powered by
send-it.me

Adventist World-Kiswahili inamshukuru kila aliyejisajili kwa ajili ya jarida hilo, kupitia kwa chaneli ya WhatsApp. Tumefurahia kupokea jumbe kutoka kwako, na vilevile ushuhuda wa jinsi umetumia jarida hili linalotia moyo kuwafikia wengine kwa ajili ya Kristo!

Tungependa kukujulisha kuwa tunahamia jukwaa jipya katika mwaka mpya. Zaidi ya yote, tungependa uhame pamoja nasi. Adventist World-Kiswahili haitaki kumwacha nyuma yeyote aliyejisajili.

 

Badala ya kupokea ujumbe wa WhatsApp pamoja na toleo jipya kila mwezi, tunakupa kiungo kwa tovuti ya bure ambayo ni nzuri kwa simu, ambapo unaweza kuyasoma makala yote, kama kawaida. Chaneli ya WhatsApp na tovuti mpya zitafanya kazi kwa wakati mmoja kwa miezi kadhaa kabla ya kuhamia hatimaye kwa chaneli mpya.

 

Pia tutakiweka kiungo hicho kwenye ukurasa wa Facebook wa Adventist World-Kiswahili kila mwezi, ambapo unaweza kututumia jumbe na taarifa kuhusu jinsi makala hii inakufaidi wewe na jamii yako. Pia unaweza kututumia maoni na mapendekezo tutakayoangalia jinsi ya kuifanya makala hii iwafae zaidi wasomaji!

Ukipenda, unaweza kutuma baruapepe:
charles@digitalpublications.co.za

Moja ya manufaa ya tovuti mpya ya Adventist World-Kiswahili ambayo ni nzuri kwa simu, ni kwamba kutakuwa na lugha zingine nyingi za kuchagua, ikiwa ungependelea Kiingereza au lugha nyingine yoyote, unaweza kuangalia kama ipo, kando na ile ya kawaida ya Kiswahili.

 

Manufaa mengine ni kwamba ni rahisi kushiriki kiungo hicho kipya cha Adventist World-Kiswahili, kwa marafiki na familia. Tunakuhimiza ufanye hivyo, kwa sababu tayari inafanya kazi. Hebu iangalie sasa hivi.

 

Tunatumai kuwa na uhusiano mrefu na wa furaha na wasomaji wa Adventist World-Kiswahili.

 

Mungu akubariki,

 

Kundi la Adventist World-Kiswahili

Tunaamini katika nguvu ya maombi, na tunakaribisha hitaji la maombi ambayo tutashiriki katika ibada ya watendakazi kila Jumatano asubuhi. Tuma maombi yako kwa prayer@adventistworld.org, na utuombee tunapofanya kazi pamoja kuendeleza ufalme wa Mungu.

 

Picha ya jalada: Vitaliy Gavrushchenko

Mara tano. Kuna mada chache ambapo Yesu anasema jambo lile lile mara tano. Katika visa vingi, wazo moja limenukuliwa katika sehemu nyingi, kama vile Mathayo, Marko, na Luka. Lakini katika Mathayo 6 Yesu anarudia jambo mara tano (mistari 25, 27, 28, 31, na 34)—na katika mpangilio mmoja, pia.

 

Na jambo lenyewe ni “Msisumbuke.” Usisumbuke, Yesu anasema. Ni rahisi kusema hivyo, bali ni vigumu sana, kama sio kwamba haiwezekani, kuishi huko kutokusumbuka. Inawezekanaje mtu asisumbuke? Ndani ya mzunguko wa saa 24, mtu anawezaje kutokufikiria migogoro midogo kuwa vita vya kimataifa; au janga lingine, au maafa mapya ya kibayolojia; au uchumi unaoelekea kuharibika? Au yote haya—na zaidi.

 

Labda wewe ndiye mtu ambaye hujiuliza maswali haya binafsi kama vile “Ni nini kitatokea katika maisha yangu? fedha zangu? mahusiano na jamaa? watoto na wajukuu? ndoa, siku zijazo, kustaafu?" (Labda ulikuwa sawa tu hadi usomapo makala hii.)

 

Kuelekea mwishoni mwa Mathayo sura ya 6, Yesu anatamka fungu Lake maarufu sana, “Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki Yake; na hayo yote mtazidishiwa” (fungu la 33). Kutafuta kunamaanisha kusakanya kwa bidii kitu ambacho hukulazimika kuanza nacho. Kwanza huashiria mpangilio na kipaumbele kinachotolewa, iwe ni katika muda, umakini, kiasi, na/au mkazo. Kwa ufupi, ufalme na haki huelekeza katika kuishi maisha ya Kristo ndani na nje, ukiwa na matunda na tabia ya Yesu.

 

Ingawa, kirai kinachovutia ni hayo yote. Mstari wa 32 unasema watu wa Mataifa huyatafuta na, kwa kuhitimisha, wafuasi wa kweli wa Mungu hawapaswi kuyatafuta. Pili, Baba anajua kwamba tunahitaji “vitu hivi vyote.” Na ikiwa tunatafuta mambo haya, sisi tena kwa kuhitimisha tunasema kwamba Baba hajui ukweli huu. Kwa maneno mengine, wasiwasi wa watoto unakataa kwamba Baba anajua yote. Je, hali yetu ya kihisia inaelekeza thiolojia yetu ya asili?

 

Je, hayo yote ni nini? Mathayo 6:19, 20 inasema hizi ni mali za dunia hii. Tatizo ni, iwe kwa nondo (kuoza kibaiolojia), kutu (uharibifu wa mazingira), au wizi, vitu hivi vya kidunia vinavyotafutwa kwa bidii, hatimaye, vitapotea. Badala ya kuvitafuta kwa shauku kubwa, Mungu atatupa hayo yote tukimtafuta Yeye kwanza. Yeye na hayo yote havichangamani; bwana mmoja lazima achaguliwe. Kama Yesu asemavyo, “Wayahudi wa kweli” wanamtafuta Mungu, lakini “Wamataifa” wanatafuta mambo hayo yote.

 

“Usisumbuke” inamaanisha kuwekeza mbinguni kwa kiwango cha faida bora zaidi ulimwenguni. Hii sio amri au ushauri, lakini ni ahadi (mara tano) yenye nguvu ya ubunifu ya kupanga upya maisha ya kiroho, ikiwa tu tutakumbatia maneno ya Yesu kwa imani. Kama nuru ilivyoibuka kutoka kusikokuwa na kitu, hebu amani Yake na ituzukie kutoka kwenye mashaka yetu.

Ana-Marija mtengeneza makala ya kuburudisha au ya kutoa mafunzo (content creator) kutoka Montenegro, akimnasa William S. Costa, Jr., mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Konferensi Kuu, huku akiomba wakati wa tukio la GAiN Europe huko Budva, Montenegro.

“Watengenezaji filamu ni wasimuliaji hadithi wa siku hizi, wakiziba pengo kati ya mambo ya kiulimwengu na ya kidini, na hatimaye kuwaongoza watu kuelekea ufalme wa Mungu.”

—Heshbon Buscato, mkurugenzi wa mawasiliano wa Divisheni ya Kusini mwa Asia-Pasifiki, alishiriki katika warsha ya siku nne ya utengenezaji wa filamu na uigizaji. Zaidi ya washiriki 50 kutoka Ufilipino ya Kati na Kusini walikusanyika katika Jiji la Cebu. Waliohudhuria walionyeshwa vipengele mbalimbali vya utengenezaji wa filamu na uigizaji, ikiwa ni pamoja na nadharia ya sinema na uhalisia, kanuni za msingi za uelekezi, usimamizi wa uzalishaji na mtiririko wa kazi, uendeshaji wa drone, uandishi wa skrini, uandaaji wa eneo, hadithi za kuona, uigizaji, mitindo ya nywele, na mbinu za uundaji wa filamu.

80

Idadi ya watu waliokusanyika katika Chuo Kikuu cha Fulton Adventist University huko Sabeto, Fiji, kuhudhuria Mafunzo ya Uanafunzi wa Dijitali 2023. Tukio hilo lilihamasishwa na idara ya vijana ya Union Misheni ya Pasifiki Ng’ambo na kusisitiza umuhimu wa kutumia zana za enzi ya dijitali huku tukiwa imara katika imani. Mpango huu uligundua eneo lenye vipengele vingi vya teknolojia, ukichunguza uwezo wake wa kuendeleza injili na kuleta changamoto.

Ujumbe wa Waadventista wa Afya na Afya ya Kiakili

Washiriki wa kanisa waliulizwa ikiwa walikubaliana na kauli ifuatayo: Ujumbe wa Afya wa Waadventista unasisitiza afya ya kimwili, ya akili, ustawi wa akili, usaidizi wa kijamii, na mahusiano kama sehemu ya ukuaji wa kiroho.

“Taasisi hii haijawaandaa tu wanafunzi kimasomo, bali pia imewajengea maadili ya utumishi na huruma. Ni mnara wa matumaini na mwangaza katika eneo letu.”

—Roger Caderma, mwenyekiti wa Divisheni ya Kusini mwa Asia-Pasifiki, kuhusu Chuo cha Waadventista cha Lakpahana na sherehe ya miaka 100 ya Seminari ya utume na huduma. Shule hiyo ambayo iko katika Mailapitiya, Sri Lanka, ilisherehekea safari yake ya ajabu kwa siku tano.

mbele wakiwa na mawazo chanya. . . . Kwangu mimi, ndivyo dawa inavyopaswa kuonekana. Inahusiana na kutumia wakati mzuri na wagonjwa, kufanya kazi nao na kufuata njia kamilifu.”

—Andrea Matthews, mkurugenzi wa afya wa ELIA Lifestyle Medical Centre (ELMC). ELMC ya kwanza ya Pasifiki Kusini imeibuka kama mwanga wa matumaini kwa watu wanaopambana na masuala ya afya yanayohusiana na mtindo wa maisha. Kituo hicho, kilicho katika Hospitali ya Waadventista ya Sydney, tayari kimetoa matokeo mashuhuri katika miezi michache tangu kuzinduliwa rasmi mnamo Machi 26.

—Andrea Matthews, mkurugenzi wa afya wa ELIA Lifestyle Medical Centre (ELMC). ELMC ya kwanza ya Pasifiki Kusini imeibuka kama mwanga wa matumaini kwa watu wanaopambana na masuala ya afya yanayohusiana na mtindo wa maisha. Kituo hicho, kilicho katika Hospitali ya Waadventista ya Sydney, tayari kimetoa matokeo mashuhuri katika miezi michache tangu kuzinduliwa rasmi mnamo Machi 26.

—Melchor Ferreyra, mkurugenzi wa huduma binafsi wa Divisheni ya Amerika ya Kati (IAD) na mtayarishaji mkuu wa mfululizo wa TV unaoitwa Conocidos, kuhusu mfululizo mpya wa TV kwenye Hope Channel ya Amerika ya Kati. Msururu huu wa vipindi nane unasimulia hadithi ya wahusika kadhaa ambao hukutana na kufahamiana kupitia kikundi cha mafunzo ya Biblia. Conocidos iliundwa ili kuelekeza katika mtandao wa urafiki ulio bora ambao unaweza kupatikana kupitia kikundi kidogo

Zaidi ya 100

Idadi ya waratibu na viongozi wa Kihispania kutoka kote katika Divisheni ya Marekani Kaskazini (NAD) waliokutana ili kushirikishana juhudi madhubuti za huduma za eneo hilo na kusaidia kuweka mikakati ya njia mpya za kufikia jumuiya za Wahispania. Kila siku wakati wa mikutano viongozi wa Union wa huduma za Kihispania na konferensi walishiriki mipango ya huduma na uzoefu wa ukuaji wa kanisa kutoka maeneo wanayohudumu ndani ya Union tisa za NAD.

