powered by
send-it.me

Adventist World-Kiswahili inamshukuru kila aliyejisajili kwa ajili ya jarida hilo, kupitia kwa chaneli ya WhatsApp. Tumefurahia kupokea jumbe kutoka kwako, na vilevile ushuhuda wa jinsi umetumia jarida hili linalotia moyo kuwafikia wengine kwa ajili ya Kristo!

Tungependa kukujulisha kuwa tunahamia jukwaa jipya katika mwaka mpya. Zaidi ya yote, tungependa uhame pamoja nasi. Adventist World-Kiswahili haitaki kumwacha nyuma yeyote aliyejisajili.

 

Badala ya kupokea ujumbe wa WhatsApp pamoja na toleo jipya kila mwezi, tunakupa kiungo kwa tovuti ya bure ambayo ni nzuri kwa simu, ambapo unaweza kuyasoma makala yote, kama kawaida. Chaneli ya WhatsApp na tovuti mpya zitafanya kazi kwa wakati mmoja kwa miezi kadhaa kabla ya kuhamia hatimaye kwa chaneli mpya.

 

Pia tutakiweka kiungo hicho kwenye ukurasa wa Facebook wa Adventist World-Kiswahili kila mwezi, ambapo unaweza kututumia jumbe na taarifa kuhusu jinsi makala hii inakufaidi wewe na jamii yako. Pia unaweza kututumia maoni na mapendekezo tutakayoangalia jinsi ya kuifanya makala hii iwafae zaidi wasomaji!

Ukipenda, unaweza kutuma baruapepe:
charles@digitalpublications.co.za

Moja ya manufaa ya tovuti mpya ya Adventist World-Kiswahili ambayo ni nzuri kwa simu, ni kwamba kutakuwa na lugha zingine nyingi za kuchagua, ikiwa ungependelea Kiingereza au lugha nyingine yoyote, unaweza kuangalia kama ipo, kando na ile ya kawaida ya Kiswahili.

 

Manufaa mengine ni kwamba ni rahisi kushiriki kiungo hicho kipya cha Adventist World-Kiswahili, kwa marafiki na familia. Tunakuhimiza ufanye hivyo, kwa sababu tayari inafanya kazi. Hebu iangalie sasa hivi.

 

Tunatumai kuwa na uhusiano mrefu na wa furaha na wasomaji wa Adventist World-Kiswahili.

 

Mungu akubariki,

 

Kundi la Adventist World-Kiswahili

Tunaamini katika nguvu ya maombi, na tunakaribisha hitaji la maombi ambayo tutashiriki katika ibada ya watendakazi kila Jumatano asubuhi. Tuma maombi yako kwa prayer@adventistworld.org, na utuombee tunapofanya kazi pamoja kuendeleza ufalme wa Mungu.

 

Picha ya jalada: Vitaliy Gavrushchenko

Ingawa tamaduni za Magharibi kwa kiasi kikubwa zina usawa zaidi, bibi arusi wa Magharibi ndiye mlengwa zaidi. Anavaa mavazi meupe ya kifahari. Yeye ndiye wa mwisho kuingia ukumbini, akisindikizwa na baba yake, huku watu wengine wote wakiwa wamesimama. Yeye ndiye kivutio kikuu cha sherehe.

 

Katika tamaduni za Mashariki, ambazo kwa ujumla ni za mfumo dume kuliko za Magharibi, bibi arusi huwa kivuta macho sambamba na bwana arusi. Wote wawili huvaa mavazi ya rangi maalum za kuvutia. Kutegemeana na utamaduni, bwana arusi, bibi arusi, au wote wawili wana namna ya kimila ya kuingia. Na, katika baadhi ya makabila, bwana arusi ndiye kivutio kikuu.

 

Ikiwa na ufanano zaidi na aina hiyo ya pili ya ndoa, taswira ya arusi za Agano Jipya, kama vile za msimamizi wa bwana arusi na bibi-arusi, zinatumika kama kielelezo cha huduma.

 

Yohana 3:28–30 inarejelea rafiki wa Bwana Arusi, ambaye anasimama, kusikia, na kufurahi kwa sababu ya Sauti ya bwana arusi. Taswira hii ya Msimamizi wa Bwana arusi inaelekeza kwenye huduma ya Yohana Mbatizaji, aliyeishi nyikani, akivaa manyoya ya ngamia, na kula asali na nzige. Alikuwa akiwatayarisha watu kwa ajili ya Masihi, akihubiri “ushuhuda wa moja kwa moja,” na kuwataka watu watubu. Sifa moja ya huduma ya Msimamizi wa Bwana arusi ilikuwa unyenyekevu wake (Marko 1:7). Kusudi lake maishani lilikuwa kuona bwana arusi akiongezeka na yeye kupungua (Yohana 3:30).

 

Waefeso 5:23-26 na Ufunuo 19:7-9 humwonyesha Kristo kama Bwana Arusi, na kanisa kama Bibi-arusi. Pamoja na 2 Wakorintho 11:2, vifungu hivi vinasisitiza usafi wa Bibi-arusi na haja yake ya kuvaa haki safi ya Kristo.

 

Sasa kielelezo hiki kina mapungufu yake, lakini majukumu haya mawili yana ulinganifu wa kisasa. Kazi inayojitegemea inafanana sana na msimamizi wa bwana arusi, yaani, huduma ya Yohana Mbatizaji. Kazi hii, pamoja na kazi ya Bibi-arusi, ambaye ni kanisa, inaweza kufanya mambo ya utukufu kwa ajili ya injili. Kanisa linafanya kazi katika nafasi yake kama shirika na chombo cha kifedha na kisheria katika nchi nyingi za ulimwengu ili injili ihubiriwe. Lakini maeneo mengine yapo ambapo kazi ya kujitegemeza inakamilisha, hata zaidi, kazi ya Yesu kwa sababu kanisa lililopangwa linaweza kuwekewa vikwazo. Wakati wawili hao wanafanya kazi kwa upatano, kuna furaha ambayo hakuna mtu anayeweza kupata peke yake.

 

Katika harusi, msimamizi wa bwana arusi hakupaswa kuwa bibi-arusi. Msimamizi wa bwana arusi hakupaswa kutafuta kuwajenga wanafunzi wake mwenyewe. Badala yake, hakuwa na furaha zaidi ya kuwapeleka kwa Bwana arusi. Wala hakumwita Bibi-arusi “kahaba wa Babeli,” pia. Alijua upendo ambao Bwana arusi alikuwa nao kwa Bibi-arusi na alifanya kila kitu ili kuhakikisha ndoa yenye mafanikio. Lengo lake pekee lilikuwa kwa muungano wa Bibi-arusi na Bwana Arusi.

 

Vivyo hivyo, Bibi-arusi hakuepuka kazi ya Msimamizi wa Bwana arusi. Hakudhibiti kila kipengele cha huduma ya Msimamizi wa Bwana arusi. Hakumpiga marufuku kutoka kwa sherehe kwa sababu alitaka Bwana arusi awe wake peke yake. Hakumkashifu Msimamizi wa Bwana arusi, kwa maana alijua kuwa ndiye Msimamizi wa Bwana arusi.

 

Washiriki wote wawili walizunguka karibu na Bwana Arusi, nyota ya Harusi Kuu. Je, msimamizi wa bwana arusi na bibi-arusi wanaendeleaje leo? Na tunakaza macho yetu kwa Yesu, Bwana Arusi wetu?

Mnamo 1952, Paul Sigira alikuwa na ndoto ambayo hatimaye iligeuka kuwa ukweli. Alitoa ardhi kwa ajili ya kanisa la Waadventista na shule kwenye eneo lake. Leo, wanafunzi kama Sharon Ngatia wanayo fursa ya kuhudhuria Shule ya Waadventista ya Kimogoro huko Kimogoro, Kenya.

“Tumetumwa na Mungu kupanua makanisa yetu ili tuwafike watu wote. Kwa neema ya Mungu, tunatumaini kwamba tunao watu walio tayari kufanya mambo makubwa sio tu katika ngazi mahalia lakini hata mwisho wa nchi.”

—Bruno Ruso, makamu mwenyekiti wa Divisheni ya Amerika Kusini, kuhusu mpango wa kuzingatia upya dhamira ya Divisheni kwa lengo la utume. Programu hii ilianzishwa kwa watu waliotayari kubakia katika eneo la utume kwa mwaka mmoja au zaidi. Washiriki watachaguliwa na kufundishwa mwaka 2024 na watatumwa mnamo mwaka 2025 ili kuyafikia mahitaji ya Divisheni nyingine ulimwenguni.

Zaidi ya 370

Idadi ya watu waliobatizwa katika kanisa la Waadventista Cúcuta, Kolombia kutokana na Mkutano wa kiinjilisti uliofanywa na Robert Costa, Msemaji na mkurugenzi wa Escrito está (It Is Written / Imeandikwa). Mkutano huo ulifanyika Oktoba 14-21, na mada kuu ilikuwa “Never give up, There’s Still Hope [Kamwe Usikate Tamaa, Bado Liko Tumaini].” Mkutano huu ulikuwa ni miongoni mwa mikutano mikubwa ya kiinjilisti yenye msukumo wa kuihubiri injili katika nchi yote. Baada ya mianzo ya awali katika Union ya Kasakazini mwa Kolombia, msafara wa wainjilisti ulielekea kwenye Union ya Kusini mwa Kolombia katika mji wa Ibague. Watu 128 walibatizwa kutokana na mikutano hiyo.

Kuhudhuria Kanisa Bila Kuwepo Hapo Kibinafsi

Washiriki wa kanisa waliulizwa ni mara ngapi wamehudhuria kanisa bila kuwepo hapo kibinafsi iwe ni kwa redio, TV, au kwa mtandao katika miezi 12 iliyopita.

“Kwa kutambua  hali ya sasa (ya Marekani) ya siasa za upendeleo na mifarakano ya kijamii, lengo letu la mkutano lilikuwa ni kutilia mkazo wa jinsi sisi kama Wakristo tunavyopaswa kupinga roho ya uhasama na kuendelea kuishi na kutumika kama mabalozi wa Kristo.”

—Melissa Reid, mkurugenzi mwenza wa huduma kwa jamii na uhuru wa dini wa Divisheni ya Amerika Kaskazini, alishiriki siku mbili za matukio ya uhuru wa dini. Mkutano ulilenga katika hali ya sasa ya uhuru wa dini na sehemu yake katika unabii wa Biblia na waligundua njia za kuzuia mgawanyiko wa kisiasa kote Marekani na kwenye makanisa.

“Tunahitaji kurudi nyumbani tukiwa tumehamasishwa kufanya mabadiliko na kuongeza ubunifu zaidi, ugunduzi, na ushirikiano katika kanisa la Waadventisha wa Sabato. . . . Tusingependa tukio hili liwe tu kama warsha lakini liwe ni mkusanyiko wa hotuba za kutia moyo zitakazowapa nguvu kufanya zaidi kwa ajili ya utume wa kanisa.”

—Abel Marquez, mkurugenzi wa mawasiliano kwa kanisa katika Divisheni ya Marekani Kati (IAD), akizungumza na mkusanyiko mkubwa wa mkutano wa mawasiliano wa Divisheni, uliofanyika Miami Novemba 7-8, Florida, Marekani.

“Mungu anataka tuyafurahie maisha ya umilele hapa na sasa. Hii haimaanishi kwamba tunatarajia kuishi hapa milele, katika maisha haya sasa. Tunatarajia na kupiga mbiu ya ujio wa Bwana ulio karibu. Lakini inamaanisha kwamba tunaweza na tunatakiwa kuzishiriki na kuziishi kanuni za upendo za ufalme Wake, hapa na sasa, kila siku na kwa kila mtu.”

—Mario Brito, mwenyekiti wa Divisheni ya Ulaya ya kati (EUD), alishiriki katika mkutano wa mwisho wa mwaka. Wajumbe wa halmasahuri kuu ya EUD walizipigia kura nyaraka zilizoweka mkazo kwenye matumizi ya teknolojia, habari na mawasiliano katika kuitegemeza kazi ya Mungu.

Zaidi ya 300

Idadi ya vijana waliojiunga kutoka katika maeneo yote ya Bulgaria kwa ajili ya mkutano wa kitaifa wa vijana uliofanyika kuanzia Novemba 3 hadi 4. Mada kuu ya tukio hilo ilikuwa “God’s Got Talent,” na wakati wa tukio vijana waligundua vipaji vyao na uwezo wao kwa ajili ya kumtumikia Mungu. Walishiriki kwenye warsha na kuvutiwa na  mahubiri.

70

Idadi ya watu waliopokea huduma ya upasuaji wa macho bure kupitia hospitali ya La Carlota (HLC) katika Chuo Kikuu cha Montemorelos, Nuevo Leon, Meksiko. Kampeni ya upasuaji wa macho ya siku tatu iliyofanyika katika taasisi ya macho HLC’s. Mbali na upasuaji 40 wa mtoto wa jicho na matitabu 30 ya retina za macho ulifanyika, upasuaji zaidi ya  watu 120 wamepangiwa ratiba ya upasuaji wa mtoto wa jicho bila gharama yoyote hadi Januari, na kuleta alama za matumaini kwa watu wanaosumbuka na matatizo haya. Hatua zote za awali za matibabu ya macho zilifanywa na timu ya wabobezi wa macho kutoka Taasisi ya Macho, waliojitolea muda wao na ujuzi wao katika mpango huo.

Makumi ya maelfu ya waumini wa kanisa la Waadventista wa Sabato, viongozi, na wageni maalum walimshukuru Mungu kwamba mvua iliyotabiriwa ilicheleweshwa walipokutana ili kusherehekea miaka 100 ya uwepo wa Waadventista Mashariki mwa Nigeria huko Aba, Jimbo la Abia, Novemba 4. Watu waliokuja kuabudu walijaza kila kiti kilichopatikana katika Uwanja wa Kimataifa wa Enyimba, na maelfu zaidi walifuatilia shughuli hiyo kutoka nje ya ukumbi huo.

 

Wageni maalum kutoka Konferensi Kuu walikuwa ni pamoja na Mwenyekiti Ted N. C. Wilson, mweka hazina Paul H. Douglas, mweka hazina mwenza George Egwakhe, na wake zao. Gavana wa Jimbo la Abia Alex Chioma Otti, ambaye ni mshiriki Mwadventista, na wawakilishi kutoka imani nyingine pia walikuwa miongoni mwa wageni maalum.

 

Maarufu miongoni mwa wageni maalum ni aliyekuwa gavana wa Jimbo la Abia Okezie Victor Ikpeazu, ambaye pia ni Mwadventista, jambo ambalo Wilson aliliongelea. “Sidhani kama nimewahi kuzungumza na hadhira ambapo gavana wa sasa na gavana wa zamani ni Waadventista wa Sabato,” Wilson alisema. “Ninyi wawili, mkifanya kazi pamoja kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, mnaweza kuleta maendeleo makubwa ya ajabu na mapatano ili kuwasaidia watu wa Jimbo kuu la Abia. Nataka kuwaombea ninyi wawili.”

 

“Ndugu na dada, tunakaribia nyumbani; Yesu anakuja upesi!” Wilson aliuambia umati mwanzoni mwa ujumbe wake. “Ibilisi atajaribu kufanya chochote anachoweza ili kuvuruga msimamo wako, lakini Mungu ana utume maalum kwa ajili yenu nyote. Umechaguliwa kwa ajili ya utume.”

 

 

VUTA KILA MTU KWA YESU

Wilson aliwataka washiriki kutafakari maana ya maneno ya Yesu katika Yohana 12:32, ambapo alisema, “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta watu wote Kwangu.” Hii sio kauli ya majigambo, Wilson alieleza. “Ni habari ya wokovu kupitia kwa Bwana wetu Yesu Kristo pekee. Ni agizo kwetu kufuata katika utume wa kazi” kila mahali, Wilson alisema.

 

Pia alitaka watu kuzingatia huduma ya patakatifu katika Agano la Kale, ambapo kila kitu kiliwakilishwa na kuakisiwa kwa njia ya Yesu. “Huduma ya patakatifu, pamoja na vipengele vyake vyote, [na] uchinjaji wa mwana-kondoo asiye na hatia . . . ulimwakilisha Yesu. Damu ambayo ilimwagwa wakati huo, iliwakilisha damu ya Yesu. Kuhani mkuu ambaye alienda kufanya upatanisho mbele za Mungu . . . Yesu pia ambaye ndiye Kuhani wetu mkuu. Yesu ni kila kitu kwetu katika mambo yote,” Wilson alisema. “Hatuna kisingizio cha kutookolewa kwa damu ya Yesu. Amefanya kila liwezekanalo ili tuwe pamoja Naye. Ni kazi yetu kuwaambia wengine kuhusu hilo. Kila mtu lazima asikie ujumbe huu. . . . Mwinue Yesu katika yote [yale] uyafanyayo.”

