pia lilikuwa na umuhimu kwa viongozi kutoka katika maeneo mbali mbali. Gail Smith-Anthony, kutoka Union Konferensi ya Caribbean, alielezea kwa matumaini kuwa tukio hili lingeweza kuunda fursa nyingi za utume huko Caribbean. “Kuna idadi kubwa ya vijana kote huko Caribbean walio tayari kujihusisha katika kazi ya utume nje ya nchi,” alisema. Alionyesha kwamba hata wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kusini mwa Caribbean kilichopo Trinidad wanayo nafasi ya kushiriki katika fursa za utume zinazotolewa na programu ya VividFaith.

 

Leonard Johnson, katibu wa IAD, anasisitiza kuhusu umuhimu wa kutambua hitaji la utume ili kutimiza kazi ya utume wa injili kote katika divisheni hii. “Hatuwezi kumuweka Yesu kuwa wa kwetu pekee” anasema. “Imani yetu haitupi nafasi ya kujitenga; tumeitwa ili tumshiriki Yesu kwa ulimwengu.”

 

 

 KANISA LENYE UMOJA KATIKA UTUME

Viongozi wanasema, kuwa na ubia baina ya IAD na programu ya VividFaith unaakisi mbinu jumuishi ya kanisa katika kazi ya utume. Erton Köhler, katibu wa Konferensi Kuu, anaeleza kuwa licha ya mgawanyiko wa kiutawala na kijiografia uliopo, kanisa linabaki kuwa na umoja katika utume wake. “Tunaweza kuwa tumegawanyika katika divisheni na fildi zilizo kwenye matazamio, lakini sisi ni kanisa moja, tunashiriki maono na malengo sawa,” anasema Köhler.

 

Divisheni zote zikiiga tukio hili la mafunzo litatuwezesha kuwa na ongezeko lenye manufaa la fursa za utume, kulingana na Kline. Aliipongeza IAD kwa kuwa na jumuiya bora na uwezeshaji wa kifedha walioutoa na kuuita “mfano wa kuigwa kwa divisheni nyingine kote ulimwenguni.”

Kwa nini ninasalia katika kanisa la Mungu

NA NICOLE PARKER

“Siwezi kufika mlangoni!” Sauti yenye kwikwi ya rafiki yangu aliyekata tamaa iliyosikika kwenye simu iliumiza moyo wangu. “Nimejitahidi sana!” Alizidi kulia. “Hawawezi hata kukaa karibu na mimi.”

 

Nilimtia moyo rafiki yangu aliyekata tamaa, huku nikimhakikishia kwamba Yesu angeweza kukutana naye nje ya mlango wa kanisa juma hili. Kisha, taratibu nilijiandaa kwenda kanisani.

 

“Kanisa.” Je, neno hili linaamsha hisia gani katika fikra zako?

 

Kwa wengi, mioyo yao husisimka wanapofikiria kuhusu mahubiri, chakula cha pamoja, vipindi vya uimbaji, kutakaswa kwa nafsi–mahali pa kukimbilia wakati wa hatari.

 

Wengine hupata hasira na kububujikwa na machozi. Maumivu ya fikra za matusi, unafiki, kutuhumiwa na kukataliwa hujaa ndani yao katika mawimbi ya uchungu. “Kanisa” limechanganywa na uwasilishaji mbaya wa upendo wa Mungu.

 

 

KUJENGA UPYA?

“Kujenga upya” ni neno lililoenea katika vyombo vikuu vya habari hivi leo. Linaelezea kuhusu Wakristo wengi wanaokataa dini zenye utaratibu, au hata kupoteza imani kabisa. Japo wengi hufikia hatua hii kupitia nadharia ya kushuku au kutojihusisha, wengi hugundua uchaguzi wao moja kwa moja kwa usaliti wa kanisa na madhara yake.

 

Kama mtetezi wa wanaoonewa na mke wa mchungaji, nimeona uovu mwingi sana wa kanisa. Lakini baada ya kushuhudia uonevu mmoja hasa wa kuogofya, hatimaye nilijikuta nashindwa kuhudhuria kanisani kimwili. Moyo wangu ulidunda kwa kasi pale nilipokaa madhabahuni. Mwishowe msongo ulinivuta katika ofisi ya tabibu wa magonjwa ya mchafuko wa tumbo. Nikitambua nahitaji sababu za kina za kwenda kanisani, nilianza kujifunza na kusoma majarida.

 

 Kile ambacho kilianza kama jaribio lisilo na tumaini la kung’ang’ania kanisa kwa ukucha likageuka na kuwa safari njema ya utukufu ndani ya miezi kadhaa kuelekea kwa Mungu. Niliweza tu “kuvuta picha kwa mbali” katika picha kubwa ya kile Mungu anachokifanya ndani ya kanisa Lake lisilo timilifu. Niligundua sababu nyingi zinazomfanya Kristo atoe wito wa kudumu ndani ya kanisa, hata kama ni vigumu. Makala hii imeelezea kwa ufupi kile nilichokigundua na kilichonisaidia kupata uponyaji, kujikabidhi upya na taratibu nikarejea madhabahuni, nikatulizwa na uwepo wa Mungu ulionifariji nikiwa hapo ndani.

 

 

KWA NINI KUBAKI NDANI YA KANISA LISILO KAMILIFU?

Mungu amewaita watu Wake ili kuuelezea ulimwengu mzima kuhusu upendo Wake na hatuwezi kufanya hivyo peke yetu.

 

Kumpenda Mungu bila kuwapenda wengine hakutimilizi sheria ya Mungu ya mahusiano (tazama Marko 12:30, 31). Mungu anatutaka kuyaacha maeneo yetu ya amani, kwa unyenyekevu tufanye kazi kupitia katika tofauti mbalimbali pale inapowezekana. Lakini ikiwa nimewaalika marafiki kujiunga nami katika kuabudu kwa amani nyumbani kwangu (Ebr. 10:25), baadaye itakuwaje? “Harakati” yangu itabaki kuwa na ukomo wa muda, sehemu na udhaifu wangu mwenyewe. Sisi ni “mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake” (1 Kor. 12:27; tazama zaidi 12:12-31; 13:1-13). Ukilinganisha na upweke unaoendelea, tamaduni binafsi katika sehemu nyingi ulimwenguni, Mungu amelipa kanisa la nyakati za mwisho wito kama kundi kuonyesha namna upendo ulivyo kwa vitendo – kote ulimwenguni. Kueneza ujumbe wa injili kote ulimwenguni, waumini lazima wafanye kazi kwa umoja. Hili linatupeleka katika wazo linalofuata.

Ili kupeleka injili ulimwenguni, kanisa lazima liwe na utaratibu.

 

Nina imani thabiti kuwa kanisa la Waadventista limeshikilia maono yenye mfumo mzuri wa kiteolojia kuhusu upendo wa Mungu kuliko makanisa mengine yaliyopo. Kuendelezwa kwa vizazi na vizazi kupitia usomaji wa kina wa Biblia na wanateolojia waliojitolea sana, ujumbe huu umefunuliwa dhahiri katika imani za msingi 28.

 

Muundo wa kanisa ni chombo cha kuleta ufanisi kilichoamriwa na Mungu kushiriki nuru hii ya tabia ya Mungu ya upendo ulio mkamilifu kwa ulimwengu ulioumizwa na kuchunguzwa kwa undani. Lakini kila mmoja wetu amepewa karama chache za roho ili kukamilisha utume huo! Washiriki wa kanisa wanapaswa kushirikiana pamoja kama sehemu za fumbo zinavyokamilishana. Si lazima kila mmoja aimbe, kupika, kuhubiri au kushiriki pamoja katika kambi au sikukuu za watafuta njia na Shule ya Biblia Wakati wa Likizo. Na vipi kuhusu nje ya kanisa mahalia? Ikiwa hatutakuwa na shule, taasisi za afya na mgawanyo wa sadaka utakaosaidia kuongoza wengi kutoka katika upotovu ulioenea katika mfumo wa madhehebu mengine, tutakuwa upande gani?

 

Waasisi wa kanisa la Waaadventista wa Sabato mwanzoni waliepuka kabisa kujiunda wao wenyewe, wakiamini kuwa muundo wenyewe lazima utawaongoza katika matumizi mabaya ya madaraka. Lakini hatimaye, waligundua kwamba kueneza injili ulimwenguni kuliwalazimu kuwa na shirika. Mungu anahitaji kutegeneza mwili wa waumini kwa kitambaa kimoja bila mshono wowote, kikosi cha ulimwengu mzima kwa ajili ya kumuwakilisha katika huduma njema. Waandishi, wahubiri na wastadi lazima waunganishe nguvu zao na karama nyingine na teknolojia, wanauchumi, wasomi na wataalamu wa lugha, ili kufanikisha utume wetu wa injili ulimwenguni wa kueneza upendo wa Yesu.

 

Waasisi walikuwa sawa kuhusu changamoto za kuwa na shirika. Mungu aliwaonya Wana wa Israeli kuhusu kuwa na mfalme kwa sababu mfumo wowote wa shirika hudokeza mfumo wa matabaka unaowashawishi wenye dhambi kuunganisha nguvu kwa kiburi. Mifereji yote ya dhambi kutoka katika asili ya Shetani “Nitafanana na yeye aliye juu” (Isa. 14:14). Tangu mwanzo “mtakuwa kama Mungu” (Mwa. 3:5), wadhambi wana-mkakati wa kujivisha taji katika kiti cha enzi. Wayahudi walishindwa kumtambua Yesu kama Masihi kwa sababu ya shauku yao ya mamlaka ya juu kabisa; shambulio la pili juu ya mtazamo wa kundi la watu wenye mamlaka liliuzunguka Ukristo kwa mfumo wa uongozi wa kanisa la Zama za Giza. Kwa mshangao, Shetani aliwalenga viongozi wa kiroho kwa majaribu makuu ili kumwasilisha Mungu vibaya kwa namna walivyotumia madaraka.

 

Labda ulinzi wetu mkuu dhidi ya dhambi ni kudumu kutazama utofauti mkubwa uliopo baina ya jinsi Yesu na Shetani wanavyotumia madaraka. “Shetani alimwelezea Mungu kama mbinafsi na katili, kwamba anadai yote na hatoi chochote.”1 Lakini “mamlaka” ya ulimwengu huu ni “mamlaka ya chini.” Mfalme wetu aliwaosha miguu. Akivaa taji ya miiba, Mfalme wa ulimwengu mwenye kudura alikanusha uongo wa Shetani milele. “Alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa . . . Alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba” (Fil. 2:7-8). Kila siku anatusihi, “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu” (Fil. 2:5). Kiburi na ubinafsi huyeyuka mbele ya mng’ao wa utukufu unaoangaza kutoka Kalvari.

 

Mtawala mwingine mwenye dawa ya kupoza nguvu ya sumu ya mamlaka ya hasira ni kukumbuka kwamba kanisa si tu shirika la kidunia. Kwa makusudi Yesu alitanguliza Agizo Kuu, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani” (Mathayo 28:18). Ukumbusho huu kwa viongozi wapya wa kanisa la Wakristo wachanga kuangaza mwangaza wa tumaini kwa kanisa la nyakati za mwisho, pia. Yesu ndiye Kichwa pekee cha kanisa Lake.

 

Kwa kuwa hakuna kiongozi aliye mkamilifu, kutokukamilika kwa uongozi—na mara moja moja kupotoka—kutadhoofisha kazi ya kanisa ya injili. Makosa ya kiuongozi yalitia doa taarifa za Nuhu, Ibrahimu, Daudi, Petro na viongozi wengine wa kiroho tangu wakati wa uumbaji isipokuwa Yesu tu. Lakini ilimradi hata washiriki wachache walijazwa na Roho—7000—walikataa utawala wa kifalme na kwa mioyo yao yote wakakumbatia unyenyekevu, shirika lina msaada zaidi ya kipingamizi.

 

Muundo wetu wa kiulimwengu huwakilisha utetezi wa uwezo wetu wa kutimiza lengo la Mungu wetu la kupeleka injili ulimwenguni. Hatimaye, tunahitaji zaidi juhudi zisizo na vikwazo. Tunaweza kutimiza Agizo Kuu la Mathayo 28 tu kwa kupitia nguvu za Roho Mtakatifu. Je, tunapokeaje kumwagwa huko kwa Roho Mtakatifu?

Katika Matendo 2 Wanafunzi walimpokea Roho Mtakatifu baada ya kuacha kuomba vitu visivyo na manufaa “Ni nani basi aliye mkuu” ushindani wa mamlaka ya kidunia na badala yake wakarejea katika “nia moja” katika Matendo 1.

 

Ni msalaba pekee unaoweza kukabiliana vya kutosha na mielekeo ya kimwili dhidi ya kujiinua. Labda upeo wa gharika ndio njia pekee ya kutufikisha katika umoja unaoonyeshwa wazi katika mvua ya awali. Lakini hata nje ya janga hili, tunauhitaji uhusiano uliovunjika wa washiriki wenzetu wakosefu kama sisi.

