powered by
send-it.me

Adventist World-Kiswahili inamshukuru kila aliyejiandikisha kwa ajili ya jarida hilo, kupitia kwa jukwaa letu la awali, yaani chaneli ya WhatsApp. Tumefurahia kupokea jumbe kutoka kwako, na vilevile shuhuda za jinsi umetumia jarida hili linalotia moyo kuwafikia wengine kwa ajili ya Kristo!

Tungependa ujue kuwa tulihamia jukwaa jipya tangu Februari 2024. Zaidi ya yote, tungependa uhame pamoja nasi. Adventist World-Kiswahili haitaki kumwacha nyuma yeyote aliyejiandikisha.

 

Badala ya kupokea ujumbe wa WhatsApp pamoja na toleo jipya kila mwezi, sasa tunakupa kiungo kwa tovuti ya bure ambayo ni nzuri kwa simu, ambapo unaweza kuyasoma makala yote, kama kawaida. 

Pia tutakiweka kiungo hicho kwenye ukurasa wa Facebook wa Adventist World-Kiswahili kila mwezi, ambapo unaweza kututumia jumbe na taarifa kuhusu jinsi makala hii inakufaidi wewe na jamii yako. Unaweza kututumia maoni na mapendekezo jinsi ya kuifanya makala hii iwafae zaidi wasomaji!

Ukipenda, unaweza kutuma baruapepe: 
kwambokaj@ecd.adventist.org ukiwa na maswali yoyote.

 

Moja ya manufaa ya tovuti mpya ya Adventist World-Kiswahili ambayo ni nzuri kwa simu, ni

kwamba kutakuwa na lugha zingine nyingi za kuchagua, ikiwa ungependelea Kiingereza au lugha nyingine yoyote, unaweza kuangalia kama ipo, kando na ile ya kawaida ya Kiswahili.

 

Manufaa mengine ni kwamba ni rahisi kushiriki kiungo hicho kipya cha Adventist World-Kiswahili, kwa marafiki na familia. Tunakuhimiza ufanye hivyo. Hebu kiangalie sasa hivi.

 

Tunatumai kuwa na uhusiano mrefu na wa furaha na wasomaji wetu wa Adventist World-Kiswahili.

 

Mungu akubariki,

 

Timu ya Adventist World-Kiswahili

Tunaamini katika nguvu ya maombi, na tunakaribisha hitaji la maombi ambayo tutashiriki katika ibada ya watendakazi kila Jumatano asubuhi. Tuma maombi yako kwa kwambokaj@ecd.adventist.org, na utuombee tunapofanya kazi pamoja kuendeleza ufalme wa Mungu.

 

Picha ya jalada: sezer66 / iStock / Getty Images Plus  / Getty Images 

Katika Fan the Flames, Stowell J. Moody anaelezea shindano la mbio katika michezo ya Olimpiki ya Ugiriki ya kale. Washindani wengine walishindana ili kumaliza kwanza; katika hili, mshindi aliupita mstari wa kumaliza na tochi yake ikiwa bado inawaka. Lilikuwa shindano la mbio za ujuzi: kosa moja lingeweza kuuzima moto. Uzingatifu makini kwa mwale ulisababisha ushindi.

 

Badili mwelekeo kwa hadithi nyingine ya Olimpiki. Akizaliwa mwaka 1891, Shizo Kanakuri alikuwa mwanariadha wa kwanza wa Kijapani kufuzu kwa ajili ya michezo ya Olimpiki. Pamoja na Mishima Yahiko, wawili hao waliiwakilisha Japani katika michezo ya mwaka 1912, huko Stockholm. Cha kushangaza, Kanakuri hakuwa akijulikana kwa kuvunja rekodi ya marathoni ya muda mfupi, bali mrefu.

 

Baada ya safari ya siku 18 kutoka Japani kwenda Swedeni kwa meli na treni, alikuwa amechoka sana. Kanakuri hakuweza kulala vizuri kutokana na usiku wa majira ya joto ya Stockholm, ambapo jua halikuweza kuchwa kabisa.

 

Hakuweza kula chakula cha Kiswidi. Kocha wake alipatwa na kifua kikuu na hakuweza kufanya mazoezi. Hatimaye, Stockholm ilikabiliana na joto, ikisababisha kifo cha mshindani, cha kwanza katika mashindano ya Olimpiki.

 

Kanakuri alishindana hata hivyo, akapata homa kali, na kupoteza fahamu. Akijawa na aibu na akipungukiwa na madini yanayobeba umeme mwilini, aliondoka kimya-kimya katikati ya mbio na kurudi Japani bila kuwajulisha maofisa.

 

Uswidi ilimdhania kupotea kwa miaka 50 kabla mwandishi wa habari kumgundua akifanya kazi kama mwalimu wa jiografia Japani. Mwaka 1967, Waswidi walimpatia Kanakuri nafasi ya kumaliza marathoni yake huko Stockholm. Alikimbia, na kumaliza marathoni kwa miaka 54, miezi 8, siku 6, saa 5, dakika 32, na sekunde 20.3. Alihitimisha, “Ilikuwa ni safari ndefu. Njiani, nilioa, nikapata watoto sita na wajukuu 10.”

 

Kuna mbio ambazo lazima tuzimalize kwanza. Kuna zingine ambazo lazima tuzimalize mwisho. Na kuna mbio zingine ambazo lazima, tu, tuzimalize. Safari zetu za kiroho ni hizo: safari zinazotutaka kuwa makini na mwale hadi mwisho wenye ushindi. Tunaishi maisha yetu tukiwa na vikwazo, bila kusudi, bila nia na kisha tunajiuliza maana ya yote haya.

 

Watu wa Mungu, watu Wake wa siku za mwisho, wameitwa kuishi kwa uaminifu. Kudumisha taa ya ukweli na kuendeleza mwale ambao vizazi vimekuwa vikiuhifadhi, vuguvugu la Marejeo limeitwa kuwa aminifu hata mwisho kabisa. Hii inamaanisha aidha hadi mwisho wa historia ya dunia, au hadi mwisho wa maisha ya mtu, hata kama inamaana ya kukimbia zaidi ya miaka 54.

 

Hatuitwi kuwa na shughuli nyingi, kuwa wa kwanza, wala kuwa washindi, bali tu kuwa waaminifu. Iwe tumeanza tu, au tunaona mstari wa kumaliza mbele yetu, tumeitwa kuwa waaminifu kwa kujitoa, kutii kwa uaminifu, kuwa na tumaini kwa uaminifu, kuwa waaminifu kwa uaminifu, kwa uangalifu makini kwa mwale–haidhuru itachukua muda gani.

Almir Marroni, mkurugenzi wa Huduma za Uchapishaji kwenye Konferensi Kuu, akizungumza na zaidi ya viongozi wa uchapishaji 50 katika Warsha ya hivi karibuni ya Uchapishaji ya Divisheni tatu za Ulaya katika Chuo kikuu cha Waadventista cha Ufaransa. Warsha ilikuwa na lengo la “kuongeza ushiriki miongoni mwa taasisi za uchapishaji na waratibu wa huduma ya vitabu Ulaya yote, yakiwemo maeneo ya Ulaya-Asia.”

“Huu ni uamuzi wa kwanza na Mahakama ya Katiba au Mahakama Kuu kutambua wazi ombi la Mwadventista wa Sabato la kubadilisha ratiba ya mtihani. Inafafanua wajibu wa mamlaka za utawala wa kuzuia Waadventista wa Sabato na makundi mengine madogo kukabiliana na ubaguzi usiofaa kwa sababu ya imani zao za kidini.”

—Msemaji wa Mahakama Kuu ya Korea Kusini kuhusu uamuzi wa kihistoria ambao uliamua kwa faida ya wanafunzi wanaoomba kubadilisha ratiba ya usaili wa chuo kikuu kulingana na imani za kidini. Uamuzi huu wa kihistoria ulikubali ombi la Mwadventista wa Sabato la kubadilisha ratiba ya mtihani kwa mara ya kwanza.

Zaidi ya 4,000

Idadi ya watu waliobatizwa huko Haiti tangu mwanzo wa mwaka. Licha ya ongezeko la vurugu za genge katika miezi iliyopita, ambalo limeathiri sana utendaji wa kawaida wa kanisa, juhudi za injili za hivi karibuni zimesababisha maelfu ya ubatizo. Kutokana na ghasia, angalau makanisa 55 yamefungwa, na shule nyingi na taasisi hazifanyi kazi kikamilifu. Baadhi ya maeneo kisiwani yana nafuu kuliko mengine. Makanisa 172 na makundi 186 katika sehemu ya kaskazini ya taifa la kisiwa hicho wanaweza kukutana mara kwa mara. Katikati ya vurugu na changamoto, Mungu anaendelea kuwaangalia watu Wake.

“Utume ni kiini cha divisheni yetu, na kila kitu kinahitaji kuzingatia utume. Jukumu letu ni kuhakikisha kila mshiriki anakuwa mwanafunzi hai akifanya kitu kwa ajili ya Mungu. Tunabarikiwa kuwa hapa.”

—Gideon Reyneke, katibu wa Divisheni ya Kusini mwa Afrika-India (SID), akitafakari juu ya safari ya siku mbili kwenda katika Union ya Atlantic Caribbean. Viongozi kutoka Divisheni ya Amerika-Kati na SID walikutana huko Nassau, Bahamas, kujifunza juu ya mipango ya injili na mikakati ya utume. Aidha, walijifunza juu ya historia ya eneo la union na mipango ya ukuaji wa kanisa.

“Kutoa huduma kunafanywa kuwa rahisi katika Chuo Kikuu cha Waadventista cha Southern, na VITA (Volunteer Income Tax Assistance) ni njia moja inayosaidia wanafunzi kuona jinsi kusaidia wengine kama mikono na miguu ya Yesu kunavyoweza kwenda zaidi ya chuo kikuu na baada ya kuhitimu.”

—Colin Gleen, mwanafunzi wa usimamizi wa fedha katika Chuo Kikuu cha Waadventista cha Southern (SAU), kuhusu programu ya VITA ya chuo kikuu hicho. Mwezi Aprili mwaka huu umeadhimisha mwaka wa 11 ambapo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waadventista cha Southern wana nafasi ya kujitolea kukamilisha marejesho ya kodi kwa wanachama wa jamii wenye mapato ya chini na wazee huko Collegedale, Tennessee, Marekani, na mbali zaidi.

Zaidi
ya 70

Idadi ya maafisa wa misheni na konferensi, makatibu wa fildi na wakurugenzi wa Chama cha Huduma kutoka kote katika Union ya Indonesia Mashariki walioshiriki katika Mafunzo ya Kwanza ya Tathmini ya Tumaini la Maisha na Mafunzo ya Mdai wa Maisha. Tukio hilo lilifanyika Aprili 3-6 huko Tahuna, kwenye Sanighe, Kaskazini mwa Sulawesi, Indonesia. Lengo la mafunzo katika mafunzo ya Indonesia Mashariki lilikuwa kuwajengea wachungaji na viongozi wa kichungaji nyenzo na mikakati inayohitajika kujenga uhusiano wa kina ndani ya jamii zao na kuendeleza mbele utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato.

“Tangu kuwekwa kwa vyoo hivi, maisha yetu yamebadilika. Hatulazimiki tena kustahamili hali duni za vyoo vya zamani au kutegemea kutembelea fukwe kwa ajili ya mahitaji ya usafi. Kuingilia kati kwa ADRA kweli kumebadilisha kabisa maisha ya vijijini.”

—Patrina Lonipitu, mwalimu katika Shule ya Msingi ya United Church Kusini Mashariki mwa Vela, Visiwa vya Solomon, kuhusu mradi wa SaTo. Mradi huu wa Shirika la Maendeleo na Misaada la Waadventista (ADRA) unafunga vyoo vya shimo kwenye mazingira ya wazi na kupunguza maambukizi ya magonjwa na wadudu wanaoruka na kupunguza hali duni za usafi zinazohusiana na vifaa vya hewa-wazi.

Zaidi ya 2,500

Idadi ya watu waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa kliniki kubwa ya afya huko Mount Hagen, Papua New Guinea. Miongoni mwa wageni waliokuwepo ni gavana wa Eneo la Magharibi mwa Highlands, Wai Rapa. Kliniki ya afya ilifanyika kuanzia Aprili 16-19 na ilikuwa juhudi ya pamoja ya Kampeni ya Vidole vya Miguu 10,000 ya Kanisa la Waadventista wa Sabato na Redio ya Waadventista Ulimwenguni. Huduma zilizotolewa zilijumuisha uchunguzi wa kisukari na matibabu mengine na uchunguzi wa meno. Kliniki hiyo iliongozwa na zaidi ya watu 420 waliojitolea, ambao walikuwa ni madaktari, wauguzi, na wafanyakazi mahalia wa afya.

Uimarikaji wa hali ya kifedha uliopo wa Konferensi Kuu ya Waadventista wa Sabato ni matokeo ya baraka za Mungu na juhudi za viongozi kudhibiti matumizi huku wakiongeza fedha kwa ajili ya mipango ya utume duniani kote, mhazini wa Konferensi Kuu (GC) Paul H. Douglas alisema katika taarifa yake ya Kikao cha Mwezi Aprili tarehe 9. GC ilimaliza mwaka wa fedha ikiwa na takribani dola za Marekani milioni 310 katika jumla kuu. “Hii siyo kazi yetu–ni kwa uwezo wa Mungu na Mungu pekee,” Douglas alisema.

 

Mwaka 2023, GC ilipokea takribani dola milioni 91 kama zaka, dola milioni 13 zaidi ya bajeti ya dola milioni 78, na dola milioni 97 kama matoleo, zaidi ya dola milioni 74 iliyopangwa kutolewa. Ni asilimia 48 pekee ya fedha ya GC ilitoka katika zaka, na hivyo kuingilia mwenendo wa miaka iliyopita.

 

Matumizi ya Programu za GC mwaka 2023 yalifikia dola milioni 172, asilimia 43 ikiwa katika kuwezesha utume, asilimia 15 katika mafunzo kwa uongozi, na asilimia 13 katika vyombo vya habari na uenezi. Asilimia nyingine 9 ilitumika katika taasisi za elimu, na asilimia 20 kwa vitu vingine. Licha ya shinikizo la mfumuko wa bei, Douglas alisema, GC “iliweza kudumisha gharama zake za matumizi mwaka kwa mwaka, ambao ni ushuhuda wa umakini wetu wa matumizi.”