Zaidi ya 194,000

Idadi ya ubatizo ambao ulifanyika baada ya mfululizo wa uinjilisti wa Hope for Africa. Mfululizo wa Septemba, uliofadhiliwa na Hope Channel, kwa ushirikiano na Divisheni ya Afrika Mashariki-Kati na Redio ya Adventist World, ulishuhudia uanzishwaji wa pekee wa maeneo 20,000 ya kupunguza kasi katika nchi 11 kote katika ukanda huo. Mfululizo huo ulikuwa na usambazaji mpana zaidi wa setilaiti mbili, televisheni ya dunia kwenye vituo vya kanda vya Hope Channel, tovuti, programu ya Hope Channel, jukwaa la video la YouTube, na majukwaa kadhaa ya mitandao ya kijami

Mungu ameliita kanisa la Waadventista wa Sabato katika kipindi hiki cha mabadiliko ambayo hayajawahi kutokea, changamoto, na fursa zisizo za kawaida, katibu wa Konferensi Kuu Erton Köhler alisema kwenye ripoti yake ya ukatibu wakati wa mkutano wa kila mwaka wa 2023 mwezi Oktoba 8.

 

“Mabadiliko siyo mageni kwetu,” Köhler alisema katika taarifa yake kwa mamia ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Konferensi Kuu (EXCOM) waliokutana huko Silver Spring, Maryland, Marekani. “Lakini mabadiliko ya siku hizi ni tofauti: ni ya haraka, yana athari, na ni makubwa.” Aliongeza, “Hatuwezi kuogopa mabadiliko, bali yanaweza kutupelekea kuondoka kwenye eneo letu la faraja, kuwa macho, na kutumia rasilimali zetu zote, na mipango bora zaidi ya kushiriki ujumbe wetu wa Biblia wa tumaini kwa ulimwengu huu.”

 

Kinyume na uhalisia huu mpya, Köhler alisifu kurejea utume kulikokuwa kunaendelea kwa dhehebu imara lenye watu milioni 22. Wakati huo huo, alitoa wito kwa kanisa kuendelea kukabiliana na changamoto kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kwa ujasiri, na matendo ya utume.

 

 

JUKUMU LA KUZINGATIA TENA UTUME

“Kuzingatia tena utume ni mojawapo ya vipaumbele vyetu ili kukabiliana na wakati huu unaobadilika,” alisisitiza, akirejelea mpango wa kanisa la ulimwengu ambao unatafuta kuelekeza upya juhudi za kupanga na fedha ili kuwafikia wengine kwa ajili ya Yesu, hasa katika maeneo ya ulimwenguni yenye changamoto. Kuzingatia tena utume sio tu kuhusu kutuma wamishonari na ushirikiano, Köhler alieleza, bali pia “kurekebisha jinsi tunavyotimiza utume ili kufikia kwa ufanisi ulimwengu unaokabiliwa na mabadiliko makubwa.”

 

Matokeo kidogo kidogo yanaonekana, Köhler alitoa taarifa. “Baada ya miezi michache ya maombi, majadiliano, na tathmini, mashirika na taasisi zetu nyingi zimeanzisha mipango ya kupitisha na kutuma wamishonari kwenye maeneo yenye changamoto duniani kote,” alisema. “Inafurahisha kuona jinsi mashirika na taasisi tofauti zilivyofikiria zaidi ya mipaka yao ya kijiografia na kujitoa kuwa sehemu ya mpango huu wa ulimwengu. Baadhi ya fildi zetu ambazo zinahitaji msaada wa ziada ili kutimiza utume wao sasa pia zinachangia ili kusaidia wengine.”

 

 

CHANGAMOTO ZINAZOONGEZEKA

Köhler alitumia muda mwingi kuorodhesha baadhi ya changamoto kubwa ambazo Kanisa la Waadventista linakabiliana nazo linapojaribu kukamilisha utume wake. Alitaja pigo la UVIKO-19 na vita vinavyoendelea ambavyo vimeongeza ukosefu wa utulivu wa kisiasa duniani, na kuongeza idadi ya wakimbizi.

 

Pia alitaja mzozo wa kiikolojia usio wa kawaida na changamoto kwa uchumi wa dunia, pamoja na changamoto za kijamii, ikiwa ni pamoja na kizazi cha sayansi na teknolojia ambacho “ni dhaifu kihisia lakini, wakati huo huo, kinatafuta kutetea haki na kutafuta daima kuishi maisha yenye maana,” Köhler alisema.

 

Changamoto nyingine ni kuhusiana na uelewa wa jamii juu ya jinsia ya binadamu, Köhler alisema, ubaguzi wa kijamii na kiburi kwa mamlaka yote, na changamoto zinazoletwa na teknolojia.

 

 

FURSA KWA AJILI YA UTUME

Changamoto, Köhler alisisitiza, ni kuona mabadiliko haya ya ulimwengu na changamoto kama fursa za utume. Kuhusiana na uwekezaji wa kifedha wa kanisa katika utume, “ikiwa Mungu hutoa zaidi, hebu tuwekeze zaidi,” alisema. Pia alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuhuisha utambulisho wetu.

 

Kinyume na muktadha huo, njia bora ya kukiendea kizazi cha leo ni kwa kuangazia ujumbe wetu wa tumaini wa kibiblia, Köhler alisema. “Ulimwengu usio na tumaini unatafuta kanisa lenye matumaini,” alisema.

 

Teknolojia pia ni njia mbadala kwa utume kwa sababu inaweza kufikia kila mtu, kila mahali, kwa wakati wowote. “Tuna kila kitu tunachohitaji ili kusonga mbele kwa haraka,” Köhler alisema. “Hebu tukuze mabadiliko yanayoongozwa na Mungu [na] mabadiliko yaliyojikita katika Biblia. Hiki ndicho tunachokiita Kuzingatia tena Utume katika wakati wa mabadiliko.”

Mamia ya watoto na vijana wenye umri wa miaka 7 hadi 14 walisafiri kutoka kila kona ya Panama ili kushiriki katika mkutano wa nchi nzima, ambako walifundishwa kanuni za Biblia na kujifunza zaidi kuhusu upendo na kusudi la Yesu juu ya maisha yao.

 

Vijana walikuja na walimu na viongozi wao kutumia siku mbili kushiriki katika mfululizo wa jumbe za kiroho, maombi, na shughuli za kijamii katika bwalo la Shule ya Makao Makuu ya Waadventista katika Jiji la Panama, nchini Panama, Septemba 22-23.

 

“Kwetu sisi hili ni tukio la maana na la muhimu sana kusaidia watoto na vijana kukuza imani yao na kuimarisha uhusiano wao na Mungu kuanzia katika umri mdogo,” Rosalinda De Gracia, mkurugenzi wa huduma za watoto na vijana wa Unioni Misheni ya Kanisa la Waadventista huko Panama, alisema. Ni juu ya kuwekeza muda na rasilimali ili waweze kujifunza kumwamini Mungu, kupata ujasiri wa kuongoza wanapokua, na kuwa viongozi wa kiroho, aliongeza.

 

 

YESU NI MAHALI SALAMA PA KUKIMBILIA

Tukio hili lenye mada “Yesu Mwamba Wetu wa Milele,” lilikusudiwa kutoa ujumbe ulio wazi na kutoa zana ili watoto na vijana waweze kufanya maamuzi ya hekima na kuhakikishiwa kwamba Yesu kama “Mwamba” ndiye ulinzi na wokovu wao.

 

“Tulitaka kuwathibitishia tena kwamba Yesu ni kimbilio salama, tegemeo letu, msaada wetu, mfariji, mlinzi, na kiongozi bora na rafiki ambaye wanapaswa kuwa naye,” De Gracia alisema.

 

Wajumbe hao vijana waliwakilisha karibu watoto na vijana 13,000 waliotawanyika katika makanisa na makundi nchini Panama, De Gracia alisema. Takribani watoto 50 waliohudhuria hawakuwa Waadventista, aliongeza.

 

Mkutano huo uliona wajumbe vijana wakiwa wamevaa mavazi meupe na kila mmoja akiwa amevaa taji wakati wa programu ya ufunguzi iliyofanyika usiku, akizungumzia mavazi meupe ambayo wale waliokombolewa watavaa mbinguni. “Nilipenda jinsi sote tulivyovaa mavazi meupe,” Sofia Hernández mwenye umri wa miaka tisa alisema. “Nataka kwenda mbinguni na kuwaona watoto wote na kumwona Yesu akiwa amevaa mavazi meupe kama mimi.”

Ilikuwa juu ya kuacha mawazo ya kudumu, De Gracia alisema. Vijana walijifunza kuhusu faida ya tiba ya kukumbatiana, uumbaji, na umuhimu wa pumziko la Sabato, matumizi ya mitandao ya kijamii na hatari zake, na umuhimu wa ndoa kama taasisi ya kibiblia iliyoanzishwa na Mungu kati ya mwanamume na mwanamke.

 

 

KWENYE HEMA LA MAOMBI

Wajumbe vijana walipanga mstari kwa ajili ya hema la maombi, ambapo wachungaji walikuwa tayari kusikiliza na kuomba kwa ajili ya dukuduku na maombi yao mahususi. “Mstari ulikuwa mrefu sana kwamba wachungaji wengine wawili walilazimika kusaidia katika hema la maombi,” De Gracia alisema. Maombi mengi yalijumuisha sala kwa wazazi wao kupata ajira au kutotalikiana, na maombi ya uponyaji, alisema.

 

“Mtoto mmoja aliomba ili yeye na familia yake wapate chakula kwa sababu wazazi wake hawakuweza kupata kazi na walikuwa na njaa,” De Gracia. Muda mfupi baadaye, viongozi wa Panama wa Shirika la Maendeleo na Misaada la Waadventista (ADRA) waliarifiwa kutembelea nyumba hiyo wakiwa na chakula pamoja na msaada.

 

 

YESU KAMA MWASISI

Mzungumzaji mkuu Edith Ruiz de Espinoza, mkurugenzi wa huduma za watoto na vijana wa Divisheni ya Ulaya Kati ya kanisa la Waadventista wa Sabato, aliwahimiza wajumbe vijana kuambatana na Yesu na kumfanya kuwa msingi na chanzo cha hekima katika maisha yao wanaposafiri katika shughuli zao za kila siku. “Ninyi ni nuru ya Yesu na mnahitaji kuangaza kwa wale walio karibu nanyi,” aliwaambia.

Mnamo tarehe 8 Oktoba, wanachama wa Dorcas na AMO (DORCAMO) walisherehekea ufunguzi rasmi wa awamu ya kwanza ya Kituo kipya cha Mafunzo ya Ujuzi cha DORCAMO huko Choma, nchini Zambia. Mamia ya washiriki wa kanisa na viongozi kutoka Konferensi ya Zambia Kusini (SZC) walihudhuria.