 

Tabia ya Mungu inaelezewa katika sheria ya uhusiano. Tunaitwa kuwa mfano wa Mungu, si kwa mapambano ya kibinafsi ili kufikia utakatifu, bali kama jumuiya ya wamishonari wenye hekima ya Musa, wenye uelekeo mmoja wa upendo wa kujitoa mhanga. “Pale tabia ya Mungu itakaporudishwa upya kikamilifu ndani ya watu Wake, atakuja kuwatangaza kama watu Wake tena.”2 Kutoka katika mwangaza wa nadharia ya ukamilifu binafsi, muktadha wa kauli hii unarejelea matunda ya Roho yaliyoonyeshwa katika mwili wa Kristo pale tunapoacha kujifurahisha binafsi na kuhudumiana kwa kujitoa. 

 

Kuunganishwa kwa unyenyekevu na miili anuai ya waumini pia itakufanya ujikute katika ukereketwa wa kupindukia au makosa ya kiteolojia. Inatoa muundo wa ibada ya kila juma, kutumia vipaji mbalimbali na kutoa fursa thabiti vinavyokuza matunda ya Roho. Japokuwa baadhi ya watu wanaweza kudumisha teolojia kamilifu na usawa wa uhusiano wakiwa peke yao, kutojihusisha na waumini wengine hakutaonyesha njia salama kwa watoto wao–na wengine watavutwa kwa Kristo–na kuwafuata. Waumini wanahitaji umoja.

 

Unahitaji sababu nyingine moja itakayokufanya usikate tamaa na kufuata utaratibu wetu mpya? Hebu tutazame unabii.

“Wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu Zake” (2 Tim. 3:5) inaelezea wale wanaodai kuwa wafuasi wa Mungu katika nyakati za mwisho.

 

Tangu mwanzo, Mungu anawaita waumini wenye dhambi kuungana kuuambia ulimwengu kuhusu Yeye. Ngano na magugu vinakua pamoja hadi wakati wa mavuno na “wakati wa mavuno ndio mwisho wa wakati wa kujaribiwa.”3 Kitabu cha Ufunuo hakielezei muujiza wa kujiondoa kwa Laodekia mwenye uvuguvugu, kanisa la mwisho. Kusimama kinyume na uovu katika kanisa vuguvugu hakika haiepukiki katika nyakati za mwisho, kama ambavyo “upendo wa wengi utapoa” (Mat. 24:12). Lakini kama ambavyo mwanateolojia Diane Langberg alivyosema, “Sisi ni wapinzani wa Mungu . . . hatupaswi kukubali kabisa ‘kulinda’ jina la Mungu kwa kujifunika ubaya. Waefeso 5:11, Paulo anatuonya kutoshiriki matendo ya giza badala yake tuyafunue. Tambua kwamba hauwezi kubadilisha mfumo mzima wewe peke yako; haujaitwa kufanya hivyo. Bado tunapaswa kusema kweli kuhusu mfumo wetu. . . . Watu ni watakatifu, wameumbwa kwa mfano wa Mungu. Mifumo haipo ivyo. Inathamini tu watu waliomo ndani yake na wale inaowahudumia. Na watu wanatakiwa kutendewa kama ambavyo Kristo alivyokuwa akiwatendea, hata kama awe mmoja au wengi.”4 Manabii walipigwa kwa mawe kwa sababu–hawakukaribisha makaripio yaliyohitajika. Je, tunawezaje kutarajia upinzani wa uovu kuwa rahisi katika nyakati za mwisho?

 

Mfano wa Yesu haukuwa wa mtunza amani wa juu juu, bali wa mtengeneza amani wa kweli. Aliwatia hamaki viongozi wa kiroho kwa ghadhabu kubwa, hata kuwasonga na mijeledi na kupindua meza. Utukufu wa Mungu uliinuliwa kinyume na uovu mkubwa uliokuwepo kanisani. Lakini makaripio kutoka ndani hufaa zaidi. Yesu aliendeleza ushirika pamoja na washiriki wa Kiyahudi kadiri alivyozidi kukemea dhambi. 

 

Watafuta amani wanapaswa kujihadhari: kujiinua nafsi ni mtego ambao hutoka kila mahali. Unyenyekevu ndio njia pekee ya kujilinda dhidi ya unafiki unaochafua. Kweli lazima isemwe kwa upendo, wokovu ukiwa ndio lengo kuu. Tunatakiwa kuonyesha upole pale tunapokemea, tukitambua kwamba tunatakiwa kusimama hukumuni na kazi njema zisizo na madhara.

 

 

KWA NINI NADUMU KUWA KANISANI

“Ni kanisa la Mungu. Sitaondoka.” Rafiki yangu aliyekata tamaa mwanzoni mwa makala hii aliniambia hivi.

 

Tangu Mwanzo hadi Ufunuo, Maandiko yanarudia ahadi ya hakika: “Japokuwa kanisani kuna uovu, utakuwepo hata mwisho wa ulimwengu, kanisa katika nyakati hizi za mwisho linapaswa kuwa nuru ya ulimwengu uliochafuliwa na kuharibiwa na dhambi. Kanisa, lililodhoofishwa na lenye mapungufu, linatakiwa kukemewa, kuonywa na kushauriwa, ndicho chombo pekee kilichopo ulimwenguni ambapo Kristo ameweka kipaumbele chake.”5 Anaeleza zaidi: “Kanisa ni wakala aliyechaguliwa na Mungu kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Lilianzishwa kwa ajili ya kutoa huduma, na utume wake ni kupeleka Injili ulimwenguni… kwa njia ya kanisa lake, hatimaye atadhirishwa ‘kwa falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho,’ dhihirisho la mwisho kamilifu la upendo wa Mungu.”6

 

Kanisa la Mungu la kweli si tu shirika. Ni harakati ya watu wa Mungu wanaoeneza upendo wa Mungu kwa umoja. Yesu ndiye Kichwa chetu; ulimwengu ndio eneo letu la utume. Watu Wake wanapaswa kuungana ili kutimiliza ombi la Yesu, “Ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma” (Yohana 17:23).

1 Ellen G. White, The Desire of Ages (Mountain View, Calif.: Pacific Press Pub. Assn., 1898), uk. 57.

 

2 Ellen G. White, Christ’s Object Lessons (Washington D.C.: Review and Herald Pub. Assn., 1900), uk. 69.

 

3 Ibid., uk. 72.

 

4 Diane Langberg, Redeeming Power: Understanding Authority and Abuse in the Church (Grand Rapids, Mich: Brazos Press, 2020), kur. 86, 87. 

 

5 Ellen G. White, Counsels for the Church (Nampa, Idaho: Pacific Press Pub. Assn., 1991), uk. 240.

 

6 Ellen G. White, The Acts of the Apostles (Mountain View, Calif.: Pacific Press Pub. Assn., 1911), uk. 9.

Nicole Parker ni mwandishi wa mfululizo wa kitabu cha Tales of the Exodus na profesa wa dini katika Chuo Kikuu cha Kiadventista cha Kusini, Collegedale, Tennessee. Yeye na mume wake Alan wana watoto wanne.

Mungu ni mkuu zaidi ya kizuizi chochote ambacho tunaweza kukutana nacho 

NA ALICIA MARIE HARDING

Kisiwa chenye mamba*, kisiwa cha zamani sana zaidi ya kilometa elfu moja kutoka katika shamba lililopo kando ya mto mahali ambapo familia yangu iliweka kituo kama wamishonari, ni safari ya siku 2 hadi 3 kwenye njia yenye mawe mawe katika mikoa ya kaskazini mwa Zambia. Wainjilisti waliopo maeneo ya pembezoni mwa mto na kikundi cha madaktari waliandaa mpango wa kufanya mkutano mkubwa—waliandaa wiki 3 za mikutano, katika vijiji vitatu tofauti tofauti katika kisiwa kile iliyofanyika kwa wakati mmoja, wakati kikundi cha wataalamu wa meno na tiba wakitoa huduma bure na kikundi cha wajenzi kikijenga makanisa matatu. Kisiwa kile, kilichopo karibu na Ziwa Tanganyika, kilipewa jina kulingana na muundo wake, lakini jina hilo bila shaka liliwakilisha pia maisha asili yasiyozuilika na ya hatari yaliyokuwepo pale. Licha ya kuwa na idadi ya watu kama 5,000 katika vijiji vitatu, hawakuwa na kanisa, shule na vifaa vya tiba. Pamoja na mikutano mingi ya injili kwa mwaka mzima, mkutano huu ulipangwa kwa uangalifu mkubwa sana. Kwani hakuna hata mmoja wetu ambaye amewahi kukutana na hali ya utata na vizuizi mbalimbali njiani. 

 

Baada ya kusafiri kwa gari kwa muda wa siku mbili, tulikuwa tumebakisha mwendo wa dakika 45 kufika mwisho wa safari yetu. Nilikuwa nikistaajabia upepo mkali uliovuma barabarani, nikifikiri jinsi ambavyo hakuna badiliko tangu nilipochukua picha ya mahali pale mwaka mmoja uliopita. Tulipoona tumekaribia kufika tulifurahia. Nilidhani kuwa ziwa lilikuwa upande wa pili wa barabara uliokuwa hauonekani kwa kufichwa na milima iliyokuwa mbele yetu. Kisha, pasi na tahadhari, gari na tela letu lilianza kuvutwa nyuma na kupoteza mwelekeo. Wote tulitazama upande ule wa mlima tuliokuwa tunauelekea. Muda ulionekana kama unaenda taratibu. Mawazo yangu yalifikiri zaidi juu ya hatari itakayotokea katika kila sekunde. Mambo yote yalifanyika kwa haraka zaidi kiasi kwamba nilishindwa kufanya lolote au hata kuruhusu akili yangu kuomba. Tuligonga mlima na tela la nyuma lilifyatuka na kutupwa pembeni mwa barabara. Gari lilibingirika kuelekea kushoto na kuanza kuserereka barabarani hadi lilipogonga mtaro na kurejea barabarani.

 

Kulikuwa na nusu sekunde ya ukimya na giza, wingu zito la vumbi lilipoziba mwangaza. Shauku yangu kwanza ilikuwa ni kuwatazama watoto lakini sikuona kitu. Kisha wote kwa pamoja, walianza kupiga kelele. Vijana waliokuwa na damu nyingi waliinuka wakipiga kelele, “Winston!” Kichwa cha mwanangu wa kiume mwenye umri wa miaka 5 kiliburuzwa barabarani kupitia dirisha lililopasuka na kupasua ngozi ya kichwa hadi kwenye fuvu wakati gari liliposerereka kilimani. Wakati kila mmoja alipokuwa akijichunguza kama ni mzima, nilituma ujumbe wa redio kwa gari kubwa lililokuwa mbele yetu kwa ajili ya msaada. Kwa sababu hawakutuona wakati tukio hili likitokea, sina hakika kama waliona ajali ile. Rafiki yangu wa karibu, Rebecca pamoja na mwanaye Benjamin, waliokuwa ndani ya gari langu, walishuhudia tukio zima wakiwa na mshtuko.

 

Ndio, huu ulikuwa wakati wa kuogofya. Lakini hivi punde tutaona kuwa tukio hili halikuwa lisilo la kawaida. Adui hakufurahia mipango yetu ya kushiriki habari za Yesu katika Kisiwa chenye Mamba na alijaribu kupambana nasi.

 

 

MASHAMBULIZI YA ADUI  

Wiki mbili kabla ya ajali ile, basi lililokuwa likiwasafirisha wanamkutano wengi lilimgonga na kumuua mtu mmoja aliyekuwa anakimbia barabarani kwenda kujiua. Dereva alijitahidi sana kumuepuka lakini hatimaye ilitokea, hata hivyo, tukio hilo la kiwewe lilisababisha pia kuchelewa kusikokuwa na matumaini. Kwa ufupi baada ya hapo, wakati tulipoanza safari yetu, mume wangu, Craig, kwa shida alizuia hatima kama ile ile. Alikata kona kuelekea katika barabara nyembamba iliyokuwa mkabala na sisi, alikwepa kumgonga mtu aliyetokea nyuma ya gari kubwa alipokuwa akivuka barabara. Alikaribia kuua mtu!

 

Wakati kazi ilipoanza kisiwani pale, kiongozi wetu wa huduma za kitabibu, Beaver Eller, alipigwa shoti mbaya sana ya umeme na kama asingekuwa imara, ingemuua. Projekta na spika zilizokuwa mwanzo zikifanya kazi vyema ghafla zilipata hitilafu mara moja kabla mikutano haijaanza. Lori lililokodishwa ili kuleta vifaa vyote vya ujenzi wa kanisa lilitekwa nyara, hii ilihatarisha kazi ya ujenzi wa kanisa.

 

Wakati kanisa lilipokuwa likiendelea kujengwa moto ambao haukuwashwa na mtu ye yote uliwaka ghafla katika maeneo ya kuzunguka kanisa. Wafanya kazi waliweza kuzima moto na kuendelea kujenga, kisha moto mwingine uliwaka tena. Waliuzima na kisha kurudi kujenga. Jambo hili lilitokea mara zote walipokuwa wakiendelea na ujenzi.