 

Takwimu za mtaji wa kazi na mali rahisi kubadilishika kwa pesa taslimu pia zilikuwa na manufaa, Douglas aliripoti. Sera ya kanisa inapendekeza angalau miezi sita ya mtaji wa kazi na miezi mitatu ya mali rahisi kubadilishika kwa pesa taslimu. Mwishoni mwa mwaka 2023, GC ilikuwa na miezi 13.9 ya mtaji unaopatikana wa kazi na miezi 11.1 katika mali rahisi kubadilishika kwa pesa taslimu.

 

 

MIFUKO YA MATUKIO MAWILI YA UTUME

Mwaka 2021, GC ilianzisha Mfuko wa kwanza kabisa wa Matukio ya Utume ambao hutoa rasilimali ili kusaidia miradi ya utume inayozalishwa na makanisa mahalia. Kusudi ni kuwekeza katika mstari wa mbele wa utume wa makanisa mahalia na kuubadilisha ulimwengu kwa ajili ya Kristo, jamii moja kwa wakati, Douglas alisema. Aliripoti kuwa mwaka 2025, dola za Marekani milioni 5 zipo kwa ajili ya kugawiwa mfuko huo.

 

Mfuko wa pili wa Matukio ya Utume, ulioanzishwa hivi karibuni, utatoa rasilimali za kifedha kwa divisheni ulimwenguni na filidi zilizoambatanishwa za Kanisa la Waadventista ambalo linatekeleza mpango wa uinjilisti wa eneo lote katika mwaka 2024, 2025, 2026, au 2027. Lengo litakuwa katika maeneo ambayo “yanawasilisha mpango wa kina unaohusisha union zao, konferensi mahalia, na makanisa mahalia,” Douglas alieleza.

 

Uwekezaji kwa kila chombo cha kanisa huangazia nia ya GC ya kuwaunga mkono viongozi na washiriki wa kanisa katika mpango wa uinjilisti wa eneo lote, kuwekeza rasilimali za kifedha na teknolojia, na “kuleta katika ufalme wa Mungu mavuno mengi ya roho ambazo nazo zitageuka na kuwa wanafunzi hai wa Yesu Kristo,” aliongeza. “Tumejitoa kutoka Konferensi Kuu kusaidia kila divisheni na kila chombo kilichoambatanishwa [kushughulikia] hadi asilimia 20 ya jumla ya gharama ya programu hadi dola 500,000 kwa kila chombo.”

 

Baadhi ya divisheni tayari zimeanza kufanya mipango ya kina ya uinjilisti. Divisheni ya Afrika Mashariki-Kati ina Msukumo wa Uinjilisti wa mwaka 2025, ambao utawezesha mikutano ya uinjilisti katika maeneo 33,000 katika eneo lake. Katika Divisheni ya Amerika Kaskazini, mpango wa Pentekoste 2025 unatafuta kutekeleza “Mipango Elfu Tatu ya Uenezaji” kwa mwaka 2025, Douglas aliripoti.

 

Hatua za hivi karibuni ni sehemu ya mabadiliko ya dhana ambayo yanalenga kusisitiza juhudi za pamoja za kuzingatia tena utume, Douglas alisema. “Tunahitaji kuwa na nia zaidi na mipango.”

 

“Tunafurahia matunda ya [Mfuko wa Matukio ya Utume], ambao unahusika na shughuli za uinjilisti katika eneo lote,” Robert Osei-Bonsu, mwenyekiti wa Divisheni ya Afrika Magharibi-Kati, alisema wakati wa maoni kuhusu taarifa ya mhazini. “Tunaamini hii ni yenye kusifika na imetutia moyo kwenda katika uinjilisti.”

Kanisa la Waadventista wa Sabato nchini Romania hivi karibuni lilitoa filamu ya Cine Sunt Adventistii? (Who Are the Adventists?), filamu juu ya Waadventista wa nchini Romania. Filamu hiyo ya dakika 93 inaliweka Kanisa la Waadventista ndani ya historia ya Ukristo na inaangazia michango mikuu ambayo Waadventista wamefanya kwa nchi ya Romania, zikiwemo nyanja za afya na elimu na msaada wa kijamii.

 

Ulimwenguni kote, Waadventista wanawakilisha chini ya asilimia 1 ya idadi ya Wakristo na ni sehemu ya kundi la Waprotestanti (asilimia 36), pamoja na Wakristo wa imani ya Orthodox (asilimia 12) na Wakatoliki (asilimia 50). Duniani kote, idadi ya Waadventista ni takribani washiriki milioni 22.

 

“Tangu walipojitokeza nchini Romania, Waadventista wamechochea ubishani,” waandaaji walisema. “Watu wa Romania ambao wamesikia habari zao wanawaona kuwa hatari au wanaojiona kuwa bora kuliko Wakristo wengine. Tulitaka kujibu swali, ‘Ukweli ni upi?’”

 

Miongoni mwa mada ambazo filamu hiyo inazungumzia ni maswali ya kama Waadventista ni Wakristo kweli, kwa nini wana shabihiana sana na Waislamu na Wayahudi, na jinsi wanavyofasiri unabii wa nyakati za mwisho.

 

Who Are the Adventists? inajumuisha mahojiano si na watu wa Romania mitaani tu lakini pia na watu binafsi kama vile katibu wa serikali wa masuala ya kidini, Ciprian Olinici; mwenyekiti wa Chuo cha Romania, Ioan-Aurel Pop; rais wa zamani wa Romania, Emil Constantinescu; wawakilishi wa taasisi mbalimbali za kidini, ikiwa ni pamoja na Ionuț Corduneanu wa Kanisa la Orthodox, Virgil Achihai wa Ushirika wa Kiprotestanti, na Murat Iusuf, mufti wa Kiislamu kutoka nchini Romania, pamoja na mwanahistoria Adrian Cioroianu; mtu mwenye ushawishi George Buhnici; na mwanasosholojia Dumitru Bortun.

 

Picha katika filamu hii ni kutoka katika zaidi ya maeneo 30 ya ibada ya Waadventista yaliyochaguliwa kutoka katika kanda zote nchini. Msimuliaji ni Ioan Paicu, mhariri wa Radio ya Vocea Speranței na mzee wa kanisa. Sauti ya wimbo inajumuisha utohoaji uliofanywa kwa nyimbo 26 kutoka kwenye kitabu cha nyimbo za kanisa.

 

Maeneo muhimu ambayo hali ya kiroho ya Waadventista inawekwa wazi, yaliyopo kama vipande muhimu katika video, ni michango katika afya, utoaji wa misaada, shughuli za uinjilisti, na elimu ya Waadventista.

 

Miongoni mwa waumini zaidi ya elfu moja wanaoonekana kwenye filamu ni familia mbili zenye mfululizo wa vizazi vinne hadi sita vya Waadventista, vinavyoakisi mabadiliko ya kijamii ya dhehebu hilo katika ardhi ya Romania.

 

Who Are the Adventists? pia inaonyesha mafundisho muhimu zaidi mawili kutoka katika mtazamo wa toba: kwa nini Waadventista wanaadhimisha Jumamosi kama siku ya saba na kile ambacho Waadventista wanaamini juu ya ujio ulio karibu sana wa Yesu Kristo katika dunia hii. Uelewa wa Waadventista wa wakati ujao unaonyeshwa kwa kuangazia kazi iliyofanywa na Waprotestanti katika Mapinduzi ya Romania (Timişoara) ya Desemba 1989, sambamba na jinsi dini inavyoathiri dhahiri migogoro ya kisiasa na kijamii.

 

“Filamu hiyo inajibu swali la kama Waadventista ni Wakristo kweli na kwa nini, kati ya Wakristo wote, Waadventista wanashiriki vitu vinavyofanana zaidi na Waislamu pamoja na Wayahudi, jambo linalosisitiza tena kazi ambayo wanaamini Waadventista watafanya katika siku zijazo, katika matukio ya mwisho kabla ya Kristo kurudi duniani,” watayarishaji waliandika kwenye ukurasa wa YouTube wa filamu hiyo.

 

Who Are the Adventists? ni zao la Union Konferensi ya Romania ya Kanisa la Waadventista wa Sabato

Mpango wa uinjilisti wa Impact 24 huko St. Croix, Visiwa vya Virgin vya Marekani, ulizinduliwa rasmi kote kisiwani mwezi Machi tarehe 30. Katika Kanisa Kuu la Waadventista wa Sabato upande wa magharibi wa kisiwa hicho, washiriki wa kanisa hilo na idadi kubwa ya wageni walihudhuria mkutano wa kwanza wa mfululizo wa “Your Journey to Joy” (Safari Yako kwenda katika Furaha), ambao uliendelea hadi tarehe 23 mwezi Aprili na ulijumuisha mikutano ya ana kwa ana wakati wa jioni mara sita kwa juma, kliniki ya afya, na mpango wa kuifikia jamii.

 

Mfululizo huo ulikuwa matokeo ya jitihada za pamoja za Idara ya Fedha ya Konferensi Kuu ya Kanisa la Waadventista, Divisheni ya Amerika ya Kati, Union Konferensi ya Caribbean, na Union Konferensi ya Caribbean Kaskazini, pamoja na msaada kutoka katika Chuo Kikuu cha Afya cha Loma Linda, Hope Channel International, na Adventist Review.

 

“Jumbe tutakazosikia zitakuwa zenye kutia moyo, zikituunganisha wote katika safari ya kuelekea katika jambo kubwa,” mtangazaji wa mkutano huo aliwaambia mamia ya watu kanisani. “Katika majuma haya mawili, mnayo nafasi ya kusitisha ratiba yenu yenye shughuli nyingi, kutulia, na hata kugundua njia za furaha, utimizaji, na furaha. Nani hataki jambo hilo?” Aliuliza. “Tunaomba kwamba unapomaliza safari hii, upate furaha katika Bwana.”

 

 

ENEO LA UTUME

Idara ya Fedha ya GC (Konferensi Kuu) katika makao makuu ya Kanisa la Waadventista huko Silver Spring, Maryland, ilielekeza mawazo yake katika eneo hili la Marekani kama mpango wao maalum wa utume kwa mwaka 2024 kwa sababu St. Croix imekabiliwa na changamoto kubwa katika miaka ya hivi karibuni. Kimbunga Maria kiliharibu kisiwa hicho mwaka 2017. Baada ya janga hilo, wakazi wengi, ikiwa ni pamoja na baadhi ya washiriki wa kanisa la Waadventista, waliondoka kisiwani hapo na kwenda kuishi na kufanya kazi katika ardhi ya Marekani. Ndipo janga la UVIKO-19 lilipiga, ambalo lililazimisha wengi kujiweka mbali na kanisa na wengine hatimaye kuishi mahali pengine.

 

Licha ya mafundisho yake yenye nguvu ya Kikristo, St. Croix ni jamii ya magharibi inayozidi kuongezeka, na Waadventista wanapata ugumu kushiriki ukweli wa Biblia na kuwashirikisha watu katika mafundisho ya Biblia na kujitoa kiroho kuliko hapo awali, viongozi mahalia walieleza.

 

Na licha ya kuwa na washiriki zaidi ya 4,700 Waadventista kwenye vitabu vya kanisa, asilimia kubwa hawajulikani waliko, iwe kwa sababu walihama au waliacha kuhudhuria. Kuna mambo mengi ya kufanya kwenye kisiwa ili kubadilisha jambo hili, viongozi wa fedha walisema.

 

 

KUIFIKIA JAMII

Tarehe 10 mwezi Aprili, timu ya watu 20 kutoka Chuo Kikuu cha Afya cha Loma Linda walisafiri hadi St. Croix kutoa kliniki ya afya bila malipo katika bwalo lililoko kando ya Kanisa Kuu la Waadventista wa Sabato. Timu hiyo ilitoa huduma ya kusafisha meno, kuziba na kung’oa, huduma ya kwanza, shinikizo la damu na upimaji wa sukari, vifaa vya kuweka miwani ya kusomea, na ushauri wa afya ya akili na familia. Watu walipokuwa wakisubiri huduma, wangeweza kuchagua kati ya matibabu kadhaa yasiyohitaji dawa, ikiwa ni pamoja na kusingwa kwenye kiti, kusingwa mabegani, kurekebishwa macho, na usoni.

 

Idara ya Fedha ya GC ilisema pia wanataka mradi ambao ungekuwa wa kuonyesha msaada kwa jamii inayozunguka kanisa. Walipata walichokuwa wakitafuta kwenye viwanja vya kanisa, ambapo uwanja wa mpira wa kikapu ulikuwa umeharibika baada ya kimbunga. Fedha kutoka kwa wafadhili na wengine zikiwa zimewekwa kando, viongozi wa kanisa waliweza kukarabati na kurejesha mahali pa kuchezea, kwa matumaini kwamba ingewavutia washiriki wa kanisa vijana na rafiki zao katika jamii kwa ajili ya mchezo wa kirafiki unaojenga uhusiano wenye maana. “Tungependa uwanja huu wa mpira wa kikapu hatimaye uwe kituo cha mvuto katika jamii,” viongozi mahalia walisema.

Kundi la wamishonari 55 lilikusanyika mjini Tokyo, Japani, mwezi Machi kwa shughuli ya juma moja ya kufikia mamia ya maelfu kupitia vijizuu vilivyojikita katika Biblia. Kundi la washiriki wa kanisa lilitoka nchi kadhaa zikiwemo Australia, Canada, Marekani, na baadhi ya nchi za Amerika Kusini. Safari hiyo iliandaliwa kwa kushirikiana na Union Konferensi ya Japani (JUC) ya Kanisa la Waadventista wa Sabato.

 

Kundi hilo lilisambaza vijizuu karibu 750,000, vilivyojulikana kama GLOW (Giving Light to Our World/Kutoa Nuru kwa Ulimwengu Wetu). Vijizuu hivyo, vilivyochapishwa katika lugha ya Kijapanii, viliandikwa na kutayarishwa na idara ya Uchapaji ya Konferensi Kuu na vilihusisha mada kama vile wokovu, afya, uumbaji, na kutambua thamani ya maisha—mada ambazo JUC ilitambua kuwa za muhimu kwa wakazi wa Tokyo.

 

Kila siku, wamisionari walikuwa na lengo binafsi la kugawa vijizuu 3,000. Kwa sehemu kubwa, vijizuu hivyo viliwekwa katika nyumba za watu kupitia masanduku yao ya posta.

 

“Wengi wetu tulizoea kutembea kwa wastani wa hatua elfu ishirini hadi thelathini kwa siku, lakini Jumanne moja yenye mvua ilileta changamoto kubwa,” mwanakikundi wa kujitolea Catherine Ge alisema. “Soksi zilizolowa, vijizuu vya GLOW vilivyolowa, na hali ya hewa ya baridi viliwavunja moyo wamishonari wengi, hata mimi pia.”