 

Vituo hivyo, ambavyo vinatarajiwa kuendesha mipango mbalimbali ya ustadi wa maisha baada ya kukamilika, viliagizwa na waziri wa Sayansi na Teknolojia wa Zambia Felix Mutati.

 

Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na mkurugenzi msaidizi wa mipango Michael Inambao, Mutati alisema, “Hili ni tukio muhimu ambalo linaashiria hatua kubwa ya maendeleo katika elimu, uwezeshaji na maendeleo ya jamii kama taifa. . . . Kwa niaba ya rais Hakainde Hichilema, serikali inashukuru kwa kujitoa na kujitolea kwa dhati katika kujenga vituo hivi.”

 

Mutati aliongeza kuwa serikali ya Zambia inapenda sana kuona mashirika kama vile Kanisa la Waadventista wa Sabato yakifanya kazi kwa bidii ili kuongeza juhudi za serikali katika kupunguza ukosefu wa ajira. “Ninashukuru kuona Kanisa la Waadventista wa Sabato likiboresha maisha ya watu binafsi na jamii,” alisema. “[Huu ni] ushuhuda kwa kujitoa kusikoyumba katika kuleta matokeo chanya sio tu katika ulimwengu wa kiroho bali pia katika nyanja ya kivitendo ya maisha.”

 

Alieleza kuwa vituo hivyo vipya “vinaakisi imani yetu ya pamoja katika umuhimu wa kuwaandaa watu kwa ujuzi na maarifa wanaohitaji ili kustawi katika ulimwengu unaobadilika kila mara. Inaunganisha imani ya Kanisa la Waadventista wa Sabato na kujitoa kwa maendeleo kamili,” Mutati alisema.

 

Zambia na Afrika kwa ujumla kwa sasa zinakabiliwa na changamoto ya wafanyakazi wasio na ujuzi, maofisa wa serikali walieleza. “Leo tunafurahi kuona baadhi ya changamoto hizi zikishughulikiwa na Kanisa la Waadventista wa Sabato,” walisema.

 

Mutati alitumia vyema muda huo kutangaza kozi hizo ambazo hatimaye zitaendeshwa katika kituo hicho na watumishi wenye sifa stahiki, zikiwemo ufundi stadi wa vyuma, umakanika, upishi, ushonaji na usanifu, ufundi bomba, ujenzi wa matofali, na upigaji lipu. Pia alitaja kozi zitakazotolewa siku zijazo, kama vile kozi za umeme na ujasiriamali, programu za shule za chekechea, mazoezi ya viungo na ushauri, pamoja na mipango ya kuwasaidia wahitaji.

 

Mamia ya washiriki wa kanisa na wanajamii waliohudhuria sherehe ya uidhinishaji ni pamoja na viongozi wa DORCAMO na wajumbe, waliokuja kushuhudia “ndoto yao iliyosubiriwa kwa muda mrefu jimboni” ikitimia. Mwenyekiti wa zamani wa SZC Dorcas Miriam Scott pia alihudhuria na kutoa ng’ombe kulisha wajumbe mwishoni mwa sherehe ya uidhinishaji.

 

Wasamaria wema kutoka maeneo mbalimbali ya SZC pia walihudhuria. Miongoni mwao alikuwa mwenyekiti wa konferensi Gladwin M. Mang’watu, wakurugenzi wote wa idara, na viongozi wa mitaa.

 

Mkurugenzi wa huduma binafsi wa SZC Bednock Banji alitoa historia ya mpango huo. Alieleza kuwa kituo hicho kilianzishwa mwaka 2005 kwa manunuzi ya kiwanja hicho. “Kwa sababu ya ukosefu wa fedha, kazi hazikuweza kuanza mara moja,” alisema. “Kati ya mipango 15 iliyoidhinishwa na Halmashauri ya Manispaa ya Choma, iliyofunguliwa kwanza ni jengo la madarasa ya Ushonaji na Upishi,” Banji alishiriki.

Muundo wa sasa ulijengwa na chama cha DORCAMO kupitia michango iliyotolewa wakati wa mikutano, alisema. “Hadi sasa, washiriki wapatao 26,000 wamechangia kukusanya fedha hizi kwa ajili ya mradi huu mzuri,” Banji alisema. “Tunamsifu Mungu kwa [vituo hivi vipya], ambavyo vitaleta maendeleo na kuandaa na kuwezesha jamii mahalia pia.”

Kulingana na Yesu, wafuasi Wake wanaweza kuchagua watakavyofanya wanapofikiria kuwa Bwana wao “anakawia kuja” (Luka 12:45).

 

Wanaweza kulala usingizi (angalia Mathayo 25:1–13). Au wanaweza kuanza kuwapiga watumwa wao na kula na kunywa (angalia Luka 12:45). Aidha, wanaweza kuendelea kukesha (angalia Mt. 25:13) na kuendelea kuwa watendaji, wakisimamia mali Zake na kutimiza maagizo Yake (angalia Luka 12:35–44). Waadventista wa Sabato wanaweza kushukuru kuwa asilimia kubwa ya washiriki na viongozi wengi wamechagua chaguo la mwisho.

 

Waadventista wa Sabato kwa namna ya pekee wamechaguliwa kwa ajili ya utume, mwenyekiti wa Konferensi Kuu Ted N. C. Wilson aliwakumbusha wajumbe wa Kamati Tendaji ambao walikusanyika kwa ajili ya Mkutano wa kila mwaka wa 2023 kwenye makao makuu ya kanisa huko Silver Spring, Maryland, Marekani. Ni utume wa kina ambao kwa miaka 160 umewabidisha wamishenari kwenda kila mahali kushiriki ujumbe wa Mungu na watu wanaotafuta tumaini.

 

“Kazi ya Mungu ya ulimwenguni pote inastawi kwa sababu tumechaguliwa kwa ajili ya utume,” alisema Wilson. “Hakuna kitakachozuia utume wa Mungu.”

 

Mnamo mwaka 2024, Kanisa la Waadventista litaadhimisha miaka 150 tangu kanisa lilipotuma wamishenari wake wa kwanza katika nchi za mbali. Katika maneno ya David Trim, mkurugenzi wa Ofisi ya Hifadhi ya Kumbukumbu, Takwimu, na Utafiti ya kanisa hilo, hiyo ingekuwa “miaka 150 ya Kanisa la Waadventista kutanguliza ulimwengu, badala ya masilahi ya kidini.”

 

Hata mabadiliko na changamoto ambazo hazijawahi kutokea, katibu wa GC Erton Köhler alisema, zinapaswa kuonekana kama fursa za utume. “Kila mtu anaweza kufanya kitu ili kulenga utume na kutusaidia kukabiliana na changamoto zetu kubwa za dunia nzima,” alisisitiza.

 

Mipango rasmi na mipango ya kanisa la ulimwengu na maoni na ripoti za matukio zinaonyesha kwamba Waadventista wengi waaminifu wanalitunza hai hamasisho la utume. Wafuasi hao wa Yesu wenye nia ya utume hawajazuiwa na eneo au hata umri. Kuanzia kwa vijana wa kujitolea kwa Utume kwa jina la Caleb huko Puerto Rico hadi wafanyakazi wa kimishenari wa kitabibu nchini Chad hadi wafanyakazi wa ADRA nchini Romania na wafanyakazi wa kujitolea waliostaafu kote Marekani, maelfu ya washiriki wa kanisa wanaendelea kutoka katika maeneo yao ya starehe ili kuhudumu na kusaidia kubadilisha maisha kupitia nguvu za Roho Mtakatifu.

 

Viongozi Waadventista wa Sabato wanaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na mashirika na makundi mengine kutafuta njia za ubunifu za kutimiza utume. Hata wanazoesha roboti kutoa mafunzo ya Biblia na kushiriki imani za Waadventista zilizojikita kwenye Biblia. Zana mpya zimetengenezwa ili kuunganisha na kuoanisha matumaini wamishenari na fursa za huduma. Haijalishi ni programu na mipango mingapi ambayo mashirika ya kanisa na huduma zinazosaidia huja nazo, hata hivyo, mahitaji bado ni makubwa.

 

Na bado, hakuna programu au mpango ambao ungefaulu bila wanachama kukubaliana nao. Ni shauku hiyo ya utume iliyopandikizwa kupitia visa vya utume ulimwenguni, lakini pia katika kila Shule ya Sabato, katika kila kanisa mahalia, katika kila darasa, zahanati, kiwanda cha chakula, na kituo cha vyombo vya habari ambacho huwezesha utume wa Waadventista kusonga mbele. Na wakati wa Baraza la Mwaka la 2023, programu ya utume ya Oktoba 6 ilitumika kwa viongozi wa kanisa kujifunza, kutafakari, na kujitolea tena kwa utume wa Waadventista wa Sabato.

 

Mara kwa mara, watabirio mabaya hutangaza kwamba utume wa Waadventista umekufa. Wanaokataa wanakashifu pesa zilizotumika kwa utume wakati wa kukusanya pesa ili kueneza maoni yao ya kukata tamaa zaidi. Wale wanaopenda utume wa Bwana wanasonga mbele, kwa sababu bado kuna ulimwengu wenye kiu ya tumaini, unaofikiria njia ya kutokea. Ni fursa ya kila mshiriki kujihusisha katika kazi kama hii iliyoidhinishwa mbinguni.

Waebrania 11 inaorodhesha mashujaa wa Biblia waliowekwa na Mungu—watu wa imani. Inamaanisha nini kuwa mtu wa imani? Je, hawakuwa na dosari? Hawakuwa na hofu? “Kwa imani,” je, waliepuka mikasa yote ya kimwili1, msukosuko wa kihisia2, mateso ya kiakili? Hapana, kama mapitio ya haraka ya maisha yao yanavyoonyesha.

 

Lakini Mungu anawasifu katika sura ya imani; akiwaelezea kuwa wenye moyo kama Wake; akishirikiana nao katika kusherehekea uaminifu wao huku wakati uo-huo wakikabiliana na msukosuko wa kihisia usio na kikomo wa kila siku, dhiki ya utambuzi, na tabia mbaya. Vile vile, Yesu anaonyesha wale wanaokufa katika ajali mbaya si wenye dhambi kuliko mtu mwingine yeyote (Luka 13:4) na mvua (halisi na ya kimfano) huwanyeshea wenye haki na wasio haki. Katika ulimwengu uliojiingiza katika pambano kuu la kuvutia upande wa machafuko, wakati na bahati huleta dhiki kwa kila mtu (Mhu. 9:11). Hakuna ahadi, upande huu wa mbinguni, kwamba taabu ya kimwili, msukosuko wa kihisia, na dhiki ya utambuzi havitawapata waaminifu.

 

 

MAMBO YANAYOCHANGIA

Kwa hiyo, ni nini chanzo cha matatizo ya kiakili? Kuishi katika ulimwengu ambapo mamia ya vizazi viko mbali na uumbaji wa Mungu uliopangwa kikamilifu hutuweka sote katika uwanja wa vita ambapo mambo makuu matatu yanasababisha matatizo ya afya ya akili: mambo ya muda mrefu, vichochezi, na mambo ya kudumu.