 

Katika mikutano, msichana mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa akipagawa na pepo alikuja akitafuta kufunguliwa. Walipokuwa wakimwombea na kuchoma nguo za tambiko, alishindwa kujidhibiti na alisukumwa kwenye moto na nguvu isiyoonekana. Baada ya maisha yake ya kale kuteketezwa, alifunguliwa na kujifunza Biblia pamoja na mwanakikundi mwenzetu.

Siku iliyofuata kulikuwa na mjadala mkali kuhusu kile Biblia inachosema kuhusu uchawi na usihiri. Kikundi cha wataalamu wa meno na tiba walijaribu kuvuka ng’ambo ya ziwa ili kufanya mkutano wa kitabibu katika upande mwingine ambapo chombo chao kilinusurika kupinduliwa na mawimbi makali. Maji yalikuwa shwari na anga lilikuwa la bluu wakati walipoanza safari yao, ghafla baadaye, mawimbi yalikuwa yakija na upepo mkali. Injini ya boti ilizima na haikuweza kuwaka tena. Kikundi kidogo kilichokuwa ndani ya boti kilianza kuomba, kuimba na kuabudu. Baada ya maombi injini iliwaka. Waligeuka kurejea wakati watu waliokuwa kilimani wakitazama ikiwa wataweza kufika ufukweni wakiwa hai. “Kuna mtu alitakiwa kufa,” mtu mmoja aliyeshuhudia pambano lile alisema.

 

Siku hiyo hiyo gari letu moja lilipata hitilafu katikati ya safari. Mume wangu alisubiri msaada kutoka katika mji uliokuwa karibu hadi siku iliyofuata. Baadaye kidogo tukapata habari kuwa breki za gari ya nne iliyokuwa njiani kuja kuungana nasi zilishindwa kufanya kazi. 

 

Na haya ni baadhi tu ya mifano ya vizuizi tulivyokutana navyo wakati wa mikutano ya injili.

 

Lakini Mungu . . .

 

Kisha nilikaa katikati ya barabara ya udongo, nikigandamiza kitambaa kichwani kwa Winston ili kuzuia damu iliyokuwa inatoka. Moyo wangu ulisononeka nilipotambua kuwa mwanangu alikuwa na majeraha na njia rahisi ambayo ingemsaidia kuwa na afya ni kupata vifaa vya kumhudumia. Hata sasa, machozi yanabubujika machoni mwangu kila ninapokumbuka mawazo haya. Tulikuwa mbali na nyumbani ndani ya siku mbili tu.

 

Lakini nilijiepusha kuelezea tena kazi za ibilisi. Ninataka kusisitiza zaidi jinsi Mungu alivyo mkuu kuliko ibilisi.

 

Mara baada ya Rebecca kushuhudia ajali ile, alimwita mume wake Beavar, mhudumu wa afya mwenye uzoefu wa kufanya kazi katika chumba cha dharura ambaye alikuwa mmoja kati ya wale waliokuwa kwenye boti iliyokuwa karibu kuzama siku ile. Kwa sababu walipanga upya safari yao, alikuwa amemaliza kushuka katika kambi iliyokuwa karibu—walipopata usafiri. Rebecca alikuwa na rada inayowezesha kupata mtandao ili kupiga simu lakini haikuwa na namna ya kuwafikia watu waliopo mjini. Baada ya kumpigia Crag, mtandao wa simu yangu ulitoweka pia. Wenyeji waliosikia kisa chetu walituthibitishia kuwa hatuwezi kupata mtandao katika eneo lile. Lakini Mungu aliunganisha simu ya Rebecca na Beaver aliyetukuta katika hospitali ya kijiji kile kwa haraka zaidi ya uhodari wa tumaini letu. Usimamizi wake wenye ujuzi ulikuwa ni faraja kubwa katika hospitali ile ndogo katika wakati wote tuliokuwepo pale.

 

Baada ya muda kupita, kwa majonzi Craig alipiga simu ili kutafuta ndege binafsi au ndege ya kuhamisha wagonjwa ambayo ingeweza kutuchukua na kutupeleka Lusaka (mji mkuu wenye vifaa vilivyozatitiwa vya wagonjwa wa dharura).  Hakukuwa na mtu aliyepatikana kutusaidia hadi siku iliyofuata. Lakini Mungu aliingilia kati. Bila kuunganishwa na yeyote kati yetu, Mungu alileta ndege ya kijeshi, katika saa za usiku wa manane! Tulifika Lusaka saa 2 na dakika 45 baada tu ya kuondoka. Baadaye tuliambiwa jinsi ambavyo kuingilia kwetu kati kulikuwa hakuwezekani—Jeshi la Anga halikufanya uhamisho ule, matibabu wala vinginevyo. Lakini Mungu ndiye aliyetengeneza njia.

 

Winston katika huzuni yake kuu alikuwa akilia sana juu ya maumivu makali ya tumbo zaidi ya maumivu ya jeraha lake la kichwani. Baadaye marafiki zangu wawili wa karibu walisema kuwa walikuwa na maombi maalum kwa Mungu ili aweze kuponya kila aina ya damu iliyokuwa ikitoka ndani ya mwili. Wakati tuliwasili hospitalini maumivu yake ya tumbo yalikuwa yamepungua na majibu ya uchunguzi yalikuja yakiwa sawa. Mungu alifanya jambo.

 

Huko Marekani, rafiki wa karibu wa Ellers (ambaye mtoto wake wa kiume alikuwa ndani ya gari langu) alisema kuwa aliamka katikati ya saa za usiku wa manane na kuhisi ushawishi wa kufanya maombi maalumu kwa ajili ya Benjamini. Tunashukuru, baada ya kupata fahamu kutokana na jeraha lake la ubongo, alionekana kuwa sawa kabisa.

 

Katika mkutano wa ibada ya mwisho kabla hatujaondoka kwenye safari ile ya uinjilisti, mnenaji alishiriki ibada ya dhati na kulisihi kanisa liweze kukiombea kikundi cha wainjilisti. Alieleza kuhusu wana kikundi wenzetu ambao wangesafiri siku mbili baadaye ili kujiunga pamoja nasi. Nakumbuka kufikiri, Hiyo ni sawa, lakini hatuhitaji maombi maalum. Tulipata uzoefu wa safari hizi kila mwaka na haikua jambo gumu sana kwenda. Kwa kiasi fulani naelewa jinsi tulivyoyahitaji maombi hayo, lakini Mungu alijua kile kilichowekwa mbele yetu na maombi ya kusihi yanayopelekwa Kwake kwa ajili yetu kabla hata hatujatambua sababu.

MUNGU WETU NI MKUU

Wanandoa wamishonari wanaoishi umbali wa kilometa chache kutoka hospitali tulipowasili mara ya kwanza baada ya ajali walijitokeza kutoa msaada. Walitupokea kwa furaha nyumbani kwao usiku ule. Wamekuwa wakitumika mahali hapo kwa uaminifu kwa miaka 25. Waliposikia kuhusu mahali tulipokuwa tunaelekea, walisema “Hilo ni eneo baya sana! Tumewahi kuwaona wamishonari wengi sana waliokuja na kuondoka baada ya kujaribu kufanya kazi katika eneo hilo lakini waliishia kuondoka na magonjwa mabaya na ya kutisha.” Sio sisi tu ambao ibilisi alikuwa ametushambulia. Lakini Mungu ni mkuu kuliko kazi za adui yetu! Katika Sabato ya mwisho ya mikutano ya uinjilisti roho 68 zilitoa maisha yao kwa Yesu na kubatizwa!

 

Kabla hatujaenda kwenye safari yetu niliandaa wimbo mkuu kwa ajili ya kikundi chetu. Ni wimbo uliotungwa kutoka katika kitabu cha 2 Wakorintho 4:6-9. Niliwafundisha watoto wangu na tulikuwa tukiuimba katika ibada ya familia kila siku usiku. Nilijifunza pia kuuimba kwa kutumia gita na niliwafundisha baadhi ya marafiki zangu pia. Maneno ya mafungu haya yalikuwa yakipita katika mawazo yangu kwa siku kadhaa: “Kwa kuwa Mungu aliyesema, Nuru itang’aa toka gizani, ndiye aliyeng’aa mioyoni mwetu atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo. Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu. Pande zote twadhikika, bali hatusongwi, twaona shaka, bali hatukati tamaa; twaudhiwa bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi” (2 Kor. 4:6-9).


Baada ya kuakisi uzoefu wangu na kusikiliza visa vyote ambavyo tumevisikia, maneno ya fungu hili yaligonga akilini mwangu yakiwa na maana mpya. Ambayo ni hii: Nuru ya neno la Mungu iliyokuwa ikiangaza gizani ndiyo ilikuwa inapigwa vita hapa! Mungu alikuwa akiangaza kupitia katika mioyo ya wanakikosi katika Kisiwa Mamba ili kushiriki Neno la Mungu na Upendo Wake! Tulipitia hayo yote lakini tulikuwa wanyenyekevu, vyombo vya kawaida vya udongo—njia ya kushiriki hazina hii kuu kutoka katika Neno la Mungu. Na ibilisi alikuwa akivishambulia vyombo vya udongo vilivyobeba hazina hiyo ya ukweli na upendo mtakatifu.

 

Ndiyo, sisi pamoja na wengine tumekuwa tukisumbuliwa kila mahali. Nimewapitisha kwa ufupi tu katika visa hivi vilivyopita. Kulikuwa na nyakati za kufadhaisha. Tulitupwa chini, lakini kwa neema ya Mungu, hatukuangamizwa! Ni kwa namna gani Mungu alikuwa na makusudi na mipango binafsi, huku akijua yale yaliyokuwa mbele yetu, kunipatia ahadi ya kuidai na kuishikilia, kabla hatujatambua kama tunaihitaji. Mungu ni mwema sana kuweka akilini mwangu maneno ambayo baadaye ningeweza kuyarejelea kwa ajili ya kunitia moyo.

 

Na nimetiwa moyo hakika! Mimi binafsi nimetiwa hamasa zaidi ya ilivyowahi kuwa mwanzo kuruhusu nuru ya Yesu iangaze katika maisha yangu. Namruhusu Yeye afanye kile apendacho! Kuna ulimwengu uliofunikwa na giza na kujaa dhambi. Uovu mwingi. Huzuni kuu. Nia yangu imeamshwa upya ili kumtafuta zaidi Yesu ili aweze kuangaza ndani yangu kwa mwangaza mkuu. Mwovu hatashinda. Amekwisha kushindwa. Tunamtumikia Mungu mwenye nguvu anayepaswa kupewa utukufu wote, katika hali zote za huzuni na ushindi. Ninanyenyekezwa, ninathibitika na kufurahia kumtumikia Yeye.

 

Mungu hajawahi kusema kuwa hatutapitia uzoefu wa majonzi. Kwa hakika aliahidi kuwa nyakati hizo zitatupata. Lakini ameahidi pia kwamba Yeye atakuwepo pamoja nasi katikati ya hayo yote. Mungu tunayemtumikia ni wa ajabu, mwenye nguvu na mwema sana.

 

Kisiwa Mamba kwa sasa kina watendakazi wa kudumu wa kazi ya Mungu. Mwaka mmoja baadaye, kikosi kilichopo kando ya mto waliwatembelea ili kuwatia moyo waumini wapya na kukuta kanisa jipya lenye waumini takribani 80 waliobatizwa. Ndilo kanisa pekee lililopo hapo kisiwani.

 

Na kuhusu mwanangu Winston, Mungu alikuwa mwenye rehema sana! Baada ya ndege kuwasili Lusaka, gari la wagonjwa ilikuwa linatusubiri ili kutupeleka katika hospitali binafsi. Alifanyiwa upasuaji ili kuondolewa tishu zilizoharibika kidondani mwake na kushona ngozi yake ya kichwa na kufuatiwa na wiki mbili za uangalizi wa vidonda. Dalili zote za majeraha ya tumboni na kwenye ubongo yaliondoka na majibu ya uchunguzi wa mwisho yaliletwa yakiwa sawa kabisa. Hivi leo, watu wakiuliza jinsi ambavyo Winston alipona, ninatoa taarifa nikijichekea kuwa hana hatari ya kudhoofu. Ikiwa kuna jambo lolote, aliinuka kwa nguvu mpya, akiwa na akili timamu, anajishughulisha zaidi ya alivyokuwa mwanzo. Kovu lake lililopo kichwani kila siku linanikumbusha juu ya uaminifu wa Mungu na utume aliotuitia—kuangaza nuru ya upendo Wake kwa wale wanaotuzunguka.

* Kisiwa hiki pia kinafahamika kwa jina la Mutondwe. 

Alicia Marie Harding ni mmishonari anayetumika nchini Zambia kwenye taasisi iitwayo (Riverside Farm Institute), akiwa pamoja na mume wake, Craig na watoto wao wanne.