 

Safari ya utume ya Japani ilikuwa ni mwendelezo wa juhudi za kila mwaka za kimataifa ambazo kihistoria zimekuwa zikiongozwa na Konferensi ya Kati ya California nchini Marekani, ambako huduma ya vijizuu vya GLOW ilianzia. Ilikuwa ni jitihada ya kufikia watu katika eneo kubwa la ulimwengu na ambalo halijafikiwa na kazi hiyo tayari imetoa matokeo ya kutia moyo.

 

“Union Konferensi ya Japani inashukuru sana timu ya utume ya GLOW kwa huduma yao iliyotukuka mjini Tokyo,” Yasunari Urashima, mkurugenzi wa vijana wa Idara za Uchapishaji na Mawasiliano alisema. “Kutokana na huduma yao, ‘VOP Online,’ ambayo ni tovuti ambapo Kituo cha Uinjilisti cha Kidijitali cha JUC kinatoa mafundisho ya Biblia mtandaoni, ilikuwa na watembeleaji mara nne hadi tano zaidi ya kawaida wakati wa usambazaji. Pia, kulikuwa na watu waliojiandikisha mara nne hadi tano zaidi kwa ajili ya kujifunza Biblia mtandaoni.”

 

Takwimu hazikuwa matunda pekee ya ufikiaji.

 

Kwa mfano, wanakikundi wa kujitolea waligundua kwamba maafisa usalama katika baadhi ya majengo waliacha kuzuia usambazaji wa vijizuu katika vyumba vya ghorofa na kuwa wamishonari wenyewe na kusaidia kuvigawa. Baadhi ya wakazi walichukua vijizuu vya ziada ili kuvigawa kwa marafiki, pamoja na mchungaji wa kanisa mahalia ambaye alisema alitaka vijizuu awapatie waumini wake. Wengine waliguswa sana kwa kupokea vijitabu hivyo vya kiroho hata kusababisha kuangua kilio.

 

Safari ya utume ilipoisha, walioshiriki walionyesha shukrani zao kwa ukuaji wa kiroho walioupitia.

 

“Nilichopata kutoka katika safari hii ya GLOW kilikuwa tofauti na safari yoyote ya mikutano au utume ambayo nimefanya hadi sasa. Nilihisi kama sisi sote ni familia, kana kwamba nilipata uzoefu wa jinsi mbingu itakavyokuwa pamoja na ndugu na dada zangu katika Kristo,” Erica Mendez alisema.

 

“Ninapotafakari tukio hilo, ninagundua kwamba Mungu ameniongoza mara kwa mara kupitia taabu ndogo ambazo ni sehemu ya kazi Yake ili kuimarisha imani yangu na kumtumaini Yeye,” Ge alisema.

 

Urashima alieleza kuwa mipango zaidi ya usambazaji wa vijizuu nchini Japani ni pamoja na Mkutano wa Huduma ya Wanawake huko Kyoto mwezi Aprili na mkutano wa uinjilisti mtandaoni utakaosimamiwa na Kituo cha Uinjilisti cha Kidijitali cha JUC mwezi Juni.

 

Safari nyingi za utume kwa njia ya vitabu na wamishonari kutoka kote ulimwenguni zitaendelea kutokea, waandaaji walisema. Safari ya usambazaji wa vijizuu milioni moja imeratibiwa Paris wakati wa Michezo ya Olimpiki katika majira ya joto ya mwaka 2024, na Redio ya Waadventista Ulimwenguni na idara ya Huduma za Uchapishaji ya Konferensi Kuu inaandaa mipango ya kupanua fursa hizi ili kufikia mamilioni kupitia vitabu.

MAISHA YA AWALI

Mama yake Mark Finley alikuwa Mkatoliki na baba yake alikuwa Mprotestanti. Baada ya kukutana kwa kudra za Mungu na Mwaadventista mlei, baba yake akawa Mwadventista wa Sabato. Mark hakufikiria sana juu ya hilo wakati huo. Baba yake alishiriki pamoja naye baadhi ya imani zake, lakini aliheshimu ahadi aliyomwahidi padri alipomwoa mama yake Mark kwamba angewalea watoto wake katika dini ya Katoliki.

 

Mark alipokuwa na miaka 17 na akijiandaa kwenda mwaka wake wa mwisho wa shule ya sekondari, baba yake alimwambia, “Nimekulea wewe kama Mkatoliki kama nilivyomwahidi padri. Lakini sasa umekua, na unakwenda chuoni. Ninataka kushiriki nawe mambo fulani.”

 

Mark alifanya kazi na baba yake katika duka lao la mashine, na kila asubuhi baba yake alikuwa akimshirikisha mafundisho ya Biblia wakiwa njiani kwenda kazini. Hilo lilimfanya Mark kusoma Biblia kwa ajili yake mwenyewe.

 

Alibatizwa Machi 1963, na kujiunga na programu ya teolojia katika chuo cha zamani cha Atlantic Union College (AUC) huko South Lancaster, Massachusetts. Shule hiyo ilifungwa mwaka 2018.

 

Hapo ndipo alipokutana na Ernestine (Teenie) Tenney na kufunga naye ndoa. Baada ya kuhitimu, Mark alifanya kazi kwa miaka miwili huko Hartford, Connecticut, wakati Teenie akifundisha katika shule ya kanisa iliyokuwa karibu.

 

Mchungaji Mark anasema alihisi ni bora kutokwenda moja kwa moja kwenye seminari. “Nilihitaji muda wa kuwa na huduma yangu yenye uzoefu. Nilihitaji muda wa kweli kusimama mwenyewe, kwa hivyo nilifanya kazi kwa miaka kadhaa katika Taasisi ya Kimishonari ya Tiba ya Wildwood na Mzee W.D. Frazee. Alikuwa mlezi wangu. Nilijifunza kufanya mwito wa madhabahuni kutoka kwake, nilijifunza kuhubiri mahubiri ya kibiblia kutoka kwake, nilijifunza kuona Roho wa Mungu akigusa kwa nguvu.”

 

Kutokea hapo, wenzi hawa walihamia kwenye Konferensi ya Kusini mwa New England, ambapo Mchungaji Mark mara moja alihisi kwamba kanisa lilikuwa linahitaji aina mpya ya uinjilisti. Badala ya kwenda mjini kwa majuma matatu au manne na kufanya mikutano ya muda mfupi ya umma, alileta timu za vijana na akaanza kufanya kazi na makanisa kwa kipindi kirefu.

 

Uamuzi huu ulijikita katika maono ambayo Ellen White aliyapata Februari 27, 1910, ambapo alisema kwamba “inapaswa kuwepo na mabadiliko makubwa kutoka kwenye njia za kazi za zamani. Kwa miezi mingi hali hiyo imekuwa ikinisukuma,” aliandika, “na nilisisitiza kuwa makundi yawe na utaratibu na kufundishwa kwa bidii ili kufanya kazi katika miji yetu muhimu. Wafanyakazi hawa wanapaswa kufanya kazi wawili kwa wawili, na wakati kwa wakati wote wanapaswa kukutana pamoja kuelezea uzoefu wao, kuomba na kupanga jinsi ya kuwafikia watu kwa haraka, na hivyo, ikiwezekana, kuukomboa wakati.”1 Huo ndio mfano wa uinjilisti ambao Mchungaji Mark ameufuata kwa miaka mingi.

 

Kutoka New England, akina Finley walihamia Lake Union katika Marekani ya kati na kufanya mikutano ya injili katika eneo lote, lakini haswa Chicago. Walianzisha shule ya mafunzo ya uinjilisti iliyoitwa Taasisi ya Lake Union Sowing, mradi wa ushirikiano kati ya Lake Union na Seminari ya Chuo Kikuu cha Andrews. Baada ya miaka miwili, Divisheni ya Kaskazini ya Amerika ilichukua udhamini wa taasisi hiyo ya kuongoa roho. Mchungaji Mark anakumbuka kwa furaha uzoefu wao. “Kwa hakika ilinipa changamoto sana kujaza akili yangu kwa mawazo ya kibiblia na kuwa makini linapokuja suala la maswali ambayo wanafunzi wa seminari walikuwa wakiuliza,” anasema.

 

Baada ya miaka sita huko Chicago, Mchungaji Mark alipokea wito wa kutumika Kanisani huko Ulaya. Kutoka 1985 hadi 1990, alikuwa Katibu wa Huduma katika Divisheni ya Ulaya Ng’ambo. Ilikuwa hapo, anasema, “tulipoanza kufanya kazi katika nchi za kisoshalisti, nchi za kikomunisti. Tulikuwa na nchi tatu za kisoshalisti katika divisheni yetu: Polandi, Hangari, na Yugoslavia. Kazi ya ughaibuni inakupanua. Kazi ya ughaibuni inakupatia upana wa kazi ulimwenguni ambao vinginevyo huwezi kuwa nao.”

 

Baada ya kurudi Marekani kwa ajili ya elimu ya watoto wao, Mchungaji Mark alipewa nafasi ya kuwa mhubiri/mkurugenzi wa It Is Written (Imeandikwa), kipindi cha televisheni cha kimataifa kilichoanzishwa na George Vandeman mwaka 1956 kikiwa na lengo la kushiriki umaizi kutoka katika Neno la Mungu na ulimwengu. Mchungaji Mark alisafiri na kuhubiri pamoja na It Is Written hadi 2004.

 

Mwaka 2004, alipata wito wa kwenda makao makuu ya Kanisa Ulimwenguni huko Silver Spring, Maryland, kuhudumu kwanza kama mkurugenzi wa Uinjilisti Ulimwenguni, kisha kama makamu mwenyekiti wa Konferensi Kuu baada ya kuchaguliwa kwake mwaka 2005 katika uchaguzi wa Konferensi Kuu huko St. Louis, Missouri.

 

 

MIAKA YA MACHWEO

Mchungaji Mark hucheka akikumbuka jaribio lake la kustaafu katika Uchaguzi wa Konferensi Kuu huko Atlanta, Georgia. “Mwaka 2010, Teenie pamoja nami tulikuwa watu wazima kidogo, tukiwa katika miaka yetu ya mwisho ya 60. Nilikuwa nikijiandaa kwenda jukwaani kutangaza kustaafu kwangu. Mzee Wilson alikuwa ndiyo amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Konferensi Kuu. Nilipokuwa nikitembea kwenda jukwaani, alinipa mkono na kusema kitu, ‘Ningependa sana ubakie kama mmoja wa wasaidizi wangu.’ ” Kwa hivyo, kwa miaka 14 iliyopita, Mchungaji Mark amehudumu kwa muda wa ziada kama msaidizi wa mwenyekiti wa Konferensi Kuu.

Sasa wakiwa wastaafu nusu, akina Finley wamepanua huduma zao katika maeneo mengine.

 

Kwa miaka kadhaa, Teenie amekuwa akitoa semina kuhusu umuhimu wa kila kanisa kuwa shule ya mafunzo kwa wafanyakazi wa Kikristo.2 Mnamo mwaka 2009 walihama kwenda Dominion Valley huko Haymarket, Virginia. Hapo ndipo ambapo Teenie aliona sehemu ya ardhi ikiwa na ishara ikisema, “Kiwanja cha Kanisa la Baadaye.” Alimgeukia mumewe na kusema, “Hilo linahitajika kuwa kanisa la Waadventista na shule ya mafunzo.” Mchungaji Mark alijibu kwamba alikuwa akifanya kazi katika Konferensi Kuu na haikuwa busara kuongeza kitu kingine kwenye programu iliyokwisha kupangwa. Teenie alijibu, “Sawa, nitaomba.” Kwa pamoja walifanya maombi ya dhati kwamba Mungu angewafungulia milango ikiwa ingekuwa ni mapenzi Yake kusonga mbele na mradi huo.

 

Jibu lao lilikuja kwa njia ya kustaajabisha. Teenie anaeleza, “Nilikuwa nikifundisha semina na kutoa wazo zima la jinsi unavyofunza kanisa katika uinjilisti, maandalizi ya pamoja katika kazi ya kabla ya uinjilisti na kisha katika uinjilisti.

 

Nilisema kwa upole tu kwamba kulikuwa na sehemu ya ardhi inayouzwa, na labda, sasa tulikuwa tunazeeka, tunahitaji zaidi kustaafu na kukaa mahali pamoja. ‘Na unajua,’ nilisema, ‘ningependa kuwa nayo kwa ajili ya shule ya mafunzo.’ Baadaye, mtu ambaye sikuwahi kukutana naye hapo awali alikaribia na kuniuliza, ‘Unaweza kuniambia zaidi kuhusu shule hiyo ya mafunzo?’ Nilifanya hivyo na siku iliyofuata alinirudia na kusema, ‘Mungu ameniambia nikupatie $50,000 kwa ajili ya hiyo ardhi hiyo.’” Alienda nyumbani na kumwambia Mchungaji Mark kwamba Mungu amewapa $50,000 kwa ajili ya shule ya mafunzo. Mara tu walipoweka akaunti maalum kwa ajili ya ununuzi wa ardhi, walipokea simu. Kuna mtu alikuwa amesikia kuhusu mchango wa $50,000 na alitaka kuungana naye katika kutoa. Mtu mwingine aliwapatia $7,000. Ilikuwa wazi kwao kwamba Mungu aliwataka waendelee mbele.

 

Walikwenda Virginia na kutazama ardhi, kisha wakala wa kiwanja akawaambia kuhusu kiwanja kingine hapo mjini ambacho kilikusudiwa kuwa maktaba, lakini mji haukuwa umeamua kukitumia. Je, wangependa kukitumia kwa ajili ya kanisa? Mmiliki angeuza ardhi kwao kwa takribani nusu ya gharama ya kuuzia. Akina Finley waliwaza kuwa huenda hapa palikuwa mahali ambapo Mungu alikuwa akiwaongoza na walianza kutafuta zaidi majaliwa Yake. Muda si mrefu baadaye, walipokea simu ya kwamba gharama yote waliyoihitaji ingepatikana. Walipaswa tu kununua ardhi hiyo.

 

Walinunua ardhi hiyo huko Haymarket, Virginia, wakaanzisha shule ya mafunzo na, kama anavyosema Teenie, “tupo hapa leo bado katika kustaafu kwetu.” Kanisa jipya, Living Hope, lilianzia katika kanisa huko Warrenton, Virginia, ambalo lilikuwa na idadi ndogo sana ya waumini. Ushirika wao ulianza kukua, na kundi hilo la kanisa lilikwenda ili kuunda msingi wa kanisa la Living Hope huko Haymarket.