 

 

MACHO YALIYOKAZWA KWENYE LENGO

Kisha Wilson alinukuu ujumbe wa Paulo kwa Wafilipi, ambapo aliwaita waumini wasikengeushwe bali wasonge mbele. “Natenda neno moja tu, nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele, nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu [Flp. 3:13, 14],” Wilson alisoma, alipokuwa akimwita kila mshiriki kujihusisha katika “kilio cha mwisho” cha ujumbe wa Mungu kwa ulimwengu.

 

“Mungu anawaita kila mmoja wenu kumtazama Yesu, kukaza macho yenu kwenye lengo la mwisho.” Wilson alisema. “Tunashukuru kwa yale ambayo Mungu amefanya katika miaka hii 100. Lakini tumaini letu kuu ni kwamba hatuhitaji kusherehekea kumbukumbu ya miaka mia moja mingine. Hatimaye tunakaribia nyumbani.”

Makusanyiko mapya ya waumini Waadventista wa Sabato yanapata kutambuliwa kote katika Divisheni ya Amerika (IAD). Washiriki wanakusanyika katika maeneo mengine mbali na majengo ya kanisa. Ibada ya kuabudu haifuati utaratibu wa kawaida wa Shule ya Sabato ikifuatiwa na mahubiri. Hakuna viambatishi vya kanisa au hata nembo ya Kanisa la Waadventista wa Sabato inayoonekana. Lakini kuna uimbaji, ujumbe unaotolewa unaozingatia Biblia, na shughuli na matukio mahsusi siku ya Sabato na wakati wa juma.

 

Yakiitwa Makanisa Rafiki, makusanyiko hayo yanafuata mpango uliozinduliwa mnamo mwaka 2021, wakati viongozi wa Divisheni walipofikiria kuwafikia wasioamini katika maeneo mahususi katika maeneo ya mijini. Vikundi au makutano madogo yanasimamiwa na Kanisa la Waadventista katika konferensi au misheni ambapo wanahudumu.

 

 

KUFIKIA JAMII YA WASIOAMINI

Makanisa Rafiki hutafuta wanafunzi wa vyuo vikuu, wamiliki wa biashara, wenye taaluma, na watu ambao hawapendi kutembelea jengo la kanisa au kushiriki katika huduma rasmi ya kanisa, alisema Hiram Ruiz, mkurugenzi wa huduma za chuo cha umma cha IAD. Hawapendezwi na taratibu za dini. Mpango huo ulikuja baada ya tandavu ya UVIKO na kuangazia hitaji la kuwafikia waumini na wasioamini ambao hawapendezwi na aina yoyote ya kanisa la kidini, aliongeza. “Tuliona uhitaji wa kuandaa mahali pazuri ambapo wangeweza kuzungumza na kusikiliza mambo ya kiroho, bila muziki kuwa jambo kuu, kanuni mahsusi ya mavazi, bali kwa fursa ya wao kumwelewa Mungu maishani mwao.”

 

Kuna makutaniko 10 kamili ya aina hii kote huko Meksiko, Panama, Kolombia, na El Salvador. Mengi yamekuwa yakitoa huduma tangu mapema mwaka huu.

 

 

MBINU TOFAUTI

IAD ilikuwa eneo la kwanza la kanisa la ulimwengu kushiriki katika mpango mpya ulioandaliwa, alisema Kleber Gonçalves, mkurugenzi wa Kituo cha Utume Ulimwenguni kwa ajili ya Mafunzo kwa Wasiomjua Mungu na wa Kisasa katika Konferensi Kuu.

 

“Hii imekuwa njia tofauti kabisa na yale ambayo wachungaji wamefunzwa kwa kawaida katika kanisa letu,” Gonçalves alisema. “Mchakato wa kuwaongoza wengine kwa Kristo unaweza kuchukua muda mrefu zaidi kuliko viongozi wa kanisa au washiriki wanavyotarajia katika mazingira ya utamaduni wa Kanisa la Waadventista lakini hadi sasa umethibitika kuwa na ufanisi. Tumeona jinsi Mungu alivyokuza huduma ya kutafuta watu wenye mawazo ya kidunia wanaotafuta majibu,” alisema.

 

Kila moja ya Makanisa ya Kirafiki yaliyoanzishwa liko katika jiji kubwa lenye watu wasiopungua milioni 1. Makanisa yameundwa kuwa aina tofauti ya kanisa la Waadventista, na mbinu inayoendelea ya kufanya wafuasi, Ruiz alisema. “Imekuwa jambo la kustaajabisha kuona matokeo ya kiroho ambayo makutaniko hayo yanafanya katika maisha ya watu wengi wanaoishi katika majiji makubwa,” akasema.

 

 

HAKUNA HAJA YA KUJUA IDADI

Mafanikio ya mradi wa Kanisa Rafiki hayapimwi kwa idadi ya ubatizo, wageni kabisa, na wageni wa kawaida, Ruiz alisema. “Muungano huo, ukuaji wa kiroho wa kundi hilo hufanya kazi kupitia programu ya uanafunzi iliyozingatia muktadha tofauti, sio muundo wako wa utamaduni wa uinjilisti wa Kiadventista,” alisema. Hata hivyo, vikundi katika Makanisa ya Kirafiki hutoa zaka na matoleo yao na kutoa mchango katika muundo wa Kanisa la Waadventista ambalo wako chini yake, Ruiz alisema.

 

Sasa Kituo cha Utume Ulimwenguni kwa ajili ya Mafunzo ya Kidunia na ya Kisasa katika Konferensi Kuu na IAD wanafanya kazi katika kuweka pamoja kitabu cha mwongozo chenye jinsi ya kuchakata, mapendekezo, na matokeo yaliyopatikana kutoka kwa Makanisa Rafiki yaliyoanzishwa kote katika eneo hilo. Inatarajiwa kupatikana kabla ya mwisho wa 2024.

Familia zinazolala kwenye mahema na makazi ya muda baada ya tetemeko la ardhi la Septemba 8 katika Milima ya Atlas nchini Morocco tayari wanafurahia makazi zaidi ya kudumu kabla ya hali ya hewa ya baridi kushuka, viongozi wa Shirika la Maendeleo na Misaada la Waadventista (ADRA) nchini Uhispania walisema.

 

Tarehe 28 Oktoba ilikuwa siku ya kusherehekea kwa wote, kwani ADRA Uhispania ilishiriki katika makabidhiano rasmi ya funguo kwa familia 32 ambazo tayari zinamiliki makazi manane ya muda yaliyofadhiliwa kwa msaada wa mtandao wa kimataifa wa ADRA. Maafisa wa serikali ya Morocco pia walihudhuria hafla hiyo.

 

Daniel Abad, mratibu wa ADRA Uhispania nchini Morocco, alishuhudia hafla ya kukabidhi funguo na kusaini mikataba ya muda. Katika mikataba iliyotiwa saini, familia zinajitolea kutunza nyumba kwa muda wote watakaokaa, hadi vijiji vyao vitakapojengwa upya. Katika siku zijazo, vifaa hivi vitatumiwa tena kuwa nyumba, miongoni mwa matumizi mengine, shule au maghala ya ufundi ya ndani ambayo yanaweza kutoa kazi kwa wanawake katika eneo hilo, viongozi wa ADRA walisema.

 

 

ZAIDI YA NYUMBA ZILIZOTENGENEZWA KWA KUUNGANISHWA

“Nyumba hizi zilizojengwa awali na kisha kuunganishwa zilitengenezwa kwa namna nzuri ili kuzuia unyevu na joto zinakodishwa kwa muda mrefu mpaka pale watakapomaliza kujenga mji,” Abad alisema. “Baadaye, zitavunjwa na kupelekwa katika maeneo mengine ambapo ni muhimu kuweka shule au kuhifadhi nyenzo kutoka kwenye maghala.”

 

Abad aliongeza kuwa mitaa yote katika eneo hilo imejengwa kwa lami ili kwamba wakazi wasiathiriwe na mvua. ADRA imejumuisha vitanda vya maua, kituo cha choo cha jumuiya, na eneo la watoto. "Nyumba zote zinafuata taratibu za eneo hilo na zina umeme,” Abad alisema. “Na kila mtu anaweza kutumia jiko la jumuiya lililo na vifaa vyote.”

 

Mpango huo, uliotekelezwa kwa ushirikiano na shirika mahalia lisilo la faida, lilishuhudia nyumba zikipanda haraka kama siku mbili hadi tatu, viongozi wa ADRA walisema.

 

Mradi huu unajumuisha nyumba nane zenye ukubwa wa futi za mraba 172, ambazo ni pamoja na mabweni manne, vyoo, bafu na jiko la jumuiya katika kila moja.

 

 

ZAIDI YA WATU 4,000 WALIHUDUMU

ADRA Uhispania, kwa ushirikiano wa karibu na ADRA International, inaendelea kuratibu mwitikio wa dharura wa kibinadamu uliotokea katika Milima ya Atlas ili kukabiliana na matokeo ya tetemeko la ardhi la Marrakesh-Safi.

 

Awamu ya kwanza ya mwitikio huo ilihusisha uwekezaji wa dola za Marekani 150,000, ambao uliwezesha kusaidia moja kwa moja familia 812 na jumla ya watu 4,226 walioathirika. Katika wiki hizo nne za kwanza, ADRA ilisambaza jumla ya vifaa vya dharura 2,595 kwa jumla ya familia 519. Seti zilizogawiwa ni pamoja na chakula, blanketi na nguo za joto, tochi, soksi, sabuni za kujisafishia, pedi za wanawake, na wipes ambazo zinaweza kutumika mahali ambapo hakuna maji.

 

ADRA pia ilisambaza soksi za watoto na nguo za joto, pamoja na vifaa vya shule, ikiwa ni pamoja na mikoba, daftari, penseli za rangi, na kalamu.

 

 

MBUZI KWA FAMILIA 30

Mradi mwingine uliozinduliwa na ADRA ni utoaji wa mbuzi 150 na chakula cha kuwalisha kwa muda wa miezi miwili kwa jumla ya familia 30 katika vijiji vinne vilivyopo kwenye milima ya Atlas. Mradi huo, ambao ADRA ilianzisha kwa ushirikiano na shirika mahalia lisilo la faida, ulijumuisha uwekezaji wa takribani yuro 10,000.

 

Miradi hii, na mwitikio mzima wa kibinadamu uliotumwa nchini Morocco na ADRA, vinawezekana kutokana na ufadhili wa kujitolea wa washirika kadhaa, ADRA Uhispania ilisema. Ilijumuisha matawi mengine ya mtandao wa ADRA Kimataifa, ikiwa ni pamoja na ADRA Ujerumani, ADRA Japani, ADRA Australia, ADRA Ufaransa, ADRA Kanada, ADRA Uholanzi, ADRA Ubelgiji, ADRA Austria, miongoni mwa mengine mengi, walisema.

Divisheni ya Marekani Kusini (SAD) ya Waadventista wa Sabato itaongeza idadi ya wamishonari watakaotumwa katika maeneo mengine ulimwenguni, viongozi wa kanisa walisema. Lengo letu ni kushiriki Neno la Mungu, hasa ukweli wa ujio wa Yesu mara ya pili, katika maeneo ambayo kuna, Waadventista wachache au hawapo kabisa, walisema.

 

Viongozi wa kanisa walisema hatua ya kwanza ya mwelekeo huu ilifanyika mwaka 2015, wakati familia 25 zilipojiunga na programu ya kimishonari ulimwenguni, ambayo bado inaendelea. Programu hii karibuni itaingia katika hatua ya pili, kwa wingi wa rasilimali na fursa za watu wengi kuhudumia na kuitegemeza katika maeneo yanayohitaji msaada wa uenezaji wa Injili.

 

Mpango huu uliwasilishwa katika Mkutano wa mwisho wa Mwaka 2023 (SAD) ambao ulizihusisha nchi nane za Amerika ya Kusini, huko Brazili, Novemba 6. Na upanuzi ulio na lengo la kuimarisha Kulenga Upya Utume, ni msisitizo wa Waadventista unaotafuta kuwaandaa watumishi katika taasisi za Kiadventista, Maafisa wa ndani, na washiriki wa makanisa mahalia.

 

Viongozi walisema Kulenga Upya Utume kunaangalia watu walio tayari kukaa katika utume kwa mwaka mmoja au zaidi. Pia inatoa ziara fupi za utume kwa ajili ya mahitaji maaluum. Ili iwezekane kanisa la Waadventista wa Sabato litategemea rasilimali kutoka katika uongozi wa kanisa, na viongozi walitoa taarifa.

 

Wataradhia watachaguliwa na kufunzwa mwaka 2024 baada ya kuangalia vigezo vichache ikijumuisha maono wazi ya mmishonari, ujuzi wa lugha ya Kiingereza na afya ya kihisia. Wataradhia wamepangiwa ratiba ya kutumwa mwaka 2025 kuyafikia mahitaji ya divisheni zingine ambazo zimeshapeleka programu ambazo zinahitaji msaada.

 

 

JINSI INAVYOFANYA KAZI

Baada ya familia za kimishenari kuwasili katika eneo lao la kazi, watapewa muda wa miezi mitatu na kupata muda wa kuangalia mandhari ya mazingira na changamoto na kutafuta programu ambazo zimejifungamanisha na changamoto kuu za jamii hiyo, ambazo zitawasilishwa kwa SAD. Mapendekezo ya mradi yatapitishwa katika uchunguzi na kama yatakubaliwa baada ya miezi sita, itawaruhusu wamishonari kuwakaribisha watu wawili kujitolea kutoka kwa watu wa Kujitolea wa Huduma za Kiadventista (AVS).

 

Gharama za mahali pa kuishi, chakula na misharaha ya watu hawa wa kujitolea itatolewa na SAD. “Kazi ya utume katika fildi mara nyingi huwa ya upweke. Tunataka wanaume na wanawake waimarishe mahitaji muhimu yalioorodheshwa katika kila mkoa na kazi inayofanywa na wamishonari,” Alisema Dieter Bruns, katibu mwenza na mkurugenzi wa SAD AVS.

 

Mwaka mmoja baada ya familia ya wamishonari kuwasili katika eneo hilo, wanaweza kuwa tayari kupokea ziara moja au zaidi za utume, ama kutoka katika ofisi za kanisa au taasisi au kutoka kwa washiriki wa kanisa mahalia, viongozi walisema. Madhumuni ya ziara hizi ni kuwezesha na kuendeleza mipango iliyoanzishwa katika jamii, kama huduma katika maeneo mbalimbali ya mikutano ya injili.

 

 

KUJIANDAA MAPEMA

Lakini watu wengi watatoka wapi? Katika makanisa mahalia, Bruns alisema. ”Tunataka kila mshiriki aelewe changamoto za kiulimwengu na kukuza uhalisia huu kwa kujihusisha katika shughuli za kimishonari, ambazo mpaka sasa hazijawahi kuongelewa kwa kina” Bruns alisema.

 

Viongozi wa kanisa kwa sasa wanawatia moyo vijana pamoja na familia zao kuomba, kupanga na kuwezesha uenezwaji wa ujumbe wa kibiblia katika maeneo ambayo wanahitaji kusikia kuhusu Kristo. “Hii inaweza kufanywa kwa kuanza kushiriki katika shule za kimishenari, kwa kujihusisha katika maeneo mahalia na maeneo mengine lengwa na zaidi ya yote, kwa kujifunza lugha ya Kingereza ili iwe rahisi kujenga madaraja katika jamii na tamaduni nyinginezo,” Walisema.

Katika zulia la Kanisa la Waadventista wa Sabato, huduma zinazojitegemeza zinaibuka kama nyuzi mahiri, zikiongeza thamani na utofauti katika utume wa kanisa. Vyombo hivi vinavyojitawala, vikiwa huru kabisa na mfumo wa utawala wa uongozi wa kanisa, vinashiriki imani za msingi na maadili ya Uadventista, vikifanya kazi kwa upatanifu ili kuendeleza wito mkuu wa injili. Mizizi yao, utume, na malengo yao yanatofautiana kadiri ya mahitaji wanayokutana nayo, hata hivyo wote wanashiriki lengo moja: kuonyesha kielelezo cha upendo wa Kristo na kutangaza jumbe za malaika watatu wa Ufunuo 14:6-12.

 

 

UTUME NA LENGO

Lengo la huduma zinazojitegemeza ni kubwa sana na linatofautiana toka idara moja hadi nyingine. Hata hivyo, lengo kuu linabaki kukamilisha na kuongezea kazi ya kanisa la Waadventista wa Sabato katika kufikia jamii na watu binafsi, mara nyingi zaidi ya mbinu za kawaida. Huduma hizi, kwa mtindo wake wezeshi, hujishughulisha na elimu, afya, uchapishaji, vyombo vya habari, uinjilisti, na misaada ya kibinadamu. Zimefungwa na kusudi la pamoja: kuendeleza injili na kuwaandaa watu kwa ujio wa pili wa Yesu.