Kukubali zawadi bora

NA TED N. C WILSON

Kitabu cha Mathayo kimeandika kisa cha kuvutia sana cha Yesu. Kisa kinahusu harusi na vazi sahihi la harusi. Katika kitabu cha Mathayo 22 tunasoma kuwa harusi kubwa iliandaliwa na mfalme. Kulikuwa na vitu vingi vya kusisimua wakati mfalme alipokuwa anamuandalia kijana wake sherehe. Tunasoma katika fungu la 3, “Akawatuma watumwa wake wawaite walioalikwa kuja harusini.”

 

Kwa masikitiko, wale waliopokea mwaliko hawakuonyesha msisimko. Unaweza kufikiria kuhusu jambo hili, mfalme aalike watu kwenye harusi na walioalikwa wasije? Tunapaswa kukumbuka kwamba kisa hiki kina ujumbe kwetu leo–Yesu anatuita kuingia katika sherehe ya harusi Yake. Je, tumepanga kuwepo pale?

 

Katika kisa hiki si kwamba walioalikwa walikataa mwaliko tu; waliwakamata watumishi wa mfalme, wakawatendea ukatili na kuwaua.

 

Jambo la kusikitisha ni kwamba hata sasa wajumbe wa Mungu pia hutendewa kama watumwa wa kwenye kisa hiki walivyotendewa. Pale tunapoupokea wito wa Mungu na kusema, “NITAKWENDA” tunapaswa kuwa tayari kutafsiriwa vibaya, kukataliwa, kuteswa, kutengwa na hata kuuawa. Kwa miaka sasa Wakristo wengi, pamoja na Waadventista wa Sabato, wamekuwa wakiuawa kwa ajili ya imani yao.

 

Lakini hatupaswi kuogopa kwa sababu ya wakati ujao. Tunahakikishiwa uwepo wa Kristo hata mwisho wa nyakati. Na kila mmoja ambaye anatazama matukio yanayoendelea atatambua kwamba unabii unatimia kama ambavyo Mungu alitabiri. Tunaishi katika wakati usio wa kawaida.

WALE WALIOKUJA

Tukirejea katika kisa chetu, baada ya mfalme kupata habari jinsi watumishi wake walivyotendewa, alighadhibika sana. Alituma wanajeshi wake, wakawaangamiza wauaji wale na kuteketeza mji wao.

 

Kisha mfalme akaanza upya. Akawaambia watumishi wake, “Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili. Basi enendeni hata njia panda za barabara na wote mwaonao waiteni arusini” (Fungu la 8, 9). Watu wengi walikuja – wote wema na waovu – na sherehe ilikuwa imefurika wageni (Fungu la 11).

 

Leo hii, ujumbe wa Bwana unapotangazwa, watakuwepo watu ambao hawatafungamana na Neno Takatifu la Mungu, lakini watakuwa sehemu ya wale walioitikia wito. Katika nyakati za mwisho watakuwepo wema na waovu, ngano na magugu (tazama Mat. 13:24-30). Lakini Biblia inatuhakikishia kwamba kutakuwepo na pepeto na kwa hakika, ninaamini pepeto limekwisha kuanza.

 

Kuna njia moja pekee ambayo mimi na wewe tunaweza kujizuia wenyewe ili tusije tukafagiliwa mbali pamoja na mawazo maovu na kujiingiza katika tamaduni ambazo zitatusukumia mbali na Neno la Mungu. Ipo njia moja pekee ambayo itatufanya tusitikiswe na kutupwa nje ambayo ni kwa kuweka tumaini lote katika haki ya Yesu Kristo huku tukijifunza katika haki yake kwa kusoma Neno Lake Takatifu, kujifunza maagizo ya Roho Yake ya Unabii na kudumisha maisha yetu ya maombi pamoja Naye nyakati zote. Lazima tupokee nguvu ya Kristo itiayo haki, nguvu yake inayotakasa na nguvu Yake ya uamsho na matengenezo. Hebu na tushiriki pamoja na wengine zawadi hii ya ajabu na kuhusiana Naye katika haki Yake na kujihusisha katika mkakati wa Kila Mshiriki Kujihusisha Kikamilifu.

 

Biblia imejaa ahadi nyingi tamu zinazoonyesha kile ambacho Yesu anaweza kufanya na atafanya kwa ajili yetu pale tutakapolikubali vazi la haki Yake: “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12). Wafilipi 2:5 inatutia moyo “Iweni na nia iyo hiyo mioyoni mwenu ambayo ilikuwa pia ndani ya Kristo Yesu.” Na ufunuo 3:18 inatuambia kabisa sisi ni akina nani na namna tunavyookolewa kutoka katika laana ya kutisha ya ubinafsi: “Ununuwe kwangu dhahabu . . ., upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa . . ., na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. Wote niwapendao mimi nawakemea na kuwarudi; basi uwe na bidii ukatubu.”

 

 

KUPEWA VAZI ZURI

Tukirejea katika kisa chetu, tunapata ufahamu wa kina wa utume wa Kristo. Katika kitabu cha Mathayo 22:11 tunasoma kwamba mfalme alipokuwa akiwasalimu wageni wake, aligundua kwamba mmoja wao hajavaa vazi la harusi.

 

Akamwambia “Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi?” (Fungu la 12). Mtu yule hakuwa na cha kujibu! Japokuwa alikuwa amepewa vazi zuri, aliamua kutolivaa.

 

Hivi leo Mfalme si kwamba anatuita tu kwenda kwenye sherehe ya Mwanaye; bali pia ameandaa vazi la haki kama zawadi. Kristo anapotupatia vazi Lake la haki, ni vazi zuri na linamtosha kila mmoja! Tunatakiwa tu kulikubali na kulivaa. Vazi hili la harusi linawakilisha “tabia safi, isiyo na waa ambayo wafuasi wa kweli wa Kristo watakuwa nayo.”1

 

Tafadhali, tambua neno hili: si tabia yetu; ni tabia ya Kristo “Ni haki ya Kristo, tabia Yake pekee isiyo na kasoro, ambayo kwa njia ya imani inawekwa ndani ya wote wanaompokea Yeye kuwa mwokozi wao binafsi.”2 Je, tunaamini jambo hili kwa hakika?

 

Tunapoendelea tunasoma ahadi hii ya ajabu: “kuvikwa, vazi la haki Yake, Kristo ataliweka juu ya kila roho itubuyo na kuamini . . . Vazi hili, limefumwa katika nyumba ya mfumaji wa mbinguni, halina uzi hata mmoja wa kibinadamu. Kristo akiwa katika hali yake ya ubinadamu alitengeneza tabia kamilifu na tabia hii anaitoa ili kutupatia. ‘Na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi.’ . . . kupitia utii wake mkamilifu amefanya iwezekane kwa kila mwanadamu kutii amri za Mungu.”3 

 

 

KRISTO ANAISHI NDANI YETU

Usiangukie katika mtego ambao watu wanatuwekea kwa kusema, “Haiwezekani kushika sheria. Haiwezekani kuishi maisha makamilifu.” Wakati ni kweli kwamba hatuwezi kuishi maisha makamilifu kwa nguvu zetu wenyewe, kwa kupitia vazi la haki ya Kristo ikitufunika na nguvu Yake akiishi ndani yetu, tunaweza kufuata kila njia anayotuongoza kwayo.

 

Kisha, utakaso unaanza–haki ya Kristo iko ndani yetu. “Ikiwa tutajisalimisha wenyewe kwa Kristo, mioyo yetu ikaunganishwa pamoja na moyo Wake; mapenzi yetu yanaungana na mapenzi yake; mawazo yetu yanakuwa sawa na mawazo Yake, fikra zetu zinatekwa na Yeye; tunaishi maisha Yake. Hii ndiyo maana ya kufunikwa na vazi la haki Yake. . . . Haki ni kufanya mapenzi mema na kila mmoja atahukumiwa kwa matendo yake. Tabia zetu zinafunuliwa dhahiri kupitia kile tunachotenda. Matendo yanaonyesha kama imani ni halisi.”4 

 

Je, uko tayari kupokea, kutoka katika mkono wa Kristo, vazi la kukufunika ambalo litakuwezesha kuwa mtendakazi pamoja na mbingu? Kukubali zawadi nzuri ya vazi la Kristo linalotufunika na kutubadilisha na kutufanya kuwa na mfano Wake ni msingi mkuu unaotuandaa ili kuwa wafuasi wa Kristo na watendakazi pamoja Naye. Hebu na tuikubali zawadi Yake ya ajabu ya nguvu Yake itakasayo na kutusafisha na kutufanya kuwa tayari kwa sherehe ya arusi ya mbinguni ya Mwana-Kondoo!

1 Ellen G. White, Christ’s Object Lessons (Washington, D.C.: Review and Herald Pub. Assn., 1900, 1941), uk. 310.

 

2 Ibid.

 

3 Ibid., kur. 311, 312. 

 

4 Ibid., uk. 312.

Ted N.C. Wilson ni Mwenyekiti wa Konferensi Kuu ya Waadventista wa Sabato. Makala nyingine na vitabu vya maelezo zaidi vinapatikana katika X (awali Twitter):@pastortedwilson na kwenye Facebook: @Pastor Ted Wilson.

Kisa cha Redio ya Waadventista Ulimwenguni

NA ALLEN STEELE PAMOJA NA WATUMISHI WA AWR

Pamoja na kuwapo kwake na utume wa kushiriki injili katika “maeneo ambayo ni magumu kufikiwa hapa duniani,” inawezekana wengi katika kanisa la Waadventista wanahisi kwamba Redio ya Waadventista Ulimwenguni (AWR) imekuwepo “daima.” Si hivyo. Ingawa huduma hii ilianzishwa miaka 54 iliyopita, chimbuko lake lilianza muda mrefu zaidi ya miaka hiyo.

 

Kuanzishwa sahihi kwa AWR kunaweza kuwa ni wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Baada ya vita kuisha mwishoni mwa miaka ya 1930, mataifa yaliyoshinda yalielewa nguvu ya redio kupitia kumbukumbu za watu waliovutiwa na kuhama kutokana na mambo yaliyokuwa yanaenezwa kupitia redio. Ndani ya miongo michache tangu ilipogunduliwa, redio imekuwa kaya ya ulimwengu na ilikuwa njia kuu ambayo kupitia kwayo watu walitambua kile kilichokuwa kikitendeka ulimwenguni. 

 

Raia walioanzisha walifikiwa na muujiza huu wa mawimbi ya redio pia na vituo vingi vya redio binafsi vilienea kote Barani Ulaya. Mtu mmoja pekee ndiye alikuwa katika mstari wa mbele kwa maendeleo ya redio. Jina lake aliitwa Jacques Trémoulet, aliyejulikana zaidi kama mmiliki wa redio Luxembourg, lakini mtandao wake wa vituo ukawa mojawapo ya mashirika makubwa ya redio yanayomilikiwa na watu binafsi barani Ulaya.

 

Wakati vita vilipoanza, mataifa yaliyoshinda yaliamrisha vituo vyote vya matangazo ya redio kuongeza maeneo yao kwa haraka kadri wawezavyo. Redio ya Tremoulet ilitaifishwa naye akapata kimbilio katika nchi isiyofungamana na upande wowote, akiwa na tumaini kuwa angeweza kuishi. Mgogoro ulipoisha, alirejea nyumbani kwake Ufaransa ili kuangalia kama vituo vyake vingeweza kurejeshwa.

 

Wakati huu ndipo alikutana na Waadventista wa Sabato. Kanisa la Waadventista lilikuwa likisaidia bara la Ulaya kujiimarisha tena baada ya miaka ya vita na walikuwa wakitafuta vituo vya redio ambavyo vingewaruhusu kupepeperusha vipindi vilivyoangazia ujumbe wa kiroho na kutangaza juhudi za hisani zao. Walijisajili kwa ajili ya vipindi kwenye redio Luxembourg, na kipindi cha Sauti ya Matumaini kwa lugha ya Kifaransa kilirushwa hewani mwaka 1947. Mwaka 1951 kipindi cha Kingereza cha Sauti ya Unabii kilipeperushwa kwa mara ya kwanza redioni. Hivyo, ubia kati ya Waadventista na Tremoulet ulianza.

KUPANUA UTUME

Mwaka 1971 Tremoulet alikuwa na ombi jipya kwa Waadventista: “Sasa ninamiliki mtambo wa kusafirisha mawimbi ya sauti (transimita) nchini Ureno ambao utawapa nafasi ya kutoa taarifa za matukio katika masafa mafupi kote Mashariki na Magharibi mwa Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskini. Je, mngependa?”

 

Viongozi wa kanisa, kwa majina Robert Pierson Mwenyekiti wa Konferensi Kuu, Neal Nelson Mwenyekiti wa Divisheni ya Amerika ya Kaskazini, walitaka kutumia fursa hii njema kulifikia eneo muhimu ulimwenguni kwa njia ya redio, lakini bajeti ya kanisa haikuwa na akiba iliyowekwa ili kunufaika na jambo hilo jipya, kubwa na la muda mrefu. Hivyo swali liliibuka: “Ikiwa huu ndio uelekeo ambao Mungu anatuongoza kuuelekea, tutawezaje kupata pesa kwa ajili ya kutegemeza mpango huu?”