 

Leo hii, Living Hope lina takribani ya washiriki 250 na kanisa linaendelea kustawi. Wanapanga kuanzisha upya umati wa waumini huko Warrenton. Mamia ya wachungaji kutoka Amerika ya Kaskazini nzima wamehudhuria vipindi vyao vya mafunzo katika shule ya uinjilisti. Wanafanya vipindi vya mafunzo kati ya saba hadi tisa kwa mwaka mahali popote, kwa kawaida kwa takribani siku tano kila mmoja.

 

Yote haya, Mchungaji Mark na Teenie wanasema, yalikuwa baada ya kustaafu kwao. Wameendelea kusafiri ulimwenguni kuhubiri na kufundisha, kufanya mifululizo ya injili, kumsaidia mwenyekiti wa Konferensi Kuu, na kuandika vitabu vya kushiriki. Kwa kweli, akina Finley hivi karibuni walishiriki katika Hope for Africa (Tumaini kwa Afrika), tukio la injili kupitia setilaiti nchini Kenya na vituo 20,000 vya kupakua kwa mtandaoni katika nchi 11 na kwa lugha saba. Takribani watu 197,000 walibatizwa katika mikutano hiyo. Wanaendesha shule ya mazoezi ya uinjilisti asubuhi na takribani wachungaji 300 hadi 400 na walei wengine wakihudhuria, wakijifunza jinsi ya kushiriki injili kwa ufanisi zaidi.

 

“Inaonekana tumekuwa tukishughulikia mambo kwa haraka kidogo (katika kustaafu kwetu) na tunafanya kile tulichokuwa tukifanya awali lakini tunaongeza vipengele kama shule ya mafunzo, nyumba ya raha na mipango mingine ya injili,” Teenie anasema.

 

 

MIRADI MIPYA

Baadhi ya mambo mengine anayoyazungumzia ni pamoja na huduma mpya ya YouTube, utangazaji wa redio, na mikutano ya wachungaji na wafanyakazi wa kanisa.

 

 

YouTube

Akina Finley walianzisha huduma ya YouTube katika kanisa lao mahalia na “walei—bila wataalamu wa vyombo vya habari,” anasema Mchungaji Mark. “Sasa tumeanzisha huduma ya YouTube ambapo tunayo timu ambayo ni bora sana. Wamejitolea kumshiriki Kristo pamoja na ulimwengu kupitia vyombo vya habari.” Kituo chao cha YouTube, HopeLives365, kufikia wakati wa kuandika haya, kinao, zaidi ya wafuatiliaji 238,000 na kuwagusa watu katika kila nchi ambapo YouTube inapatikana.

 

Kila juma, wanazalisha angalau vipindi viwili hadi vitatu. Watu kutoka ulimwenguni kote wanakuja kwa Kristo na kubatizwa. Mchungaji Mark alitumia huduma ya YouTube kwa mfululizo wa uinjilisti kwa watu wanaozungumza Kichina ulimwenguni kote. Walikuwa na watazamaji milioni 10 kutoka mikutano hiyo pekee.

 

 

Redio

Katika miezi sita iliyopita tu, Salem Broadcasting, mtandao mkubwa wa redio ya Kikristo nchini Marekani, umeweka mahubiri ya Mchungaji Mark katika orodha yao ya programu. Katika tukio la hivi karibuni la chakula cha mchana cha watangazaji, waongozaji wa programu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi walifurahia kuwa na Mchungaji Mark akihubiri mahubiri ya kibiblia. Sasa wametoa zaidi ya vipindi vya redio 200. “Kwa kweli,” Mchungaji Mark anasema, “ndani ya Salem Broadcasting tumeweza kuunda uhusiano mzuri na watu katika jamii ya kiinjilisti. Tunawathamini sana. Wanathamini huduma yetu. Wanakusanya fedha kwa ajili yetu!”3

NYUMBA ZA MAPUMZIKO

Akina Finley wameanzisha asasi isiyoingiza faida ya Hope Lives Evangelistic Ministries na nyumba mbili za mapumziko ambapo wanakaribisha wachungaji kuwa wageni wao kwa mikutano ya kimya. Nyumba hizi ni mahususi kwa ajili ya wachungaji, wafanyakazi wa kanisa, na vikundi vya huduma kufikia na kupumzika, kula chakula bora cha mimea, na kufanya mazoezi, wakati wote wakijifunza jinsi ya kusaidia huduma zao kukua. Wanahudhuria madarasa kuhusu ukuaji wa kanisa, uinjilisti, ujumbe wa malaika watatu, na zaidi katika kanisa la Living Hope. Ni njia kamili ya kukaribisha mikutano ya huduma.

 

“Haya ndiyo maisha kwetu,” Teenie anasema, “katika miaka yetu ya kustaafu . . . ikiwa unaweza kuipa jina hilo!” Anaongezea kwa haraka, “Tunalipenda hili. Tunajichangamsha.” Mchungaji Mark anakubaliana. “Tunafurahia huduma yetu. Tunaamini kwamba Mungu amefungua milango kwetu leo ambayo hatukuwa nayo miaka 10 au 20 iliyopita. Leo tuna maono mapana zaidi kuliko hapo awali. Sasa tunaweza kuufikia ulimwengu kupitia huduma zetu za YouTube, redio, na nyumba zetu za mapumziko zinatupatia fursa ya kufanya kazi na kufundisha wachungaji.”

 

Anahitimisha: “Furaha kuu maishani ni kumtumikia Yesu. Kumtumika kwa ajili ya Kristo inatupatia kila mmoja wetu kusudi la kuishi katika miaka yetu ya kustaafu. Inatoa sababu ya kuamka asubuhi. Inatupatia nguvu na kututia moyo pamoja na maono mapya. Tafuta eneo la huduma ambalo unalifurahia na jitolee katika huduma hiyo kwa sehemu tu ya muda wako kila juma. Utafurahia kwamba ulifanya hivyo na wengine watabarikiwa.”

Mengi yanaweza kuandikwa kuhusu safari ya kiroho ya Harrison Kathumbi Mwathi katika maeneo yenye joto na magumu ya Kenya.

 

Akizaliwa mwaka 1952 na wakulima maskini, Harrison hakuwa na utoto rahisi. Kilimo kilikuwa kigumu katika eneo la nusu jangwa na familia ilipitia wakati mgumu. Hata hivyo, alifanikiwa kujiunga na Shule ya Kyandili kwa ajili ya elimu ya msingi. Baadaye alihamia katika Sekondari ya Central kwa ajili ya cheti chake cha shule ya sekondari.

 

Baada ya sekondari, Harrison alipata ajira karibu na Jiji la Nairobi kama mwendesha mashine katika kiwanda cha usindikaji wa nyama. Muda mfupi baadaye aliteuliwa kuwa afisa msaidizi wa serikali. Kwa sababu ya huduma yake ya kuigwa akiwa kama daraja kati ya serikali na wananchi, alipandishwa cheo kuwa kiongozi wa kijiji chake cha nyumbani, Itetani.

 

Daima akiwa Mwadventista wa Sabato, Harrison alikabiliana na maisha ya huduma ya umma na maisha ya kanisa. Haikuwa rahisi kwake kuzingatia yote mawili, lakini roho yake ya uthabiti ilimfanikisha. Alikuwa na mke na watoto wawili wa kuwalea, na aliwahakikishia kupata kilicho bora kwa alichokimudu.

 

Muda wote wa maisha yake, Harrison alijua kuwa ameumbwa kwa kazi ya adhimu—kuwavuta watu kwa Kristo kupitia ujumbe wa malaika watatu. Alihudumu kama mzee mwaka 1988 katika majukumu mbalimbali, akisimamia uanzishwaji wa makanisa na akiwa kama mwakilishi wa konferensi katika mikutano.

 

Harrison alistaafu mwaka 2008 na kujitoa maisha yake kwa ajili ya injili. Uzoefu wake kama kiongozi wa kanisa mlei punde ulihitajika. Alipewa jukumu la kusimamia ujenzi na uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Itetani. Shule hiyo sasa ina wanafunzi 240, ambapo 23 kati yao ni Waadventista wa Sabato. Anashirikiana na walimu wawili Waadventista wa Sabato katika malezi.

 

Yuko katika bodi za taasisi kadhaa, ikiwa ni pamoja na shule hiyo ya wasichana.

 

Kama mlei, Harrison ni mhusika wa mawasiliano kati ya washiriki na viongozi wa utawala wa konferensi mahalia. Anasaidia kupanga mikutano ya uinjilisti na vikundi vya kanisa na taasisi kutoka Marekani. Ziara za kimishonari kama hizi mara nyingi huleta matunda. Dawa za bure hutolewa. Watu wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali wanatibiwa. Nguo kwa ajili ya wahitaji hutolewa. Wanafunzi wenye uhitaji wa karo zao hufutiwa. Jitihada hizi husaidia makanisa mbalimbali kuunga mkono kazi yao ya uinjilisti.

 

Katika ziara ya hivi karibuni na timu kutoka Kanisa la Kimataifa la Waadventista la Houston, Texas, na nyingine kutoka Chuo Kikuu cha Weimar kutoka California, makanisa matatu mapya yalianzishwa na zaidi ya watu 200 walibatizwa. Wengi zaidi wanaendelea kupata malezi katika imani. Hitaji kubwa ni kukamilisha jengo la kanisa ambapo hawa waumini wapya watakuwa wakiabudu. Makanisa mahalia yaliamua kununua ardhi na ujenzi umeanza.

Mke wa Harrison amekuwa nguzo imara inayomtia moyo katika jitihada zake zote. Umri unakwenda kwa haraka, lakini yeye ni thabiti na shupavu.

 

Njozi yake ni kuona watendakazi wengi wa Biblia wakijihusisha, wakifikia maeneo ambayo hayajafikiwa katika kanda za Kitui, Machakos, na Makueni. Pia anataka kuona ujenzi wa makanisa katika maeneo ambayo roho mpya zimeongolewa.

 

Sasa akiwa na miaka 72, Harrison anawapa changamoto wawakilishi wengine wa kawaida kudumu kuwa waaminifu na kujitoa kikamilifu, kumweka Mungu kwanza, kuwa na mtazamo chanya juu ya kazi ya Mungu, kuongoza kwa kuwa mfano bora, na kuimarisha uhusiano mzuri na washiriki wengine. Anasubiri kwa shauku ujio wa Yesu.

Mimi ni mtendakazi wa Chuo cha Waadventista cha Concepcion huko Gregorio del Pilar, Ilocos, Ufilipino. Nilikuwa profesa wa chuo cha Philippine Union College (PUC), kinachoitwa sasa Adventist University of the Philippines (AUP), wakati, takribani miaka 50 iliyopita, nilianzisha na kusimamia Philippine Union College Adventist Collegiate Taskforce (PUC ACT), baada ya kusukumwa na makala niliyoisoma ya Youth’s Instructor, iliyoandikwa na Ellen White.

 

Wakati wa likizo ya shule, PUC ACT iliwatuma wanafunzi kufanya mikutano ya matibabu na Kampeni za Maisha Bora katika maeneo yaliyotengwa ambapo huduma za matibabu hazipatikani kwa urahisi. Mikutano ya matibabu na Kampeni ya Maisha Bora huko Concepcion ilivuta roho za thamani 11 kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Waasisi hawa 11 walikuwa washiriki wa kanisa la kwanza la Waadventista katika eneo hilo.

 

Kupitia rafiki serikalini, nilifanikiwa kupata jengo la shule lililobuniwa mapema kutumika kama sehemu ya kukusanyikia kwa idadi inayozidi kuongezeka ya vijana wanaohudhuria mikutano ya Kujitolea ya Vijana Wamishonari kila Jumamosi alasiri. Nilipoondoka kwenda Marekani mwaka wa 1976, viongozi wenye njozi wa Kanisa katika Misheni ya Majimbo ya Mlima, Mountain Provinces Mission (MPM), waligeuza jengo hilo kuwa madarasa ya chuo cha Concepcion Adventist Academy (CAA) kilichoanzishwa hivi karibuni.

 

Nilifanya kazi huko Marekani kama katibu wa kitengo cha matibabu katika Kituo cha Matibabu cha Waadventista cha Glendale na kama mwanachama wa Uga msaidizi katika Chuo Kikuu cha Glendale huko Kusini mwa California ili kutoa msaada wa kifedha kwa walimu na wanafunzi wa CAA. Nilistaafu kutoka Kituo cha Matibabu mwaka 2007 lakini nikabaki na nafasi yangu ya kufundisha katika chuo hadi mwaka 2014 ili kuendelea kutuma fedha shuleni. Nilirudi Ufilipino mwaka 2014 ili kuongoza huduma za shule za ufadhili na huduma za kijamii.

Kutokana na miundombinu duni na baadhi ya mapendekezo yasiyotimizwa ya Wizara ya Elimu nchini Ufilipino, CAA ilionekana kuwa hatarini kufungwa. Hata hivyo, Bwana alingilia kati. Kupitia kwa maombi ya dhati na uaminifu, kujitoa kwa dhati kwa walimu, wanafunzi na wazazi wao, na msaada wa kimaadili na kiroho kutoka kwa MPM na viongozi wa kisiasa wa mkoa, shule haikufungwa. Walifanya kazi pamoja kudumisha CAA. Milango yake kwa miaka 48 iliyopita imekuwa wazi kwa ajili ya vijana wetu wanaotamani kupata elimu itakayowawezesha katika safari yao kuelekea kwenye ufanisi wa kiroho na kitaaluma kutoka duniani hapa hata nchi mpya. Mimi ni muumini wa dhati na mtetezi mwenye shauku wa elimu ya Kikristo na CAA itabaki daima kuwa sehemu yangu.

 

Kama wastaafu, hatuhitaji kusubiri kufanya mambo makubwa kwa ajili ya Bwana. Tunaweza kufanya mambo madogo kwa upendo. Mwulize mchungaji wako wapi msaada wako unahitajika zaidi, iwe ni katika konferensi yako mahalia au katika nchi zinazoendelea zinazoteseka kutokana na vurugu za kisiasa, umaskini, ubaguzi na ukosefu wa elimu.

 

Kwa wale wanaoishi Amerika, msaada wa kifedha unachangia pakubwa. Unapolala usiku, dola zako, pamoja na maombi na upendo, vitafanya miujiza katika kuongoa roho za thamani kwa ajili ya ufalme wa Mungu.