 

Mambo ya muda mrefu yanaweza kuwa ya kinasaba, ya kuzaliwa nayo, au yale yanayojitokeza mapema. Japokuwa yanaweza kusababisha matatizo moja kwa moja, mara nyingi yanamweka mtu katika hatari ya kukuza mfadhaiko. Mfano wa mambo ya muda mrefu kimwili ni kuwa na urefu wa futi saba—hili halimfanyi mtu kuwa na msongo, lakini linamweka mtu kuwa katika hatari ya kupatwa na msongo katika jamii ambapo milango huwa na urefu wa futi sita na inchi nane.

 

Vichochezi ni matukio yanayotukia kabla tu ya mwanzo wa matatizo. Kichochezi cha kisaikolojia kwa mtu aliye na tabia ya kuathiriwa na matukio yatokeayo papo kwa papo kinaweza kuwa kifo kisichotarajiwa cha rafiki wa karibu, ambacho kinaweza kusababisha mfadhaiko mkubwa wa kihemko na kusababisha wasiwasi kuhusu kifo cha wapendwa wengine, magonjwa yanayoweza kutokea, au shida za kifedha zinazoweza kutokea.

 

Mambo ya kudumu ni matukio ambayo yanafanya hali inayosumbua kuendelea kuwepo. Kipengele kinachodumu cha kisaikolojia kinaweza kuwa kushindwa kwenda kazini kwa siku moja wakati wowote mtu anapokuwa na wasiwasi kuhusiana na uwezekano wa kushutumiwa, kutoendana na wengine, au kufanya makosa ya kijamii kazini. Kwa kukosa kwenda kazini, kwa ajili ya kupunguzwa kwa dhiki ya haraka kunahusishwa na kuepuka kazi; kwa hivyo, mtu huepuka kufanya kazi zaidi na zaidi anapofadhaika, ambayo hudumisha wasiwasi.

 

Mungu aliumba hisia ili kututahadharisha sana kuhusu mahitaji ambayo hayajatimizwa. Hisia hazituelezi namna ya kutatua matatizo, bali zinatupatia ishara ya uwepo wa tatizo na kutupatia nguvu. Kupuuza viashiria huongeza fadhaa.

KUTAFUTA SULUHISHO

Wakati mtu wa imani anapopata dhiki ya utambuzi na msukosuko wa kihisia, nyakati fulani Mungu hutatua suala hilo kimuujiza, lakini uingiliaji kati huu wa haraka haukuahidiwa. Badala yake, Mungu aliweka wazi kwamba kuwa peke yako sio vyema na akaandaa jamii ya watu ambao wanashughulika na wengine kwa hekima, maarifa, na utambuzi kwa ajili ya uponyaji wa wale walio na fadhaa (Efe. 4:11, 12, 1 Kor. 12:7–11).

 

Wasaidizi hawa mara nyingi hutumia njia za utatuzi ikijumuisha mabadiliko ya ndani, kama vile kujifunza kitu kipya au kuhamia kwenye fani tofauti; mabadiliko ya nje kutumia dawa, kufanya mazoezi, na lishe ili kusaidia mwili na kemikali za mtu kurudi kwenye utendaji bora; ustahimilivu, ambayo ni pamoja na kukuza ujuzi wa kiakili na kihemko wa kudhibiti dhiki sugu, kwa mfano, kuendeleza ucheshi unaohusiana na changamoto hizo, kurekebisha matarajio, au kuzungumza mara kwa mara na watu wanaoweza kukusaidia kuhusiana na ugumu huo.

 

Dunia ni uwanja wa mapigano ya Pambano Kuu. Hata watu wa imani wanapokuwa katika upande wa ushindi, bado tutapata fadhaa hadi pale Mungu atakapokomesha vita. Wakati wote, uwe msaada salama kwako mwenyewe na kwa wale ambao wako chini ya kizuizi cha msukosuko wa kimhemko na dhiki ya utambuzi4.

Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke ambaye alikuwa Msabato kwa miaka mingi. Alikuja kanisani kwangu kumtembelea mpwa wake. Alionekana mtanashati sana na aliimba vizuri. Baada ya ibada tulifanya mazungumzo mafupi. Aliniambia, “Nilifiwa na mume wangu miezi kadhaa iliyopita. Tulilala pamoja usiku uliopita lakini nilipoamka, nilimkuta akiwa ameshafariki pembeni kwangu. Baada ya ibada ya mazishi kufanywa, nilihisi wasiwasi kila usiku, nikiogopa kwamba mtu fulani angekuja na kuniua.” Miezi michache baada ya kukutana naye, nilisikia kwamba alikuwa amerukwa na akili.

 

 

KUGUNDUA MAHITAJI YANGU YA AFYA YA KIHISIA

Kwa zaidi ya miaka 30 nimekuwa mchungaji katika Kanisa la Waadventista wa Sabato. Nina imani na shauku kwa ajili ya injili; Nimewaongoza watu kwa Kristo na kuwatumikia watu wa Mungu. Kuamini Neno la Mungu na kuishi kwa imani ndio kiini cha maisha yangu. Ninapotafakari miaka yangu ya utumishi, ninaona kwamba mahubiri yangu mengi yamekuwa kuhusu imani. Katika ushauri wangu wa kichungaji, nimezungumza kuhusu imani. Ninaamini kwamba imani inapaswa kutumika katika nyanja zote maishani. Lakini hii ilinifanya nipuuze na kukandamiza hisia zangu za ndani kabisa.

 

Mke wangu ni mwanamke mwenye bidii. Ana tabia ya hadhari na anahusiana vyema na wengine. Kama mke wa mchungaji anabeba mzigo mzito sana, na ameweza kufanya hivyo kwa roho nzuri. Kuna nyakati, siku za nyuma, nilimgombeza na kuonyesha hasira kwake tukiwa peke yetu. Baada ya ukweli, ningegundua kuwa hakuna sababu ya kuishi kwa njia hiyo. Hata hivyo nilipomwomba msamaha, hatia hiyo isingetoweka kwa sababu nilifikiri kama ningekuwa na imani ya kutosha katika Yesu, nisingeweza kumtendea vibaya. Wakati huo, sikutambua kwamba nilikuwa na hisia zisizofaa ambazo hazikuwa zimeshughulikiwa. Nilifikiri kwamba imani na afya ya kihisia ni kitu kimoja. Kwa hivyo ikiwa ningekuwa na imani yenye nguvu basi singehisi hasira, wasiwasi, huzuni, kukatishwa tamaa, na kufadhaika. Ikiwa nilihisi hisia hizo, basi nilifikiri inamaanisha kwamba sikuwa na imani thabiti.

 

Shahada yangu ya uzamivu ni katika huduma ya familia. Niliandika tasnifu yangu kuhusu “Kuzuia na Elimu kwa ajili ya Unyanyasaji wa Majumbani.” Nilipokuwa nikisoma unyanyasaji wa nyumbani nilitafiti unyanyasaji wa kimwili na kihisia katika mahusiano ya karibu. Wakati uo huo nilijitazama na kugundua kuwa nilikuwa namnyanyasa kihisia mke wangu mpendwa. Nilimfokea, nikampuuza, na kukiuka nafasi yake. Nilishangaa kugundua kwamba nilikuwa mwenzi na mchungaji asiye na afya kihisia. Ingawa nilijiamini kuwa mchungaji mwenye imani thabiti kwa Yesu.

KUGUNDUA AFYA BORA KIBIBLIA

Miitikio ya kihisia kwa matatizo maishani inapatikana katika Biblia. Hofu ni itikio la kwanza la kihisia kwa hali hasi inayotajwa katika Biblia. Adamu alikula tunda lililokatazwa na Mungu na kujificha kutoka kwa Mungu kwa sababu ya hofu (Mwanzo 3:10). Baada ya Adamu kupitia uzoefu huo, hofu ikawa hisia ya kawaida katika uzoefu wa mwanadamu. Ayubu, mtu wa imani, alionyesha pambano lake la kihisia: “Kuugua,” “kunguruma,” “[woga],” “[hofu],” “sina raha,” “wala situlii,” “wala kupumzika,” “taabu tupu,” (Ayu. 3:24–26). Musa alilemewa sana kiasi kwamba alimwomba Mungu amuue kwa sababu “mzigo” wa kuwaongoza wana wa Israeli waliokuwa wakilalamika ulikuwa “mzito sana” kwake (Hes. 11:14, 15).

 

Kama viumbe wa Mungu, wanadamu hupokea matukio mabaya kwa hisia: hofu, wasiwasi, hasira, kukata tamaa, msongo, majuto, na hatia kwa mfano. Hisia ni miitikio ya asili inayotoka ndani kabisa lakini hisia hizo zinapoachwa bila kushughulikiwa, husababisha hali isiyofaa ya kihisia. Hatimaye, zitatupatia magonjwa ya akili kama vile wasiwasi na sonona. Ni muhimu kutunza afya yetu ya kihisia.

 

Paulo anaandika, “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo” (1 Thes. 5:23). Kuna utatu kwa ajili ya afya: kimwili, kiroho, na kihisia—vipengele vitatu, vinavyotengana lakini vinaungana kwa karibu. Kama vile Wakristo waaminifu wanavyoweza kupoteza afya yao ya kimwili, wanaweza pia kupoteza afya yao ya kihisia.

Nimekuja kuelewa kwamba mara nyingi mimi, au washiriki wengine waaminifu kanisani wanapoonyesha tabia zisizokubalika, ni kwa sababu ya hisia zisizofaa ambazo hazijashughulikiwa.

 

 

KUANZISHA HUDUMA YA KUFARIJI KIHISIA

Peter Scazzero anafupisha jambo hilo vizuri anapoandika “hali ya kiroho ya Kikristo, bila kuunganishwa kwa afya ya kihisia, inaweza kuwa hatari sana kwako mwenyewe, uhusiano wako pamoja na Mungu, na watu wanaokuzunguka.”*

 

Baada ya kusomea saikolojia ya ushauri nasaha nikawa mshauri wa kitaalamu aliyeidhinishwa na kuthibitishwa kitaifa. Kanisa langu, Santa Maria Korean Seventh-day Adventist Church, lilipiga kura mwaka wa 2022 ili kuanzisha Kituo cha Kimataifa cha Uinjilisti wa Afya ya Akili na kuanzisha “huduma inayofariji hisia,” huduma ya afya ya akili inayozingatia afya ya kihisia.

Nabii Isaya anaandika, “Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu” (Isa. 40:1). Huduma ya kufariji kihisia inatafuta kwanza kuwahimiza washiriki kupata faraja kwa ajili yao wenyewe, pili, kufariji familia zao, na tatu, kuwafariji jirani zao. Lengo letu ni kwamba kila mshiriki wa kanisa awe mfariji. Paulo anasema katika 2 Kor. 1:3, 4 “Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote, atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.” Sote tunahitaji faraja kutoka kwa Mungu na kwa wanadamu wenzetu pia.

Mnamo 1997, Dkt. Martin Seligman alichaguliwa kuwa rais wa Jumuiya ya Kisaikolojia ya Marekani na aliamua kuwekeza nguvu na ushawishi wake katika uwanja mpya wa saikolojia. Dkt. Seligman alibainisha kuwa kiutamaduni, saikolojia ilijishughulisha na mambo hasi tu—ikitoa uangalifu wake wote katika kurekebisha hali za kisaikolojia zisizofanya kazi—kwa hiyo aliamua badala yake kuchunguza na kukuza kile alichokiita saikolojia chanya.