 

Ombi hilo likawa kiini cha mada kuu ya mjadala katika makao makuu ya kanisa. Wahazini waliwatahadharisha kwamba kanisa halitaweza kuhimili mpango huu kwa muda mrefu, lakini washiriki wa kawaida kwenye kamati walilisihi sana kanisa kutumia fursa hii.

 

Mzee Pierson na Wilson walisikiliza na kufikiria kuhusu faida na hasara. Mwisho wakaja na mkakati huu: Wangetoa changamoto kwa waumini wa Kanisa la Waadventista ulimwenguni kuwaunga mkono katika utume wa kuanzisha utaratibu kwa ajili ya sehemu ya ulimwengu ili iweze kufikiwa na transimita kubwa ya Tremoulet itakayowekwa nchini Ureno.

 

Walipendekeza mpango huu kwa imani, wakauita ujasiri wa kusonga mbele wakiamini kwamba washiriki wa kanisa watasukumwa na Mungu kufanya sehemu yao ili kuunga mkono mpango huu wa muda mrefu.

 

Punde mipango ikawekwa kuanzisha mradi huo. Meneja Allen Steele na mke wake, Andrea, walipangwa kwenda kusaidia katika kuweka mipango. Moja kati ya mambo ya kwanza kufanyiwa maamuzi ilikuwa ni jina.

 

Je iitwe Sauti ya Matumaini, kama walivyopenda kuita watu wa Ulaya au Sauti ya Unabii, jina lililopendwa na watu wa Marekani?

 

Allen alisema, “Suala la kuchagua jina liliachwa chini ya idara ya mawasiliano. Katika mjadala niliwasihi wenzangu kuchagua jina jipya – kwa jina hilo kanisa lingetambuliwa kama wawezeshaji wa mpango huo. Jina la Redio ya Waadventista Ulimwenguni lilionekana kufaa zaidi.”

 

Familia ya Steele walitumwa Ureno mwishoni mwa mwaka 1971, wakitahadharishwa kwamba kanisa limejitoa kuwezesha mpango huu kwa mwaka mmoja tu, hivyo mpango wa muda mrefu utategemea sadaka za waumini.

 

Allen alisema “Tulikuwa tayari kuwa sehemu ya mkakati huu.” “Hatimaye hakuna mtu ambaye alipaswa kuwa na wasiwasi, kwa sababu katika miisho ya mwaka wa kwanza pesa ya kutosha ilikuwepo kwa ajili ya mwaka unaofuata. Uwezeshwaji uliendelea na mwito wa kuendelea kuwa watangazaji ulikuwa unarudiwa mwaka baada ya mwaka.”

 

Allen na Andrea waliendelea na kazi yao hapo AWR kwa miaka mingi wakati huduma hiyo ikikua na kutambuliwa kama redio kubwa katika jukwaa la ulimwengu.

MATOKEO YASIYOKOMA  

Hivi leo AWR, chini ya uongozi wa Duane McKey, imefika ulimwenguni kote kupitia vituo 2000 kwa zaidi ya lugha 100, ikishiriki injili kupitia Redio ya Biblia inayotumia nishati ya jua “Godpods,” na kukutana na watu walio na mahitaji kupitia matukio makubwa ya huduma za kiafya, yanayoshikilia idadi kubwa ya mifululizo ya uinjilisti kwa kushirikiana na mpango wa Kila Mshiriki Kujihusisha Kikamilifu na mingine mingi.

 

Lakini yote yalianza wakati changamoto iliyotolewa na viongozi wa kanisa ilipobadilika na kuwa chombo muhimu cha kukuza kanisa na kuwaandaa watu kuwa tayari kwa ajili ya ujio wa pili wa Yesu . . . “Ujasiri wa kusonga mbele” kwa matokeo yasiyokoma yatakayofunuliwa mbinguni pekee!

 

Maoni kwa Mhariri: Taarifa nyingi hapa zinatokana na uelewa wa mwandishi. Msemo “ujasiri wa kusonga mbele” umechukuliwa kutoka kwenye makala inayopatikana katika kitabu cha Review and Herald cha mwaka 1971. Ili kujifunza zaidi kuhusu historia ya Redio ya Waadventista Ulimwenguni, tazama kitabu kilichoandikwa na Allen Steele kiitwacho Air Force kilichochapwa na Nyumba ya uchapaji ya Pacific Press. Ili kutazama visa mbalimbali vya utume vinavyotia moyo “video za miujiza” na kuunganishwa na AWR, tembelea tovuti ya awr.org.

Allen Steele, Ed.D., ni muasisi wa Redio ya Waadventista Ulimwenguni.

Kuonyesha jinsi ambavyo Mungu analitazama kanisa Lake na wajibu ambao alitarajia kanisa liufanye katika kubadilisha maisha ya watu kwa ajili ya umilele. 

NA ELLEN G. WHITE

Kanisa ni wakala aliyechaguliwa na Mungu kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Lilianzishwa kwa ajili ya kutoa huduma na utume wake ni kupeleka injili ulimwenguni. Umekuwa ni mpango wa Mungu tangu mwanzo kanisa Lake liiakisie dunia utimilifu na utoshelevu wa Mungu kwa watu Wake. Waumini wa kanisa yaani wale aliowaita toka gizani kuja kwenye nuru Yake ya ajabu, imewapasa kuudhihirisha utukufu Wake. Kanisa ni mtunzaji wa utajiri wa neema ya Kristo na kwa njia ya kanisa Lake, hatimaye atadhihirishwa “kwa falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho,” dhihirisho la mwisho kamilifu la upendo wa Mungu (Efe. 3:10). . . .

 

 

KUSUDI LA KANISA

Kanisa ni ngome ya Mungu, mji Wake wa kimbilio, na anaendelea kulitunza kwenye ulimwengu huu ulioasi. Kulisaliti Kanisa kwa namna yoyote ile ni hila na udanganyifu mbele Zake Yeye aliyewanunua wanadamu kwa damu ya Mwana Wake wa pekee. Kumekuwa na watu Wake walio waaminifu ndani ya Kanisa Lake tangu mwanzo hapa duniani. Katika kila kizazi Bwana amekuwa na walinzi Wake waliokuwa wanatoa ushuhuda kwa uaminifu katika kila kizazi walichokuwa wanaishi. Wajumbe hawa walikuwa wanatoa ujumbe wa onyo na walipotakiwa kuweka silaha zao chini, wengine walisimama kuchukua nafasi zao kazini. Mungu aliwaleta mashahidi Wake hawa kwenye agano la uhusiano pamoja Naye, akiliunganisha kanisa lake lililo duniani na lile lililoko mbinguni. Amekuwa akiwatuma malaika Wake kulihudumia kanisa na milango ya kuzimu imekuwa haiwezi kuwashinda watu Wake.

 

Mungu ameendelea kulitegemeza kanisa Lake kwa karne nyingi dhidi ya mateso, migongano na giza la kiroho. Hakuna wingu lililolishukia kanisa ambalo hakujiandaa kukabiliana nalo, wala hakuna nguvu yoyote ya upinzani aliyoiruhusu kuipinga kazi Yake ambayo hakuiona mapema. Yote yametimia kama alivyokuwa ametabiri. Hajawahi kuliacha kanisa Lake ukiwa, lakini kupitia matamko ya unabii alikuwa amefunua tayari nini kitatokea na kile Roho Wake alichokuwa amewafunulia manabii wake kukitabiri, hicho ndicho kilichokuja kutokea. Makusudi Yake yote yatatimia. Sheria yake inafungamana na kiti Chake cha enzi, na hakuna nguvu ya uovu inayoweza kuharibu kazi Yake. Mungu huutoa ukweli Wake na kuulinda na utashinda kila aina ya upinzani.

 

Wakati wa vipindi vya giza la kiroho, Kanisa la Mungu limekuwa ni mji uliojengwa juu ya kilima. Toka kipindi kimoja hadi kingine na vizazi vyote vilivyofuata, mafundisho safi ya mbinguni yamekuwa yakiwekwa wazi kila mahali. Hata kama yatakuwa yanaonekana kuwa dhaifu na yenye upungufu, Kanisa ni chombo ambacho Mungu hukihudumia kwa upekee mkubwa na kukiangalia kwa umakini wa hali ya juu sana. Ni mahali ambapo neema yake inadhihirishwa, mahali apendapo kuufunua uweza wake wa kuibadilisha mioyo ya wanadamu.

 

 

KANISA – ENEO LA MUNGU LA UTUME

Kristo aliuliza, “Tuulinganishe na nini ufalme wa Mungu? Au tuutie katika mfano gani?” (Marko 4:30). Asingeweza kuufananisha na falme za dunia hii. Katika jamii hakuona chochote kilichokuwa kinafanana nao. Falme za kidunia hutawala kwa mwenye nguvu kuingia madarakani kwa nguvu za kimwili, lakini katika ufalme wa Kristo, kila silaha ya kimwili na kila zana itumikayo kulazimishia watu hairuhusiwi kutumika kabisa. Ufalme huu upo kwa ajili ya kumuinua na kumfanya mtu kuwa mpole na muungwana. Kanisa la Mungu ni uga wa maisha matakatifu, likiwa limejawa na karama zinazotofautiana na kuwezeshwa na Roho Mtakatifu. Waumini wanatakiwa kuipata furaha yao katika furaha ya wale wanaowasaidia na kuwabariki.

 

Kupitia Kanisa Lake, BWANA anakusudia kukamilisha kazi njema sana ili jina Lake lipate kutukuzwa. Taswira ya kazi hii inaelezwa katika njozi ya Ezekieli ya mto wa uponyaji: “Ndipo akaniambia, Maji haya yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki, nayo yatashuka mpaka Araba, na kuingia katika bahari; maji yatokezwayo yataingia baharini, na maji yake yataponyeka. Tena itakuwa kila kiumbe hai kisongamanacho, kila mahali itakapofika mito hiyo, kitaishi; . . . Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayatatindika kamwe; utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yatatoka mahali patakatifu; na matunda yake yatakuwa ni chakula; na majani yake yatakuwa ni dawa” (Ezekieli 47:8–12).

 

Tangu awali Mungu amekuwa akitenda kazi kupitia watu Wake ili kuubariki ulimwengu. Kwa taifa la Misri ya kale, alimfanya Yusufu kuwa chemchemi ya uzima. Kupitia kwa uadilifu wa Yusufu, maisha ya watu wote wa taifa lile yalihifadhiwa. Kwa kumtumia Danieli, maisha ya wenye hekima wote wa Babeli yaliokolewa. Na ukombozi huu ni mafundisho hai; ni vielelezo vya baraka za kiroho zinazotolewa kwa ulimwengu kwa wale wanaojiungamanisha na Mungu aliyekuwa akiabudiwa na Yusufu na Danieli. Kila mmoja aliye na Kristo moyoni mwake na kila atakayeuonyesha upendo wa Kristo kwa ulimwengu ni mtenda kazi pamoja na Mungu kwa ajili ya kuwabariki wanadamu. Kwa kadiri anavyoipokea neema toka kwa Mwokozi ili kuwaarifu wengine habari zake, toka kwa mtu huyo yatakuwa yanatiririka maisha ya kiroho.

 

Mungu aliwachagua Israeli ili waidhihirishe tabia yake kwa wanadamu. Alikuwa amewakusudia wawe visima vya wokovu kwa ulimwengu. Hawa walikuwa wamekabidhiwa mausia ya mbinguni, ufunuo wa mapenzi ya Mungu. Katika siku za awali za wana wa Israeli; mataifa ya duniani yalikuwa yamepoteza ufahamu wa kumjua Mungu kwa sababu ya mienendo yao ya kifisadi. Kabla ya hapo walipata kumjua, “kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru, bali walipotea katika uzushi wao na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza” (Warumi 1:21). Lakini kwa huruma zake Mwenyezi Mungu hakuwaangamiza. Alikusudia kuwapatia fursa nyingine ya kumtambua kupitia kwa wateule Wake. . . .

 

 

BARAKA ZILIZOPOTEZWA

Lakini wana wa Israeli walipoteza fadhila hizi walizopewa za juu kabisa za kuwa wawakilishi wa Mungu. Walimsahau Mungu na kushindwa kutimiza utume wao mtakatifu. Baraka walizopewa hazikutumika kuubariki ulimwengu. Kila lililo jema walilokuwa wamejaliwa na Mungu walilitumia kujitukuza wao binafsi. Walijitenga mbali na ulimwengu ili kukwepa majaribu. Mipaka waliyokuwa wamewekewa na Mungu kuwalinda wasishirikiane na waabuduo sanamu ili kuwazuia wasifuatishe mienendo ya kipagani waliitumia kujenga ukuta wa utengano kati yao na mataifa mengine yote. Walimpokonya Mungu kwa nguvu huduma aliyokuwa anaitaka kwao na kuwaponya wanadamu wenzao mfano mtakatifu na uongozi wa dini njema. . . .