Tangu wongofu wangu nikiwa kijana, sijawahi, ikiwa kimwili inawezekana, kukataa mwaliko wa kuwaeleza wengine habari za Yesu au kufundisha kutoka kwenye Biblia. Nilikuwa na umri wa miaka 17 tu nilipohubiri mahubiri yangu ya kwanza, na uzoefu wa maisha yangu baadaye umenipa furaha kubwa, kuhubiri na kufundisha katika mabara matano duniani.

 

Sasa umri na afya kiasili vinaweka vikwazo. Naweza kuwa nikififia polepole kama askari wa injili wanavyofanya, lakini bado ninafurahia kuchangia kadiri hali zinavyoruhusu.

 

Ninafurahia kuhudumu kama mchungaji wa jumuia ya kanisa la takribani watu 25 huko Denmark, ambapo tunaishi na familia yangu hivi sasa. Kulingana na wazo kutoka kwa mmoja wa washiriki, mwanasheria mpya aliyeongoka, kwa sasa tunafanya kazi kwenye mfululizo wa vipindi vya redio mtandaoni kuhusu jinsi Mungu alivyozungumza kupitia Biblia, kwa kufuatisha mazungumzo ambayo mwanasheria alipitia alipokuwa akifanya maamuzi ya kuwa Mwadventista.

 

Muda wangu bado unachukuliwa na semina na mahubiri katika Skandinavia nzima. Mada zinazoombwa zaidi ni Utatu, Danieli, na Jinsi ya Kusoma Biblia. Kazi za kimataifa zimekuwa zikipungua kidogo, lakini imekuwa ni furaha kiasi gani kuhubiri mtandaoni kwa kanisa la Ghana huko Uholanzi, na kutoa mihadhara kwa wanazuoni huko Peru na wachapishaji wa vitabu vya dini huko Australia—ingawa mara nyingine kwa gharama ya kupoteza usingizi wa usiku! Kitaaluma, kuwa mhariri msaidizi mwenza wa SDA Commentary mpya ni changamoto, lakini pia ni heshima kubwa.*

 

Baadhi ya shughuli hufanywa kutoka katika ofisi yangu ya nyumbani. Wakati wa ugonjwa wa UVIKO, chaneli yangu ya YouTube ilithibitika kuwa na manufaa kwa watu wengi. Nilitoa saa nyingi kwa masomo ya kujifunza Biblia ya kila robo ya mwaka. Likiitwa “Tidbits,” jina langu la kufuatilia, @biblewithpaulpetersen, lina mfululizo wa maoni kwa Shule ya Sabato kwa Kideni na Kiingereza, inatambulisha vitabu vya Biblia kama vile Mwanzo, Waebrania, Danieli, Kumbukumbu la Torati, Zaburi nk., kwenye toleo la Kideni na mara nyingi inaambatana na vifaa vilivyoandikwa kwenye mtandao.

Jambo lingine la kuridhisha sana limekuwa kuwa mwandishi na mchapaji wa  kisa cha Ufunuo kwa watoto, kilichoandikwa kwa mashairi, na michoro ya furaha na shangwe badala ya giza na huzuni.

 

Kikiwa na kichwa cha The Prisoner on Patmos, kitabu hicho kimeuzwa vizuri. Mmoja wa wasomaji ni mwanadarasa mwenzangu asiye Mwadventista katika umri wangu wa ujana. Nilipomtembelea, ilikuwa faraja kukiona bado kitabu kwenye meza yake ya kahawa, na kusikia jinsi yeye na mumewe na wajukuu wao walivyokipenda kitabu.

 

Je, mstaafu anawezaje kuchangia? Kuwa chanya, kushiriki furaha ya kuwa rafiki wa Yesu na miujiza ya Neno la Mungu, ni mbaraka kwa wastaafu wenyewe, na inaweza kuwa na thamani kubwa kwa vizazi vichanga kuelewa jinsi sisi wazee tunavyoshangilia, kwa hekima na ufahamu, kusaidia kanisa na kumpenda Yesu hata mwisho.

Miaka mitano kabla ya kustaafu, orodha ya shughuli za baada ya kustaafu za Susy Schulz ilikuwa imeongezeka hadi zaidi ya ishirini na tano. Mawazo yote yalikuwa na kitu kimoja kinachofanana: yalikuwa mambo aliyoyapenda. “Upendo” haukutosha, hata hivyo; alitaka kufanya kitu cha umisionari pia.

 

Kwa haraka jibu likawa dhahiri: upendo wake kwa vitabu na haja ya watoto kujifunza lugha ya Kiingereza katika mji wake wa nyumbani nchini Argentina. Watoto wachache tu huko Libertador San Martin, kijiji cha Chuo Kikuu cha Waadventista River Plate, waliweza kujifunza bure Kiingereza.

 

Wakati huo, mumewe Susy, Luis, alikuwa mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Elimu katika Konferensi Kuu na Susy alifanya kazi kama mhariri na mtafsiri wa Jarida la College na University Dialogue, jarida kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Waadventista wa Sabato na vijana wataalamu linalozalishwa na Idara ya Elimu.

 

Kwa haraka hadi Aprili 24, 2022, ndoto ya Susy ilitimia. Familia ya Schulz ilihamia tena Argentina baada ya kustaafu, walikodisha sehemu nzuri katika kijiji na kuiboresha, na walikuwa wameajiri timu ya walimu na wafanyakazi wa elimu wastaafu kusimamia shughuli za bure za maktaba na kuwajali wasomaji vijana wenye shauku. Maktaba ya “The Book Garden” (Bustani ya Vitabu) ilikuwa tayari kufungua milango yake kwa watoto katika mji mdogo wa Argentina.

Kuna mengi zaidi katika maktaba kuliko vitabu 6000+. Kupitia makubaliano na Chuo Kikuu, hapa ni mahali ambapo walimu wa Kiingereza wa baadaye (na wanafunzi wengine wa Kiingereza) hutoa ushauri, matukio ya kusoma hadithi, kucheza michezo kwa Kiingereza, kuimba nyimbo na shughuli nyingine nyingi. Akina Schulz walipanga kwa miaka mingi awali kabla ya kufungua maktaba, kwa kuchagua vitabu kwa uangalifu na kufanya mikakati. Uzoefu wao wa maisha kama walimu wa Kanisa la Waadventista uliwasaidia katika maamuzi yao na kusaidia kujenga uzoefu chanya kwa wateja wa kudumu wa maktaba. Kwa kweli, wakati akina Schulz walipohamia tena Argentina kutoka Marekani, walituma kontena za vitabu walizokuwa wamehifadhi kwa ajili ya maktaba hiyo. Hadithi nyingi na vitabu vya sayansi vimejikita katika msingi wa Biblia, na vingine vinawakilisha maarifa anuwai ambayo watoto wanapaswa kufundishwa. Walakini, kuna jambo moja linalofanana kati ya machapisho yanayopatikana katika maktaba—hakuna kinachokinzana na imani ya Waadventista.

 

“Bustani ya Vitabu” imekuwa na mafanikio, si tu kwa watu katika mji huo lakini kwa familia nyingi zinazotoka miji jirani. Familia nyingi kati ya hizi si Waadventista lakini bado huja kwa ajili ya nyenzo zaidi ambazo zinaonekana kuwa na matokeo yenye amani kwa watoto wao. Ingawa maktaba ilifungua milango yake hivi karibuni, Luis na Susy tayari wana kisa kizuri cha kusimulia! Kupitia kazi ya maktaba ndogo na uteuzi wa kazi takatifu zingine, familia nzima imebatizwa na huhudhuria katika kanisa mahalia la Waadventista.

 

“Utume haukomi baada ya kustaafu,” anasema Luis. Imekuwa mwanzo tu wa fursa mpya kwa kikundi hiki cha wastaafu na kuongeza maana katika maisha ya wastaafu wanaojitolea wanaosaidia shughuli za kila siku katika maktaba.

 

Nini kinachofuata kwa “Bustani ya Vitabu”?

 

Mfululizo wa matukio ya umma, kwa Kiingereza tu, umepangwa kwa miezi ijayo na utafanyika katika miji jirani. Kuta za maktaba zimevuka jamii mahalia, na matukio haya ya kusoma vitabu hadharani, nyimbo, maigizo na mengi zaidi (yamepangwa pamoja na wanafunzi wa chuo kikuu wenye lengo la utume) yanaelezea mpaka wa pili wa kufanya marafiki katika jamii ambazo bado hazijafikiwa na injili.

“Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana” (Waefeso 6:4).

 

“Wakati tunaangalia umuhimu wa kazi ya mama na utume, hatuwezi kuacha kuona wajibu na jukumu la mume na baba katika kufundisha watoto wake. Bidii yake inapaswa kuwa katika upatanifu na ile ya mama mcha Mungu. Anapaswa kudhihirisha upendo wake na heshima kwake kama mwanamke aliyemchagua na mama wa watoto wake. . . .

 

 

KUTUMIA MUDA PAMOJA NA WATOTO

“Baba anapaswa . . . kujichanganya pamoja na watoto, kuwaonea huruma katika shida zao ndogo, kufungamana nao katika mioyo kwa kifungo cha upendo na kuanzisha ushawishi katika akili zao zinazokua kwamba mawazo yao yataonwa kuwa matakatifu. . . .

 

“Anaporudi nyumbani kutoka katika kazi zake anapaswa kuona ni badiliko la kufurahisha kutumia muda fulani pamoja na watoto wake. Anaweza kuwapeleka katika bustani, kuwaonyesha matumba yanayochanua na rangi ya vivulivuli mbalimbali vya maua yaliyochipua.

 

Kwa njia hiyo anaweza kuwapatia mafundisho ya muhimu sana kuhusu Mwumbaji, kwa kufunua mbele yao kitabu kikuu cha asili, ambapo upendo wa Mungu unaonyeshwa katika kila mti, ua, na jani la nyasi. Anaweza kushawishi katika akili zao ukweli kwamba ikiwa Mungu anajali sana miti na maua, Yeye atajali zaidi viumbe vilivyoumbwa kwa mfano Wake. Atawaongoza mapema kuelewa kwamba Mungu anawataka watoto kuwa wazuri sana, wasio na mapambo bandia, bali wenye uzuri wa tabia, haiba ya wema na upendo, utakaofanya mioyo yao kunang’anika kwa shangwe na furaha. . . .

 

“Akina baba, saa nzuri utakazozitumia kufahamu kwa ukamilifu mwenendo na tabia ya watoto wako, na njia nzuri ya kushughulika pamoja na akili zinazokua, ni . . . za thamani.”—Sign of the Times, Des. 6, 1877.

 

“Wajibu wa baba kwa watoto wake unapaswa kuwa shauku yake ya kwanza. Haupaswi kuwekwa pembeni kwa ajili ya kubahatisha, au ili kupata umaarufu ulimwenguni. Kwa kweli, hiyo hali ya ukwasi na heshima mara kwa mara imemtenga mwanamume na familia yake, na kupoteza mvuto wake kwao zaidi kuliko kitu kingine chochote. Ikiwa baba angewafanya watoto wake kukuza tabia zenye kuridhisha na kuheshimiwa na kuwa mbaraka kwa ulimwengu, anayo kazi mahususi ya kufanya.”—Signs of the Times, Des. 20, 1877.

 

 

AKINA BABA KUWAONGOZA WATOTO KATIKA NURU YA IMANI

“Bwana asipoijenga nyumba waijengao wafanya kazi bure” (Zaburi 127:1).

 

“Tungependa kuwasihi kwa uaminifu akina baba, vile vile akina mama, jukumu kuu ambalo wamechukua kwa kuwaleta watoto duniani. Ni jukumu ambalo hakuna chochote isipokuwa kifo kinachoweza kuwaachilia. Ni kweli, huduma kuu na mzigo unamwangukia mama wakati wa miaka ya awali ya maisha ya watoto wake, lakini hata hivyo, baba anapaswa kuwa tegemeo lake na ushauri, kumtia moyo kuegema katika mapenzi yake makubwa, na kumsaidia kadiri iwezekanavyo. . . .

“Katika siku kuu ya kutoa hesabu, ataulizwa: Wako wapi watoto niliowakabidhi katika uangalizi wako ili wapate elimu kwa ajili Yangu, midomo yao itoe sifa Zangu, na maisha yao yawe kama taji la uzuri ulimwenguni, na waje kuinuliwa kwa ajili Yangu milele?

 

“Kwa baadhi ya watoto nguvu za kimaadili zinashinda sana. Wanao uwezo wa kudhibiti akili na vitendo vyao. Wengine, hata hivyo, mapenzi kwa wanyama yanakuwa karibu kutowezekana kudhibitiwa. Ili kupatana na mienendo hii tofauti, ambayo mara kwa mara huonekana katika familia moja, baba, vile vile mama, wanahitaji uvumilivu na hekima kutoka kwa Msaidizi mtakatifu. . . .

 

“Baba anapaswa mara kwa mara kuwakusanya watoto wake karibu naye, na kuelekeza akili zao katika njia za nuru ya kimaadili na kidini. Anapaswa kuchunguza mwelekeo na uwezo wa tofauti, na kuwafikia kupitia njia rahisi zaidi.

 

Baadhi wanaweza kushawishiwa vyema kwa kumheshimu na kuwa na hofu ya Mungu; wengine kupitia ufunuo wa ukarimu Wake na majaaliwa Yake yenye hekima, wakitoa shukrani kuu; wengine wanaweza kuathiriwa zaidi kwa kufungua mbele yao miujiza na siri za ulimwengu wa asili, pamoja na upatanifu wake wenye kuvutia na uzuri wote, unaoongea na roho zao kumhusu Yeye aliye Muumba wa mbingu na nchi, na vitu vyote vya kuvutia vilivyomo.

 

“Watoto wenye kipaji au wenye kupenda muziki wanaweza kupokea athari ambazo zitadumu maisha yao yote, kwa matumizi yenye busara kwa uathirikaji huo kama njia ya mafundisho ya kidini... wengi wanaweza kufikiwa vema kwa picha takatifu, matukio yenye mifano katika maisha na utume wa Kristo. . . .

 

“Wakati inapaswa kuwa na usawa katika nidhamu ya familia, inapaswa kubadilika kukidhi mahitaji ya wanafamilia tofauti. Inapaswa kuwa ni somo la wazazi . . . kuwahamasisha kuelekea kwenye akili na ukamilifu wa tabia.”—Signs of the Times, Des. 20, 1877.   