 

Hapo awali, fasihi ya saikolojia chanya ililenga furaha: Ni nini husababisha furaha? Je, unaipataje? Ina uzuri gani? Hata hivyo, japokuwa inastahili kuitafuta furaha, uwanja wa saikolojia chanya umebaini kwamba inahitajika zaidi ya tabasamu na kucheka ili kustawi maishani. Hivi karibuni, Dkt. Seligman amependekeza kuwa kuna bora zaidi: Ili kustawi.

Hebu tuangazie njia tano za kina ili kustawi.

 

 

MAENEO MATANO

Hisia Chanya. Hisia chanya ni msingi wa maisha yanayostawi. Ingawaje hisia chanya huwakilisha zaidi ya misisimko hafifu au raha. Kujaribu kujenga ustawi wako na furaha kwenye raha pekee ni shida.

 

Raha huwa haidumu, na kicheko hakina kikomo. Ili kuunda maisha mazuri kupitia kutafuta raha, utahitaji kujishughulisha kila wakati kuitafuta. Kwa kweli, tafiti kadhaa zimegundua kuwa raha haichangii katika tathmini ya watu ya kuridhika kwa maisha yao kwa ujumla kama vile mambo mengine yaliyojadiliwa hapa chini.

 

Kujishughulisha. Mtafiti mkongwe katika uwanja wa saikolojia chanya, Dkt. Mihaly Csikszentmihalyi amechunguza kwa kina uzoefu anaoutaja kama “kuzama kabisa katika kitu fulani.” Kuzama kabisa ni hali ya umakini zaidi na starehe ambayo hutokea katika shughuli kama vile sanaa, mchezo na, amini usiamini, hata kazi.

 

Haishangazi, watu binafsi wanaoripoti viwango vya juu vya kuzama kabisa kunakosababisha kujishughulisha katika shughuli zao za kila siku, pia huripoti viwango vya juu vya kuridhika kwa maisha na kustawi. Kwa kuzingatia kwamba “kujishughulisha” ni mchangiaji mkubwa katika uwezo wako wa kustawi, ni bora kupata ajira ambayo inakushughulisha kwa sababu unatumia muda wako mwingi kazini. Ninatumai kuwa unajishughulisha na kazi yako, lakini ikiwa sivyo, na hali ya mambo inakuzuia kufanya mabadiliko, ni muhimu zaidi ushiriki katika mchezo wa kawaida—mambo unayofanya kwa starehe kamili bila malipo ya nje yanayohitajika.

 

Ufanikishaji. Hisia ya ufanikishaji, kufanikiwa, kufaulu, au ustadi husaidia watu kusitawi. Wakati mwingine mafanikio hupimwa kupitia viwango vilivyokubaliwa kama vile mashindano, tuzo au kupitia uchezaji katika kiwango fulani. Kuwa na hisia ya kufanikiwa kunaweza kuboresha maisha yako bila hisia chanya au kujishughulisha.

 

Mahusiano. Pamoja tunajisikia vizuri na Mungu alituumba ili kustawi katika jamii. Wanadamu ni viumbe wenye uhusiano na viwango vyetu vya kina vya ustawi vinaonekana kufikiwa kwa kupenda na kupendwa. Tunatafuta muunganisho na muunganiko huo hutusaidia kustawi.

 

Maana. Kuwa mtu wa maana ni hitaji la msingi la mwanadamu. Ni vigumu, labda haiwezekani, kuishi maisha mazuri bila kuwa mtu mwenye maana. Katika suala hili, inaweza kuchukuliwa kuwa muhimu zaidi ya sifa zote. Unaweza kuishi maisha yaliyojawa na nyakati za kufurahisha, kujishughulisha na shughuli zako za kila siku, kufikia mafanikio makubwa, na kuwa na mahusiano mazuri, lakini katika wakati wako tulivu, unajiuliza Ni nini maana ya yote hayo?

 

Seligman anafasili maana kuwa “kuhisi kuwa mtu wa na kutumikia kitu kikubwa kuliko wewe mwenyewe.”1 Hivi karibuni, Emily Esfani Smith alipanua ufafanuzi wa Seligman katika kitabu chake cha The Power of Meaning kwa kuchunguza njia nne za maana.

NJIA NNE

Njia moja ni kuwa mtu wa, ambayo inahusisha kuunganishwa na wengine na kuhisi kwamba sisi ni watu wa kitu kikubwa kuliko sisi wenyewe. Kama tulivyojadili, tumeumbwa kuishi katika jamii, na hii inafanya maisha yetu kuwa yenye maana. Kwangu mimi, kuamini kwamba mimi ni wa kitu fulani au Mtu fulani mkubwa kuliko mimi hujenga hisia kali ya kujithamini na utambulisho thabiti. Unahitaji kujua kwamba wewe ni mtu wa thamani, pia.

 

Mtoto wangu wa kati—Eliya—alipokuwa mchanga tu, nilimbusu kila jioni nikimlaza kitandani na kusema, “Baba anakupenda,” na kila jioni alikuwa akiniuliza “Kwa nini?”

 

Likawa jambo la mchezo, kwani kila jioni nilimpa sababu tofauti: “Kwa sababu wewe ni hodari sana wa kupanda miti” au “Kwa sababu wewe ni mwerevu sana.” Ilikuwa tu baada ya mwezi au zaidi ndipo nilipogundua jinsi majibu yangu hayakuwa ya kutosha, na nikatambua jinsi nilivyopaswa kujibu. Jioni hiyo, nilipombusu usiku mwema na kusema, “Baba anakupenda,” bila shaka alirudia kuuliza “Kwa nini?” Bila kusita nilisema, “Kwa sababu wewe ni wangu. Na hakuna kitu unachoweza kufanya—kizuri au kibaya—kubadili hilo.”

 

Tunaona wazo hili likisisitizwa katika Maandiko kwenye Isaya 43:1: “Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako; wewe u Wangu.”

 

Kuelewa na kukiri upendo wa Mungu hutupatia kusudi. Kusudi linahusisha kuchangia na kumtumikia Mmoja mkubwa kuliko wewe mwenyewe. Inafurahisha kwamba kuwa na kusudi maishani kunahusishwa na kuishi muda mrefu zaidi. Katika utafiti mmoja, watu walio na alama za juu za “kusudi maishani” walikuwa karibu na asilimia 50 ya uwezekano wa kufa kutokana na sababu zote.2

 

Njia ya tatu ni kuvuka mipaka, ambayo inahusu uzoefu wa kuinuliwa kwa kitu kikubwa kuliko wewe mwenyewe. Watu hupitia hali ya kupita kiasi kwa njia tofauti-kupitia viumbe asili, sanaa, muziki, au matendo ya kidini. Kuvuka mipaka huleta nyakati za kicho na kustaajabisha, na hutukumbusha kwamba kuna ubora zaidi maishani kuliko kawaida.

 

Hatimaye, njia ya nne ya maana ni kupitia kusimulia hadithi. Usimuliaji hadithi umekuwa sehemu ya ustaarabu wa binadamu tangu zama za kale na vipengele vya kusimulia hadithi miongoni mwa jamii za kiasili. Kusimulia hadithi hutusaidia kuelewa ulimwengu na uzoefu wetu ndani yake, na hii ni njia mojawapo ambayo kwayo usimuliaji hadithi hukuza maana. Hadithi zinazoshirikishwa na wengine zinaweza kuwa na maana kubwa.

 

Je, unasimulia hadithi gani? Je. Unahusika katika sehemu gani? Ikiwa unakusudia kufanya hivyo au la, unasimulia hadithi kupitia jinsi unavyoishi maisha yako. Je, unataka hadithi yako isimuliwe vipi? Unataka hadithi yako iishe vipi? Kamwe hujachelewa kuandika sura mpya.

Nilisimama katika mfereji wa kuogea na kuanza kulia. Ilikuwa imepita juma moja tangu upasuaji wangu wa kinywa, na nilikuwa nikijitahidi kuwa imara. Ilikuwa rahisi zaidi wakati dawa za kutuliza maumivu hazikunipa chaguo lingine. Lakini sasa dawa zilikuwa nyingi sana ukilinganisha na maumivu kidogo niliyokuwa nikipata, na niliachwa niweke ratiba ya kupumzika niliyohitaji mwenyewe. Mazungumzo ya ndani akilini mwangu yalikuwa juu ya hitaji langu la kupumzika, ingawa, yalikuwa yananichosha. Nilijikuta tena kwenye pambano la kiakili na Mazungumzo Hasi Binafsi, ambaye alikuwa akiongezeka kwa nguvu.* Hakuwa mshindani mpya mawazoni Mwangu. Hapana, alikuwa adui wa zamani. Na kwa mtazamo wake pumziko hili mwili wangu ulifikiri ulihitaji halikuhitajika.

 

Juma hilo mambo hayakuwa magumu sana. Upasuaji ulikuwa wa moja kwa moja. Mikono yenye upendo ilinifariji nilipoamka nikiwa sielewi kitu chochote. Mikono yenye nguvu ilikuwa imenishika, na kuhakikisha kwamba nilifika nyumbani salama. Marafiki walikuwa wameleta milo na walinitembelea ili kuhakikisha kwamba mimi na familia yangu tulikuwa tunaendelea vizuri. Na nilikuwa na saa 24 za usingizi wa utulivu, usiokatizwa, uliosababishwa na dawa ya kutuliza maumivu huku watoto wakiwa wamepelekwa mbali ili kunipa pumziko nililohitaji. Upendo ulioenea na kumiminika katika familia yetu ulifanya kupata nafuu kuwa kwepesi. Kwa hiyo hapakuwa na haja ya kupumzika.

 

“Hakuna cha kupumzika kutoka kwacho.  Amka na usonge mbele. Kurudi tena katika hali hii!” Mazungumzo Hasi Binafsi (NST) yalihimiza. Lakini kila wakati nilipomsikiliza na kujaribu kupika, au kufua nguo, au kumsaidia mteja mmoja au wawili, mwili na akili yangu vilinijulisha kuwa nilikuwa nimechoka. Muda na mapumziko bado vilikuwa vikihitajika ili majeraha ya kinywani mwangu yapone na mwili wangu upate nafuu kabisa kutokana na dawa zilizokuwa zikisukumwa ndani yake. NST, hata hivyo, alikataa kukiri ukweli huu. Badala yake, jitihada zake zililenga kunitia hatiani katika kutenda, kupunguza athari za upasuaji niliofanyiwa, kama alivyofanya kwa matukio muhimu katika utoto wangu ambayo yaliimarisha utawala wake katika maisha yangu.