 

Viongozi wa Kiyahudi walijiona ni wenye busara sana kuweza kusikiliza maelekezo, wenye haki sana kiasi cha kutohitaji wokovu, wenye kuheshimika sana kiasi cha kutohitaji heshima itokayo kwa Kristo. Mwokozi aliachana nao na kugeuzia kwa wengine fadhila walizozitumia vibaya na kazi waliyokuwa wameidharau. Utukufu wa Mungu ni sharti udhihirishwe na neno Lake lithibitike. Ufalme wa Kristo ni lazima usimikwe kwa uthabiti duniani. Ilikuwa ni lazima wokovu wa Mungu uenezwe katika miji ya jangwani; na wanafunzi wa Kristo waliitwa kuifanya kazi ambayo viongozi wa Kiyahudi walikuwa wameshindwa kuifanya.

Waadventista wa Sabato wanaamini kwamba Ellen G. White 1827-1915 aliitumia karama ya unabii kwa muda wa miaka zaidi ya 70 ya utume. Dondoo hii imechukuliwa kutoka katika kitabu cha The Acts of the Apostles, kur. 9-16.

Chaguzi ndogo dhabiti huleta matokeo makubwa. 

NA MARION PEPPERS

Kwa kipindi cha muda mrefu nimekuwa nikiichukulia afya yangu kama jambo la ziada–nikipuuza kufanya mazoezi na lishe na kutumia matibabu ya haraka. Baada ya miaka ya mapambano, mwisho nilianza kuelewa kwamba kutunza afya yangu haikumaanisha tu kujiona au kujihisi kuwa na hali fulani njema; bali ilimaanisha kumheshimu Mungu kwa maisha ambayo amenipatia.

 

Mungu ametuumba ili tuwe mawakili wa mambo mengi, ikiwa ni pamoja na miili aliyotupatia (taz.1 Kor. 6:19, 20). Swali ni hili: Je, tunaitendea miili yetu vyema na kwa heshima sawa sawa na vile ambavyo Mungu angeitendea? Pale tunapojitunza, hatufanyi tu mapenzi Yake bali tunadumu pia kufuata mwongozo Wake.

 

Sijui kwa upande wako, lakini maisha yangu yamekuwa na shughuli nyingi! Je, tutapata wapi muda wa kuihudumia miili yetu? Hatujapewa motisha bado. Ni vigumu kuwa na utaratibu thabiti wa mazoezi na kula vizuri. Tunashukuru kwa kuwa Mungu ndiye mpaji wa vitu vyote vizuri, ikiwemo zawadi ya nidhamu na nidhamu ndio hutengeneza motisha. 

 

Vifuatavyo ni vidokezo rahisi vinavyoweza kukusaidia kutengeneza afya yako:

 

 

ANZA NA MABADILIKO KIDOGO, ENDELEVU.

Marekebisho ya taratibu mara nyingi ndiyo yanaweza kwa kiasi kikubwa kuleta athari nzuri kuliko marekebisho ya haraka haraka na yasiyo na kiasi katika mtindo wa maisha. Mfano, kuwa na tabia ya kulala na chupa ya maji pembeni ya kitanda chako. Usikubali kuamka kitandani na kuanza kufanya mambo yako kabla haujanywa maji. Kisha weka kitu ambacho kitakukumbusha kunywa maji kwa siku nzima! Wale wanaoanza pole pole wanaweza zaidi kumaliza vyema.

 

 

KUSONGA NI ZAWADI.

Mazoezi hayapaswi kutazamwa kama adhabu. Tafiti zinaonyesha umuhimu wa kujongea kwa kila kiungo cha mwili pamoja na mazoezi ya moyo na mazoezi ya nguvu ili kuweka viungo na misuli katika afya njema. Hii haimaanishi kwamba unapaswa kutembea umbali wa maili 10 kwa siku au kutumia saa mbili kufanya jambo usilolipenda. Anza kwa kufanya mazoezi ndani ya dakika 10; fanya kuwa tabia yako kutembea kila baada ya kuamka; tafuta kitu ambacho wanafamilia wako watafurahia kukifanya pamoja na wewe. Kwa ufupi songa zaidi.

 

 

CHAKULA NI MAFUTA.

Badala ya kuwa na hofu kuhusu mlo kamili na kalori zipatikanazo katika chakula, pendelea kula vyakula kamili ambavyo tumepewa na Mungu. Kitazame chakula kama mafuta kama ambavyo ilitakiwa kuwa. Kula “chakula halisi” kula mlo kamili kwa kupata vyakula vya nyuzi nyuzi, protini na mafuta yenye afya na usiendelee kula ukiwa umeshiba.

 

 

PATA MUDA WA KUPUMZIKA NA KUPATA NGUVU TENA.

Kama ambavyo mazoezi yalivyo muhimu, kupumzika pia ni jambo la muhimu. Panga kuwa na muda mwingi wa kulala na furahia raha ya Sabato ambayo Mungu alitupatia katika kila siku ya saba.

 

 

IPE KIPAUMBELE JAMII YAKO NA KUWAJIBIKA

Jamii ni muhimu kwa afya zetu, kwani hutoa mfumo wa msaada, uwajibikaji na uhusiano wa kijamii. Tunapokutana kuabudu kama jamii ya waumini, hebu na tutiane moyo kila mmoja – kimwili, kiroho, na kihisia! 

 

Afya yako haitakiwi kuwa na changamoto. Kwa kuchukua hatua pole pole na kufanya uamuzi thabiti, unaweza kujenga maisha yenye afya. Kuuhudumia mwili wako ni njia pekee ya kumheshimu Yeye aliyekupa uhai. Anza hapo ulipo, kwa kutumia kile ulichonacho na amini kwamba kila hatua moja unayoipiga huelekea katika ustawi unaodumu.

Marion Peppers ni mke, ni mama anayefundisha watoto wake nyumbani, mkufunzi binafsi na muasisi wa kituo cha mazoezi cha Peppers Total Fitness. Yeye na familia yake wanaishi Marekani katika jimbo la Tennessee.

Ubatizo wa Yesu lazima uwe na umuhimu mkubwa kwa sababu ndilo jambo la kwanza lililofanywa na Yesu ili kuanza huduma Yake ya hadhara. Ni muhimu pia kwamba ubatizo Wake umeandikwa au kuelezewa katika vitabu vyote vinne vya Injili (Mathayo 3:13-16; Marko 1:9-11; Luka 3:21, 22; Yohana 1:32, 33). Swali lako ni swali zuri sana. Mawazo kadhaa yameelezewa kwa mpangilio.

 

 

HAUKUHITAJIKA, LAKINI NI WA LAZIMA 

Mwanzoni Yohana hakutaka kumbatiza Yesu, lakini Yesu alimfahamisha kuwa jambo hilo linapaswa kufanyika ili kutimiza mpango wa Mungu (Mt. 3:13-15). Kweli, wanadamu wenye dhambi wanahitaji ubatizo, lakini si Yesu. Hapa, mtu asiye na dhambi anadhihirisha kile ambacho, kulingana na mpango mtakatifu, wadhambi lazima wafanye. Ni makusudi ya Mungu kwamba wadhambi waungame dhambi zao, watubu na kubatizwa. Yesu akiwa kama mwakilishi wetu alitufanyia kile ambacho, kwa wakati ule, tusingeweza kufanya lakini tunatarajia kufanya. Katika kubatizwa Kwake Yesu alitufahamisha utaratibu wa wokovu: kuungama, kutubu, kubatizwa na kupokea Roho. Inaweza kusemwa kuwa kupitia kubatizwa Kwake Yesu alipanda kutoka kwa ubatizo wa Yohana wa toba kupitia kwa maji mpaka kwa ubatizo halisi wa Ukristo kupitia kwa maji na Roho. 

 

 

UWEPO WA UUNGU

Wakati Yesu akipanda kutoka majini, aliingia katika majibizano na Baba kwa njia ya maombi, Baba na Roho walionyesha uwepo wao pale Yordan. Baada ya anguko Mwana wa Mungu alifanyika kuwa mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu wenye dhambi, lakini sasa Baba tena anazungumza moja kwa moja na Mwanadamu, Mungu aliyechukua umbo la mwanadamu. Mshirika mmojawapo wa Uungu alikuwa hapa na sasa anaungana na wenzake wawili kwa ajili ya kulitangaza tukio la muhimu kupita uwezo wa mwanadamu. Kama ambavyo Kristo alivyo mwakilishi wetu, maneno ya Baba yalikuwa yakisemwa kwetu pia (Mt. 3:17; Marko 1:11; Luka 3:22). Huu ulikuwa ni wakati muhimu sana katika historia ya ulimwengu mzima. Sauti ya Mungu inasikika katika sayari yetu iliyoasi ikitangaza kuwa mwanadamu ni mali ya Uungu na kuwaelezea wanadamu kama wana wapendwa wa Mungu! Jambo hili lingewezekana kwa sababu Mwana angeshuka chini kaburini na kutoka nje ya kaburi akiwa hai na mwenye ushindi. Katika ubatizo wa Yesu Nafsi tatu za Uungu, ambazo kwa asili ndio waliotengeneza mpango wa wokovu, sasa wapo katika sayari yetu katika tukio makini kwenye kisa cha ukombozi.

 

 

TANGAZO LA VITA

Kupitia tukio la Yesu kufanyika mwili, Mwana wa Mungu alikuja kwetu ili kuzikabili nguvu za uovu zaidi ya vile ilivyokuwa mwanzo. Bado alikuwa amejificha Galilaya kwa muda wa miaka 30. Katika kalenda ya Mungu kila tukio linatendeka kwa wakati uliopangwa. Danieli alitabiri juu ya wakati wa kutiwa mafuta kwa Masihi (Dan. 9:25) na sasa muda huo umefika. Yesu aliondoka Galilaya na kuelekea Yordani ili kutangaza kuwa pambano Lake la wazi na Shetani hapa duniani, lilikuwa linaanza. Ubatizo wake ulikuwa ni tukio la wazi ambalo kupitia kwalo alitambulishwa kwetu si tu kama Mwana mpendwa wa Mungu bali pia kama Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu (Yohana 1:29, 36) kwa njia ya kufanya vita na nguvu za uovu zisizokuwa sambamba na historia ya ulimwengu. Pambano liamualo hatima ya mwanadamu lilikuwa limeanza. Lilikuwa ni pambano kwa ajili ya moyo wa mwanadamu na ukombozi wa mwisho wa Sayari Dunia. Hakukuwa na muda wa kupoteza! Mara tu baada ya ubatizo Wake Yesu aliongozwa na Roho hadi nyikani ili kukabiliwa na Shetani na alimshinda, akitazamia ushindi Wake wa mwisho msalabani. Tukio la ubatizo wa Yesu ni la muhimu hasa katika historia ya ukombozi ambalo litawafanya wanadamu kuungana Naye kupitia ubatizo.

Ángel Manuel Rodríguez, Th.D., amestaafu baada ya kutumika kama mchungaji, profesa na mwanateolojia.

Je, vikoleza sukari visivyo vya asili ni mbadala wenye afya?

Ninajaribu kuishi na kula kiafya zaidi na nina marafiki ambao hawapungui uzito hata wanapotumia vikoleza sukari visivyo vya asili. Je, vikoleza sukari hivi ni salama na sahihi kwangu kutumia kwa ajili ya mahitaji yangu ili kutengeneza afya bora na kupunguza uzito?

Vikoleza sukari vya asili na vikoleza sukari visivyo vya asili vinatofautiana kimsingi katika asili yake, utengenezwaji wake na jinsi vinavyoathiri mwili. Vikoleza sukari visivyo vya asili, ambavyo mara nyingi hupigiwa debe kama vyenye afya kuliko sukari vimekuwa lengo kuu la tafiti nyingi za kisayansi kwa kuzingatia hatari za kiafya zinazoweza kutengenezwa na vikoleza sukari hivi. Tafiti mbalimbali zimetoa majibu mchanganyiko, ikisababisha midahalo inayoendelea kuhusu usalama wake na athari zake za muda mrefu.

 

Vikoleza sukari vya asili, kama vile asali, maji maji ya mti wa mwaloni na Stevia, vinatolewa kwenye mimea au wanyama na hupitia mchakato mdogo wa utengenezwaji. Mara nyingi hubakiza baadhi ya virutubishi na kemikali zurulaji mwilini, ambazo zinaweza kutoa faida za ziada mwilini. Asali ina vitu vinavyopambana dhidi ya bakteria, na Stevia inafahamika kwa kuwa na kiwango kidogo cha kalori huku ikiwa na athari ndogo sana kwenye viwango vya sukari kwenye damu. Asali inaweza kuwa chaguo zuri zaidi kiafya kuliko sukari na inapaswa kutumiwa kwa kiasi.

 

Vikoleza sukari visivyo vya asili ni mchanganyiko uliotengenezwa ili kutoa utamu kama wa sukari asili isiyokuwa na kalori. Mifano ya kawaida ni pamoja na kiungo kitamu kuliko sukari kiitwacho aspartame, sukralosi, erythritoli na sakrani. Ingawa ni tamu zaidi kuliko sukari, athari zake za muda mrefu za kiafya bado ni mada ya mjadala na imefanywa kwa miongo kadhaa. Baadhi ya tafiti zinahusianisha na matatizo ya kimetaboliki, kuongezeka kwa hamu, na matatizo ya afya ya utumbo ambayo hayahusiani na vikoleza sukari vya asili. Vikoleza sukari vya asili huwa na manufaa zaidi kwa kiasi, wakati vikoleza sukari visivyo vya asili vinaweza kubeba hatari zinazohitaji tahadhari.