 

“Baba ndiye kuhani mkuu wa familia. Roho ya mke na watoto wake, kama mali ya Mungu, zinapaswa kuwa na thamani kubwa kwake, na kwa uaminifu anapaswa kuongoza katika uumbaji wa tabia zao. Kuwajali watoto wake tangu utoto wao inapaswa kuwa fikira yake ya kwanza; kwa maana ni kwa faida yao ya sasa na ya milele kwamba wanaendeleza tabia sahihi. Anapaswa kwa uangalifu kuzingatia maneno na matendo yake, akizingatia athari zake, na matokeo wanayoweza kuzalisha.

Mikutano ya makambi ni utamaduni uliosheheni mengi ndani ya vuguvugu la Uadventista—ikivuta fikra zetu nyuma hadi wakati wa William Miller na Mwamko wa Ujio wa Pili wa miaka ya 1840 nchini Marekani. Kuanzia mikutano mitatu ya mwaka 1842, idadi ya mikutano ya makambi ya Waadventista iliongezeka kwa haraka, mikutano 40 ikiendeshwa mwaka 1843 na 55 mwaka 1844.1

 

Baada ya Kukatishwa tamaa Kukuu, waumini wa awali wa Marejeo waliacha kuendesha mikutano ya kambi kwa muda. Hata hivyo, kufikia mwaka wa 1867, miaka minne baada ya kuasisiwa rasmi kwa Kanisa la Waadventista wa Sabato, mfululizo wa mikutano midogo ya kambi ilifanyika. Kutokana na mafanikio ya mikutano hii midogo, Konferensi Kuu ilijadili kuhusu kuandaa “mkutano wa kambi kwa ajili ya fildi nzima.”2

 

Lengo la mkutano mkuu huu wa kambi lilikuwa kukidhi malengo mawili: “kwanza, kama chanzo cha ‘mambo ya kiroho,’ na pili, ‘kueneza imani yetu miongoni mwa watu.”3 Iliamuliwa kuwa mazingira ya mashambani yangekidhi vizuri malengo ya mkutano wa aina hii, na hivyo Ephraim H. Root, Mwadventista wa Sabato, alijitolea shamba lake huko Wright, Michigan, kama mahali pa mkutano.4

 

 

KUKUA KWA MIKUTANO YA KAMBI YA WAADVENTISTA

Huu ulikuwa mkutano wa kwanza wa kambi rasmi wa Waadventista wa Sabato, na desturi hii iliendelea kukua katika miaka ya 1870 na mikusanyiko ya kila mwaka kote Amerika Kaskazini. Kufikia miaka ya 1880, mikutano ya kambi ilikuwa madhubuti, na kulikuwa na “msimu wa mikutano ya kambi” ambapo waumini walikusanyika kwa ajili ya kutiwa moyo na kujengwa kiroho. Pia ilikuwa mahali pa kutangaza machapisho ya Waadventista, elimu, na zaidi.

 

Mikutano ya kambi iliendelea kuongezeka, na “kufikia mwaka wa 1904 Kanisa liliweza kujivunia kuwa mikutano sitini na nane ilifanyika Amerika Kaskazini na mingine kumi na tano ilifanyika kimataifa.”5

 

Lengo lingine muhimu la mikutano ya kambi ilikuwa kutumika kama chombo cha uinjilisti. Na hii ilithibitika kuwa hivyo kwa njia binafsi sana kwa familia ya Wilson.

 

 

MWALIKO KWA MKUTANO WA KAMBI

Palikuwa na mtu aliyeitwa William ambaye alikuwa mhandisi, mkulima na mfanyabiashara. Alizaliwa Ireland, alihamia Marekani mnamo mwaka 1870. Yeye pamoja na mkewe, Issabella, waliishi Philadelphia, ambapo alifanya kazi kama mhandisi wa injini za treni. Baadaye, walielekea magharibi mwa Redwoods ya Kaskazini mwa California kufanya ukataji wa miti, kabla ya kuweka makazi karibu na Healdsburg, ambapo William alikuwa mkulima wa matunda na mfugaji wa ng’ombe na mmiliki wa duka eneo la mashambani.

 

Hatimaye, wenzi hawa walikuwa na watoto wa kiume wanne—William (Jr.), Ray, Nathaniel na Walter. Wakati fulani, Isabella alikuwa Mwadventista wa Sabato, lakini mumewe hakuvutiwa sana na dini.

 

Mwaka 1905, mahema yalijengwa karibu na Healdsburg, California, kwa ajili ya mkutano wa kambi. Isabella na wavulana wake walihudhuria, na alimwalika mumewe kuwa pamoja nao kwa huduma ya Sabato. Kwa kumfurahisha, alikubali.

 

William alipokuwa chini ya hema, mhubiri alianza kufunua ukweli mzuri kuhusu Yesu, akishiriki haja ya wenye dhambi wote kuwa na Mwokozi na kumruhusu kubadili maisha yao. Mhubiri alitoa wito wa dhati na, kwa mshangao na furaha ya Isabella, William alisimama na kwenda mbele, akitoa moyo wake kwa Bwana.

 

Alijifunza ujumbe muhimu wa Marejeo kwa mwaka mmoja. Alifunga duka lake Jumamosi na kumtumainia Mungu kwa ajili ya mustakabali wake. Alibatizwa na baadaye akawa kiongozi wa wazee wa Kanisa la Waadventista wa Sabato huko Healdsburg. Kristo alibadilisha maisha yake.

William na Isabella Wilson walikuwa ni babu na bibi yangu na mhubiri aliyehubiri kwa bidii kuhusu Yesu alikuwa Ellen G. White. Baada ya kifo cha James White, alihamia Healdsburg na alikuwa akiishi karibu na Chuo cha Healdsburg – ambacho ni Chuo cha Pacific Union.

 

Babu yangu, Nathaniel, alikumbuka jinsi Ellen White alivyokuja nyumbani kwao alipokuwa mvulana, na jinsi alivyowasimulia kisa kwa upendo yeye na ndugu zake walipokaa miguuni pake. Familia ya Wilson inawiwa sana maarifa ya ujumbe huu wa thamani wa Marejeo kwa shughuli za moja kwa moja, za vitendo, za kiinjilisti za Ellen White.

 

 

USHUHUDIAJI MUHIMU

Leo hii mikutano ya kambi inaendelea kukidhi kusudi muhimu. Sio tu mahali pazuri pa kujumuika pamoja na waumini wengine, kusikiliza muziki na mawasilisho yenye kuvutia, na kufurahia warsha za vitendo, lakini inaendelea kuhudumu kama chombo muhimu cha kufikisha injili kwa watu.

 

Ellen White aliandika, “Mkutano wa kambi ni moja ya mawakala muhimu sana katika kazi yetu. Ni moja ya njia zenye ufanisi zaidi za kuvutia watu na kufikia matabaka yote kwa ajili ya mwaliko wa Injili.”6

 

Anaendelea, kana kwamba anaandika leo, “Tamaa na vita, furaha na kupata fedha, vinateka akili za watu. Shetani huona kwamba wakati wake ni mfupi, na ameweka mawakala wake wote kazini, ili watu wahadaiwe, wadanganywe, wajazwe, na kuvutiwa, hadi upelelezi utakapomalizika na mlango wa rehema kufungwa milele. Ni kazi yetu kutoa kwa ulimwengu wote—kwa kila taifa, jamaa, lugha, na watu—kweli zinazookoa za ujumbe wa malaika wa tatu.”7

 

Marafiki, tunapokaribia kurudi kwa Kristo kwa hivi karibuni, nawakaribisha leo hii si tu kuhudhuria mikutano ya kambi, bali kuwaalika watu kuja pamoja nawe—huenda mtu ambaye hajawahi kupata uzoefu kama huo awali—ili wao, pia waweze “onjeni, mwone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini” (Zab. 34:8).

Kwa Waadventista wa Sabato, “mkutano wa kambi” unaweza kuonekana kuwa tukio la Waadventista pekee. Kwa kuwa tunapenda sana asili, nini kinachoweza kuwa cha asili zaidi—au kwa hakika cha Kiadventista zaidi—kuliko kutoka kwenye nyumba, vyumba vya kuishi, au hoteli na kuweka kambi mashambani, kulikotengwa na ulimwengu, fadhaa zake na majaribu, na kufurahia ushirika na ibada iliyozungukwa na uzuri wa uumbaji wa Mungu?

 

Lakini mkutano wa kambi ulikuwepo kabla ya Waadventista. Mikutano ya kambi iliibuka kwenye mpaka wa Amerika, ambapo umbali mkubwa ulimaanisha walowezi ambao mara nyingi waliishi umbali mkubwa kutoka kwa kila mmoja. Mkutano wa kwanza wa kambi uliofahamika ulifanywa na Wapresbiteri katika jimbo la Kentucky la Marekani mwaka 1800.

 

Mwaka mmoja baadaye, mkutano mwingine wa kambi wa Wapresbiteri katika jimbo hilo hilo ulihudhuriwa na zaidi ya watu 10,000, na wazo hilo likachukuliwa haraka na Wamethodisti na madhehebu mengine ya Marekani, na kuenea mbali na mipaka ya Marekani, kote nchini. Mikutano ya kambi ya madhehebu tofauti mara nyingi ilishindana kila msimu wa joto.

 

 

KURIDHIWA KWA WAADVENTISTA

Waanzilishi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato walikua na mikutano ya kambi, na Wamiller waliipokea kwa shauku. Lakini baadhi ya Waadventista wa awali walikuwa na mashaka, kwa kuwa mikutano ya kambi, kama inavyofanywa na makanisa mengine, inaweza kuwa matukio ya kihuni, na ulevi. Ilifaa, hata hivyo, kwa jamii ya Marekani, ambapo umbali ulikuwa bado mkubwa zaidi kuliko Uingereza au Ulaya, na ambapo jamii ilikuwa ya usawa sana.

 

Hii ilikuwa tofauti na Ulimwengu wa Kale, lakini katika ulimwengu mpya, watu wa tabaka zote za kijamii wangeweza kukaa pamoja kwa furaha, hasa wanaposhiriki katika ibada.

 

Aidha, Waadventista wa Sabato walikuwa watumiaji wa kawaida wa mikutano ya mahema kwa madhumuni ya uinjilisti, na hivyo huenda lilikuwa ni jambo lisiloepukika kwamba wangekubali mikutano ya kambi. Shughuli za vikao vya Konferensi ya Wisconsin vilifanyika katika kambi yenye mahema mwaka 1867, ambayo iliwavuta wapiga kambi 300; na ilionekana kwamba, kwa sababu hiyo, viongozi wengi zaidi wa kanisa, chini ya uongozi wa Ellen White, waliamua kupokea mkutano wa kambi.

 

Kikao cha Sita cha Konferensi Kuu mwezi Mei mwaka 1868, kilichofanyika Battle Creek, Michigan, kwa hakika kilichukua hatua juu ya jambo hilo, huenda kwa sababu Waadventista wachache bado walitilia shaka ikiwa wafuasi wa malaika wa tatu walipaswa kujiingiza katika mikutano ya kambi. “Imeamuliwa, kwamba mkutano huu unapendekeza kwa watu wetu kufanya mkutano mkuu wa kambi kila mwaka wakati wa vikao vya shughuli za mashirika yetu. Mikutano ya kambi ni mfululizo wa mikutano inayofanyika kwa siku kadhaa, kwa kawaida katika mazingira ya vijijini au mashambani, pamoja na kutoa kwa ajili ya kupiga kambi katika viwanja hivyo; aina ya mikutano ambayo sasa ni ya pekee kwa Kanisa la Waadventista wa Sabato na madhehebu mengine machache.”1

 

Mkutano rasmi wa kwanza wa kambi ya Waadventista wa Sabato ulikuwa ule wa Konferensi ya Michigan, uliofanyika Wright, Michigan, mwezi Septemba 1868. Kufikia miaka ya 1880, “msimu wa mikutano wa kambi” ulitambuliwa vyema Amerika Kaskazini na ulirejelewa hivyo katika majalida ya kanisa. Vipi, hata hivyo, kuhusu mkutano wa kambi nje ya Marekani?

USHIRIKISHWAJI KIMATAIFA

Mkutano wa kwanza wa kambi uliofanyika nchini Uingereza ulikuwa Mei 31, 1807, karibu na Stoke on Trent, tukio lililofanywa na Wamethodisti, lililosababishwa na mhubiri wa uamsho mwenye haiba na utata wa Marekani, Lorenzo Dow. Mamlaka ya Wamethodisti wa Wesley yaliona mikutano kama hiyo kuwa yenye mashaka, lakini kundi la Wamethodisti liliendelea hata hivyo na lengo moja lilikuwa kuunda dhehebu mpya, Wamethodisti wa Kale.

 

Mikutano ya kambi haikufanyika Uingereza, hata hivyo, na miaka themanini baadaye, kwa wananchi wa Malkia Victoria ilikuwa dhana ngeni, ambayo wamishonari Waadventista wa Marekani waliofika katika miaka ya 1880 walilazimika kufanya kazi kwa bidii ili kuwashawishi wenyeji. Mwaka 1884, The Present Truth, jarida lililoanzishwa na Waadventista huko Uingereza, liliripoti juu ya mfululizo wa mikutano ya kambi ya Waadventista wa Sabato huko “Missouri, Minnesota, Tennessee, na California” na kubainisha kwamba: “Mkutano mkubwa zaidi kuwahi kufanyika Michigan ulikuwa umefanyika katika jiji la Jackson mwezi Septemba 18-30. Tunatamani kwamba lingekuwa jambo geni kwa wasomaji wetu wa Uingereza kuona mojawapo ya makambi haya.”2

 

Bila shaka “wasomaji wa Uingereza” wangeshangazwa na kiwango kikubwa ambacho mkutano huo wa kambi ulifanyika. Ripoti nyingine kwenye The Present Truth, iliyochapishwa tena kutoka kwenye jarida la Waadventista la Marekani, ilisema: “Simu hutuunganisha na mji pamoja na ulimwengu. Maji hutolewa kupitia mabomba kutoka katika taasisi za maji za mji. . . . Bodi ya utoaji na bodi ya usambazaji wa mahema kwa gharama ya wastani kwa wale wanaoitaka. Ofisi ya posta hupokea na kusambaza barua.”3 Yote haya, bila shaka, yaliwezeshwa na hali ya hewa ya joto na kavu ambayo kwa kawaida ingeweza kuhesabiwa wakati wa kiangazi huko Marekani—tofauti na Uingereza.