 

Lengo lao ndani ya Uadventista ni kufanya kazi kama chombo cha uvumbuzi kwa ajili ya utume. Wanajaribu kwa njia mpya za uinjilisti, na kuitika kwa haraka kwa mahitaji yanayotokea, na mara nyingi wanafika kwenye maeneo au idadi ya watu ambapo kanisa rasmi halijafika kwa kiwango kikubwa. Yanatumika pia kama maeneo ya kujifunzia kwa walei, ikiwawezesha kuchukua majukumu hai kwenye huduma na uinjilisti.

Uhusiano kati ya kanisa la Waadventista wa Sabato na huduma zinazojitegemeza ni kushirikiana. Huduma zinazojitegemeza zinatoa nyongeza nyumbufu na thabiti kwa mkakati rasmi wa kanisa. Mara nyingi ndiyo wahamasishaji wakuu kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa au kati ya makundi ya watu ambao hawajafikiwa. Kwa hivyo, kanisa hutoa msingi wa kiteolojia, mtandao wa kiulimwengu, na utambulisho wa pamoja unaoleta uaminifu na msaada kwa huduma hizi.

 

Kwa afya ya uhusiano huu, kunapaswa kuwe na roho ya ushirikiano na kuheshimiana. Viongozi wa kanisa wanahimizwa kutambua michango ya huduma zinazojitegemeza kama sehemu ya mwili wa Kristo, kuwezesha badala ya kudhibiti juhudi zao. Mawasiliano ya wazi na ushirikiano yanaweza kusababisha matokeo bora zaidi ya utume.

 

 

URITHI WA CHUO CHA MADISON

Huduma zinazojitegemeza zinaweza kurejelewa hadi mwanzoni mwa karne ya 20. Miongoni mwa waanzilishi mashuhuri zaidi katika jambo hili ni Chuo cha Madison, kilichoanzishwa mnamo 1904 huko Tennessee.

 

Waanzilishi E. A. Sutherland na Percy Magan, wakiongozwa na mashauri ya Ellen G. White juu ya elimu na uinjilisti, walitaka kuunda taasisi inayojitegemea. Madison akawa kinara wa uvumbuzi, akifanya kazi pasipo ufadhili wa kanisa, alilenga katika Ukristo wa vitendo, afya, mafunzo ya kilimo, na uinjilisti.

 

Mfano wa Madison uliwasha harakati. Wanafunzi na wafanyakazi, baada ya kuondoka Madison, mara nyingi walianzisha taasisi au huduma zinazojitegemeza zinazofanana, ambazo zilistawi kwa kanuni za kujitegemea na huduma ya Kikristo. Wimbi hili halikuwa uasi dhidi ya muundo wa kanisa, bali mwitikio kwa hitaji linalokua la mbinu mbalimbali za ufikiaji na uinjilisti.

 

Mbinu ya chuo cha Madison juu ya elimu na utume ukawa mwongozo kwa huduma nyingi zinazojitegemeza. Ilijumuisha kanuni kwamba kila mshiriki ni mtenda kazi, akifungamanisha kazi ya kiulimwengu na huduma ya kiroho. Roho ya Madison inasonga mbele leo kupitia kazi ya Adventist-laymen’s Services and Industries (ASi), ambayo inatambuliwa rasmi na Divisheni ya Amerika-Kaskazini (NAD) ya Kanisa la Waadventista wa Sabato.

 

ASi inafanya kazi kama idara ya NAD, ikihudumu kama idara jumuishi ya huduma zinazojitegemeza na wajasiriamali Waadventista. Ina jukumu muhimu katika kukuza umoja na ushirikiano kati ya idara mbalimbali zinazojitegemea. Uanachama wa ASi ni mfumo wa wafanyabiashara, wataalamu, na viongozi wa huduma wanaoshiriki ahadi moja kwa Kristo na ujumbe wa Waadventista.

 

Kupitia ASi, wanachama wanapata fursa za kuungana na watu, kufanya ushirika, na kushirikiana. Mikutano na vikao vya ASi ni vitovu ambapo mawazo hubadilishana na ubia huundwa. Kwa kutoa fursa hizi za kuchangamana na watu, ASi husaidia taasisi zenye nia kama hiyo kuunganisha juhudi zao ili kufikia matokeo makubwa katika kazi ya utume.

 

Katika safari ya pamoja ya utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato ulimwenguni, matawi ya kimataifa ya Adventist-laymen Services and Industries yanasimama kama washirika muhimu. Matawi haya si mashirika tu; ni jumuiya mahiri za waumini waliojitoa kueneza upendo wa Mungu katika mataifa yote. Kwa kushirikiana kwa karibu na taasisi za kanisa, wanaunda kisa cha imani na kujitolea ambacho kinaujaza ulimwenguni wote.

 

Kila tawi la ASi kote ulimwenguni linaakisi utajiri mbalimbali wa kanisa letu. Wanaelewa tamaduni za pekee wanazoshughulika nazo, wakibuni njia za kushiriki ujumbe wetu wa Waadventista unaogusa mioyo ya wenyeji huku wakishikilia kwa uaminifu imani zetu tunazoshirikiana.

Matawi haya ya kimataifa ni zaidi ya miundo ya usaidizi; ni washiriki hai katika utume wa pamoja. Kwa kuleta pamoja huduma zinazojitegemeza, yanaunda mtandao wa malengo ya pamoja, kuimarisha ufikiaji wetu wa watu kiulimwengu. Ushirikiano huu unaenda mbali zaidi ya mkakati; ni ushirikiano wa dhati unaoendeshwa na lengo moja la kushiriki injili. Huku ikiheshimu upekee wa kila huduma, ASis husaidia kuunganisha juhudi zake katika ukanda mpana wa utume wa kanisa.

 

Katika jukumu lake la ushauri, ASis ya kimataifa inatoa zaidi ya ushauri; inashiriki sauti na hadithi zilizo kitovu cha huduma, ikihakikisha kwamba mikakati yetu ya utume duniani kote inakidhi mahitaji na misukumo mahalia. ASis hufanya zaidi ya kukusanya rasilimali; inakuza moyo wa kushirikiana na imani ya pamoja, ikihimiza huduma kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kukua pamoja katika Kristo.

 

Juhudi za ushirikiano za ASis ya kimataifa ni sehemu muhimu ya masimulizi ya utume ya kanisa letu. Inaonyesha kujitoa kwetu kwa pamoja kueneza Neno la Mungu kwa njia mbalimbali na zenye maana, kufikia kila kona ya dunia na ujumbe Wake wa tumaini.

KUJIHUSISHA NA HUDUMA ZINAZOJITEGEMEZA

Viongozi na washiriki wa kanisa la Waadventista wa Sabato wanaweza kujihusisha na huduma zinazojitegemeza kwa njia kadhaa:

 

Ushirikiano katika Miradi: Makanisa mahalia yanaweza kushirikiana na huduma zinazojitegemeza kwenye miradi maalumu au mipango inayofungamana na utume na malengo ya kanisa. Juhudi hizi zinaweza kuleta rasilimali na utaalamu wa ziada kwa ufikiaji wa jamii, programu za afya, na kampeni za uinjilisti.

 

Mafunzo ya Pamoja: Washiriki wa kanisa wanaweza kunufaika katika programu za mafunzo zinazotolewa na huduma zinazojitegemeza, wakiimarisha ujuzi wao katika maeneo mbalimbali ya huduma na utumishi.

 

Uwekaji wa Mkakati: Wakati vyombo vya kanisa vinaposhiriki katika mpango mkakati, ikijumuisha huduma zinazojitegemeza katika majadiliano inaweza kuongoza katika mikakati jumuishi kwa ajili ya ufikiaji na uinjilisti. Huduma hizi zinaweza kuwa na uelewa wa msingi wa mahitaji ndani ya jamii na zinaweza kutoa maarifa muhimu.

 

Maombi na Msaada wa Kiroho: Maombi hayawezi kupuuzwa kama njia muhimu ya msaada. Kuomba kwa ajili ya mafanikio ya huduma hizi na kutambua changamoto na michango yake ndani ya kanisa kunahimiza mazingira rafiki.

 

Ushirikiano wa huduma zinazojitegemeza na kundi kubwa la kanisa lazima udumishe uwiano mzuri kati ya uhuru na umoja. Huduma hizi zinafurahia uhuru wa kuvumbua na kuendana na mazingira maalumu huku zikifungamana na imani, utume na viwango vya maadili vya Kanisa la Waadventista wa Sabato.

 

Ili kudumisha usawa huu, njia za wazi za mazungumzo na uwajibikaji ni muhimu. Huduma zinazojitegemeza zinaweza kufaidika kutokana na ushauri na msaada wa viongozi wa kanisa, na vivyo hivyo, viongozi wa kanisa wanaweza kupata mitazamo na mawazo mapya kutoka katika huduma hizi za ujasiriamali. Mabadilishano haya ya pande mbili yanakuza mazingira ya ukuaji na heshima, na kuendeleza utume wa pamoja wa kanisa.

 

Katika kuunda juhudi shirikishi zinazoheshimu huduma binafsi wezeshi na Kanisa la Waadventista wa Sabato, ni muhimu kufuata njia ya mkakati bayana na heshima ya pande zote mbili, iliyokita mizizi katika kanuni za Biblia:

Agano la Utofautishaji na Msaada wa Pande zote Mbili: Katika sitiari ya Paulo ya mwili wenye viungo vingi, kila kimoja kikiwa na kazi yake (1 Kor. 12), huhakikisha kwamba majukwaa ya mawasiliano kutoka katika nyaraka rasmi kwenda kwenye vyombo vya habari vya kidijitali zinaeleza jukumu la huduma kama chombo tofauti ambacho kinafanya kazi kwa upatanifu, lakini si sehemu halali, ya muundo wa madhehebu ya Waadventista wa Sabato. Kujitoa huku kwa uwazi kunaunga mkono utume wa kanisa na kudumisha uadilifu wa huduma kama mshiriki mahususi katika mwili wa Kristo.

 

Mafundisho na Uadilifu katika Ushirikiano: Inafungamana kwa karibu na kudumu kwa mitume katika mafundisho yenye uzima (Matendo 2:42), mara kwa mara kushauriana na viongozi wa kanisa ili kuhakikisha ulinganifu wa teolojia. Inakubali uwazi wa kifedha unaoakisi uwakili wa kibiblia, na rasilimali zinaelezwa kinaganaga, ikisisitiza dhamira ya pamoja ya kuendeleza injili.

 

Jitihada za Kimkakati na Ushirikiano wa Huduma: Tafuta fursa za kimkakati za huduma zinazofanana na ujenzi wa kushirikiana wa Nehemia wa kuta za Yerusalemu—wakifanya kazi bega kwa bega, lakini kwa sehemu zilizowekwa wazi. Shiriki kikamilifu ndani ya jumuiya ya Waadventista, ukiimarisha matokeo ya huduma kupitia jitihada za ziada.

 

Ushirikiano Unaojenga Pamoja na Uongozi wa Kanisa: Kufuata mfano wa Kristo wa kutambua majukumu mbalimbali ndani ya huduma Yake (Yohana 13:14–17), changamana na uongozi wa kanisa katika roho ambayo inatambua wajibu wa kuunga mkono wajibu wa huduma na utambulisho wake wa utendaji.

 

Maadhimisho ya Kujitoa ya Pamoja na Mafanikio ya Pamoja: Shiriki na usherehekee mafanikio ya huduma kama mwangwi wa umoja ambao Kristo aliomba (Yohana 17:21-23). Hebu visa hivi vya ushirikiano vionyeshe kujitoa kwa pamoja kwa utume, vikisisitiza umoja katika huduma badala ya ushirikiano wa shirika.

 

Kwa kujumuisha mikakati hii, huduma zinazojitegemeza zinaweza kueleza kwa ufasaha uhuru wake wa kujitegemea lakini ukiunga mkono katika uhusiano wa Kanisa la Waadventista, yakiimarisha utume wao wa pamoja kupitia ushirikiano lakini ushirikiano uliofafanuliwa wazi.

 

 

MAONO KWA AJILI YA WAKATI UJAO

Urithi wa vyombo kama vile Chuo cha Madison na ASi unasisitiza kujitoa kwa kanisa kwa ushiriki hai, na jumuishi katika uwanja wa utume. Kupitia ushirikiano unaoendelea na kusherehekea tunu ya pamoja, Kanisa la Waadventista linaweza kutumia nguvu mbalimbali za huduma hizi zinazojitegemea lakini zenye kuunga mkono kikamilifu.

 

Kwa kuunga mkono kikamilifu na kushirikiana kimkakati na huduma zinazojitegemeza, kanisa linatambua vyombo hivi kama washirika muhimu katika kueneza ujumbe wa matumaini na uzima. Uhusiano kama huo, uliojengwa juu ya maombi, heshima, na ushirikiano, utahakikisha kwamba kanisa linasonga mbele kwa umoja ili kushiriki injili ya milele na ulimwengu wenye uhitaji.

Waadventista wa Sabato kuanzia siku za awali walianzisha taasisi ili kueneza injili. Haijalishi kama lilikuwa Shirika la Kimataifa la Uhuru wa Dini la mwaka 1893, jarida la Adventist Review la 1849 ama Taasisi ya Tiba ya Battle Creek (the Battle Creek Sanitarium) ya mwaka 1866, yanayounda muundo na taasisi yako katika asili yetu.

 

Kwa muda na kupitia uzoefu mgumu wa kujifunza, kanisa la Waadventista limeendeleza sera na namna ambavyo taasisi hizi tofauti za kisheria zinavyohusiana. Pasina shaka, hii ni nyongeza kwa muundo wa kanisa letu mahalia, konferensi, union, divisheni na Konferensi Kuu. Kufahamu namna ambavyo makundi haya tofauti hufanya kazi kwaweza kuwa jambo la kuogofya.

 

Tofauti ya muhimu zaidi ni kati ya taasisi za kidini na huduma wezeshi. Taasisi za kidini zimeshikamana moja kwa moja na kanisa. Zaidi ya konferensi mahalia na unioni, taasisi kama nyumba ya uchapaji ya Stanborough (Stanborough Press) au Hope Channel ni taasisi tofauti za kisheria lakini zimefungamanishwa kimuundo na Kanisa la Waadventista.

Taasisi za kidini zina ama ofisi ya kijimbo (kama vile konferensi) au bodi ya uanachama iliyoainishwa inayoundwa na maofisa wa kanisa.

 

Huku zikidumisha hadhi tofauti ya kisheria na kujiendesha na kujisimamia kwa sheria zao ndogondogo, bodi, na majimbo, zina uhusiano na kanisa lote kwa ujumla. Taasisi zote hizi hufanya kazi za kiutawala pamoja katika masuala kama vile malipo, kustaafu na mahitaji ya kielimu. Taasisi hizi pia ni sehemu pana ya kanisa la Waadventista wa Sabato na zinasaidia kuainisha imani, utume na malengo ya kanisa. Mashirika yanayoorodheshwa katika kitabu cha Mwaka cha Kanisa la Waadventista wa Sabato ni taasisi za kidini.

 

Huduma wezeshi (ama zinazojiendesha zenyewe), sio sehemu ya muundo mpana wa Kanisa, japo hushiriki malengo na makusudi ya Kanisa la Waadventista wa Sabato. Licha ya kuwa bodi na uongozi utakuwa na Waadventista walei waaminifu, lakini zaidi ya kuwa washiriki wa kanisa la Waadventista wa Sabato, si wao wala huduma zao zilizo na uhusiano wa kisheria na muundo wa Kanisa.

 

Huduma kama vile Three Angels Broadcasting Network au Fletcher Academy vilivyopo Karolina Kaskazini nchini Marekani kwa miaka mingi vimekusudia kuendeleza mafundisho ya kanisa la Waadventista. Lakini huduma hizi sio taasisi za kanisa kwa sababu zimejijenga nje ya mfumo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato.

 

Hii haimaanishi kuwa viongozi wao sio Waadventista waaminifu wala haimaanishi kuwa wanafundisha na kuhubiri injili kinyume na imani ya Kanisa la Waadventista wa Sabato. Huduma hizi wezeshi kwa sababu anuwai huamini kuwa huduma zao hufanywa vyema zaidi kama wezeshi kuliko taasisi za kidini.

 

Hapo awali, huduma wezeshi zilikuwa zikijulikana kama “huduma huria.” Nyingi za huduma wezeshi zinahisi kuwa istilahi hii humaanisha kuwa hawafanyi kazi kwa mwafaka na ushirikiano na kanisa, hivyo huepuka kuitumia. Hili hutofautiana na kundi la “waliomeguka” (offshoot) ambalo hufanya kazi ya kukosoa au kulibomoa kanisa zaidi ya kushirikiana nalo ili kulitegemeza. Huko Amerika ya Kaskazini, huduma wezeshi huainishwa kama Adventist-laymens Service & Industries (ASi).

Katika miaka 30 iliyopita, nimepata fursa ya kutumika katika nafasi tofauti nyumbani na nje ya nchi katika mazingira mbalimbali. Niliona kwamba washiriki wanapofanya kazi pamoja kama timu, mambo mengi yanatimizwa kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Ninamaanisha nini kwa hilo? Hebu tuchunguze mfano wa kibiblia.