 

Tafiti zinaonyesha kwamba baadhi ya vikoleza sukari visivyo vya asili vinaweza kusababisha mvurugiko wa viumbe wadogo sana wanaopatikana kwenye utumbo waitwao mikrobiota, ambao hufanya kazi muhimu sana katika mmeng’enyo wa chakula na katika afya kwa ujumla. Kutumia aspartame inaweza kubadilisha muunganiko wa bakteria waliopo tumboni, ambapo hupelekea athari za kimetaboli. Tafiti nyingine zinaonyesha uwiano uliopo baina ya watumiaji wa vikoleza sukari visivyo vya asili na kuongezeka kwa dalili hatari za matatizo ya kimetaboliki, unene uliokithiri, na aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari, ikiashiria kwamba dutu hizi hazina madhara makubwa kama ambavyo wengi wanaamini.

 

Tafiti za hivi karibuni zinaonyesha wazi hatari za matukio ya ugonjwa wa moyo na mishipa (shambulio la moyo na kiharusi) yanayohusiana na matumizi ya erythritol, kileo kinachotumika kama sukari kinachanganywa katika utengenezaji wa vyakula. Zaidi tafiti mbalimbali za kimajaribio zinaonyesha kwamba erythritol inaongeza uchochezi wa seli sahani zilizopo kwenye damu ambazo ni kinga ya damu inayoifanya damu kuganda zaidi na kupelekea mtu kuwa na ugonjwa wa kiharusi na shambulio la moyo. Kutumia kinywaji kimoja chenye erythritol inaweza kusababisha utengenezwaji wa kinga hiyo ya damu kwa kiwango kikubwa zinazochochea seli sahani kufanya kazi.

 

Kwa ufupi, baadhi ya vikoleza sukari visivyo vya asili vinaweza kusaidia katika kupunguza ulaji wa kalori lakini hatari zake za kiafya haziwezi kupuuzwa. Ingawa kiasi ni muhimu, njia salama zaidi ni kupunguza ulaji wa vikoleza sukari visivyo vya asili na kuzingatia lishe bora iliyo na vyakula kamili. Utafiti zaidi unahitajika ili kuelewa kikamilifu athari za muda mrefu za dutu hizi na kubaini ni ipi, ikiwa ipo, inaweza kupendekezwa kwa usalama. Tunashauriwa kufanya mazoezi, kupumzika, kuwa na kiasi, kuhakikisha usawa wa virutubisho na kuzingatia vyakula vyote ili kuendeleza afya zetu kwa ujumla.

 

“Mausia yako ni matamu sana, kupita asali kinywani mwangu. Kwa mausia yako najipatia ufahamu . . .” (Zab. 119:103, 104).

Zeno L. Charles-Marcel, mkufunzi wa magonjwa ya ndani aliyeidhinishwa na bodi, ni mkurugenzi wa Huduma ya Afya ya Waadventista katika Konferensi Kuu. 

 

Peter N. Landless, mtaalamu wa magonjwa ya moyo aliyeidhinishwa na bodi na mkurugenzi mstaafu wa Huduma ya Afya ya Waadventista ya Konferensi Kuu, ni mkufunzi pia.

Kisa cha Jim Lanning

Siku moja nilipokea simu kutoka Konferesi Kuu. Unaelewa jinsi mfumo unavyofanya kazi: Mtu akipiga simu; na mimi sipo, anaacha ujumbe wa sauti ambao naweza kuusikia mahali popote pale nitakapokuwa.

 

Jim Lanning alikuwa akifanya kazi kwa ajili ya Maendeleo ya Waadventista na Shirika la Maendeleo na Msaada (ADRA) na kwa nadra sana alikuwepo katika ofisi yake ya nyumbani. Miadi aliyokuwa nayo ilimfanya yeye kuzunguka kila mahali nchini Marekani na takribani katika nchi zote ulimwenguni. Ikiwa ungehitaji kumpata, ulitakiwa kupiga simu ofisini kwake, unaacha ujumbe wa sauti na kungoja. 

 

“Nilipiga simu kufuatilia kuhusu ujumbe wangu karibu kila siku” alisema Jim. “Niliipigia namba ya ujumbe wa sauti wa Konferensi Kuu, na kuingiza mkondo wangu na kisha kusikiliza ujumbe uliosalia katika mfumo.”

 

Kwa juma moja Jim alikuwa Seattle, Washington na kuzunguka nchi ya marekani kutoka makao makuu ya Konferensi Kuu huko Silver Spring, Maryland, mahali ambapo alitakiwa kukutana na waandisi mbali mbali huko Boeing. Jioni moja, kabla hajala chakula chake cha jioni, Jim aliamua kupitia ujumbe wake. Jumbe za kwanza zilikuwa muhimu sana, lakini pia zilikuwa rahisi kushughulikia. Lakini ujumbe mmoja ulikuwa wa tofauti.

 

“Ulikuwa ni ujumbe mrefu usio na mpangilio nilioachiwa na mwanamke aitwaye Susan Headly. Alisema kuwa alipiga simu kutokea Leavenworth na kisha akaendelea na hadithi yake hii ndefu kuhusu hadubini aliyoificha katika chumba chake cha faragha kwa miaka mingi. Ujumbe wake uliendelea zaidi na zaidi hadi hatimaye alivuta pumzi kidogo na kisha kusema, ‘tafadhali nipigie.’ ”

 

Kwa bahati mbaya, hapo ndipo ujumbe wa sauti uliishia. Badala ya kumsikia akitaja namba yake ya simu, Jim alisikia mlio wa simu unaokera.

 

“Nipigie,” bila kutaja namba ya simu!

 

 

UTUME WA KISHUJAA

Kumbuka, Jim alikuwa Seattle, Washington, sehemu ya mbali sana kutoka mahali ofisi yake ya nyumbani ilipokuwa. Na hakumfahamu mtu yeyote aitwaye Susan Headly! Hakuwahi hata kusikia habari zake.

 

Rafiki yake aliungana naye katika chakula cha jioni na Jim alimuelezea kuhusu simu iliyohusu hadubini.

 

“Mwanamke huyo alisema kwamba anaishi Leavenworth. Mahali pekee ninapopafahamu huko Leavenworth ni gereza lenye ulinzi wa hali ya juu linalosimamiwa na serikali nchini Kansas. Inawezekana ni mfungwa nchini Kansas!”

 

Wote walicheka; kisha rafiki yake Jim aliinua mkono. “Subiri. Hapa Washington pia kuna Leavenworth! Kwa kweli, ni mojawapo ya maeneo mazuri zaidi ulimwenguni! U.S. Route 2 upande wa pili wa Wenatchee Pass. Kwa kuwa upo Boeing, unaweza kutumia saa mbili tu kufika huko kwa gari. Inakupasa uende huko juu ili kumpata Susan Headley.”

 

Jim alianza kuwaza kuhusu safari ya kwenda uwanjani siku za mapumziko mwishoni mwa juma kuelekea milima ya Washington. “Wana vikapu bora vya maua vinavyoning’inia ulimwenguni,” rafiki yake aliongezea. “Na barabara inayopita huko juu ni nzuri sana . . .”

 

Jim alichagua kufanya safari yake siku ya Jumamosi mchana, lakini hakuwa na wazo lolote kuhusu jinsi atakavyompata Susan, hata kama angekuwa anaishi pale. Aliendesha gari hadi alipoona lori la ofisi za posta lililoegeshwa pembezoni mwa barabara.

 

Najua hii inaweza ikawa ajabu kidogo, lakini Jim aliendesha hadi akalifikia lori la posta, alishuka kwenye gari lake na kuelekea kwa mwanamke msambaza barua.

 

“Samahani naweza kukuuliza swali la kijinga?” Mwanamke yule alimtazama Jim na kutikisa kichwa chake akiashiria kukubali. “Je, unaweza kumfahamu mwanamke aitwaye Susan Headley? Ninadhani labda anaweza kuwa anaishi hapa Leavenworth.”

 

“Hakika namfahamu,” mwanamke alisema. “Ni mtu mzuri sana. Anaishi hapo juu karibu na barabara hiyo. Je, ungependa kupata anwani yake?”

 

 

KUNA MTU ANAYEWEZA KUHITAJI 

Jim aliendesha gari lake kuelekea kule ambako anwani ile ilimwelekeza na akagonga mlango.

 

“Habari. Jina langu ni Jim Lanning. Ulinipigia simu na kunielezea kuhusu hadubini.”

 

Alitambua kwamba Susan amewahi kufanya kazi kama mwangalizi wa mbuga kadhaa za wanyama za taifa la Marekani. Pia aliwahi kuwa kiongozi mkuu (Master Guide) wa watafuta njia na kufanya kazi ya ufarishi. Alimuonyesha Jim dazani mbili za vitambaa alivyokua anavipenda alivyovitengeneza, kisha akampeleka katika chumba ambacho alihifadhi jabali lake la kustaajabisha, vipepeo na aina mbali mbali za ndege. Alimuonyesha vitu vingi sana!

 

“Mama ulinipigia simu na kunieleza kuhusu hadubini,” Jim alimkumbusha.

 

“Ipo hapo mbele yako” alisema huku akiashiria sanduku moja lenye muundo wa kustaajabisha lililokuwa juu ya meza yake ya jikoni.

 

“Niliichukua hadubini hii na kusafiri nayo kwa ndege hadi nyumbani,” Jim alikumbuka. “Kisha nikaiweka katika chumba changu cha juu cha ofisi ya ADRA na kuiweka chini karibu na dawati langu. Nilikaa ofisini pale muda wa kama majuma mawili au matatu na nilikuwa na shughuli nyingi na hata nikasahau kama hadubini iko pale.”

 

Ofisi ya Jim ilikuwa ni chumba cha makumbusho kwa ajili ya vifaa vya matibabu yaliyotolewa na ADRA. “Labda unaweza kuitumia hii mahali fulani ulimwenguni,” mfadhili alisema. Mara kadhaa Jim alikuwa akituma kontena la kusafirishia vifaa na kuvisambaza katika hospitali au zahanati kote ulimwenguni. Safari yake ya kimataifa iliyokuwa inafuata ilipangwa kuelekea America ya kusini, ambapo atatembelea zahanati ya afya iliyopo Peru na Bolivia. Wakati alipokuwa akiondoka, msaidizi wake alimwambia, “Jim, unapaswa kuchukua hadubini hii. Inawezekana kuna mtu anaweza kuihitaji.”

 

“Aliifunga kwenye sanduku na hata kuifunga na kamba nzuri ndogo ya katani. Niliichukua na kusafiri nayo kwa ndege.” 

 

Kituo cha kwanza alipofikia ni katika zahanati ndogo ya Waadventista iliyopo Cochabamba, Bolivia. Zahanati hii haikuwa na njia ya kuwawezesha kufikia umeme wa kawaida, hivyo walikuwa wanatumia betri ya volti 12 ili kuwasha taa katika chumba chao cha upasuaji. Jim aliwaletea jenereta linaloweza kubebeka ambalo litatoa umeme wa kawaida kwenye zahanati ile.

 

“Siku tuliyofika walikuwa wakifanya vipimo kwa mwanamke aliyebainika kuwa na ugonjwa wa kansa. Mwuguzi mmoja aliangua kilio kwa sababu hadubini yao ilikuwa imeharibika na hawakuweza kuona vipimo vile walivyokuwa wamevichukua. Vipimo vile vingewasaidia kuonyesha ikiwa wanaweza kuondoa uvimbe au wanatakiwa kufanya upasuaji mkubwa. Hawakuelewa nini cha kufanya!”

 

Jim alisikiliza, kisha akatimua mbio kuelekea kwenye gari lake, akanyakua sanduku lenye muundo wa kustaajabisha lililofungwa kwa kamba nzuri na kurudi mbio kwenye vyumba vya upasuaji. 

 

“Niliwakabidhi sanduku na kumwambia mwuguzi kulifungua haraka. Alipoona hadubuni, alimwita daktari kwa sauti ya juu na wote wawili walisimama pale, wakiwa wameshindwa kabisa! Hadubuni ya Susan ilikuwa sawa na ile waliyokuwa nayo – ile ile haswa waliyokuwa wanaihitaji!”

 

Jenereta mpya ilifanya taa kuwaka na kifaa kingine ambacho Jim alikuja nacho kilisaidia zahanati ya Cochabamba kuwahudumia mamia ya wagonjwa kwa huduma bora. Kubwa zaidi, hadubini ya Susan “iliyokuja katika wakati sahihi” (hadubini ambayo ilikuwa imeshikiliwa na kamba nzuri ndogo iliyokuwa imening’inizwa ukutani) ilikuwa ikifanya kazi nyingi za kuokoa maisha ya watu kila siku.