 

Mkutano wa kwanza wa kambi ya Waadventista wa Sabato uliofanyika nje ya Marekani ulikuwa Canada mwaka 1879. Mara tu baada ya makala katika gazeti la The Present Truth kutokea, mkutano wa kwanza wa kambi nje ya Amerika Kaskazini ulifanyika Moss, mashariki mwa Norway, mwezi Juni 1887. Ellen G. White na mwanawe Willie, ambao wote walikuwa wakitembelea Ulaya, walihudhuria mkutano wa kambi wa Moss—Ellen White anaweza tu kuonekana upande wa kushoto wa picha ya wakati huo ya wale waliohudhuria. Mkutano wa kambi huko Moss ulitangazwa kama tukio la Waadventista wa Sabato wote kote Ulaya kuhudhuria, ikiwa ni pamoja na kutangazwa kwa Waadventista wa Uingereza katika gazeti la The Present Truth.

 

Ilionekana kuwa yenye mafanikio—ni “baraka kubwa sana kwa kanisa, na kwa kazi kwa ujumla” kama taarifa ilivyosema—kwamba kiangazi kilichofuata, katika mwaka 1888, Konferensi ya Ulaya-Kati ilipanga mkutano wake wa kwanza wa kambi, “uliofanywa katika Upper Tramelan, Uswisi, ambayo bado ilikuwa na mafanikio zaidi, ikihudhuriwa na watu wengi zaidi, Waadventista, na watu kwa ujumla.”4

 

Baada ya hapo, mikutano ya kambi ilienea kote Ulaya na katika mabara mengine na kuwa matukio ya kawaida ya kila mwaka, wakati huo huo konferensi zote za Marekani na Canada zilifanya mikutano yake ya kambi kila mwaka pia. Mikutano ya kambi kwa hakika imekuwa sehemu ya jamii na utamaduni wa Waadventista.

Hili ni swali kubwa katika uga wa misiolojia, hasa kuhusiana na dini za ulimwengu zilizojitolea kwa kutukuza na kuabudu roho za mababu wafu. Taratibu hizi si tu imani ya kidini lakini, kwa baadhi ya visa, ni suala la utambulisho wa watu kijamii na kitaifa. Taratibu hizi za kidini zilikuwa maarufu katika Mashariki ya Kati ya kale na zilikuwa na athari kwa baadhi ya Waisraeli. Mungu hakupuuza hali hii lakini alishughulikia moja kwa moja.

 

 

Msingi wa Matambiko ya Mababu Wafu

Kuna dhana moja iliyo msingi inayofanana katika matambiko ya zamani na ya kisasa ya mababu waliokufa—mtazamo wa pande mbili wa asili ya binadamu ambapo binadamu wanajumuisha vipengele viwili, kimoja ambacho kinaendelea kuishi baada ya kifo cha mwili. Roho au nafsi inayosalia kuwa na uhusiano fulani na wanafamilia wengine katika familia kubwa kwa njia ya fadhili au yenye utisho. Wanafamilia walio hai wanawajibika kutoa mahitaji ya roho hizo hivyo kuonyesha heshima na utukufu kwa wafu. Kama mwitiko, inaaminiwa kwamba mababu waliokufa hulinda na kujali familia.

 

Kulingana na mtazamo huu, wakati jukumu la kutunza roho za wafu halitekelezwi, roho hizo zitakasirika na kuwa na haja ya suluhu. Inaaminiwa pia kwamba roho hizi zina maarifa ya kimwujiza hivyo walio hai wanaweza kuwauliza kwa ajili ya maarifa ya siku zijazo.

 

 

MAJIBU YA BIBLIA

Mungu kwa hakika anakataza kutaka shauri kwa “roho” za wafu (Kumbukumbu la Torati 18:11-12). Ushauri huu kwa kawaida unahitaji mtu wa kati ambaye anadai kupokea ujumbe kutoka kwa wafu au ambaye anaweza kumilikiwa na roho (1 Sam. 28:11-19; Walawi 19:31; 20:6, 27). Katazo hili linajikita katika uelewa wa Kibiblia wa asili ya binadamu. Binadamu ni umoja usiogawanyika wa mwili na maisha ambayo hukoma mtu anapokufa. Maisha ya kiakili ya wale wanaokufa yanapotea (Zab. 146:4), hawafanyi kazi, hawawezi kupanga mipango na hawana maarifa au hekima (Mhu. 9:10). Kumbukumbu yao haiendelei tena na uwezo wao wa kupata maarifa na maisha yao ya kihisia hupotea—hawawezi kupenda, kuchukia au kuhisi wivu (aya ya 5, 6). Maisha yao ya kidini (aya ya 5; Zab. 30:9; 115:17) pamoja na maisha yao ya kijamii yanafikia mwisho kwa sababu hawashiriki tena kabisa katika ulimwengu wa walio hai (aya ya 6). Kwa maneno mengine, WAMEKUFA! Matumaini yao pekee ni ufufuo kutoka katika wafu (Isa. 26:19; 1 The. 4:16-17).

 

 

KIFO NI ADUI

Kifo ni adui wa mwisho ambaye atashindwa milele na Kristo atakapokuja mara ya pili (1 Kor. 15:26). Katika kaida za kidini za Agano la Kale, chuki ya kifo ilielezewa kupitia ishara ya uchafu.

 

Uchafu wa kaida za kidini uliwatenga watu na Mungu na jamii, ukifanya kifo kuwa mfano wa uchafu na kutokuwepo kwa utakatifu (linganisha Walawi 5:2; 19:2; 21:1; Hesabu 6:9). Kuwa na mawasiliano na wafu kulikuwa ni kuanzisha urafiki na adui badala ya Mungu aliye hai. Ikiwa maarifa fulani yanamfikia binadamu ambayo yanaonekana kutoka katika ulimwengu wa wafu, ni kwa sababu nguvu za uovu zinajifanya kuwakilisha wafu. Wakati mwaguzi alipomwelezea Sauli aliyoyaona, alisema, “Naona mungu [’elohim, mungu] anatoka katika nchi” (1 Sam. 28:13; linganisha na Walawi 17:7).* Mungu wa kweli tu ndiye anayesimamia mustakabali na Yeye hushiriki maarifa Yake, mipango na mapenzi Yake na walio hai kupitia neno Lake. Hakuna haja au sababu ya kuwauliza wafu.

Katika athari, ndiyo! Katika miaka ya hivi karibuni, kirai “kukaa ni uvutaji mpya wa sigara” kimekuwa kikitumiwa zaidi katika duru za afya na ustawi. Kauli hii inayovuta usikivu inasisitiza matokeo hatari ya mtindo wa maisha wa kukaa sana, ikilinganisha madhara mabaya ya kukaa kwa muda mrefu na hatari zilizothibitishwa vizuri za uvutaji wa sigara.

 

Hatari za uvutaji wa sigara zilikataliwa na kufichwa kwa miaka mingi. Jamii imekuwa ya kukaa zaidi kwenye meza na kusukumwa na teknolojia. Wataalamu wa afya wanaiomba jamii kufanya tathmini upya ya tabia na mazingira yetu ya kazi kwa sababu ya hatari na madhara yaliyothibitishwa ya kukaa kwa muda mrefu.

Ulinganishi wa uvutaji wa sigara ni mkubwa lakini unatumika kama mwito wa kutufanya tuchukue hatua. Kama vile uvutaji wa sigara hapo awali ulivyozingatiwa kuwa tabia inayokubalika na isiyo na madhara, kukaa kumekuwa sehemu ya maisha yetu, haswa katika shughuli za ofisi. Ushahidi unaokua unaonyesha kuwa kukaa kupita kiasi kunaweza kuchangia katika matatizo mengi ya kiafya.

 

Utafiti umethibitisha kuwa kukaa kwa muda mrefu kunaweza kuathiri afya ya moyo kupitia mzunguko mbaya wa damu na hatari kubwa ya magonjwa ya moyo. Mtindo wa maisha wa kukaa sana unaongeza utando katika mishipa ya damu, ongezeko la shinikizo la damu na viwango vya juu vya lahemu. Kwa muda, mabadiliko haya yanaweza kuonekana kama mashambulizi ya moyo au kiharusi.

 

Utafiti umeonyesha kwamba watu ambao hukaa kwa zaidi ya saa nane kwa siku, haswa bila mapumziko ya mara kwa mara kwa shughuli za mwili, wanakabiliwa na hatari kubwa sana ya masuala ya moyo ikilinganishwa na wale wanaoishi maisha yenye shughuli zaidi. Tabia ya kukaa sana imeunganishwa na hatari kubwa ya hali kama vile unene na kisukari, yakizidi kuuathiri mwili.

 

Afya ya mfumo wa musculoskeletal inaathiriwa na kukaa kwa muda mrefu. Saa zilizotumiwa katika mkao zinaweza kuchangia mkao mbaya, maumivu ya mgongo, na ugumu. Ukosefu wa mwondoko huweka uzito usiohitajika kwenye uti wa mgongo na unaweza kusababisha kudhoofika kwa misuli ya msingi.

 

Afya ya akili na ustawi wa kihisia unaathiriwa vibaya na mtindo wa maisha wa kukaa sana. Shughuli za mwili husaidia kutolewa kwa endorphins, ongezeko la hali ya asili ya mwili. Wakati watu wanapotumia muda mrefu kukaa, wanakosa mabadiliko muhimu ya kuboresha hali hizi za kihisia. Kwa hivyo, mtindo wa maisha wa kukaa sana umeunganishwa na hatari kubwa ya sonona na wasiwasi.

 

Utambuzi unaokua wa madhara mabaya ya kukaa kwa muda mrefu unahitaji sisi kubuni upya kazi zetu/kujifunza mazingira na tabia. Miradi inayopendekeza meza zinazoweza kusimama, mikutano ya kutembea, na mapumziko ya mara kwa mara yanapata umaarufu. Kujumuisha shughuli za mwili katika mazoea ya kila siku, kama matembezi mafupi, mazoezi ya kujinyoosha, au kuchagua usafiri wa kutenda, vinaweza kupunguza athari mbaya za kukaa kwa muda mrefu.

 

Hatimaye, ujumbe kwamba “kukaa ni uvutaji mpya wa sigara” hutumika kama onyo ambalo tabia zinazoonekana kuwa za kawaida zinaweza kuwa na athari kubwa kwenye afya zetu. Tunahitaji kufanya kazi kwa bidii na kupanua misuli yetu kwa makusudi kwa hivyo tunahifadhi ustawi wetu wa kimwili na kihisia hata tunapofanya kazi kwenye meza zetu na/au kuhudhuria mikutano na vikao vingi na virefu. Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunaishi maisha ya kiafya na mafanikio zaidi, na hata kufanya maamuzi bora, kwa neema ya Mungu!

Hatimaye Miguel alikuwa “amefanikiwa.” Alikuwa ameoa na aliishi maisha ambayo serikali ilisema aishi, kuvuta sigara na kunywa pombe na kufundisha shuleni.

 

Nyumbani kwao Miguel ilikuwa ni Afrika, katika nchi ya Msumbiji. Wazazi wake walikuwa wakulima wa mazao kwa ajili ya familia karibu na Beira, ambapo mama, baba, kaka na dada zake wote walifanya kazi nyumbani. Anakumbuka siku zile za kuchunga ng’ombe, kukamua maziwa ya mbuzi, kubeba maji kutokea mbali kisimani na kuvuna mbogamboga kutoka kwenye shamba dogo la familia, machamba (mashamba) yao.

Yalikuwa ni maisha mazuri, lakini hakuona mstakabali ndani yake, isipokuwa angalau kwenda shule. Mara nyingi alibishana na wazazi wake, akiwasihi kumruhusu kwenda katika shule ya msingi ya Kikristo iliyokuwa karibu.

 

Mwishowe walimkubalia ombi lake, ijapokuwa ilikuwa ni uchaguzi ghali.

 

 

MWANZO WA UPADRI

Akijua kwamba wazazi wake walikuwa wakijinyima ili kulipa karo yake, Miguel alisoma kwa uaminifu na alijifunza kwa haraka. Baada ya miaka sita katika shule ya parokia, alifanya vizuri kiasi kwamba Padri wa Parokia alimwandikisha ili kujiunga na upadri. Miguel alifikiria kuwa ingekuwa ni kazi nzuri yenye kipato kizuri, hivyo alikubali. Baada ya mahafali alitumia miaka minne akijifunza kumtumikia Mungu akiwa kama kiongozi wa kiroho, ikifuatiwa na miaka miwili ya uanafunzi wa utawa ili kuwa padri.

 

Mara tu alipokaribia kuhitimu na kuanza kazi yake ya upadri, serikali mpya ilitawala Msumbiji. Mara moja, serikali ilitangaza dini kuwa “dawa ya kutuliza watu,” na kufunga makanisa yote. Ghafla, mipango thabiti ya Miguel ikaharibika!

 

Kwa vile hakukuwa na kazi za mapadri, Miguel akakubali kazi ya kufundisha katika shule ya umma na kwa haraka akagundua kuwa alipenda kuwa mwalimu.

 

“Nilioa na tukapata watoto wawili,” Miguel anakumbuka. “Cha kuhuzunisha, watoto wetu wote walifariki wakiwa wa wadogo. Walipofariki, tulitakiwa kwenda kwa mchawi mara nyingi ili kujua kwa nini walifariki na nani aliyesababisha vifo vyao. Kafara za mnyama, zilizohitajika ili kudhibiti hasira za mashetani, zilikuwa ghali sana! Lilikuwa jambo la uchungu kwangu na kwa mke wangu mdogo.”

 

Kwa kipindi hiki chote Miguel alikuwa akinywa na kuvuta sigara na kuishi maisha ya mwituni, kama serikali ilivyosema kuwa ndivyo vizuri kuishi.

 

 

SWALI LA UDADISI

Siku moja baada ya madarasa, mwanafunzi mmoja mdogo alikuja kwenye dawati la Profesa Miguel na kuomba ruhusa ya kuuliza swali. “Hakika,” profesa alijibu. “Ungependa nini?”

 

“Profesa,” mwanafunzi alitabasamu. “Je, umewahi kufikiria kuhusu kuacha kuvuta sigara?”

 

Swali hilo lilimfanya Profesa Miguel akasirike. “Kwa nini unaniuliza hivyo, kijana?”

 

“Kwa sababu Profesa, ungekuwa mwalimu mzuri zaidi ikiwa ungekuwa hukohoi sana.”

 

Profesa Miguel alicheka na kumfanya kijana aondoke.

 

Baada ya majuma machache, kijana yule alikuja tena kwenye dawati la mwalimu.

 

“Profesa,” mwanafunzi alisema, “Je, umewahi kufikiria kuhusu kuacha kunywa pombe?”