 

Yesu aliwachukua wanafunzi Wake kwenda safari ya kutembelea na wakapita karibu na mtu ambaye hakuwa mmoja wa wanafunzi kumi na wawili, lakini alikuwa mfuasi wa Kristo. Alikuwa akitoa pepo kwa jina la Yesu. Wanafunzi walimwendea Yesu na kusema, “Mwalimu, unapaswa kumzuia mtu huyu kwa sababu yeye si sehemu ya kundi letu.” Wanafunzi walikuwa na mtazamo finyu. Kwa mtazamo wao, wao pekee ndio walioweza kutenda kazi au kushiriki katika huduma pamoja na Yesu. Lakini, katika majibu Yake kwa wanafunzi, Yesu anapanua uelewa wao wa ni nani aliye kwenye timu. Alisema, “Msimkataze, kwa kuwa yeye ambaye si kinyume chenu yu upande wenu” (Marko 9:38-39).

 

Wazo la Yesu kuhusu timu lilikuwa kubwa zaidi kuliko lile walilokuwa nalo wanafunzi katika mtazamo wao wenye ukomo. Walidhani kuwa wao pekee ndio wanaoweza kumtumikia Mungu. Mifano mingine ya kibiblia inaonyesha kwamba Yesu alikuwa na mtazamo mpana juu ya utume ambao ulijumuisha aina mbalimbali za watu, ikiwa ni pamoja na watoza ushuru, Mafarisayo, Wakanaani na wengine, ukijumlisha na wanafunzi waliokuwa wakisafiri Naye kila siku.

 

 

MAFUNDISHO MATATU

Kuna mafundisho matatu ambayo nimejifunza kwa kufanya kazi na huduma wezeshi kwa ajili ya kueneza ufalme wa Mungu.

 

Kila mmoja anao wito na wajibu katika kuendeleza na kushiriki ujumbe wa malaika watatu. Wajibu na kazi za huduma zinazounga mkono utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato ni kufuata wito wao kulingana na dhamiri zao, ndani ya mfumo wa kisheria wa jiji, jimbo, au nchi wanayofanyia kazi, ili kusaidia kuwafanya wanafunzi miongoni mwa makundi ya watu wasiofikiwa. Hii inafanyika kwa kusaidia utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato na kufanya kazi kwa pamoja.

 

Tukiangalia historia ya kanisa, tunaona aina mbalimbali za kazi ya injili zikifanyika Jijini New York katika miaka ya 1890 hadi 1900. Baadhi ya taasisi au washirika wa huduma waliohusika walikuwa wafanyabiashara na wajasiriamali wa Kiadventista, si watendakazi wanaolipwa na kanisa. Walikuwa sehemu ya timu ile ile ya kumshiriki Kristo jijini na kuwafanya wanafunzi miongoni mwa tabaka la wafanyakazi, mawakala wa hisa kwenye Wall Street na kati ya makundi ya watu wasiofikiwa ya wakati huo.

 

Kwa kawaida kanisa linazingatia kuhubiri injili, kufundisha, huduma ya afya na huduma za kusaidia kama kutunza wajane, mayatima, na wale wenye mahitaji maalum. Wakati mwingine tunapata mashaka, hata hivyo. Hapo ndipo hatua ya pili inapoingia.

 

Kwa pamoja tunaweza kwa sababu tunakamilishana kazi zetu. Baadhi ya taasisi zinaweza kuona huduma wezeshi kama ni ushindani. Najua kwamba mara zingine, kumekuwa na migogoro na kutokuelewana ambako kumesababisha kutokuaminiana, machafuko na ukosefu wa umoja kati ya huduma wezeshi na taasisi ya madhehebu thabiti kama vile kanisa mahalia, konferensi, union, divisheni au hata Konferensi Kuu.

 

Lakini tukichunguza Waefeso 4 na kuona jinsi Mungu alivyowaandaa waumini wote kwa kutumia vipawa vya kiroho, tunaona kunaweza kuwa na wajibu wa kukamilishana kwa ajili ya huduma wezeshi katika maeneo na miongoni mwa makundi ya kijamii ambapo kanisa halina uwepo wa moja kwa moja. Kwa pamoja tunaweza.

 

Tunapaswa kujua wajibu wetu. Ninamaanisha nini? Kama mchungaji wa Waadventista wa Sabato, mmishonari, mwanzilishi wa kanisa na wakili, ninashirikiana na kuwa sehemu ya mabaraza ya taasisi mbalimbali za kanisa. Hii ni pamoja na kanisa mahalia ambapo nami ni mshiriki, konferensi yangu mahalia, pengine union yangu au hata divisheni au Konferensi Kuu. Katika ngazi hizo za uwakilishi, ninaweza kuwa na sauti, kupiga kura juu ya masuala, kutoa mwongozo na mwelekeo na kuwa sehemu ya mchakato. Hapo ndipo ninaweza kutoa mchango wangu kama kiongozi wa kanisa.

 

Basi, ni kwa jinsi gani viongozi wa kanisa au watendakazi wanaungana na wale walio na huduma wezeshi? Tukifanya kazi kulingana na wajibu wetu, tunaweza kuwasiliana na wenzetu. Kuna changamoto gani za utume mbele yetu? Zipi zinabaki? Tunaweza kusali pamoja kumwomba Mungu atuongoze, atuhamasishe na kuwasha mioyo ya wanawake, wanaume, wajasiriamali na vijana, walioitwa na Yeye, wenye vipawa, fedha na walioandaliwa na Yeye kwa njia zingine isipokuwa ya kanisa. Hivyo, tunaungana kupitia mawasiliano, kuweka mikakati na maombi.

 

Njia nyingine tunayoitumia miongoni mwa wajibu wetu ni kupitia ushirikiano. Sehemu ya ushirikiano huo ni kuuliza, “Hitaji ni lipi na tunawezaje kufanya kazi pamoja?”—kila mmoja ndani ya mfumo na taasisi yake halali. Inaweza kuwepo roho ya ushirikiano kati ya hizo mbili kwa kusudi la kuendeleza utume, na si moja yenye kujaribu kudhibiti nyingine, kuheshimu mipaka halali ndani ambayo kila moja inafanya kazi. Inakuwa vyema tunapofanya kazi pamoja na kusaidiana.

 

 

KUENDELEZA KAZI

Katika Sera ya Kazi ya Konferensi Kuu, kuna sehemu iliyotengwa* katika kuunga mkono huduma wezeshi na jinsi zinavyofafanuliwa. Kuna namna ambayo taasisi za kisheria zinazounga mkono (au mashirika yasiyo ya faida nchini Marekani) zinaweza kufanya kazi kwa pamoja na kanisa katika kazi yake ya utume, lakini ndani ya muktadha wa kila mmoja.

 

Katika baadhi ya miji iliyojificha (maeneo makubwa duniani ambapo utume unapaswa kushughulikiwa kwa tahadhari) niliona jinsi Mungu alivyotumia taasisi tofauti kusaidia kuwafikia baadhi ya makundi ya watu wasiofikiwa na kanisa lisingeweza kuwafikia.

Hicho sicho kipawa pekee. Kuna vipawa vya kutoa msaada na uponyaji pia. Yule aliye na ujuzi au uwezo huo, pamoja na hati ya utambulisho kutoka katika mafunzo yao, anaweza kufanya kazi katika mazingira yenye utamaduni tofauti ambayo mimi nisingeruhusiwa. Hivi ndivyo kanisa na huduma wezeshi wanavyoweza kufanya kazi kwa ushirikiano, kuendeleza utume wa kanisa, si kwa ajili ya kudhibiti mtu mwingine, bali kwa kutumia vipawa vyetu vya kiroho na kuonyesha wito wetu wa kimbingu wa kuwafanya wanafunzi na kujenga mwili wa Kristo.

 

Hivyo, timu yako ni kubwa kiasi gani? Inatutaka sisi sote kufanya kazi pamoja ili kutimiza utume ambao tumepewa—kutoa tumaini na uponyaji kwa ulimwengu uliojaa maumivu na giza. Tunapaswa kuonyesha roho ya ufahamu wa ushirikiano na heshima kwa aina mbalimbali za vipawa na wito ambao Bwana ameweka kwa kila mmoja wetu, tukifanya kazi pamoja kuendeleza ufalme wa mbinguni.

Huduma wezeshi zipo katika namna nyingi tofauti za utume na utumishi. Baadhi ni taasisi za afya, nyenzo za kielimu, uinjilisti kamili au kutoa huduma. Kwa namna yoyote, hizi taasisi zenye kujiwezesha zinashabihiana katika kitu kimoja, kuwaleta watu katika kuwa na uhusiano uokoao pamoja na Yesu na kuwaongoza katika Chanzo cha tumaini na uponyaji.

 

Maelezo yafuatayo yanatoa mtupo wa jicho katika eneo kubwa la huduma wezeshi kiulimwengu.

Mtandao wa Kiinjilisti wa Tiba ya Kiadventista (Adventist Medical Evangelism Network [AMEN])

 

Mtandao wa Kiinjilisti wa Tiba ya Kiadventista (AMEN) ni shirika pana lenye ukingano wa afya na ufikiaji kiimani, lililojitoa kuendeleza ustawi kimwili na kiroho wa kila mtu na jamii ulimwenguni kote. Pamoja na historia nzuri na kujitoa kikamilifu kwa ujumbe wa afya wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, AMEN inafanya wajibu katika kutangaza uponyaji kamili na kueneza injili ya Kristo.

 

AMEN ilianzishwa katika kanuni za huduma ya Mkristo, elimu ya afya na uinjilisti wa tiba. Tangu mwanzoni, imekua na kuwa mtandao mkubwa wa wanataaluma wa afya, wanaojitolea na wanaounga mkono wakiunganishwa na utume mmoja. Lengo la msingi la taasisi ni kutoa huduma ya tiba na kushiriki upendo wa Yesu pamoja na idadi ya watu wanaofikiwa na huduma pungufu na wasio salama. AMEN inatoa safu ya huduma, kutoka kliniki za afya za bila malipo na umishonari wa tiba mpaka programu za elimu ya afya na ushauri juu ya mtindo wa maisha.

 

Nembo za AMEN ni tiba na kliniki ya meno, mara nyingi hufanyika katika maeneo yasiyofikika kirahisi ambapo huduma za afya ni haba. Kliniki hizi zinatoa huduma ya tiba muhimu, huduma ya meno na elimu ya kulinda afya, ikiwafaidia maelfu ya watu ambao huenda wasingepata huduma ya afya inayofaa. Timu za shirika la wataalamu wa tiba na wanaojitolea wanafanya kazi kuhakikisha kwamba matukio haya sio tu yanaponya mwili bali pia kulea roho kupitia maombi na msaada wa kiroho.

 

Kujitoa kwa AMEN kwa ajili ya elimu ya afya na ufundishaji wa mtindo wa maisha kunaonekana wazi katika warsha, semina na programu za ustawi. Wanaandaa watu kwa maarifa na nyenzo ili kufanya maamuzi thabiti kuhusu afya zao na kuwapa nguvu ya kuishi maisha yenye afya.

 

Kujitoa kwa dhati kwa mtandao huu kwa ustawi wote kunaakisi msisitizo wa Kanisa la Waadventista juu ya mtindo wa maisha wenye usawa na afya, kutoka katika mizizi ya imani. Kwa kushughulikia nyanja za afya kimwili, kiakili na kiroho, AMEN wanaendelea kuleta mabadiliko katika maisha na jumuiya. Kazi yao ni agano la mashirika kwa nguvu iliyojengwa kiimani katika kuleta badiliko lenye maana kwa maisha ya wale wanaowahudumia.

AMEN huleta tumaini, uponyaji na huduma ya kiroho katika ulimwengu ambao mara nyingi umepigwa na baa la kimwili na mateso ya kihisia. Pamoja na kujitoa kwake kwa huduma za afya na ufikiaji uliojengwa kiimani, AMEN inasimama kama mfano angavu wa jinsi huruma, imani na utaalamu unaweza kujumuishwa ili kuleta matokeo chanya kwa watu binafsi na jumuiya ulimwenguni kote.

 

Pata taarifa zaidi katika tovuti yao:
https://amensda.org.

Usimamizi wa Watoto Kimataifa (International Children’s Care [ICC])

 

Usimamizi wa watoto kimataifa (ICC) ni shirika ulimwenguni lisiloingiza faida lililojitoa ili kuleta maendeleo kwa maisha ya watoto na familia zinaoishi maeneo hatarishi ulimwenguni kote. Ikianzishwa mwaka 1978, ICC imetoa usimamizi mpana, elimu na kuwasaidia watoto wenye mahitaji.

 

ICC inafanya kazi katika mataifa mbalimbali, ikijitahidi kuvunja duru ya umaskini, dhuluma na kutojali kupitia mbinu zake za jumla. Programu zake hujumuisha huduma kwa yatima, elimu na uwezo wa kuimarisha familia, pamoja na msingi wa lengo ili kuhakikisha kwamba kila mtoto anapata uzoefu wa upendo, usalama na nafasi ya kesho angavu.

 

Moja ya sifa bainifu za ICC ni njia ya usimamizi wa kifamilia, ambayo inatoa kipaumbele kwa kuwapa watoto upendo, familia thabiti kuliko maeneo ya taasisi. Watoto wanaishi katika familia pamoja na baba na mama wa asili yake. Njia hii imeonyeshwa kufaa katika kutangaza kukua katika afya kihisia na kujenga dhana ya umiliki.

 

Japokuwa kuna upungufu wa kifedha, shirika hujaribu kutoa fursa ya elimu bora kwa kiwango cha shauku ya watoto. ICC huelewa kwamba, elimu ni ufunguo wa kuvunja baa la umaskini.

Sehemu muhimu ya programu ni kuunganisha “watoto pamoja na wadhamini wanaotaka kuonyesha uhusiano na mtoto. Wadhamini wa watoto wanatiwa moyo kuhusiana na watoto. Hili ni muhimu kwa watoto hawa, wakati ICC ikifanya kazi ili kuwasaidia watoto kujenga taswira binafsi iliyo chanya. Ni muhimu pia kwa wadhamini, kama mwanamke/mwanaume mwenye nafasi ili kuzingatia mahitaji ya wengine.”1

Utume wa ICC wa kulea, kulinda na kuelimisha watoto wanaoishi mazingira hatarishi unawafanya kuwa nguzo ya tumaini katika mandhari ya ulimwengu wa ustawi wa mtoto.

 

Tembelea: https://forhiskids.org kwa maelezo zaidi ili kudhamini mtoto au programu nzima.

Canvasback Missions

 

Canvasback Missions ni huduma inayounga mkono Kanisa la Waadventista wa Sabato, ikiwa na lengo la kuboresha afya na ustawi wa jamii katika Visiwa vya Pasifiki. Ikiwa na mkazo mkubwa kwenye huduma za afya, elimu, na maendeleo ya jamii, shirika hili lisilo la kifaida limekuwa likileta maendeleo chanya kwa maisha ya watu wanaoishi katika maeneo yasiyofikika kirahisi ya Pasifiki kwa zaidi ya miongo mitatu.

 

Canvasback Missions ilianzishwa mwaka 1985 na Larry na Cindy Hart, waliokuwa na msukumo kutokana na imani yao na hisia kubwa ya huruma. Tangu kuanzishwa kwake, shirika limekuwa katika utume wa kuleta tumaini, uponyaji, na mabadiliko kwa wale walio wahitaji. Wanashirikiana na misheni za Waadventista wa Sabato za eneo mahalia na washirika wengine kutoa huduma muhimu za matibabu na msaada wa kijamii.

 

Moja ya maeneo muhimu kwa Canvasback Missions ni huduma za afya. Shirika hilo hutuma timu za wataalamu wa afya, ikiwa ni pamoja na madaktari, wauguzi, madaktari wa meno, na wataalamu wa upasuaji, kutoa huduma za matibabu na upasuaji bure kwa jamii zisizostahiki katika Visiwa vya Pasifiki. Umishonari huu wa matibabu hausaidii tu mahitaji ya afya ya dharura bali pia kukuza afya na ustawi wa muda mrefu kwa kutoa rasilimali kwa wafanyakazi mahalia wa afya.

 

Maendeleo ya jamii ni nyanja nyingine muhimu ya kazi ya Canvasback Missions. Kupitia Kituo cha Afya cha Canvasback huko atoll ya Majuro, wataalamu wa tiba wanasisitiza kuboresha maisha kwa jumla kupitia lishe na mazoezi; kuelimisha wanajamii jinsi ya kupanda mbogamboga safi ambazo si rahisi kupatikana visiwani; na kupambana na mabadiliko ya tabianchi kupitia kilimo endelevu.