 

“Ninavutiwa kuamini katika uongozi wa Mungu,” alisema Jim. “Hasa hasa pale ninapofikiri kuhusu vitu ambavyo anavipatanisha kwa pamoja, kila kimoja kwa wakati sahihi, kwa ajili ya kufika kwangu Cochabamba nikiwa na hadubini. Ndiyo! Mimi ni muumini!”

Dick Duerksen, mchungaji na msimuliaji wa hadithi, anaishi Portland, Oregon, Marekani.

Imba kwa Ajili ya Mtoto Wangu

Ushuhuda usiotazamiwa wa muuguzi mmoja

NA HOMER TRECARTIN

“Whaaaa! Whaaa! Whaaa. . . .”

 

Mtoto wa kiume mwenye umri wa miezi mitatu aliendelea kulia. Mama yake maskini na asiyejua cha kufanya alikuwa amejaribu kila kitu nyumbani. Sasa, alifika katika chumba cha dharura akiomba msaada.

 

Madaktari walifanya vipimo vya aina zote lakini hawakuweza kupata tatizo lolote kwa “Mpiga mayowe” kama kila mtu alivyomwita. Aliendelea kulia siku nzima. Madaktari walifadhaishwa. Wauguzi walifadhaishwa. Wagonjwa hospitalini walifadhaishwa. Lakini hakuna aliyeweza kumfanya aache kulia.

 

Jioni ile, kikundi kipya cha wauguzi kiliingia katika zamu. Hii ilikuwa ni Hospitali ya umma katika nchi ya Mashariki ya Kati. Kwa kuwa hakukuwa na wauguzi wa kutosha, walikuwa wakiajiri watu kutoka mataifa mengine. Mmoja wa wauguzi walioingia katika zamu usiku huo alikuwa ni Mwadventista wa Sabato.

 

Alipoingia tu hospitalini, aliona mara moja kuwa kuna kitu hakikuwa sawa. Kila mtu alikuwa amekasirika na mwenye fadhaa. Kilio chenye kuumiza masikio kilisikika katika ukumbi wote wa hospitali.

 

“Kulikoni?” alimwuliza muuguzi mmoja aliyekuwa akitoka zamu.

 

“Aa! Hakuna tatizo! Isipokuwa wote tumeshaanza kuwa viziwi, wagonjwa hawawezi kulala usingizi, na hakuna anayejua nini cha kufanya kwa sababu hakuna tatizo lolote kwa huyo mtoto. Hawezi tu kuacha kupiga mayowe.”

 

Muuguzi wetu alifanya majukumu yake kimya kimya kisha akaenda katika chumba ambacho mtoto alikuwa akipiga yowe, na mama yake maskini, mwenye hofu alikuwa akikausha mikono na kufuta machozi kwenye macho yake alipokuwa akimtazama mtoto wake pamoja na wafanyakazi waliokasirika. Muuguzi wetu alimbeba mtoto na kujaribu kumbembeleza na kumtikisa. Hakufanikiwa. Aliendelea kulia.

 

Kisha, bila kujua, alianza kuimba wimbo aliokuwa akiwaimbia watoto wake. Hakusema kitu chochote, aliimba tu, lakini moyoni mwake maneno yaliyokuwa yakiimbwa ni: “Yesu ananipenda, hilo najua.” Ghafla, mtoto alinyamaza!

 

Muuguzi akaacha kuimba kwa mshangao, na mara tu aliponyamaza, mtoto alianza kulia tena. Akaanza kuimba mtoto akanyamaza kulia. Kwa hivyo, usiku kucha alimbeba mtoto huku akifanya kazi zake nyingine na kuendelea kuimba kwa upole.

 

Asubuhi iliyofuata, wauguzi wa zamu ya mchana waliporudi kazini, kila mtu alikuwa akinong’ona. Hatimaye, muuguzi mmoja alimfuata muuguzi Mwadventista na kusema: “Ulifanya nini? Huyo mtoto alilia jana mchana kutwa, na wamesema alivyokuwa na wewe alikuwa kimya usiku kucha.

 

Muuguzi wetu hakujua nini cha kusema. Alitabasamu tu na kuinua mabega yake akisema: “Natumaini atanyamaza kwenu leo.” Lakini hakunyamaza. Aliporudi katika zamu usiku huo, Madaktari na wauguzi waliochoshwa walisema amelia mchana kutwa. Muuguzi wetu alimbeba mtoto na kuanza kuimba. Mara moja, mtoto alinyamaza na akanyamaza usiku kucha—maadamu muuguzi aliendelea kumwimbia “Yesu Ananipenda.”

 

Asubuhi iliyofuata, madaktari waliamua kumruhusu mtoto na mama yake warudi nyumbani. Hawakuweza kuona tatizo lolote kwake, na wasingeweza kuwa naye hospitalini akilia wakati wote. Mama mwenye majonzi alimfuata muuguzi wetu kabla hajaondoka kazini na kumsihi, “Nitafanya nini? Mume wangu atakasirika na kunipa talaka nikirudi nyumbani na mtoto huyu anayelia. Lakini nimegundua kuwa unamwimbia naye ananyamaza. Hii hapa simu yangu, unaweza kuimba ule wimbo kwenye simu yangu ili niweze kumchezea nyumbani na huenda ukamnyamazisha?” 

 

Sasa muuguzi wetu aliogopa. Unajua, katika nchi ambayo muuguzi wetu alifanya kazi, ilikuwa ni kinyume cha sheria kumwambia mtu yeyote kuhusu Yesu au kuzungumza juu ya Ukristo. Na baba wa mtoto alikuwa askari polisi! Angefanya nini? Lakini mama huyo aliendelea kumwomba na kumsihi, na hatimaye muuguzi wetu akachukua simu, akaingia katika pembe ya chumba cha kuhifadhia vifaa, na kuimba kwa kwa upole, “Yesu ananipenda, hilo najua, kwa sababu Biblia inaniambia hivyo . . .”

 

Kisha, kwa hofu kubwa, alimrudishia mama huyo simu na kuondoka hospitalini. Badala ya kulala, alikesha usiku kucha akimwomba Mungu. Alikuwa na hakika kwamba wakati wowote polisi wangekuja mlangoni kwake na kumkamata. Huenda wangempeleka gerezani au kufanya jambo baya zaidi ya hilo. Huenda wangemrudisha tu nyumbani. Lakini alikuwa na hakika ya kwamba angeingia katika shida.

 

Jioni ile alichungulia nje ya mlango kuona kama kuna mtu yeyote alikuwa anamsubiri, hakukuwa na mtu, hivyo akatoka nje kwa tahadhari. Alitembea kwenda kazini na kuanza zamu yake. Hakuna kilichozungumzwa kuhusu jambo hilo usiku kucha. Asubuhi iliyofuata hakuna mtu aliyekuwa akimsubiri ili amkamate atakapofika nyumbani. Kwa kweli siku baada ya siku zilipita bila tatizo. Kisha majuma na miezi. Taratibu alisahau kila kitu kuhusu jambo hilo. Kisha siku moja, miaka mitano baadaye mama mwenye watoto wawili alikuja hospitalini.

 

“Oh! Hatimaye nimekuona,” mwanamke alisema kwa mshangao. “Nimetafuta mji wote, lakini ulibadilisha hospitali na sikuweza kukuona hadi leo. Unanikumbuka?”

 

Muuguzi wetu alitabasamu tabasamu lenye mkanganyiko na kusema, Hapana, “Samahani, lakini sikukumbuki.” Mama huyo alitikisa kichwa kuonyesha kuelewa na kusema, “Huyu ni mwanangu wa kiume mdogo. Ana miaka mitano sasa, lakini alikuwa na miezi mitatu nilipomleta hospitalini kwa sababu alikuwa akilia bila kunyamaza.”

 

“Oh, sasa nakumbuka,” alisema muuguzi wetu huku mikono yake ikielekea masikioni kwa mshangao. Kisha, kwa kuona haya kidogo, alimsogelea na kumpapasa kichwani akasema, “Anaonekana kuwa kijana mzuri.”

 

“Ndio,” mama alisema, “ni mzuri sana. Na yote ni kwa sababu ya ule wimbo ulioimba kwenye simu yangu kwa ajili yangu. Lakini sasa nina tatizo. Nilipoteza ile simu. Unaweza kuimba tena kwenye simu yangu ili nimchezee yeye na mdogo wake wa kike?”

 

Wakati huu, muuguzi wetu alitabasamu na kusema kuwa angefurahi kufanya hivyo. Bado alijua kuwa ilikuwa ni kinyume cha sheria, Lakini alichukua simu, akaingia kwenye chumba cha kuhifadhia vifaa, na kuimba “Yesu Ananipenda.” Kisha akaongeza “Yesu Anawapenda Watoto Wadogo.”

 

Inanipa msisimko kufikiria jambo hilo kwa miaka kadhaa sasa, watoto wa askari polisi, wanaokua katika nchi ya Kiislamu, wamekuwa wakisikiliza nyimbo kuhusu Yesu anayewapenda, Biblia ikiwaambia, na Yesu akiwapenda watoto wadogo ulimwenguni kote pasipokujali wao ni akina nani!

 

Muuguzi hakuwa mchungaji wala mwinjilisti. Hakujenga makanisa wala kutoa mafundisho ya Biblia. Kwa unyenyekevu na kwa ujasiri aliruhusu nuru yake iangaze katika hali zote Mungu alizoruhusu apitie. Naamini kutakuwa na watoto, akina mama, na hata askari polisi mbinguni kama matokeo yake.

Homer Trecartin ni mchungaji mstaafu, mwalimu, msimamizi, na mmishonari.

Mchapishaji
Jarida la Adventist World, jarida la kimataifa la Kanisa la Waadventista wa Sabato. Konferensi Kuu, Divisheni ya Asia Pasifiki ya Waadventista wa Sabato ndio wachapishaji.

Mkurugenzi Mtendaji/ Mkurugenzi wa Huduma za Adventist Review
Justin Kim

Meneja wa Uchapishaji wa Kimataifa
Hong, Myung Kwan

Kamati ya Uratibu ya Jarida la Adventist World 
Yo Han Kim (chair), Tae Seung Kim, Hiroshi Yamaji, Myung Kwan Hong, Seong Jun Byun, Dong Jin Lyu

Wakurugenzi wenza/ Wakurugenzi, Huduma za Adventist Review
Sikhululekile Daco, John Peckham, Greg Scott

Wahariri waliopo Silver Springs, Maryland, Marekani
Enno Müller, Beth Thomas, Jonathan Walter 



Wahariri waliopo Seoul Korea


Hong, Myung Kwan; Park, Jae Man; Kim, Hyo-Jun

Mkurugenzi wa Mambo ya Kidijitali
Gabriel Begle

Mkurugenzi wa Muungano wa Mifumo na Uvumbuzi
Daniel Bruneau

Meneja wa Shughuli
Merle Poirier

Mratibu wa Tathmini ya Uhariri
Marvene Thorpe-Baptiste

Wahariri/Washauri wengine
E. Edward Zinke

Meneja wa Fedha
Kimberly Brown

Mratibu wa Usambazaji
Sharon Tennyson

Bodi ya Utawala
Yo Han Kim, chair; Justin Kim, secretary; Hong, Myung Kwan; Karnik Doukmetzian; SeongJun Byun; Hiroshi Yamaji; Tae Seung Kim; Ray Wahlen; Ex-officio: Paul H. Douglas; Erton Köhler; Ted N. C. Wilson

Maelekezo ya Usanifu na Muundo
Types & Symbols

Kamati ya Adventist World ya Divisheni ya Afrika Mashariki – Kati:
Blasious Ruguri, Musa Gideon Mitekaro, Tom Ogal, Emanuel Pelote, Yohannes Olana

Tafsiri
Ufunuo Publishing House, Southern Tanzania Union Mission.

Msomaji wa prufu
Lilian Mweresa

Usanifu wa toleo la Kiswahili
Daniella Ingram, Ashleigh Morton, Digital Publications

Uchapishaji wa Kidijitali
Charles Burman, Digital Publications (www.digitalpublications.co.za)

Muelekeo wa Sanaa na Ubunifu
Mark Cook, Brett Meliti, Ivan Ruiz-Knott
/Types & Symbols

Kwa Waandishi: Tunakaribisha miswada huria. Tuma barua zote kwa uhariri kwa 12501 Old Columbia Pike, Silver Spring, MD 20904-6600, U.S.A. Faksi ya ofisi ya Uhariri ni: (301) 680-6638

Waraka pepe: worldeditor@gc.adventist.org Tovuti: www.adventistworld.org

Rejea zote za Biblia zimechukuliwa kutoka kwenye Swahili Union Version Bible Toleo la Chama cha Biblia la mwaka 1952.

Jarida la Adventist World linachapishwa kila mwezi na kuchapwa kwa wakati huo huo huko Korea, Brazili, Indonesia, Australia, Ujerumani, Austria, Ajentina, Meksiko, Afrika Kusini, na Marekani.

Vol. 21, Na. 5

swipe down
powered by
SEND-IT.ME

Swipe left

swipe left To move to the next page

Swipe right

swipe right To move to the previous page
Please wait ...