MATUKIO MAKUBWA KIDOGO

Nilikuwa kwenye mstari wa kulipa katika duka la mboga la jirani Ijumaa moja alasiri wakati mtu aliyekuwa nami alipotaja bila kukusudia kwamba nilidhulumiwa kingono kabla hata sijaweza kuzungumza. Unyanyasaji wa kijinsia ulikuwa ukweli usiojulikana ambao uligusa sehemu kubwa ya familia yangu, kwa hivyo sikushtushwa sana na habari hiyo. Kilichonishtua, hata hivyo, ni wazo kwamba kwa sababu ilikuwa imetokea zamani sana, haipaswi kuniathiri. Kwa mtazamo wa mtoa habari wangu ndoa yangu ilikuwa sawa, na nilikuwa na nyumba thabiti na familia nzuri. Kulingana naye nilikuwa nimeepushwa na uharibifu wowote “halisi”. Lakini hakujua kuhusu mapambano yangu ya ndani yanayohusu ukaribu wa kimwili na hulka yangu ya kuzitupilia mbali hisia zangu kuhusu mapambano yangu.

Unaona, muda mrefu kabla sijajua jina lake, NST alikuwa ameanzisha sauti maishani mwangu ambayo iliungwa mkono na hisia za watu walionizunguka. Ingawa kitaaluma, kithiolojia, na kiuzoefu sikukubaliana na tathmini ya mtoa habari wangu kwamba sikuathiriwa na unyanyasaji huo, ndani kabisa nilikuwa nikijitahidi kukataa hitimisho lao. “Sio jambo kubwa,” NST ilinidhihaki nilipoingia kwenye gari langu ili kuondoka. “Yaani huwezi hata kukumbuka chochote. Ni kitu gani cha kukufanya ujisikie vibaya? Wengine wamepitia mabaya sana kukuliko. Acha kulia.” Lakini kumbatio la mume wangu nilipofika nyumbani lilizungumza jambo tofauti kabisa. Nilikuwa salama hapa. Sikuhitaji kuwa na nguvu; mikono yake ingeweza kushikilia uzito wangu.

 

Hatimaye nilipoenda kuonana na mtaalamu, niligundua tukio ambalo nilikuwa nikilipuuza tangu lilipotokea katika ujana wangu lilikuwa, kwa kweli, unyanyasaji wa ngono, na kwamba nilikuwa nikionyesha dalili za ugonjwa wa msongo wa baada ya kiwewe (PTSD). Picha za kiakili kutokana na pambano hilo la tukio la ujana mara kwa mara zilipiga kumbo akilini mwangu, na kunifanya nikose raha hasa ninapomnyonyesha mtoto wangu, au wakati tunapokuwa karibu na mume wangu. Haya hayakuwa matukio ambayo mtu anapaswa kuyakasirikia tu, bali yalikuwa ishara za kidonda ambacho hakijatibiwa.

 

Mara nyingi nilifadhaika kwa urahisi na kuhisi vibaya sana, nikitarajia hatari wakati wowote. Kwa hivyo majibu yangu kwa hata kosa dogo zaidi yalikuwa makubwa sana. Milipuko ya hasira na kuzira vilikuwa njia zangu za kawaida za mawasiliano. Kwa sababu ya milipuko yangu, mara nyingi nilihisi kwamba sikustahili kuwa karibu na mume au watoto wangu na kwamba ingekuwa bora kwa kila mtu kama nisingekuwa nao. Mawazo kama vile Ni nini maana ya mimi kuwa hapa, hata hivyo? hatimaye yangeongezeka katika kujikosoa zaidi, kujitenga zaidi, na, ilipokuwa mbaya sana, mawazo ya kujiua. “Una shida gani, Candis? Maisha yako ni mazuri! Jikusanye!” NST ingeamuru. Lakini sikuweza kujikusanya, kwa hivyo nilitafuta msaada wa kitaalamu.

 

Ikiwa ungekuwa kama mimi wakati huo, kutafuta msaada wa kitaalamu kusingekuwa jambo la kwanza. Unyanyasaji wa kijinsia, kwa mtazamo wangu mdogo, ulihusiana na ubakaji tu, na uzoefu wangu haukuwa mbaya kama huo. Ikiwa ungekuwa kama mimi, labda ungefikiri kwamba kwa kuwa sikubakwa, sikuwa na chochote cha kulalamikia—nitakuwa sawa. Ukweli kwamba matukio niliyoyapitia zamani yalikuwa yakinijia sasa, hata hivyo, uliashiria kwamba ulikuwa umeniathiri kwa kina zaidi kuliko nilivyojiruhusu kukubali. NST alifurahishwa kwa sababu matukio haya yalitoa nafasi ya kuunda simulizi ambazo ziliathiri imani yangu ya msingi kunihusu, ziliniarifu jinsi nilivyojihusisha na ulimwengu na jinsi nilivyohusiana na wengine. NST alijaribu kupunguza matukio haya kwa sababu yalikuwa chanzo cha nguvu zake.

KIAPO CHANGU NA CHAKE

Niliamua kupambana dhidi ya NST nilipogundua kwamba ikiwa ataachwa bila kudhibitiwa, hofu yangu mbaya zaidi ingetimia; NST hatimaye angeathiri mawazo ya watoto wangu. Nilipopata ufahamu wa jinsi majeraha yangu ya utotoni ambayo hayajashughulikiwa yalikuwa yakichangia upungufu wa kihisia niliokuwa nikifanyia kazi, na jinsi yalivyokuwa yakichangia mifumo ya kutofanya kazi vizuri katika mahusiano yangu na watoto wangu na mume, nilijua nilipaswa kufanya kitu. Sikuweza kutumika kueneza madhara kama haya kwa watoto wangu. Nilikataa kuwa mpatanishi wa kutofanya kazi katika maisha yao kadiri niwezavyo. Hapo ndipo nilipoapa kuvunja mzunguko wa unyanyasaji na kutofanya kazi vizuri ambao uliendelea kwa vizazi vingi katika familia yangu.

 

NST alipata nguvu kutokana na ukiukaji wa ngono katika utoto wangu ambao, kama kuongezeka kwa nguvu nyingi, ulipunguza uwezo wangu wa kushughulikia unyanyasaji ipasavyo na kuleta maana ya ujumbe wa uharibifu ulioambatana nao. Ili kuharibu nguvu za NST, ilinibidi kushughulikia uharibifu mkubwa, kutathmini athari za kihisia, kijamii, na kiroho za kile kilichofanywa, na kusahihisha ujumbe unaolingana nao. Iwapo najua kwamba ujumbe wa NST umejaa uongo na haufai, basi sina budi kujiimarisha na kile ambacho Mungu amekuwa akiniambia ni kweli. Kukabiliana na NST ilikuwa sehemu muhimu ya jinsi ambavyo angeweza kupoteza nguvu na ushawishi juu yangu. Kila nilipopambana na NST, uongo wake ungepotea, na angedhoofika.

 

Kulikuwa na nyakati, kama kuvunjika kwangu kihisia nilipokuwa nikioga kulionyesha, wakati, ingawa nilijitolea kwa mchakato huo, nilichoka. Nilikua nimechoka kupinga mguso wa kupooza wa NST kwenye akili yangu wakati wa mchana. Nilichoshwa na mashaka ambayo mara nyingi alikuwa akizua kuhusu maamuzi niliyokuwa nimefanya, akitaka kunifanya niamini kwamba chaguo langu lilikuwa baya tena. Nilichoshwa na uongo wake ulioimarishwa kwamba sikuwa wa kutosha, tija hiyo ilithibitisha uwepo wangu, na kwamba kukataa hisia zangu ilikuwa njia pekee ya kurejesha uhusiano wa karibu na wengine, mume wangu na watoto wangu. Nilichoka kulazimika kudhibiti na kuweka upya hisia zangu ili kuhisi kuthibitishwa binafsi.

Kilichonisaidia kutoka katika mawazo yangu na kuchukua bendera tena ilikuwa ushauri wa Mungu kwangu: Tumainia uweza Wangu mkamilifu katika pambano hili (2 Kor. 12:9). Usikate tama, sitakuacha (Zab. 37:7), kwa sababu akili timamu isiyo na NST ni shauku Yangu kwenu (2 Tim. 1:7). Ikiwa Yesu anasema ninaweza kuwa na akili timamu na mvuto wa kuheshimika, basi nataka!

 

 

MWALIKO

Kushughulika na kovu la zamani moyoni sio mchakato rahisi. Inachukua muda. Haihitaji kufikiria kuliko kufanya maamuzi. Inahitaji ujasiri. Inahitaji kujizatiti. Inahitaji kujitolea. Inahitaji maombi. Inahitaji ushirikiano na maombi hayo. Inahitaji msaada wa nje. Inahitaji msaada kutoka katika uhusiano mzuri maishani mwako. Inahitaji muujiza. Inamhitaji Mungu. Ndio, kusuluhisha kidonda moyoni kutoka katika siku zako za nyuma ni ngumu. Lakini, rafiki yangu, ikiwa Mungu anasema jambo bora zaidi baada ya jaribu hili kwisha, basi linastahili sana. Mungu anatoa mwaliko wa kuifanya akili yako kuwa timamu, kuorodhesha mawazo na imani inayokuhusu wewe na jinsi unavyohusiana na wengine si sahihi na kuzibadilisha. Kilio kinaweza kudumu kwa usiku mmoja, lakini tafadhali usikatishwe tamaa—furaha itakuja asubuhi.

“Mwalimu Lynette, Nakupenda. Usiende. Usiende. Usiende tafadhali!” Moyo wangu ulivunjika kidogo niliposoma maneno ya mwanafunzi wangu yaliyoandikwa juu ya picha ambayo alikuwa ameichora tukiwa wawili. Nilikuwa nikipata barua za namna hii nyingi na michoro kutoka kwa wanafunzi wangu hivi karibuni, hesabu ya siku kwenye ubao wangu mweupe ilipotukumbusha kwamba siku yangu ya kuondoka ilikuwa karibu.

 

Baada ya miaka miwili nikiwa mwalimu mmishenari afundishaye Kingereza katika shule hii, ulikuwa wakati wangu kuondoka. Ilikuwa furaha yenye uchungu. Nilifurahi kuwa nimefanya mabadiliko katika maisha haya ya thamani ya vijana. Nilikuwa nikifurahi kwamba hatimaye ningeweza kuwa na mume wangu baada ya miezi kadhaa ya kuwa “wanandoa wa mwishoni mwa juma” huku nikimaliza ahadi zangu za utume. Lakini pia ningewakosa watoto wangu. Na nilihuzunika kupoteza jumuiya na muundo ambao ulikuwa umeunda wakati wangu huko Korea hadi wakati huo.

 

Nikiwa tayari kwa ajili ya kitu kipya, nilifurahishwa na nafasi ya kuandika sura mpya katika maisha yangu. Hata hivyo pia nilihisi kulemewa kwa kiasi fulani na mabadiliko yote—kuondoka na kufungua mizigo (mara ya tatu nilikuwa nikihama nyumba ndani ya mwaka mmoja); kuzoea kanisa jipya ambapo nyakati fulani nilihisi kutengwa kwa sababu ya tofauti za lugha na kitamaduni; na kukaa na kuzoea tena jamii mpya.

 

Mume wangu alikuwa akinitia moyo, na kanisa lilikuwa na ukarimu sana, lakini nyakati fulani nilihisi kuvunjika moyo, kukasirika, au kuchoka tu niliposhughulika na mambo yote mapya. Kwa ndani nilishindana na “jinsi ambavyo mambo yanapaswa kufanyika.” Kwa kweli, ilikuwa tu jinsi nilivyopendelea, au jinsi nilivyozoea kufanya mambo. Nilijua ilikuwa hali ya kujihami, na nilitaka kupata ahueni zaidi kwa tofauti ambazo nilikuwa nikikabiliana nazo sasa, huku pia nikishikilia maadili na mipaka yangu binafsi.