 

Maadili ya msingi ya shirika yamefungwa katika imani yao ya Kikristo, wakisisitiza upendo, huruma, na huduma kwa wengine. Canvasback Missions inaonyesha mfano wa kanuni za Kanisa la Waadventista wa Sabato kwa kutafuta kwa bidii kuleta tofauti kivitendo katika maisha ya wale wanaowahudumia. Uwekezaji wao unaonyesha nguvu ya kazi ya ubinadamu inayotokana na imani.

 

 

Tembelea https://canvasback.org kwa habari zaidi.

SHAMBA LA KIBIDULA

 

Likipatikana kusini-kati mwa Tanzania, Shamba la Kibidula linasimama kama mfano angavu wa kilimo endelevu. Shamba hilo lilianzishwa mwaka 1989 na lina ukubwa wa ekari 4,776. Ni zaidi ya shamba, hata hivyo.

 

Kibidula inaendesha shule ya kutwa kwa wanafunzi wa eneo mahalia na “shule ya kilimo, inayotoa mafunzo ya utaalamu, kiroho na mafunzo ya ujuzi wa maisha kwa ajili ya vijana ambao wanashindwa kuendelea katika elimu ya sekondari; na shule ya uinjilisti.” Shirika lao “pia linaendesha kituo cha mtindo wa maisha, kujenga makanisa, uchapaji wa maandiko mbalimbali (afya ya mwili, akili na roho), uchapaji wa masomo ya Biblia, vijuzuu na vitabu vidogo, hutoa Biblia na hufanya kazi ili kuwafikia watu ili kuwa na tumaini la Yesu Kristo kupitia watumishi wa Biblia na zaidi.”2

 

Utume wa Kibidula ni kuleta maendeleo kwenye maisha “kupitia elimu ya kiutendaji, kilimo, afya na huduma kwa jamii.”3

 

Soma baruapepe zao na kufuatilia kinachoendelea shambani katika https://kibidula.org.

Sayansi ya Ulimwengu wa Kiadventista ya Ufundi wa Vyombo vya Anga (Adventist World Aviation [AWA])

 

Sayansi ya Ulimwengu wa Kiadventista ya Ufundi wa Vyombo vya Anga (AWA) ni shirika lisiloingiza faida, taasisi ya ubinadamu yenye lengo la kutoa huduma za anga katika maeneo yasiyofikika kirahisi na yasiyopata huduma stahiki ulimwenguni kote. Ikianzishwa kwa misingi ya huruma na utumishi, AWA inaunga mkono utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato ulimwenguni.

 

Ikianzishwa mnamo mwaka 1995, AWA hutumia manowari ya ndege na wafanyakazi wenye ujuzi ili kuunganisha jamii zilizotengwa na raslimali muhimu. Utume wao ni kuleta tumaini, uponyaji, na ujumbe wa upendo wa Mungu kwenye maeneo ambayo vinginevyo yasingepatikana kutokana na changamoto za kijiografia, logistiki, au miundombinu.

 

Timu ya AWA iliyojitoa ya marubani, mafundi, na wafanyakazi wengine hutoa huduma ya tiba, kusafirisha timu za matabibu, kutoa misaada ya kibinadamu na kusaidia katika juhudi za kupunguza maafa. Ahadi yao ya kutumikia wale walio katika maeneo yasiyofikika kirahisi na mara nyingine maeneo magumu, imeleta matokeo makubwa katika maisha ya watu na jamii nyingi.

 

Tembelea tovuti yao https://flyawa.org kwa habari zaidi.

LifestyleTV

 

LifestyleTV ni kipindi cha televisheni chenye mvuto katika mji wa Sweden, kikiwapatia watazamaji mchanganyiko wa pekee wa maudhui yanayosaidia maisha bora na kushiriki kanuni za imani ya Waadventista wa Sabato. Kwa dhamira yake ya kuendeleza ustawi na ukuaji wa kiroho, LifestyleTV imepata wafuasi ulimwenguni, ikivuka mipaka ya kitamaduni na dini.

 

Katika msingi wa utume wa LifestyleTV ni kukuza mtindo wa maisha kwa wote. Programu hiyo inajitolea kuelimisha watazamaji wake kuhusu faida za mlo kamili, mazoezi ya mwili, afya ya akili, na ustawi wa kiroho. Kupitia vipindi anuwai, ikiwa ni pamoja na maonyesho ya upishi, mazoezi, na ujumbe wa kuvutia, LifestyleTV inawawezesha watu kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya afya zao kimwili na kiroho.

 

Ikianzishwa na makao yake makuu yakiwa Sweden, LifestyleTV imekuwa nguzo ulimwenguni kwa wale wanaotafuta kuishi maisha yenye afya na yenye maana zaidi. Uenezi wake unavuka mbali zaidi ya sehemu zote za Kiskandinavia, ikiwa na mvuto kwa watazamaji ulimwenguni kote kupitia matangazo ya setilaiti na mtandaoni. Kwa kufanya maudhui yao kupatikana kwa kila mtu, bila kujali eneo la kijiografia, LifestyleTV imesambaza ujumbe wake wa ustawi kamili na imani kwa hadhira anuwai, kimataifa.

Vipindi vya LifestyleTV vinakidhi maadili ya Waadventista wa Sabato, kwa kushiriki kwa kujitoa kwa lishe ya mbogamboga, kufuata Sabato, na kukuza hisia ya jumuiya na ushirika. LifestyleTV inajenga daraja kati ya jamii ya Waadventista na umma kwa jumla, kutoa ufahamu na mwongozo muhimu kwa wote.

 

Katika ulimwengu wa programu za televisheni, LifestyleTV inatoa mtazamo wa pekee kuhusu uhusiano wa imani na mtindo wa maisha. Iwe wewe ni Mwadventista mwaminifu, anayependa afya, au ni mtu tu anayetafuta mwongozo wa kuboresha mtindo wako wa maisha, LifestyleTV inatoa hazina ya rasilimali nzuri ya kukusaidia katika safari yako ya maisha yenye mafanikio zaidi.

 

Tazama https://arkiv.lifestyletv.se/about/ kwa habari zaidi kuhusu LifestyleTV. Baadhi ya vipindi vinapatikana kwa Kiingereza.

Sio siri kwamba muziki—hasa muziki wa kidini—ni moja ya mada inayojadiliwa zaidi katika Ukristo. Wakati wowote tunapokabiliwa na suala tata kama hilo na gumu kusuluhisha, ni muhimu kujifunza Maandiko na maandishi ya Ellen G. White ili kupata kanuni zinazoongoza jinsi muziki wetu wa ibada unavyopaswa kuwa.

 

Mada hiyo inazidi kuwa muhimu tunapokaribia zahama ya mwisho ya historia ya ulimwengu huu. Kulingana na Ufunuo 13 na 14, ibada itakuwa suala kuu litakalobainisha hatima ya kila mwanadamu. Itatubidi kuchagua kati ya kumwabudu mnyama (na sanamu yake) na kumwabudu Mungu. Kumwabudu Mungu wa kweli ni muhimu kama vile kumwabudu kwa njia ifaayo. Je, inaweza kuwa kwamba hata kwa nia nzuri, kwa kutumia muziki usiofaa Wakristo wengi wanaabudu kwa njia isiyofaa?

 

Biblia inatoa mifano mingi ya watu waliomwabudu Mungu na kutoa taarifa ya sababu za kufanya hivyo. Kulingana na habari hii, tunaweza kufasili ibada kama “mtazamo wa unyenyekevu, uchaji, heshima, kujitoa, na kuabudu”2 toka kwa viumbe kwenda kwa Muumbaji wao, kwa kutambua sifa Zake (Zab. 99:9; Ufu. 15:4) na kazi zake za uumbaji (Ufu. 4:10; 14:7), ukombozi (2 Wafalme 17:36; Ufu. 5:9), na majaliwa (Zab. 59:16; 118:21).

     

Ibada ni uzoefu binafsi, lakini pia ni kazi ya familia na jumuiya. Ufahamu wetu juu ya Mungu unaamua jinsi tunavyomkaribia na kumwabudu.3 Kwa hiyo, ni muhimu kujua Mungu ni nani kwa mujibu wa Biblia. Sifa ya Mungu ya utakatifu inadhihirika kuwa muhimu kwa asili ya Mungu.

 

 

UTAKATIFU WA MUNGU NA WATU WAKE

Baada ya anguko la Adamu na Hawa, ibada iliyofanywa na wanadamu ilitiwa doa kwa sababu dhambi ilikuwa imetuathiri sisi sote. Si hivyo kwa malaika, ambao hawajaanguka katika dhambi.

     

Moja ya vifungu vinavyofundisha zaidi kuhusu ibada ya mbinguni ni Isaya 6, “fungu kuu la Biblia kuhusu ibada.”4 Isaya alimwona Bwana ameketi katika kiti Chake cha enzi, akizungukwa na maserafi wakiimba, “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake!” (Isa. 6:3). Kurudiwa huko kunaonekana katika kitabu cha Ufunuo, ambapo Yohana aliona wenye uhai wanne wamezunguka kiti cha enzi cha Mungu, “wakisema: ‘Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja!’ ” (Ufu. 4:8).

     

Ukweli kwamba Mungu ni mtakatifu unahitaji kwamba watoto wake wawe watakatifu pia. Tatizo ni kwamba sisi ni wenye dhambi kwa asili. Tunapotubu dhambi zetu, hata hivyo, na kuziungama kwa Mungu, anatupokea kama watoto Wake, hutusamehe dhambi zetu, na kututangaza kuwa watakatifu, akitutenga kwa ajili Yake. Hadhi hii mpya inatuwezesha, kwa njia ya imani katika yeye na kwa neema yake, kukua katika mchakato wa utakaso, ambao ni kazi ya “maisha yote”5 (Rum. 6:19, 22; 1 Thes. 4:3).

     

Mungu mtakatifu, ambaye kwa neema huwapa watoto wake hadhi takatifu na kuwaamuru wakue katika utakatifu wa kimaadili katika maisha yao yote, anahitaji pia kwamba kila kitu kinachohusiana na ibada kiwe kitakatifu, iwe katika maisha ya faragha, nyumbani, au kanisani.

     

Wimbo unaoimbwa na kwaya ya maserafi (Isa. 6:3; Ufu. 4:8) ni kielelezo cha kile tunachopaswa kufuata tunapofanya muziki katika uwepo kwa Bwana. “Muziki ni sehemu ya ibada ya Mungu katika nyua zilizo juu, na tunapaswa kujitahidi, katika nyimbo zetu za sifa, kukaribia kadiri iwezekanavyo ulinganifu wa kwaya za mbinguni.”6 Wimbo wa kuabudu wa malaika unadhihirisha kwamba kukiri utakatifu wa Mungu ndio msingi wa ibada ya kweli na muziki wa dini.

 

 

UTAKATIFU WA MUNGU NA MUZIKI WA DINI

Kutokana na ufahamu wetu wa dhana ya kibiblia ya utakatifu wa Mungu na kutoka katika maandishi ya Ellen G. White, kanuni maalum zinajitokeza kwa ajili ya muziki wa kidini, katika ngazi binafsi na ya pamoja.

     

Uhitaji wa “kupambanua kati ya yaliyo matakatifu na hayo yaliyo ya siku zote” (Law. 10:10) katika muziki leo ni muhimu zaidi kuliko hapo awali. Muziki wote kwa asili unaleta kwa wasikilizaji muunganiko wa mawazo na uzoefu. “Mitindo ya muziki inakuja na kifurushi cha kiutamaduni. Mara nyingi inahusishwa na mahali, watu, na matendo.”7 Tunahusisha aina fulani za muziki na mazingira mahususi, mitazamo, na mitindo ya maisha. Kwa hiyo, “muziki mtakatifu haupaswi kuwa na ushirika na muziki wa kidunia au kukaribisha kupatana na mitindo ya kitabia ya kidunia ya kufikiri au kutenda.”8

     

Kuhusu muziki wa sauti, maneno ya wimbo yanayopatana na Biblia hayatoshi kwa wimbo kufaa kumwabudu Bwana. Sifa ya muziki wenyewe unapaswa “kuwa kwa ajili ya kusudi takatifu, kuinua mawazo kwa kile kilicho safi, adili, na chenye kuinua, na kuamsha kujitoa kwa nafsi na shukrani kwa Mungu.”9

     

Walakini, sio mitindo yote ya muziki inayotimiza kusudi hili. Mitindo ya muziki ilibuniwa ili kufikia makusudi ya wazi katika mazingira maalum. Kwa hiyo, kinyume na wazo lililoenea, mtindo wa muziki si mbebaji wa ujumbe wa Kikristo asiyeegemea upande wowote. “Jamii kubwa ya utaalamu wa elimu ya  muziki imeonyesha kwamba, badala ya kuwa kipao kitupu cha kuingiza maudhui ya  kupitia kwa maneno ya wimbo yanayoimbwa, mtindo wa muziki wenyewe unawasilisha seti maalum ya mawazo na maadili kwa wasikilizaji wanaopatana na mitindo ya kitamaduni ya jamii yao.”10 Kwa kweli, “mitindo ya muziki ina thamani na kanuni za kidini—ni vielelezo halisi vya imani kuhusu ukweli.”11

     

Hata hivyo, mchanganyiko wa maneno ya kidini na mitindo ya muziki wa kidunia unazidi kusikika. “Kwa bahati mbaya, muziki mwingi wa kisasa wa Kikristo unategemea ladha ile ile ya mdundo wa muziki unaopigwa kuambatana na wimbo, upigaji ala, mpangilio na sauti kama muziki wa kidunia. Lakini kwa namna fulani maneno ya nyimbo za kidini yanatarajiwa kugeuza muziki huu wa kidunia kuwa wimbo mtakatifu.”12 Lakini Maandiko yanafundisha kwamba vitu vitakatifu havitakasi vitu vichafu; kinyume chake, wakati makundi haya mawili yanapokutana, kundi la kidunia huchafua kundi takatifu (Hagai 2:12, 13). Matokeo ya mchanganyiko huu ni kwamba athari ya muziki wenyewe, ulio kinyume na maadili ya Kikristo, zinashinda kabisa na kudhoofisha ujumbe wa maneno. Muziki ufaao zaidi ni ule ambao ndani yake kuna ulinganifu kamili wa maneno na muziki,13 hivyo maneno ya wimbo na muziki vinatoa ujumbe sawa.

 

Sio siri kwamba muziki—hasa muziki wa kidini—ni moja ya mada inayojadiliwa zaidi katika Ukristo. Wakati wowote tunapokabiliwa na suala tata kama hilo na gumu kusuluhisha, ni muhimu kujifunza Maandiko na maandishi ya Ellen G. White ili kupata kanuni zinazoongoza jinsi muziki wetu wa ibada unavyopaswa kuwa.

 

Mada hiyo inazidi kuwa muhimu tunapokaribia zahama ya mwisho ya historia ya ulimwengu huu. Kulingana na Ufunuo 13 na 14, ibada itakuwa suala kuu litakalobainisha hatima ya kila mwanadamu. Itatubidi kuchagua kati ya kumwabudu mnyama (na sanamu yake) na kumwabudu Mungu. Kumwabudu Mungu wa kweli ni muhimu kama vile kumwabudu kwa njia ifaayo. Je, inaweza kuwa kwamba hata kwa nia nzuri, kwa kutumia muziki usiofaa Wakristo wengi wanaabudu kwa njia isiyofaa?

 

Biblia inatoa mifano mingi ya watu waliomwabudu Mungu na kutoa taarifa ya sababu za kufanya hivyo. Kulingana na habari hii, tunaweza kufasili ibada kama “mtazamo wa unyenyekevu, uchaji, heshima, kujitoa, na kuabudu”2 toka kwa viumbe kwenda kwa Muumbaji wao, kwa kutambua sifa Zake (Zab. 99:9; Ufu. 15:4) na kazi zake za uumbaji (Ufu. 4:10; 14:7), ukombozi (2 Wafalme 17:36; Ufu. 5:9), na majaliwa (Zab. 59:16; 118:21).

     

Ibada ni uzoefu binafsi, lakini pia ni kazi ya familia na jumuiya. Ufahamu wetu juu ya Mungu unaamua jinsi tunavyomkaribia na kumwabudu.3 Kwa hiyo, ni muhimu kujua Mungu ni nani kwa mujibu wa Biblia. Sifa ya Mungu ya utakatifu inadhihirika kuwa muhimu kwa asili ya Mungu.

 

 

UTAKATIFU WA MUNGU NA WATU WAKE

Baada ya anguko la Adamu na Hawa, ibada iliyofanywa na wanadamu ilitiwa doa kwa sababu dhambi ilikuwa imetuathiri sisi sote. Si hivyo kwa malaika, ambao hawajaanguka katika dhambi.

     

Moja ya vifungu vinavyofundisha zaidi kuhusu ibada ya mbinguni ni Isaya 6, “fungu kuu la Biblia kuhusu ibada.”4 Isaya alimwona Bwana ameketi katika kiti Chake cha enzi, akizungukwa na maserafi wakiimba, “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake!” (Isa. 6:3). Kurudiwa huko kunaonekana katika kitabu cha Ufunuo, ambapo Yohana aliona wenye uhai wanne wamezunguka kiti cha enzi cha Mungu, “wakisema: ‘Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja!’ ” (Ufu. 4:8).