 

Kwa mara nyingine tena, swali lilimfanya Profesa Miguel akasirike. “Kwa nini unaniuliza hivyo, kijana?”

 

“Kwa sababu wewe ni mwalimu mzuri zaidi ukiwa mtulivu.”

 

“Nilifahamu kwamba kunywa na kuvuta sigara viliharibu afya yangu na furaha yangu, lakini sikujua jinsi ya kuacha. Hivyo, nilimtazama mwanafunzi na kusema, NDIYO! Je, unaweza kunisaidia kuacha?”

 

“Hapana, siwezi,” mwanafunzi alisema. “Lakini njoo pamoja nami na nitakupeleka kwa mtu mmoja anayeweza kukusaidia kubadilika.”

 

 

NJOO PAMOJA NAMI

Mwanafunzi alimchukua Miguel mbali na mji katika kibanda kidogo na kumtambulisha kwa mchungaji kijana wa Waadventista wa Sabato aliyekuwa akiishi pale.

 

“Ungependa nikufanyie nini?” mchungaji aliuliza.

 

“Ninahitaji kuacha kuvuta sigara na kunywa pombe,” Miguel alijibu.

 

“Je, hayo ni yote?” mchungaji alicheka. “Tunaweza kulishughulikia hilo mara moja. Hili ni rahisi. Njoo ndani.”

 

“Mchungaji kijana hakuwa na kitabu chochote au dawa maalum au chochote ambacho kingenifanya nifikiri kuwa alikuwa mshauri mwenye hekima ambaye angeweza kunisaidia kufanya lisilowezekana,” anasema Miguel. “Niliuliza kuhusu usuli na shule aliyosoma. Mtu yule alicheka na kusema kwamba alihitimu elimu ya msingi tu, hakukaribia hata ya elimu niliyokuwa nayo. Kisha nikacheka kwa nguvu, nikifikiri kwamba nilikuwa mpumbavu kumwamini mtu mjinga kwamba angeweza kunisaidia.”

 

Mchungaji alimwomba Miguel ajiunge pamoja naye, watu hao wawili wakapiga magoti katika sakafu ya kibanda.

 

“Aliniombea,” Miguel anasema. “Ombi lilipokwisha, aliniambia kuwa matamanio yangu ya kuvuta sigara na kunywa pombe yaliondoka kabisa. Kisha akaniambia nikae chini.”

 

“Ilifuata sehemu ngumu,” mchungaji kijana alizungumza huku akifunua Biblia, “Sasa ninahitaji kukufundisha kuhusu Yesu.”

 

Licha ya mafundisho yake, Miguel hakuwa amewahi kushika Biblia. Kwa saa iliyofuata, mchungaji Mwadventista alimwonyesha vitu kuhusu Yesu ambavyo hakuwa amewahi kuvisikia au kuvifikiria.

 

Akirudi nyumbani mchana ule, Miguel alipita katika baa alipokuwa akienda baada ya kutoka shuleni, lakini hakuwa na matamanio ya kuingia ndani. Upendeleo wake wa tumbaku na pombe kwa hakika uliondolewa!

 

Nyumbani, mke wake aliuliza kwa nini hakuwa akivuta sigara. Kisha akamuuliza kama angependa kunywa pombe kabla ya chakula cha jioni.

 

“Ilikuwa ni vigumu kumweleza ukweli,” Miguel anakumbuka, “kwa sababu nilijua kuwa angekasirika kwamba nimekuwa nikizungumza na Waadventista wa Sabato wenye kuchukiza na wenye wazimu.”

 

 

MTU ALIYEBADILIKA

“Nani aliyekupeleka?” aliuliza. “Waadventista ni watu wapumbavu! Hupaswi kwenda huko tena!”

 

Lakini Miguel hakutii. Aliendelea kwenda kisirisiri kwenye nyumba ya mchungaji, akisoma Biblia pamoja naye na kumwacha Mungu ambadilishe maisha yake.

 

“Maisha yangu yaliendelea vizuri mpaka baada ya miezi kadhaa baadaye mke wangu aliniuliza kwa nini nilikuwa tofauti. Nilipokiri kuwa bado nilikuwa nikikutana na mchungaji Mwadventista, aliniomba ikiwa angekuja pamoja nami. Miezi mitatu baadaye, mke wangu na mimi tulibatizwa pamoja katika Sabato moja. Hiyo ilikuwa ni siku bora katika maisha yetu yote!”

 

Miguel na mke wake wakawa viongozi imara katika kanisa lao mahalia. Baada ya mafunzo ya ziada, Miguel aliwekewa mikono akiwa kama mchungaji wa Waadventista wa Sabato na kuwa kiongozi imara wa kanisa na elimu huko Afrika Kusini. Aliponiambia kisa hiki, nilimwomba anitambulishe kwa mwanafunzi mdogo aliyezungumza naye baada ya darasa.

 

“Samahani, Mchungaji Dick,” Mchungaji Miguel alikunja uso. “Wakati mke wangu nami tulimwomba mchungaji kijana kututambulisha kwa mwanafunzi aliyenipeleka nyumbani kwake, alionekana kuchanganyikiwa. “Hakuna aliyekuleta. Ulikuja mwenyewe,” alisema.

Moja ya vitu vyangu ninavyovipenda kuhusu majira ya kuchipua na kiangazi ni maua yote yanayochanua; wewe je? Karibu na ninapoishi, Washington, D.C. inaonyesha kipindi kizuri cha majira ya kuchipua ambapo miti 3,750 ya cheri karibu na Tidal Basin inachanua, na mandhari ya vivutio kihistoria vya Marekani vinavyoheshimu historia ya Marekani vyote viko kwa umbali wa kutembea.

 

Wazo la kupanda miti ya cheri lilianzishwa na Eliza Scidmore mnamo mwaka 1885, alipotetea kupanda miti ya cheri ya Kijapani huko Washington, D.C. Mnamo mwaka 1906, David Fairchild aliingiza na kupanda miti 75 ya cheri kuona kama ingechanua katika hali ya hewa hiyo, na kwa hakika ilichanua! Meya wa Tokyo wakati huo, Yukio Ozaki wa Jiji la Tokyo, aliamua kutuma miti 3,000 kama zawadi kwa jiji la Washington, D.C. mnamo mwaka 1912, kusherehekea urafiki unaoongezeka kati ya nchi hizo mbili.

 

Je, wajua kwamba tunaweza kuchanua kwa ajili ya Yesu popote tulipopandwa, kama vile miti ya cheri ya Kijapani? Ikiwa tunakubali zawadi ya upendo ambayo Yesu anataka kupanda mioyoni mwetu, upendo Wake utakua na kuchanua kupitia maneno na matendo yetu. Tunaweza kuonyesha upendo wa Mungu kwa njia za vitendo kupitia maneno na matendo yetu ya fadhili.

 

Basi, ilikuwa mwisho wa juma wenye shughuli nyingi na miti ya cheri ikichanua kwa wingi, mume wangu na mimi tulijiunga na marafiki kadhaa kwenda kuona maua kwa macho yetu. Vema, sio sisi pekee tuliokwenda kuiona miti ya cheri mchana huo. Kila mwaka, zaidi ya wageni 700,000 wanakwenda eneo hilo kustaajabia uzuri wa matumba yenye rangi ya waridi na petali!

 

Baada ya kutembea kwa muda na kupiga picha nyingi nzuri za miti kutoka pembe nyingi tofauti, tuliamua kutafuta mahali pa kukaa na kupumzika na kuangalia picha zetu. Nilifurahi kupata benchi tupu kati ya umati na kwa haraka nililifanya kuwa mali ya kikundi chetu. Nilipofika kwenye benchi, niliona mkoba mdogo ukingoni lakini sikumwona yeyote karibu ambaye angeweza kuwa mmiliki. Nilidhani labda mtu alikuwa anahifadhi nafasi, lakini sikumwona yeyote akija kwenye benchi. Kisha nilifikiri jinsi ambavyo ningehuzunika ikiwa ningepoteza mkoba wangu.

 

Rafiki zangu na mimi tulijadili hali hiyo na ni nini tungefanya. Tukaamua kutafuta ndani ili kuona kama kuna kitambulisho au namba ya simu ambapo tunaweza kuwasiliana na mmiliki. Pia tulitazama kote ili kuona ikiwa tutaona mtu ambaye alionekana kutafuta kitu kilichopotea. Hatukumwona, lakini kulikuwa na mkoba na Leseni ya Dereva, fedha, kadi za benki, na vinginevyo, ambapo ilinifanya nijisikie vibaya hata zaidi kwa mmiliki. Tukaamua kuomba kwa ajili ya mwongozo na msaada wa kurejesha mkoba huu kwa mmiliki wake. Ikiwa tusingeweza kufanikiwa baada ya dakika 20, tungejaribu kuupeleka katika vitu vilivyopotea na kupatikana.

 

Macho yangu yakizuru nyuso za umati wa watu wanaopita, ghafla niliona uso ambao ulionekana kama picha kwenye Leseni ya Dereva, na alipokuwa akikaribia kwetu, nilikuwa na uhakika kuwa, kweli, huyu alikuwa mmiliki wa mkoba huu. Kitu pekee kisichoeleweka ilikuwa ni kwamba, hakuonekana mwenye kutafuta kitu chochote; alikuwa tu akicheka na kuzungumza na rafiki zake walipokuwa wakitembea. Tukamwendea mwanamke na kumwita kwa jina lake. Alituangalia kwa mshangao kwa sababu tulikuwa wageni.

 

Kisha tukamwambia kwamba tulipata mkoba wake kwenye benchi lililokuwa karibu. Aliduwaa alipotambua kuwa, kweli, alikuwa amepoteza mkoba wake. Alishukuru sana! Alikuwa akitembelea kutoka nje ya mji na alifurahi sana kuwa na kitambulisho chake na kila kitu kingine kwenye mkoba wake. Asingeweza kusafiri kurudi nyumbani bila kitambulisho chake na aliendelea kutushukuru.

 

Tukamwambia kwamba Mungu alijibu maombi yetu na kwamba tulikuwa tumeomba kwa kutaja jina lake! Aliguswa na alikuwa akishukuru tu. Tulijisikia wenye ahueni kwa ajili yake na tulishukuru kwamba tulikuwa na uwezo wa kumwonyesha upendo wa Mungu kwa njia ya vitendo. Natumai mbegu ya upendo wa Mungu tuliyopanda siku hiyo itakua na kuchanua katika maisha yake.

 

Mungu anajua tunachohitaji hata kabla hatujajua, kitu ambacho ni cha kuvutia sana! Ninakupa changamoto ya kutafuta njia za kuonyesha upendo wa Mungu kwa njia za vitendo na kuchanua kwa ajili ya Yesu leo!

Mchapishaji

Jarida la Adventist World, jarida la kimataifa la Kanisa la Waadventista wa Sabato. Konferensi Kuu, Divisheni ya Asia Pasifiki ya Waadventista wa Sabato ndio wachapishaji.

 

Mkurugenzi Mtendaji/ Mkurugenzi wa Huduma za Adventist Review

Justin Kim

 

Meneja wa Uchapishaji wa Kimataifa

Hong, Myung Kwan

 

Kamati ya Uratibu ya Jarida la Adventist World

Yo Han Kim (chair), Tae Seung Kim, Hiroshi Yamaji, Myung Kwan Hong, Seong Jun Byun, Dong Jin Lyu

 

Wakurugenzi wenza/ Wakurugenzi, Huduma za Adventist Review

Sikhululekile Daco, John Peckham, Greg Scott

 

Wahariri waliopo Silver Springs, Maryland, Marekani

Enno Müller, Beth Thomas, Jonathan Walter

 

Wahariri waliopo Seoul Korea
Hong, Myung Kwan; Park, Jae Man; Kim, Hyo-Jun

 

Mkurugenzi wa Mambo ya Kidijitali

Gabriel Begle

 

Mkurugenzi wa Muungano wa Mifumo na Uvumbuzi

Daniel Bruneau

 

Meneja wa Shughuli

Merle Poirier

 

Mratibu wa Tathmini ya Uhariri

Marvene Thorpe-Baptiste

 

Wahariri /Washauri wengine

E. Edward Zinke

 

Meneja wa Fedha

Kimberly Brown

 

Mratibu wa Usambazaji

Sharon Tennyson

 

Mratibu wa toleo la Kanda (Adventist World)

Penny Brink

 

Bodi ya Utawala

Yo Han Kim, chair; Justin Kim, secretary; Hong, Myung Kwan; Karnik Doukmetzian; SeongJun Byun; Hiroshi Yamaji; Joel Tompkins; Ray Wahlen; Ex-officio: Paul H. Douglas; Erton Köhler; Ted N. C. Wilson

 

Maelekezo ya Usanifu na Muundo

Types & Symbols

 

Kamati ya Adventist World ya Divisheni ya Afrika Mashariki – Kati:

Blasious Ruguri, Musa Gideon Mitekaro, Tom Ogal, Emanuel Pelote.

 

Tafsiri

Ufunuo Publishing House, South Tanzania Union Conference.

 

Msomaji wa prufu

Lilian Mweresa

 

Usanifu wa toleo la Kiswahili

Daniella Batista, Ashleigh Morton, Digital Publications

 

Uchapishaji wa Kidijitali

Charles Burman, Digital Publications (www.digitalpublications.co.za)

 

Muelekeo wa Sanaa na Ubunifu

Mark Cook, Brett Meliti, Ivan Ruiz-Knott

/Types & Symbols

 

Kwa Waandishi: Tunakaribisha miswada huria. Tuma barua zote kwa uhariri kwa 12501 Old Columbia Pike, Silver Spring, MD 20904-6600, U.S.A. Faksi ya ofisi ya Uhariri ni: (301) 680-6638

 

Waraka pepe: worldeditor@gc.adventist.org

Tovuti: www.adventistworld.org

 

Rejea zote za Biblia zimechukuliwa kutoka kwenye Swahili Union Version Bible Toleo la Chama cha Biblia la mwaka 1952.

 

Jarida la Adventist World linachapishwa kila mwezi na kuchapwa kwa wakati huo huo huko Korea, Brazili, Indonesia, Australia, Ujerumani, Austria, Ajentina, Meksiko, Afrika Kusini, na Marekani.

 

Vol. 20, Na. 6

Swipe left

swipe left To move to the next page

Swipe right

swipe right To move to the previous page
Allow Send-it to use cookies?

Send-it uses cookies to track how you use the application. Find out more about what data we collect and how we use the data in our privacy policy.