 

Baada ya siku fulani ya kufurahisha sana, nilijikuta nikitazama hatua za mabadiliko. Kulingana na Bridges’ Transition Model ilikuwa ni kawaida kujisikia kuvunjika moyo, kutojali, na kukanganyikiwa katika eneo kati ya mwisho na mwanzo mpya. Hisia hizi hazitadumu milele. Kuwa katika eneo likupalo changamoto kihisia hakumaanishi kwamba nilikuwa kwenye njia isiyo sahihi.

 

Mara nyingi Mungu hutuongoza kufanya mabadiliko. Badiliko la moyo, mahali, taaluma, au mtindo wa maisha. Anatuambia “Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa?” (Isa. 43:18, 19).

 

Lakini wakati fulani tunasahau kuwa ni vigumu kufanya mabadiliko. Hata mabadiliko mema.

Ikiwa Mungu anakuita ili kufanya mabadiliko, usifadhaike ikiwa ni mapito mgumu kuliko ulivyotarajia. Haimaanishi kwamba ulimsikia Mungu vibaya au ulipita mapito mabovu. Kufanya mabadiliko ni jambo gumu. Ni hali ya kawaida kupitia hali ya hamaki, huzuni, upinzani, wasiwasi, uchunguzi, na matumaini katika safari.

 

Katika heka heka zote za mpito, Mungu huwa yuko kila wakati ili kukupatia nguvu, msaada, na zawadi nzuri za kututia moyo njiani. Katika mabadiliko yote ya maisha, Yeye hubaki thabiti daima.

 

Yesu Kristo ni yeye Yule, jana na leo na hata milele” (Ebr. 13:8).

Huenda moja ya vifungu makini sana katika Maandiko kinapatikana katika Yohana 1: Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo Yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani Yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu” (fungu la 1 – 4).

 

Kuna nguvu katika Neno hilo! Linaumba uzima, na ni katika yeye kwamba “Tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu” (Matendo 17:28).

 

Huyu Neno “alifanyika mwili na akakaa kwetu” (Yohana 1:14), na wala hakukoma kuongea hata pale alipopaa kwenda mbinguni. Huyu Neno amekuwa akiongea nasi tangu mwanzo. Tangu Neno Lake la kwanza lililonakiliwa katika Mwanzo 1:3, “Naiwe nuru” hadi katika Neno Lake la Baraka katika Ufunuo 22:20, “Naam, naja upesi” Neno hajatuacha bila sauti Yake.

 

Neno la Mungu linazungumza katika vipengele vyote vya maisha, na ni katika hilo Neno tunasoma: “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo” (3 Yohana 2). Muumba wetu anataka tupate uzoefu wa afya njema—kimwili, kiakili na kiroho.

 

“Uhusiano uliopo kati ya akili na mwili ni wa karibu sana,” aliandika Ellen White. “Mmoja anapoathiriwa, mwingine anaingiwa huruma. Hali ya akili huathiri afya kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko wengi wanavyofikiria. Magonjwa mengi ambayo watu wengi wanakabiliwa nayo ni matokeo ya unyong’ovu wa akili. Majonzi, wasiwasi, kutoridhika, majuto, hatia, kutokuamini, yote hayo huelekea kuvunja nguvu za uzima na kukaribisha uharibifu na mauti.”1

 

Tunapozingatia kipengele muhimu cha afya ya akili, ningependa kupendekeza njia tatu ambazo Neno la Mungu linaweza kusaidia kwa njia bora zaidi katika kujenga afya njema ya akili.

 

 

UHAKIKA

Biblia inatoa mwongozo unaotegemeka, usiobadilika katika ulimwengu usio wa uhakika.

 

Kiuhalisia, ulimwengu unaotuzunguka unamegukameguka. Tunaona haya katika magonjwa yanayoathiri ulimwengu, machafuko ya kijamii, majanga yanayohusiana na hali ya hewa, vurugu zisizodhibitiwa, na changamoto nyingine nyingi za kila siku zinazowafanya watu kuogopa kuhusu ulinzi na usalama wa binafsi. Maisha yamekuwa yasiyo ya uhakika kwa kila mtu ambaye sasa amepatwa na uharibifu unaotokana na maafa makubwa. Wanahitaji kusikia ujumbe wa matumaini na uponyaji ambao Neno la Mungu, Biblia, linatoa. Kinachohitajika sio suluhisho la kisiasa, kijeshi, au kijamii, bali ni kurudi kwa shauku kubwa kwenye msingi wa Biblia—Neno la Mungu lenye uhakika.

 

“Majani yakauka, ua lanyauka; Bali Neno la Mungu wetu litasimama milele” (Isa. 40:8).

 

Wote tumepitia uzoefu wa kufikwa na majanga maishani, na bila shaka tutapitia mengi zaidi. Lakini Neno la Mungu linatupatia msingi imara ambao juu yake tunaweza kujenga imani yetu. Yesu anatuambia: “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba” (Mt. 7:24, 25).

 

 

AMANI

Biblia Inatupatia amani wakati huu sasa.

 

Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, “Magonjwa ya wasiwasi ndio magonjwa ya akili yanayojulikana zaidi ulimwenguni, ambayo yaliathiri watu milioni 301 mnamo 2019.”2 Watu wanahofu wanapouangalia kwa wasiwasi ulimwengu unapomeguka pande zote.

 

Neno lililovuviwa linatuambia, “Amani idumuyo, pumziko la kweli la roho, lina Chanzo kimoja tu. Hili ndilo lilimfanya Kristo kuzungumza aliposema kwamba, ‘Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.’ Mathayo 11:28. “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo.

 

Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.’ Yohana 14:27. Amani hii sio kitu ambacho anakitoa mbali na Yeye Mwenyewe. Amani hii iko ndani ya Yesu na tunaweza kuipata tu kwa kumpokea Yeye.”3

 

Yesu anaongea nasi leo kupitia Neno Lake lililoandikwa. Ni kwa kutumia muda mwingi katika kujifunza Neno Lake, tukiisikiliza sauti Yake, na kumfuata Yeye; ndipo tunaweza kuipata amani Yake.

 

Tunasoma katika kitabu cha The Ministry of Healing: “Hatupaswi kuruhusu wakati ujao, pamoja na matatizo yake magumu, matazamio yake yasiyoridhisha, kuifanya mioyo yetu kuzimia, magoti yetu kutetemeka, na mikono yetu kulegea. ‘Yeye azishikaye nguvu zangu,’ asema Mungu Mwenyezi, ‘Afanye amani nami; naam, afanye amani nami.’ Isaya 27:5. Wale wanaosalimisha maisha yao kwa uongozi Wake na kwa utumishi Wake kamwe hawatawekwa katika nafasi ambayo Yeye hakutaka wawepo. Hata tuwe katika hali gani, ikiwa tu watendaji wa neno Lake, tunao Mwongozo wa kuelekeza njia yetu; hata tufadhaishwe jinsi gani, tunaye Mshauri wa hakika; hata tukihuzunishwa, kufiwa, au upweke, tuna Rafiki anayehuzunika pamoja nasi.4

 

 

TUMAINI

Biblia inatoa tumaini tunaloweza kulidai sasa au hapo baadaye.

 

Matukio makuu ya kusononeka na hisia za kukata tamaa zinaongezeka. Ingawa ni vigumu kupata takwimu za ulimwenguni pote, Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Akili nchini Marekani inaripoti kwamba mwaka 2021, inakadiriwa kwamba watu wazima milioni 23 (wenye umri wa miaka 18 au zaidi) nchini Marekani “walikuwa na angalau tukio moja kuu la msongo.” Zaidi ya hayo, inaripoti “Uongezekaji wa watu wazima walio na matukio makubwa ya ugonjwa wa msongo ulikuwa wa juu zaidi kati ya watu wenye umri wa miaka 18-25 (18.6%).”5

 

Watu, hasa vijana, wanatafuta maana, na kusudi la maisha yao, na tumaini la wakati ujao. Wanauliza, “Kwa nini niko hapa?” “Kusudi langu ni nini?” “Je, haya ndiyo tu yaliyo maishani?”

Neno la Mungu linatulekeza kwenye tumaini tunaloweza kulidai sasa na hata baadaye. Yesu anatuambia, “Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” (Yohana 10:10). Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho” (Yeremia 29:11).

Na pamoja na kujua Mungu anataka tuwe na maisha tele hapa na sasa, tunaweza kutazamia kwa shauku tumaini kuu la ujio Wake wa mara ya pili hivi karibuni na mahali pa fahari alipotuandalia.

 

“Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita . . . Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kiti kile cha enzi ikisema, ‘Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake, Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao na kuwa Mungu wao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao; wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yatakuwa yamekwisha kupita’ ” (Ufu. 21:1, 3, 4).

 

Wapendwa, Neno la Mungu linatupatia tumaini na hakikisho tunalolihitaji. Ninakutia moyo kutumia muda wako kulisoma kila siku, ukisikiliza kile ambacho Mungu anataka kukuambia leo kwa ajili ya afya yako ya kiroho, kimwili, kijamii na kiafya.

Wakati wa maombi ya asubuhi katika programu ya mafunzo ya Global Mission huko Sudani Kusini nilishuhudia tukio ambalo sikutarajia kabisa. Tulipowauliza waliohudhuria kutaja mambo ya kuombea, kijana mmoja karibu na nyuma ya chumba aliinua mkono wake.

 

“Tuwaombee Al Shabaab.”

 

Al Shabaab? Niliwaza, huku nikikumbuka kuwa kundi hili la itikadi kali ndilo lililohusika na mashambulizi mengi ya kigaidi Afrika Mashariki.

 

Kisha mtu mwingine aliinua mkono wake na kuongeza, “Ndio, na Boko Haram na ISIS, pia.”

 

Hivi ni kweli? Nikadhani kwamba walimaanisha tuombe ulinzi dhidi ya makundi ya kigaidi ambayo yameikumba Afrika na sehemu nyingine za ulimwengu. Hii ingeleta maana kamili.

 

Muda mfupi baadaye nilipiga magoti pamoja na mshirika wangu wa maombi, mmoja wa wakurugenzi wa Global Mission wa kanda. Alianza kuomba, “Bwana, asubuhi hii tunaomba mahsusi kabisa kwa ajili ya Al Shabaab na Boko Haram. Tunajua kuwa Wewe ni Mungu wa Nebukadneza. Tunajua kuwa ulituma ndoto na maono na kubadilisha moyo wa mfalme huyu gaidi. Ninakuomba uifikie mioyo ya vikundi hivi viovu katika ulimwengu wetu leo kama vile ulivyofanya kwa Nebukadneza. Tuma ndoto na maono; wafikie kwa udhihirisho wa uweza Wako.”

 

Hakuwa akiomba tu kwa ajili ya ulinzi dhidi ya magaidi, kama ambavyo ni muhimu kufanya hivyo. Alikuwa akiomba kwa ajili ya kubadilishwa kwao. Na kisa kilichomtia moyo kuomba kwa imani ya namna hiyo kilikuwa ni kisa cha Mungu na Nebukadneza (angalia Dan. 1—4).