     

Ukweli kwamba Mungu ni mtakatifu unahitaji kwamba watoto wake wawe watakatifu pia. Tatizo ni kwamba sisi ni wenye dhambi kwa asili. Tunapotubu dhambi zetu, hata hivyo, na kuziungama kwa Mungu, anatupokea kama watoto Wake, hutusamehe dhambi zetu, na kututangaza kuwa watakatifu, akitutenga kwa ajili Yake. Hadhi hii mpya inatuwezesha, kwa njia ya imani katika yeye na kwa neema yake, kukua katika mchakato wa utakaso, ambao ni kazi ya “maisha yote”5 (Rum. 6:19, 22; 1 Thes. 4:3).

     

Mungu mtakatifu, ambaye kwa neema huwapa watoto wake hadhi takatifu na kuwaamuru wakue katika utakatifu wa kimaadili katika maisha yao yote, anahitaji pia kwamba kila kitu kinachohusiana na ibada kiwe kitakatifu, iwe katika maisha ya faragha, nyumbani, au kanisani.

     

Wimbo unaoimbwa na kwaya ya maserafi (Isa. 6:3; Ufu. 4:8) ni kielelezo cha kile tunachopaswa kufuata tunapofanya muziki katika uwepo kwa Bwana. “Muziki ni sehemu ya ibada ya Mungu katika nyua zilizo juu, na tunapaswa kujitahidi, katika nyimbo zetu za sifa, kukaribia kadiri iwezekanavyo ulinganifu wa kwaya za mbinguni.”6 Wimbo wa kuabudu wa malaika unadhihirisha kwamba kukiri utakatifu wa Mungu ndio msingi wa ibada ya kweli na muziki wa dini.

 

 

UTAKATIFU WA MUNGU NA MUZIKI WA DINI

Kutokana na ufahamu wetu wa dhana ya kibiblia ya utakatifu wa Mungu na kutoka katika maandishi ya Ellen G. White, kanuni maalum zinajitokeza kwa ajili ya muziki wa kidini, katika ngazi binafsi na ya pamoja.

     

Uhitaji wa “kupambanua kati ya yaliyo matakatifu na hayo yaliyo ya siku zote” (Law. 10:10) katika muziki leo ni muhimu zaidi kuliko hapo awali. Muziki wote kwa asili unaleta kwa wasikilizaji muunganiko wa mawazo na uzoefu. “Mitindo ya muziki inakuja na kifurushi cha kiutamaduni. Mara nyingi inahusishwa na mahali, watu, na matendo.”7 Tunahusisha aina fulani za muziki na mazingira mahususi, mitazamo, na mitindo ya maisha. Kwa hiyo, “muziki mtakatifu haupaswi kuwa na ushirika na muziki wa kidunia au kukaribisha kupatana na mitindo ya kitabia ya kidunia ya kufikiri au kutenda.”8

     

Kuhusu muziki wa sauti, maneno ya wimbo yanayopatana na Biblia hayatoshi kwa wimbo kufaa kumwabudu Bwana. Sifa ya muziki wenyewe unapaswa “kuwa kwa ajili ya kusudi takatifu, kuinua mawazo kwa kile kilicho safi, adili, na chenye kuinua, na kuamsha kujitoa kwa nafsi na shukrani kwa Mungu.”9

     

Walakini, sio mitindo yote ya muziki inayotimiza kusudi hili. Mitindo ya muziki ilibuniwa ili kufikia makusudi ya wazi katika mazingira maalum. Kwa hiyo, kinyume na wazo lililoenea, mtindo wa muziki si mbebaji wa ujumbe wa Kikristo asiyeegemea upande wowote. “Jamii kubwa ya utaalamu wa elimu ya  muziki imeonyesha kwamba, badala ya kuwa kipao kitupu cha kuingiza maudhui ya  kupitia kwa maneno ya wimbo yanayoimbwa, mtindo wa muziki wenyewe unawasilisha seti maalum ya mawazo na maadili kwa wasikilizaji wanaopatana na mitindo ya kitamaduni ya jamii yao.”10 Kwa kweli, “mitindo ya muziki ina thamani na kanuni za kidini—ni vielelezo halisi vya imani kuhusu ukweli.”11

     

Hata hivyo, mchanganyiko wa maneno ya kidini na mitindo ya muziki wa kidunia unazidi kusikika. “Kwa bahati mbaya, muziki mwingi wa kisasa wa Kikristo unategemea ladha ile ile ya mdundo wa muziki unaopigwa kuambatana na wimbo, upigaji ala, mpangilio na sauti kama muziki wa kidunia. Lakini kwa namna fulani maneno ya nyimbo za kidini yanatarajiwa kugeuza muziki huu wa kidunia kuwa wimbo mtakatifu.”12 Lakini Maandiko yanafundisha kwamba vitu vitakatifu havitakasi vitu vichafu; kinyume chake, wakati makundi haya mawili yanapokutana, kundi la kidunia huchafua kundi takatifu (Hagai 2:12, 13). Matokeo ya mchanganyiko huu ni kwamba athari ya muziki wenyewe, ulio kinyume na maadili ya Kikristo, zinashinda kabisa na kudhoofisha ujumbe wa maneno. Muziki ufaao zaidi ni ule ambao ndani yake kuna ulinganifu kamili wa maneno na muziki,13 hivyo maneno ya wimbo na muziki vinatoa ujumbe sawa.

KUIMBA PAMOJA NA MALAIKA

Hakuna ufumbuzi rahisi kwa suala tata la muziki wa kidini au wa “Kikristo” na muziki wa ibada. Kuwekea mpaka muziki wote wa kidini kwa nyimbo za kimapokeo sio jibu, kwa sababu suala sio kuchagua kati ya muziki wa kimapokeo na wa kisasa. Jambo muhimu zaidi sio tarehe ambayo wimbo uliandikwa, bali ujumbe unaowasilisha kwa maneno na muziki.

 

“Dini ya Kristo itasafisha kionjo, kutakasa akili, kuinua, kutakasa, na kuadilisha nafsi.”14 Badala ya kujumuisha mitindo ya muziki isiyofaa katika muziki wetu wa kidini, tutatoa muziki mtakatifu na unaoinua kwa Mungu na wale wanaotuzunguka.

 

“Hebu tujifunze wimbo wa malaika sasa, ili tuuimbe wakati tunapojiunga na viwango vyao vinavyong’aa.”15 Kwa neema ya Mungu, tunaweza “kuandaliwa kuungana na waabuduo katika nyua za mbinguni, ambako kuna usafi na ukamilifu, ambako kila kiumbe kina heshima kuu kwa Mungu na utakatifu wake.”16

Ujumbe wa Mhariri: George W. Brown, aliyekuwa mwenyekiti wa Divisheni ya Amerika Kati, anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 100 ifikapo Januari 11. Mjukuu wake wa kike, Nicole, aliketi chini pamoja naye ili kujadili urithi wake.

 

Tangu utotoni nilijua George W. Brown alikuwa mtu mashuhuri. Uelewa wangu wa ukuu wake ulikuwa jibu, si wa kuchunguza jitihada zake za huduma, bali wa uchunguzi wangu kwake katika nyakati za karibu sana. Nina fursa ya pekee sana kama mjukuu wake ya kumuona kama mume, baba, babu, na rafiki. Nimeona upuzi wake, ucheshi wake wa kustaajabisha, na utundu wake wa kufurahisha anapochangamana na wajukuu wake. Mimi pia ni shahidi mzuri wa akili yake. Opa wangu ana hekima ya kuheshimika na hufanya usuluhishi mkubwa. Kwa hakika, nimepewa ufahamu juu ya utata wa kina wa tabia yake.

 

Ilikuwa ni wakati wa Kikao cha Konferensi Kuu huko Atlanta mwaka 2010 ambapo nilianza kufahamu athari ya opa wangu kama kioo cha jamii na kiongozi wa kiroho. Kama mtoto, wanafamilia wa mtu huwapo tu katika muktadha wa majukumu yao. Mama yangu alikuwa Mama tu, si Arlene. Baba yangu alikuwa Baba, si Miguel. Na babu yangu alikuwa Opa tu, na si George W. Brown. Wakati huo sikuwa na uwezo wa kufahamu miaka yake 40 na zaidi ya utumishi katika kanisa, ambao ulijumuisha miaka 13 kama mwenyekiti wa Divisheni ya Amerika ya Kati. Nilichojua ni kwamba tuliruhusiwa kuketi kwenye ghorofa ya chini ya vikao, na kwamba ilichukua takribani dakika 40 kwetu kuondoka mahali pa kukutanikia kwa sababu ya watu kumzuia ili kumsalimia au kushiriki mafanikio makubwa katika muda wa huduma yake waliyopata katika maisha yao.

 

Kadiri ninavyokua na kuanza kujihusisha katika huduma na ubia wa kanisa, kutafuta hekima ya babu yangu na huduma yake imekuwa muhimu zaidi na zaidi. Kwa heshima ya urithi wake, nilimuuliza maswali ambayo yanaweza kuwanufaisha waumini wa rika zote.

Katika maisha yangu marefu na huduma nimejifunza mambo mengi kuhusu Mungu hatua kwa hatua. Mungu ninayemjua, ninayempenda, na kumtumikia ni zaidi ya Mungu mkuu, mwenye uwezo wote, ajuaye yote, aliyeko daima ambaye ni Muumba, anayetegemeza, na mlinzi. Yeye ni mfano halisi wa kujitoa, mwenye upendo usio na masharti, rehema, na neema ya ajabu. Yote ambayo Mungu aliyo yalidhihirishwa katika maisha, huduma, na kafara ya Yesu Kristo kwa wanadamu wote. Nimejifunza kwamba pasipo Yeye siwezi kuishi na pasipo Yeye sithubutu kufa.

Nimejifunza kwamba huduma ni mwaliko wa Mungu wa neema kwa wafuasi Wake kuwa “watendakazi pamoja Naye” (2 Kor. 6:1) katika mpango Wake wa ukombozi kwa wanadamu walioanguka. Nimejifunza kwamba neno huduma linajumuisha mengi zaidi ya huduma ya kichungaji. Shughuli zote za kanisa zinazokidhi mahitaji ya binadamu, ziwe za kiroho, kihisia, kimwili, au kiakili, zote ni sehemu ya huduma takatifu ya upatanisho—urejeshaji wa sura ya Mungu katika jamii ya wanadamu. Huduma ni kujitoa nafsi kwa ajili ya ukombozi wa watu.

Nimejifunza kwamba uongozi wa kweli unaendeshwa na kielelezo cha uongozi wa utumishi wa Yesu Kristo. Kielelezo cha uongozi wa Kristo ni kinyume cha dhana ya ulimwengu ya uongozi. Katika miaka yangu mingi ya uongozi wa kichungaji na utawala nimejifunza kwamba uongozi wa kweli siku zote ni ule uliojikita kwa Kristo, unaoongozwa na huduma, wa ukombozi, na wa kuleta mabadiliko. Wafilipi 2:5–8 inaeleza kwa ufupi kiini cha uongozi wa Kikristo. Kuiga mtindo wa uongozi wa Kristo hutuwezesha kuongoza kwa unyenyekevu, uadilifu, upendo, na uaminifu.

Mojawapo ya kanuni za msingi ambazo nimejifunza kuhusu uanafunzi ni kwamba unahitaji kujitolea. Dietrich Bonhoeffer, katika kitabu chake cha The Cost of Discipleship, alifafanua uanafunzi kama “uhusiano wa namna ya pekee” katika mwili wa Yesu Kristo. Hili ni mojawapo ya hitaji kuu la uanafunzi. Uanafunzi wa kweli unaongozwa na upendo wa kujitoa bila mipaka. Uanafunzi pia unadai utiifu wa hiari katika utawala wa Yesu Kristo. Kwa mfuasi wa kweli, utii kamwe si mzigo bali ni furaha na upendeleo wa thamani sana. Hii inadokezwa katika Mathayo 28:18. Uanafunzi ni zaidi ya kujifunza injili; ni kuishi na kushiriki injili, hivyo kufanya wanafunzi kwa ajili ya Mwalimu Mkuu.

Miongoni mwa mambo mengi ninayotamani kanisa letu lingeweza kukumbuka ni kwamba Mungu analiita kanisa lake la nyakati za mwisho kusimama imara katika mimbari ya kweli ya Biblia aliyotupatia kama watu wake wa nyakati za mwisho. Ni jambo la muhimu kwamba tukumbuke utajiri wa urithi wetu, asili yetu ya unabii, na agizo letu muhimu kwa ulimwengu lililounganishwa katika ujumbe wa malaika watatu wa Ufunuo 14:6-12. Kumbuka kwamba Waadventista sio tu kanisa lingine la Kiprotestanti. Ni harakati ya kiunabii yenye ujumbe wa pekee kwa ulimwengu—injili ya milele. Kama kanisa tunahimizwa “shikeni sana nguzo imara za imani yetu. Kanuni za kweli ambayo Mungu ametufunulia ndiyo msingi wetu pekee wa kweli. Zimetufanya kuwa jinsi tulivyo.”*

Ningependa wafahamu kwamba ufunguo mkuu wa huduma yenye mafanikio ni kutiwa nguvu na Roho Mtakatifu (Mdo. 1:8; Zek. 4:6). Roho Mtakatifu hawezeshi vyombo, taasisi, mashirika, au teknolojia ya hali ya juu. Anawatia nguvu wanaume na wanawake wanaojisalimisha kikamilifu kwa utawala wa Yesu Kristo. Wote wanaoingia katika huduma wanapaswa kujilinda kwa uangalifu dhidi ya maovu ya utaasisi, upagani, na uvuguvugu wa Laodikia. Mafanikio katika huduma yanahakikishwa pale yanapokuwa yamejikita katika Kristo, yanaongozwa na Roho, yanaenda sambamba na Biblia, na yamejawa na utume!

Wapo wachache wanaoweka kila kitu ambacho wamekamilisha katika maisha kwenye miguu ya Baba yao wa mbinguni na kumaanisha kwa moyo wote.

Akionyesha hatua za maisha yake kwa kukua kwa imani yake, Opa amekataa kukaa bila kubadilika katika eneo lolote la maisha yake, akijipa changamoto yeye na kanisa lake kurudi daima kwenye Maandiko, akisihi kujichunguza kwa nia ya kukua badala ya dhana kwamba tumekusanya kila kitu tunachopaswa kujua ndani ya uzuri mkubwa wa Neno la Mungu.

 

Maktaba yake ya nyumbani ni kazi ya mfano bora ya imani yake, familia yake, na kazi yake, na vitabu vya kila mada vikijaza rafu. Mapambo yanayosifu maisha yake katika huduma yanapamba ukuta, yaliyopangwa na picha za familia yake, wa kibaiolojia na wengineo. Opa wangu, mwenye upendo, mzuri sana, mtu mwenye akili, na hodari, ameishi maisha yake katika kumtukuza Mungu kwa unyenyekevu.

 

Wakati wote amesema, “Vyote nilivyo na nilivyotimiza ninawiwa na neema ya ajabu ya Mungu na malezi na msaada wa kanisa langu pendwa.” Kwa mujibu wa George W. Brown, Kanisa la Waadventista wa Sabato limekuwa na matokeo makubwa katika maisha yake.

Leo Ebenezeri si jina lililozoeleka. Mtu anaweza hata kusema ni jina la msimu, linalojitokeza kila Desemba. Uchunguzi usio wa kisayansi miongoni mwa marafiki na washiriki katika kazi ulionekana kuthibitisha hili. Wote walihusisha jina pamoja na Ebenezer Scrooge, mhusika mkuu katika hadithi ya Charles Dickens, A Christmas Carol. Japokuwa haijihusishi na ukweli wa hadithi ya Krismasi ya Mwokozi ambaye alizaliwa ili kuukomboa ulimwengu, lengo lake ni kuwakumbusha watu kuwapenda jirani zao.

 

Katika Biblia tunakutana na Ebenezeri tofauti. Nabii Samweli akalisimamisha jiwe la ukumbusho na kuliita Ebenezeri (1 Sam. 7:12). Maana halisi Ebenezeri ni “jiwe la usaidizi.”

 

Katika tukio hili; ilikuwa ni kuwakumbusha wana wa Israeli kwamba Bwana amewasaidia hadi katika hatua ile. Baada ya mifululizo ya kushindwa, iliyosababisha kupotea kwa Sanduku la Agano, Israeli walitubu na Bwana akawapatia ushindi. Kufuatana na ushindi, Samweli akasimamisha Ebenezeri. Ilipaswa kuwa mahali ambapo wangeweza kupeleka watoto wao na kuwaambia habari za wema wa Mungu, rehema na ukombozi.

 

Duniani pote utakapokwenda, utakuta ukumbusho wa miundo na ukubwa mbalimbali: sanamu, matao, piramidi na majengo, yote yakitoa hadithi, matukio hayo yaliyotokea zamani hayajasahaulika.

 

 

KUKUMBUKA UONGOZI WA MUNGU

Ellen G. White alielewa umuhimu wa kumbukumbu, wa kusimulia habari za uongozi wa Mungu. Katika matukio kadhaa; aliandika kuhusu uhitaji huu wa kukumbuka. Katika Life Sketches tunasoma:

 

“Katika kupitia historia yetu, kwa kusafiri katika kila hatua ya maendeleo hadi mahali tulipo, ninaweza kusema, Bwana Asifiwe! Ninapoona kile ambacho Mungu ametenda, ninajawa na mshangao pamoja na matumaini katika Kristo kama kiongozi. Hatupaswi kuogopa kwa ajili ya kesho, isipokuwa pale tutakaposahau jinsi ambavyo Bwana ametuongoza na mafundisho Yake katika historia.”*

 

Kwa ufafanuzi, tunapokumbuka jinsi Mungu alivyotuongoza hapo awali, tunaweza kwenda mbele kwa matumaini. Katika nyakati ambapo dunia inaonekana kutokuwa na uthabiti, kuwa na vita, matetemeko na majanga yanayotokea kwa haraka matukio yaliyogonga vichwa vya habari hapo kabla yanachukuliwa nafasi na matukio yajayo yasiyofikirika, tunakumbuka kwa namna gani? Tunawezaje kuwa na matumaini ambayo Ellen G. white alikuwa akiyaongelea?

Njia moja ni ya pamoja na binafsi “Ebenezeri.”

 

Huduma ya Adventist Heritage (Urithi wa Kiadventista) ni huduma maalum inayotusaidia kukumbuka. Kwa asili ikiitwa Adventist Heritage Properties (Miliki za Urithi wa Kiadventista), ilianzishwa mwaka 1981 ikiwa na kauli mbiu “The Past With a Future” (Yaliyopita Yaliyo na Mtegemeo wa Baadaye). Jina lake lilibadilishwa kuwa Adventist Heritage Ministries (Huduma za Urithi wa Kiadventista) mnamo 1994 na leo inamiliki na kuratibu maeneo manne ya urithi maalum na muhimu kwa ajili ya historia ya kanisa letu.

 

Kama jina lake linavyosadifu, Shamba la Miller lilikuwa ni makazi ya William Miller, ambaye, katika miaka ya 1830 mwishoni, hadi mwaka 1844, alihubiri kuhusu ujio wa Yesu ulio karibu sana. Karibu na nyumba; kuna kanisa dogo lililojengwa na Miller mwenyewe, na mwamba, ujulikanao kama Ascension Rock (Mwamba Mpao). Si yakini waumini walisimama juu ya mwamba wakimsubiri Yesu, lakini ni alama ya ukumbusho wa tumaini la wale waliosubiri, wenye shauku, wenye matumaini na kutarajia kumwona Yesu mnamo Oktoba 22, 1844.

 

Shamba la Hiram Edson ni ardhi na kihenge vilivyounganisha aliyoshuhudia Hiram Edson muda mfupi baada ya Kukatishwa tamaa Kukuu. Umaizi wa Edson kuhusu patakatifu pa mbinguni pamoja na vyumba viwili na Yesu kutoka patakatifu kuingia patakatifu pa patakatifu; uliongoza kwenye ufahamu sahihi wa kile kilichotokea mwaka 1884. Yesu hakuwa anarudi; bali ilikuwa ni mwanzo wa hukumu ya upelelezi. Yesu alikuwa anarudi hivi karibuni, hata hivyo.

 

Kijiji cha Historia ya Kiadventista kipo Battle Creek, Michigan. Mambo mengi ya kale ya historia ya Kiadventista kiini chake ni Battle Creek. Makazi mengi na majengo mengi yapo katika Kijiji cha Historia ya Kiadventista na karibu yake kuna maeneo mengine kama vile, Oak Hill Cemetery na makaburi ya familia ya White.

 

Makazi ya Bates huko Fairhaven, Massachusetts, ndipo Joseph Bates alipokulia. Kisa chake ni cha kuvutia si kwa ajili ya Waadventista wa Sabato bali pia kwa watu wa Fairhaven, wanaomuona kama mtu muhimu katika historia, mbali na dhima yake ya kuwa mwanzilishi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato.

 

 

MASHAHIDI WENYE NGUVU

Kila eneo ni tofauti, na bado kila moja ni shahidi mwenye nguvu kwa wema wa Mungu na uaminifu Wake kwa watu Wake katika nyakati za kukata tamaa, wakati giza lilipoonekana kuwazingira na walipohisi kana kwamba wametelekezwa. Maeneo yanasimulia visa vya wanaume na wanawake wakosefu. Walikuwa na mapungufu yao, kama tunavyotenda, na bado walitumiwa na Mungu kuwaambia wengine kuhusu habari njema ya hukumu na mwisho wa maumivu na mateso katika ulimwengu huu, na kujiandaa kwa ajili ya ujio wa Yesu mara ya pili.

 

Haya si majengo yaliyokufa, kuchukua muda, nguvu na raslimali za fedha. Hivi ni vituo halisi ambapo historia ya Kiadventista huishi, ambapo tunaweza kukumbuka uongozi wa Mungu na kujifunza masomo ya zamani. Kuna mahali ambapo vijana wanaweza kuja na kuvutiwa, na kwa watu wasiojua historia yetu wanaweza kuja na kujifunza kuhusu Mungu aliye mwaminifu. Panasimama kama kioleza kutangaza wema wa Mungu.

Haya ni maeneo machache tu; yapo mengine mengi. Ni muhimu kuyafahamu, kuyatafuta na kuyaacha yasimulie visa vyake.

 

Imewahi kusemwa kwamba, “Wale ambao hawawezi kukumbuka yaliyopita wako hatiani kuyarudia.” Ikiwa hatujui historia yetu iliyo pamoja, tuko katika hatari ya kurudia makosa yaliyopita. Vivyo hivyo inaweza kuwa katika historia zetu binafsi. Karibu na kitanda changu kuna fremu mbili zenye maandishi yenye thamani kubwa. Ninapoyatazama, ninakumbuka hali ambayo kwayo yalileta maana. Wakati wote yananipa faraja, ujasiri na kufanya upya imani katika Bwana. Yeye hashindwi.

 

Tunapouanza mwaka 2024, hebu tutafute Ebenezeri binafsi na wa pamoja na kukumbuka uongozi uliopita wa Mungu, ili tuweze kuukabili mwaka mpya kwa tumaini na ujasiri.

Bila shaka, Mungu anawafikia watu kupitia Roho katika maeneo ambapo hakuna kanisa la masalio. Swali lako linaonekana kuwa ni kwa nini Yeye asifanye vivyo hivyo kila mahali, hivyo kulipunguzia kanisa jukumu la utume. Kwa dhahiri Mungu anaweza kufanya chochote anachojua ni bora katika kukamilisha mapenzi Yake ya kuokoa. Hata hivyo, Yeye alichagua kutujumuisha sisi, kanisa, katika ufanikishaji wa utume Wake kwa kusudi jema.

 

 

KATIKA UTII KWA KRISTO

Utiifu wa kanisa kwa Yesu Kristo unajitokeza kwa njia fulani katika kutangaza injili kwa ulimwengu unaopotea. Wakati wa huduma Yake duniani, Yesu aliwapatia mafunzo wanafunzi Wake kwa ajili ya utume (Luka 10:1-11), baada ya kufufuka aliwapatia rasmi Agizo Kuu (Mt. 28:18-20), na baada ya kupaa Kwake, Kristo aliwawezesha kutimiza utume huo (Matendo 1:8). Kanisa linatoka kwenda kutimiza utume ambao Bwana aliyefufuka aliukabidhi kwa walio waaminifu Kwake. Inaweza kusemwa kwa hakika kwamba kanisa ni kanisa la Kristo wakati linapojihusisha katika kazi ya utume. Kanisa na utume ni kama roho na mwili; kanisa la Kristo huwako tu katika umoja wa vitu hivyo viwili. Utume ambao Mungu anatuitia hauwezekani bila kanisa na kanisa limekufa bila utume. Wakati kanisa, kwa utii kwa Bwana, linatimiza utume, ni kanisa lenye uhai; linaimarika kwa nguvu ya Roho.

 

 

USHIRIKI KATIKA MGOGORO WA KIULIMWENGU

Nguvu za uovu zimefunika ukweli mtakatifu na matokeo yake yamekuwa ni mgogoro mkubwa wa kiulimwengu. Maisha, huduma, kifo na ufufuo wa Kristo vilionyesha ukweli kuhusu tabia ya upendo ya Mungu, hivyo kufunua udanganyifu wa uovu. Kristo alikuwa shahidi kwa upande wa utetezi (Ufunuo 1:5; 3:14).

 

Ushiriki wetu katika mgogoro huo unafikia hatua muhimu sana ambapo kwa upendo tunakwenda kama mashahidi tukitangaza kuhusu kile alichokifanya Kristo ili kuwarejesha wenye dhambi katika upatanifu na Mungu (2 Wakorintho 5:17-20). Kwa kuwa wote wanashiriki katika mgogoro wa kiulimwengu, Shetani pia hutumia wanadamu kutoa ushahidi kwa ajili ya kusudi lake ulimwenguni linalotangaza udanganyifu na kumwondoa Kristo. Ushiriki wa kanisa katika utume ni utekelezaji wa haki ya Mungu iliyoletwa na Kristo kwa kanisa, yaani, kuwa shahidi wa Kristo katika mgogoro kati ya mwanga na giza.

 

 

KUREJESHA SURA YA MUNGU NDANI YETU

Mojawapo ya njia ambazo Mungu hurejesha sura Yake kwa wenye dhambi waliotubu ni kupitia ushiriki wao katika utume. Ni kweli kabisa kwamba utume ni kazi yenye asili yake kwa Mungu na kwamba unatekelezwa kupitia kazi ya Mungu. Kabla hakujawa na kanisa, Uungu uliandaa utume wa uokoaji ambao washirika watatu wa Uungu wangeshiriki. Kwa maana hiyo, mmishonari wa kwanza alikuwa ni Uungu, ambapo utume Wake ulikuwa dhahiri kikamilifu kupitia kazi ya utukufu wa Mwana wa Mungu. Mungu alitushirikisha katika utimizwaji wa utume Wake na wakati ambapo hakuna chombo cha kibinadamu kilichopo ili kutumiwa na Yeye, utume unaendelea hata hivyo. Roho anatimiza.

 

Tunapofanya, kwa utii kwa Kristo, kutimiza jukumu la haki ya kushuhudia kwa ajili Yake katika mgogoro wa kiulimwengu, tunabadilishwa kulingana na sura ya Yule ambaye ni katika Yeye alifanyika mwili wa utume wa Mungu.

Sababu ya kawaida ya kupanda juu kwa uzito ni kuongezeka kwa tishu za mafuta kupitia ulaji mwingi wa kalori ikilinganishwa na matumizi ya nishati kupitia mazoezi/shughuli za kuushughulisha mwili. Mabadiliko madogo ya kila siku ya uzito yanaweza kuonyesha mabadiliko katika usawa wa maji na uhifadhi wa maji. Kuongezeka kwa ulaji wa chumvi kunaweza kusababisha uhifadhi zaidi wa maji. Tofauti za homoni za kike (estrogen na progesterone) zinaweza kusababisha uhifadhi wa maji na mabadiliko ya uzito juu ya mzunguko wa kila mwezi wa hedhi kwa wanawake.

 

Baadhi ya magonjwa yanaweza kusababisha kuongezeka kwa uzito. Mojawapo ya haya ni kupungua kwa uzalishaji wa homoni za tezi (hypothyroidism). Kushindwa kwa moyo kufanya kazi kunaweza kusababisha kuongezeka kwa maji, kuhifadhi chumvi, na kuongezeka kwa uzito. Kunaweza kuhusishwa na kuvimba kwa vifundo vya miguuni, miguu na hata tumbo. Dalili zaidi zinaweza kuwa upungufu wa pumzi na uchovu. Kushindwa kufanya kazi kwa figo kunaweza pia kusababisha uhifadhi wa maji na kuongezeka kwa uzito usiohusiana na ulaji wa vyakula/kalori kupita kiasi.

 

Umetaja kuwa na ratiba iliyokubana sana. Kwa hakika hii inaweza kuchangia kuongeza uzito kwani msongo wa mawazo husababisha kuongezeka kwa homoni ya cortisol ambayo huchochea hamu ya kula na kuongeza uhifadhi wa mafuta mwilini. Msongo unaweza pia kuhusishwa na ulaji wa vyakula vya kuvutia ambavyo kwa kawaida huwa na kalori nyingi, vilivyojaa sukari, mafuta yasiyofaa na chumvi. Zaidi ya hayo, mifumo duni ya usingizi inaweza kuongeza viwango vya homoni zinazohimiza kula na kupunguza homoni zinazopatanisha hisia ya kushiba (shibe) wakati wa kula.

 

Dawa fulani zinaweza kuathiri uzito wa mtu. Dawa za kuzuia uvimbe zinazotumiwa kwa kawaida zinaweza kusababisha uhifadhi wa maji na kushuka kwa viwango vya uzito wa kila siku. Baadhi ya dawa za kuzuia mfadhaiko zinaweza kuchochea hamu ya kula na kuendelea kuongezeka uzito.

 

Tumetaja uhifadhi wa maji mara kadhaa. Kunywa maji safi na epuka vinywaji vyenye sukari. Hata juisi safi za matunda husheheni sukari ya matunda (kalori) ambayo huongeza uzito bila faida ya nyuzinyuzi zinazotumiwa wakati tunda zima linapoliwa. Jihadharini na vikoleza utamu bandia. Tutazungumza zaidi juu ya hili katika safu inayofuata.

 

Mwanzo wa mwaka mpya ni wakati mzuri wa kutathmini upya tabia zetu za afya. Hebu tusifanye tu maazimio ambayo tutayavunja hivi karibuni. Badala yake, kwa neema ya Mungu, na tuweke malengo yanayowezekana na mshirika wa kuwajibika (mwenzi wa ndoa, rafiki wa karibu). Zingatia mambo matano ya kufanya mwaka huu:

  • Jipime kila asubuhi kabla ya kifungua kinywa na kabla ya kunywa maji. Watu wanaojipima kila siku wana uwezekano mkubwa wa kupunguza uzito na kudumisha uzito wao.
  • Nakili uzito wako kwenye chati.
  • Kimsingi kunywa maji safi, na murua.
  • Kula milo ya kawaida na epuka vitafunwa katikati na kabla ya kulala.
  • Kuwa na ukaguzi wa afya wa kila mwaka na uchunguzi wa kimetaboliki, ikijumuisha sukari, kolesteroli na lipoidi, na uchunguzi wa tezi. Kupima kiwango cha homoni ya kuchochea tezi (TSH) kunaweza kuwa bora.

Kumbuka kutia moyo kwa mtume Paulo: “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu” (Flp. 4:13). Mwaka Mpya huu uwe mwaka wa afya na furaha ndani Yake. Maranatha!

Mamia ya wachungaji walikuwa wamekuja mjini, wakisalimia marafiki wa zamani, kwa haraka wakitengeneza marafiki wapya, wote wakielekea katika kituo cha mkutano kwa ajili ya mkutano mkubwa. Ishara kubwa zilionyesha kwamba walikuwa wakija kujifunza njia bora za kushiriki upendo wa Mungu.

 

Mchungaji mmoja alikaa peke yake katika maegesho ng’ambo ya kituo cha mkutano. “Sio rahisi,” aliniambia. “Nilikuja kwa ajili ya mikutano, lakini nilipouelekea mlango, Mungu alinizuia na kusema ninapaswa kukaa hapa, katika meza hii ndani ya maegesho haya, badala ya kuingia ndani.”

 

 

WANAWEZAJE?

Alitazama umati wa watu walivyo na shughuli nyingi, kisha mwanamke alivuta makini yake alipomtazama. Alikuwa mdogo, mwanamke ambaye hakuonekana kwa mamia ya wachungaji wakifungua na kufunga malango ya kituo cha mkutano.  Mmoja wa wasio na makazi wanaonekana katika umati wa watu wakiwa na mabango wakitangaza mahitaji yao na njaa yao. Alisimama karibu na mlango kadiri inavyowezekana, harufu ya mwili wake mchafu ikisambaa ndani ya ukumbi kila baada ya milango ya kioo kusogea.

 

“Nilitazama,” mchungaji aliyekaa nje alisema. “Nikisubiria mtu fulani ampatie chakula kidogo, chupa ya maji, au tabasamu. Badala yake, japokuwa wote walimwona, kila mmoja kwa tahadhari aliepuka kumtambua.”

 

Alipeperusha bango lake. Aliruka-ruka, japo si juu sana. Aliimba kwa kukosea baadhi ya noti. Alilia. Hakuna kilichofanya kazi na mifuko yake iliendelea kuwa tupu.

 

Mtiririko wa wachungaji kuingia ukumbini ulipungua wakati wimbo wa injili ulipotoka ukumbini, ukimpita mwanamke wa mtaani, kuelekea kwenye msongamano wa sauti za mihangaiko ya siku iliyohanikizwa.

 

Aliegemea katika ukuta. Akiomboleza, akitamani, akishangaa. Akifuta machozi kwa jaketi lake chafu la mikono mirefu. Leo itakuwa siku sawa na siku zingine, yenye njaa, maumivu, kukataliwa, na yenye machozi.

 

Mchungaji alianza kuandaa hubiri alilopenda kuhubiri kwa wachungaji ambao hawakumjali msichana huyo.

 

“Ilinifanya nikasirike sana,” alinung’unika. “Hapa kuna msichana mdogo mwenye bango linalosema hana makazi na kwamba hana msaada, lakini hakuna mchungaji hata mmoja aliyemsaidia! Sikumfanya Mungu ajivunie sana kwa wakati ule kwa sababu nilikuwa na mawazo mabaya. Nilikuwa ninakasirika!”

 

Ndipo Mungu alisema. “Wewe. Ndio Wewe, Mchungaji Gabe. Unajua jinsi ya kufanya hili. Kwa nini usiende na kumsalimu?”

 

“Ndiyo nitafanya,” Mchungaji Gabe alitabasamu. “Nitafurahi kufanya hivyo!”

 

 

NINGEFANYA NINI?

Alisimama na taratibu alikwenda ng’ambo ya barabara kwenye njia ya mlango wa kituo cha mkutano.

 

“Habari ya asubuhi,” alisema, macho yakikutana naye, uso wake ukiwa mkunjufu na wa kukubali. “Jina langu ni Gabe.

 

“Mimi ni Monica,” alimumunya, bila kufikiri akivuta jaketi lake akilibana, kana kwamba akijihami dhidi ya matusi ambayo alijua yangefuata.

 

“Pana meza pale pamoja na kivuli. Je, ungependa kuketi na kuzungumza?”

 

Hakutarajia mwaliko wake, alimfuata, kama mtoto wa paka aliyepewa bakuli la maziwa.

 

Alimwambia kuhusu Mungu alivyomfikiria, kwamba alikuwa mzuri na jinsi ambavyo Mungu alimpenda. Kisha alimuuliza kama alishawahi kusikia kuhusu Yesu, kama ameshawahi kukutana Naye na kama angedhani kwamba ingekuwa vyema kuwa na uhusiano Naye.

 

Monica alisema ndiyo na wote wakalia. Kisha wakaomba. Mchungaji na msichana, mezani katika kivuli, nje ya kituo cha mkutano.

 

“Unahitaji nini?” Mchungaji Gabe aliuliza.

 

“Sijawahi kabisa kuwa ndani ya nyumba kwa miaka mingi. Siwezi kulala usiku. Ni hatari. Nimechoka. Nimechoka sana. Ninataka kuoga. Sijihisi kama mwanamke tena. Ninajihisi kama mnyama.”

 

“Je, una mahali ungependa kuishi?”

 

“Ndiyo,” alijibu. Kisha aliweka kituo.

 

“Ni kiasi gani cha pesa?”

 

“Ni kiasi kikubwa sana.”

 

Mungu alikuwa amemwandaa kwa ajili ya wakati huu. Kabla hajaja kwenye mkutano, Mchungaji Gabe alitembelewa na mtu aliyefahamiana naye zamani. Mtu yule alikuwa amesafiri kwa saa tatu, akamwomba Mchungaji Gabe kujumuika naye kwa ajili ya kifungua kinywa na kisha akampatia dola za kimarekani elfu moja. Pesa taslimu. “Ni pesa ya Mungu,” mtoaji alisema. “Itumie kwa ajili ya huduma.”

 

“Vipi kama nitakutoa mtaani na kulala ndani kwa siku 10?” Mchungaji Gabe aliuliza.

 

Macho ya Monica yaling’aa kama mng’ao wa moto uliosahaulika muda mrefu.

 

Ilichukua muda kidogo, lakini Mchungaji Gabe alimtafutia chumba cha kupanga na chakula kizuri. Bafu. Kitanda safi. Peke yake. Usiku na mchana, siku kumi. Salama.

 

 

NINI ZAIDI NINGEWEZA KUFANYA?

Mchungaji Gabe alirudi katika kituo cha mkutano, taratibu, akikumbuka tabasamu kwenye uso wa Monica, akitafuta mtu mwingine anayeweza kumtambua.

“Pale,” Mungu alimnong’oneza. “Mwone mtu yule aliyekaa peke yake kwenye majani baada ya majengo makubwa mawili? Ninataka wewe umwendee, kaa pembeni yake na muulize kama anatokea Jamaica.”

 

“Jamaica?” Mchungaji Gabe alicheka kwa ucheshi wa Mungu. “Huo ni wazimu, lakini ni sawa!”

 

Mchungaji Gabe alisubiri teksi kadhaa kupita, kisha alitembea taratibu kumwelekea mtu yule aliyekuwa amekaa peke yake kwenye majani, mwenye masikitiko akikaza macho yake angani.

 

“Habari,” Mchungaji Gabe alisema, “Ninao marafiki wengi nyumbani ambao ni watu watulivu sana, watulivu sana. Na, ah, wanatokea Jamaica na wakiwa na wakati mgumu, ah unajua, huwa wanaanza kuimba tu na ghafla maisha yanaanza kuonekana tofauti na roho zao huinuliwa na ghafla wamepata furaha ambayo hawakuwa nayo hapo kabla. Je, unajua kuhusu hilo?”

 

Mtu yule alimtazama Gabe, aliitikia na kuanza kuimba.

 

Kwa siku tatu zilizofuata, Gabe na rafiki zake wapya walikuwa mjini kote. Kutoka katika maeneo ya watu wanaobaguliwa hadi kwenye maegesho hadi kwenye bustani ya wanyama, kila sehemu akiwakusanya wengine waliohitaji kuwa sehemu ya kitu maalum.

 

“Hakika nitakuwa nimemshiriki Kristo pamoja, na kuomba pamoja na mamia ya watu! Na hili kundi kubwa la watu wa zamani waliotumia siku tatu zilizofuata walizunguka pamoja nami mjini kote. Jumapili asubuhi niliwachukua wote na kuwapatia kifungua kinywa mkahawani.

 

Tulilijaza eneo hilo na kuwa na wasaa mzuri sana. Ilipendeza sana. Ningeweza kuanzisha kanisa.”

Siku moja nilimwona mwanangu mdogo Ben mwenye umri wa miaka 5, amekaa dirishani akifurahia mwanga wa jua, alikuwa amejawa na tabasamu kubwa.

 

Nikamwambia “Ben, unafurahia mwanga wa jua, ee?” alinigeukia na kusema “Jamani mama, najisikia vizuri sana kuketi na kuota jua! Lina joto la kufurahisha. Linanifanya nijisikie kama ninavyojiskia nikiwa na bibi. Lo! hilo liliniachia mguso fulani.

 

Hata mtoto mdogo amegundua kwamba watu wanaweza kuwa kama mng’ao wa jua; wanaweza kuwa wakarimu na wakaribishaji, kuwafanya watu wajiskie wenye thamani na kukubalika.

 

Je, wajua kwamba tabia yako angavu inaweza kuwa ushuhuda mkubwa kwa ajili ya Yesu? Tunaishi katika dunia ambayo imejaa kukatishwa tamaaa kwingi, lakini kuona tabasamu la kijana mdogo huleta furaha na matumaini. Kuna watu wengi wanaoithamini furaha ya mtoto mwenye heshima.

 

 

KUWAFANYA WATU KUWA WENYE FURAHA

Ninamfahamu mtu kama huyu. Nilikuwa na rafiki katika shule ya msingi na sekondari aliyeitwa Delinda, ambaye alikuwa miongoni mwa watu wenye furaha zaidi niliowahi kuwajua. Ilionekana kana kwamba alikuwa akitabasamu wakati wote na kuwatendea watu kwa ukarimu.

 

Nilipata bahati ya kufanya naye kazi katika moja ya hospitali mahalia wakati wa majira ya joto kama mtunza mazingira. Ilikuwa ni kazi yetu kuzifanya bustani za maua kupendeza. Tuliyahudumia maua kwa kuyamwagilia na kuyapalilia kwa uangalifu. Mara kadhaa wagonjwa au wageni hutoka nje na kukaa ndani ya kajumba kadogo ili kufurahia maua na hewa safi. Gazebo [kajumba kadogo bustanini] hiyo ilikuwa katikati ya uga tulipokuwa tukifanya kazi na ilikuwa na mandhari nzuri kutokea ndani ya vyumba vya hospitali.

 

Siku moja, tulipokuwa tukifanya kazi, Delinda aligundua kuwa watu wengi walionekana kuwa na huzuni, waliochoka na wenye hofu.

 

“Lo! Kuna idadi ya watu wengi wenye huzuni hapa hospitalini,” Alisema Delinda.

 

“Uko sahihi, Ningetamani kama kungekuwa na kitu cha kufanya ili kuwafanya wajisikie vizuri,” nilijibu.

 

“Ninajua! Vipi kama tutaliweka hilo kuwa lengo letu ili kuona ni watu wangapi tunaweza kuwafanya watabasamu? Delinda alijawa na shauku.

 

“Tunawezaje kulifanya hilo?” Niliuliza.

 

“Vyema, lakini sijui. Labda tunaweza kuanza kutabasamu sisi kwanza, au tunaweza kuwasalimia au kuwa na mazungumzo mafupi nao,” Alijibu.

 

“Sawa sawa, inafurahisha! Changamoto imekubaliwa” nilicheka.

 

 

KUWAFANYA WATU KUTABASAMU

Tulianza mara moja, tukijaribu kuangaliana na wageni hao kadiri ilivyowezekana wakati tungali tukifanya kazi yetu. Tulianzia katika uga wa nje, kisha kwenye vitanda vilivyo karibu mbele ya hospitali. Na kisha tulimalizia kwenye Mlango wa Kuingilia Chumba cha Wagonjwa Mahututi. Kutwa nzima tulifurahia kuwaona watu wengi wakitabasamu. Wakati mwingine tulichotakiwa kufanya ilikuwa ni kutabasamu tu. Nyakati zingine tulikuwa na mazungumzo mafupi kabla ya kuliona tabasamu. Tumepoteza idadi ya ni watu wangapi tuliwafanya watabasamu, lakini ilikuwa ni njia nzuri ya kufanya muda usonge mbele.

 

Je, lilikuwa ni jambo kubwa tulilofanya? La hasha. Tunatumaini kuwa lilileta furaha kidogo kwa wagonjwa wetu pamoja na familia zao, lakini hatukujua matokeo yake zaidi ya tabasamu chache tulizorudishiwa.

 

Jambo dogo tu kama tabasamu la mwangaza wa jua linaweza kuleta tofauti kubwa. Litasaidia kuwaonyesha watu kwamba wale wanaomfuata Yesu ni wachangamfu na wenye furaha kama Yeye. Uchangamfu wako huakisi kile kilichosemwa katika 2 Samweli 23:4 kuhusu ujio wa Yesu wa mara ya pili: ”Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua lichapo, Asubuhi isiyo na mawingu. Lachipuza majani mabichi juu ya nchi, kwa mwangaza baada ya mvua.” Sijui kuhusu wewe, lakini kunajaribu kuwa na mawingu mengi ninapoishi, pale jua lichomozapo, hunipatia furaha zaidi! Inapendeza zaidi jinsi gani jua kuangaza bila mawingu, likileta furaha kwa wale wanaokuzunguka!

 

Ninafundisha katika Shule ya Sabato, na tunaimba wimbo huu wa watoto, unaoimbika hivi: “Ulimwengu huu unahitaji tabasamu, tabasamu tunaloweza kulitoa; changamfu, tamu na tabasamu lenye kuleta tumaini, kule tunapoishi na tunapofanya kazi. Kwa hiyo T-A-B-A-S-M-U, T-A-B-A-SA-M-U, hiki ndicho ulimwengu unachokihitaji—T-A-B-A-S-A-M-U.” Ni kweli: dunia hii inahitaji tabasamu zaidi—tabasamu lako!

 

Kadiri mimi na Delinda tulivyozidi kufanya kazi ya kuhudumia maua, haikuwa tu harufu nzuri ya maua ambayo tulikuwa tukiyafanyia kazi. Sisi pia tulikuwa tukishiriki harufu ya upendo wa Mungu kwa vitendo vidogo vilivyopendekezwa na rafiki yangu. Yale matendo madogo ya ukarimu yalichangamsha mioyo ya wengine, kama Upendo wa bibi yake Ben ulivyomkumbusha miale ya joto la mwangaza wa jua. Vipi kuhusu wewe? Ni njia zipi unazoweza kufanya ili kukuza furaha yako na kuwa ushuhuda kwa Mungu? Mwombe Mungu akusaidie kupata njia  za sio tu kuangaza kama jua, lakini pia kung’aa kama MWANA—Yesu Kristo.

Mchapishaji

Jarida la Adventist World, jarida la kimataifa la Kanisa la Waadventista wa Sabato. Konferensi Kuu, Divisheni ya Asia Pasifiki ya Waadventista wa Sabato ndio wachapishaji.

 

Mkurugenzi Mtendaji/ Mkurugenzi wa Huduma za Adventist Review

Justin Kim

 

Meneja wa Uchapishaji wa Kimataifa

Hong, Myung Kwan

 

Kamati ya Uratibu ya Jarida la Adventist World

Yo Han Kim (chair), Tae Seung Kim, Hiroshi

Yamaji, Myung Kwan Hong, Seong Jun Byun,

Dong Jin Lyu

 

Wakurugenzi wenza/ Wakurugenzi, Huduma za Adventist Review

Sikhululekile Daco, John Peckham, Greg Scott

 

Wahariri waliopo Silver Springs, Maryland, Marekani

Enno Müller, Beth Thomas

 

Wahariri waliopo Seoul Korea
Hong, Myung Kwan; Park, Jae Man; Kim, Hyo-Jun

 

Mkurugenzi wa Mambo ya Kidijitali

Gabriel Begle

 

Mkurugenzi wa Muungano wa Mifumo na Uvumbuzi

Daniel Bruneau

 

Meneja wa Shughuli

Merle Poirier

 

Mratibu wa Tathmini ya Uhariri

Marvene Thorpe-Baptiste

 

Wahariri /Washauri wengine

E. Edward Zinke

 

Meneja wa Fedha

Kimberly Brown

 

Mratibu wa Usambazaji

Sharon Tennyson

 

Mratibu wa toleo la Kanda (Adventist World)

Penny Brink

 

Bodi ya Utawala

Yo Han Kim, chair; Justin Kim, secretary; Hong,

Myung Kwan; Karnik Doukmetzian; SeongJun

Byun; Hiroshi Yamaji; Joel Tompkins; Ray Wahlen; Ex-officio: Paul H. Douglas; Erton Köhler; Ted N. C. Wilson

 

Maelekezo ya Usanifu na Muundo

Types & Symbols

 

Kamati ya Adventist World ya Divisheni ya Afrika Mashariki – Kati:

Blasious Ruguri, Musa Gideon Mitekaro, Tom Ogal, Emanuel Pelote.

 

Tafsiri

Ufunuo Publishing House, South Tanzania Union Conference.

 

Msomaji wa prufu

Lilian Mweresa

 

Usanifu wa toleo la Kiswahili

Daniella Batista, Ashleigh Morton, Digital Publications

 

Uchapishaji wa Kidijitali

Charles Burman, Digital Publications (www.digitalpublications.co.za)

 

Muelekeo wa Sanaa na Ubunifu

Mark Cook, Brett Meliti, Ivan Ruiz-Knott

/Types & Symbols

 

Kwa Waandishi: Tunakaribisha miswada huria. Tuma barua zote kwa uhariri kwa 12501 Old Columbia Pike, Silver Spring, MD 20904-6600, U.S.A. Faksi ya ofisi ya Uhariri ni: (301) 680-6638

 

Waraka pepe: worldeditor@gc.adventist.org

Tovuti: www.adventistworld.org

 

Rejea zote za Biblia zimechukuliwa kutoka kwenye Swahili Union Version Bible Toleo la Chama cha Biblia la mwaka 1952.

 

Jarida la Adventist World linachapishwa kila mwezi na kuchapwa kwa wakati huo huo huko Korea, Brazili, Indonesia, Australia, Ujerumani, Austria, Ajentina, Meksiko, Afrika Kusini, na Marekani.

 

Vol. 20, Na. 1

Swipe left

swipe left To move to the next page

Swipe right

swipe right To move to the previous page
Allow Send-it to use cookies?

Send-it uses cookies to track how you use the application. Find out more about what data we collect and how we use the data in our privacy policy.