 

 

KUWAOMBEA MAGAIDI?

Akili yangu ilianza kushughulika na wazo hili lote la kuwaombea magaidi. Nebukadneza hakuwa gaidi pekee ambaye Mungu alimjali na kumbadilisha. Kulikuwa na Naamani, Muajemi (2 Wafalme 5). Mungu hakufungwa na mipaka ili kumsaidia Naamani. Alimtumia mmoja wa mateka wa Naamani mwenyewe kutoka kwenye uvamizi wa kigaidi, binti mdogo mtumwa wa Kiisraeli, ili kumshuhudia. Na vipi kuhusu watu wa Ninawi? (angalia Yona.) Orodha iliyonukuliwa ya ukatili na uovu wao hufanya shughuli za ISIS zionekane kuwa nyepesi. Zaidi ya hayo, Mungu alilazimika kufanya kazi na nabii Yona, mkaidi, mwenye chuki, asiyekuwa tayari ili kuwapa Ninawi nafasi ya kumjua Yeye. Yona hakujali, lakini Mungu alijali. Kukumbuka namna ambavyo Mungu aliwajali watu hawa waovu kulininyenyekeza sana. Kamwe sikuwahi kuwaza kuwaombea magaidi wa siku hizi. Kama vile Yona, kamwe sikuwahi kutegemea Mungu angeweza kuwaokoa. Kamwe sikuwahi kujali vya kutosha hata kuwaombea.

 

Tukio hili la maombi huko Sudani Kusini lilijaza moyo wangu kwa mtazamo mpya na namna mpya ya nguvu. Nilianza kuomba mara kwa mara kwa ajili ya magaidi ulimwenguni kote, nikijua kuwa Mungu wa Naamani, wa watu wa Ninawi, na wa Nebukadneza anawajali na anawataka wamjue Yeye. Visa vyao vinanikumbusha kuwa hakuna kilicho kigumu sana kwa Mungu. Pia vinafunua kwamba anazo njia na namna ya kuifikia mioyo ya watu ambao wangetushangaza sote.

 

Wale ambao tumekua tukiwa Wakristo tunakumbushwa kila mara kwamba tunamtumikia na kumwomba Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Pale ninapomwomba Mungu wa wazee hawa, ninakumbushwa kwamba imani yangu imekita mizizi kwa Mungu ambaye anawaita watu wa kawaida na kuwaongoza katika nyakati njema na nyakati mbaya. Anasamehe na kuongoza. Anaweza kufanya pia yasiyowezekana.

KUPANUA MAOMBI YETU

Tangu siku ile huko Sudani Kusini, Nimepanua na kuboresha maombi yangu yote kwa kukumbuka na kutumia hadithi za watu wengine katika Biblia ambao walishirikiana na Mungu. Kukita maombi yangu kwa Mungu ambaye amefunuliwa katika visa hivi vya ajabu kumekuza imani yangu sana. Visa vilivyonukuliwa hapa chini ni mifano:

Kwa namna isiyowezekana, ukizingatia visa vya namna Mungu alivyombariki Sara (Mwa. 20; 21), Hana (1 Samweli 1), na Elizabeth (Luka 1) vimenifurahisha sana.

 

Utayari wa Mungu kufanya kazi na watu wasio wakamilifu na kuwabariki bila kujali mapungufu yao uko wazi katika visa vya Gideoni (Waamuzi 6), Samsoni (Waamuzi 13 – 16), na Petro (Yohana 21:15 – 19).

 

Visa vya Mungu kumuita Musa (Kutoka 3) na Isaya (Isaya 6) na Yeremia (Yeremia 1) huimarisha imani yangu katika uwezo wa Mungu wa kufidia mapungufu yangu.

 

Ninapojihisi kuachwa peke yangu, ninamkumbuka Mungu wa Yusufu, wa Eliya na wa Daudi.

 

Kisa cha ajabu cha Mungu na Mfalme Manase (2 Nyakati 33) kinanikumbusha kwamba Mungu anaweza kusamehe hata dhambi ionekanayo kuwa mbaya sana pale tunaporudi Kwake.

 

Yupo Mungu wa Yona, aliye Mungu wa Yakobo na Yohana. Yeye ni mvumilivu kwa wanafunzi wasio wakamilifu, wakali, hata wenye kulipiza kisasi.

 

Mungu wa Mariamu Magdalena, Zakayo, wenye ukoma, na mwanamke pale kisimani huko Samaria ni Mungu anayewajali waliotengwa na jamii.

 

Orodha ni ndefu sana. Mamia ya visa kwenye Biblia vinaonyesha namna ambavyo Mungu amefanya kazi pamoja na watu wa haiba zote katika mazingira ya aina zote. Visa hivi vimejawa na uwezo wa kujenga imani “vifaavyo kwa ajili ya maombi.” Kupitia visa hivi tunaweza kujikumbusha kile ambacho Mungu amefanya hapo zamani na yuko tayari zaidi kufanya wakati huu wa sasa na hata baada ya sasa.

 

Kwa kweli, Yeye ni Mungu wa Ibrahimu, Samsoni, na Nebukadneza, ni Mungu wetu sote.

Tangu mwaka 1863, Waadventista wa Sabato wamekuwa wakifahamika taratibu kwa uhamasishaji wa maisha ya afya na mtindo wa maisha. Baadhi ya tafiti za hivi karibuni zimeonyesha kwamba Waadventista wana afya bora zaidi na wanaishi katika wastani wa miaka saba hadi kumi zaidi ya watu wote kwa ujumla.1 Ellen G. White, mmojawapo wa waasisi wa dhehebu la Waadventista, amekuwa na jukumu muhimu katika kuanzishwa kwa mtindo mahususi wa maisha ya Waadventista ambayo ndio msingi nyuma ya mengi ya matokeo haya ya hivi karibuni.

 

Alipokea maono yake mawili makuu ya afya mwaka 1863 na 1865. Kwa namna fulani, maono hayo mawili yalithibitika kuwa “kipindi muhimu” kwa dhehebu jipya la Waadventista wa Sabato. Waadventista hawakuwa tu wanamatengenezo ya afya, bali pia walijumuisha suala la afya katika utume wao wa jumla kwa ulimwengu. Ujumbe wa afya ukawa sehemu ya utambulisho wao wa pekee.

 

 

NJOZI YA AFYA YA MWAKA WA 1863

Waadventista Watunza Sabato walijipanga rasmi katika dhehebu la Waadventista Wasabato mnamo tarehe 21 Mei 1863, huko Battle Creek, Michigan. Takribani majuma mawili baadaye, mnamo Juni 6, Ellen White alipokea ndoto yake ya kwanza kubwa kuhusiana na afya. Ujumbe wake unahusisha kanuni “kuu” za jumla zinazohusiana na umuhimu wa kuishi maisha ya afya kadhalika na baadhi ya maagizo maalumu kwa James na Ellen White.

 

Ujumbe wa jumla wa njozi hii ya kwanza ulikuwa rahisi sana: Waadventista wa Sabato, wakiwemo James na Ellen White, walipaswa kuzingatia zaidi afya zao. Suala la afya ni la muhimu. Zaidi ya hayo, njozi hii ilionyesha suala la afya kwa maneno ya kina. Afya njema ilipaswa kuwa uzoefu kamili. Ilitegemea mtindo mzima wa maisha ya mtu. Huu ulikuwa mwanzo wa msisitizo wa kiafya wa Ellen White katika fikra na uandishi wake.

 

Mwaka mmoja baadaye, aliandika na kueleza zaidi kile alichokuwa ameonyeshwa. Katika maelezo yake marefu, yaliyochapishwa chini ya kichwa “Afya,” katika Spiritual Gifts, gombo la 4, aliandika kuhusu mlo na hatari za kutokuwa na kiasi, umuhimu wa kudhibiti uchu wa kula, kukataza kula nyama ya nguruwe, faida ya chakula cha mboga, athari ya sumu ya kutumia tumbaku na vichangamsha mwili vingine, umuhimu wa usafi na hewa safi, uwiano katika kufanya kazi na kupumzika, faida za maji, matumizi ya dawa za asili kwa uponyaji badala ya “kubwia dawa,” mara kwa mara, umuhimu wa kumwamini Mungu, na matumizi mengine ya kivitendo ya afya2. Alianza kuelezea suala la afya kwa namna tofauti—ikihusiana na mambo ya muhimu ya uzima kimwili, kiakili na kiroho3.

NJOZI YA AFYA YA MWAKA WA 1865

Kwa udadisi (au pengine sio kwa udadisi sana), Waadventista wachache waliitikia ujumbe wa Ellen White (au wa Mungu) ili kufanya suala la afya kuwa kipaumbele chao. Hata hivyo, Yesu alikuwa akirudi hivi karibuni na suala la afya halikuwa sehemu ya utume wa Waadventista wa Sabato, waliwaza. Mnamo Desemba 25, 1865, Ellen White alipokea njozi kubwa ya afya ya pili huko Rochester, New York. Nilionyeshwa kwamba watu wetu watunza Sabato wamezembea katika kutenda kulingana na nuru ambayo Mungu ameitoa kuhusiana na matengenezo ya afya,” aliandika, “. . . na kwamba, kama jamii, tumekuwa nyuma sana kufuata maongozi ya Mungu kama alivyochagua kutuongoza. Nilionyeshwa kwamba kazi hii ya matengenezo ya afya ilikuwa bado haijatekelezwa.” Kisha akabainisha kwamba waumini wengi hawakujali, hawakuamini umuhimu wa afya, au walikuwa wamefanya “mwonjo” na “uchu” wao kuwa mungu wao4.

 

Hata hivyo, njozi ya afya ya mwaka 1865 haikuwa tu onyo dhidi ya upuuziaji. Ellen White alionyeshwa kwamba suala la afya linapaswa kuwa sehemu muhimu ya utume wa Waadventista wa Sabato kwa ujumla.

 

Nilionyeshwa kwamba Matengenezo ya Afya ni sehemu ya ujumbe wa malaika wa tatu, na imeungana kwa karibu sana na ujumbe huo, kama mkono na mkono na mwili wa mwanadamu. Niliona kwamba sisi kama watu lazima tuchukue hatua madhubuti katika kazi hii kuu,” alifafanua Ellen White5. Waumini Waadventista wa Sabato hawakupaswa tu kuweka katika vitendo matengenezo ya afya, lakini kanisa lilikuwa na wajibu wa kiroho kufundisha wengine juu ya umuhimu na manufaa yake.

 

Njozi hii ya pili iliwataka Waadventista wa Sabato kuanzisha taasisi zao wenyewe za afya ambazo zitasaidia kazi ya juhudi za umishenari wa tiba. Kusema kweli, Ellen White aliandika kwamba uinjilisti wa kitabibu ni wa muhimu katika kufikia watu ambao wasingeweza kufikiwa na aina nyingine za uinjilisti.

 

“Watu wetu wanapaswa kuwa na taasisi yao wenyewe, katika umiliki wao wenyewe, kwa ajili ya manufaa ya wagonjwa na wanaoteseka miongoni mwetu,” aliandika. “Taasisi ya namna hiyo, ikiendeshwa vizuri, inaweza kuwa njia ya kufikisha ujumbe wetu mbele ya wengi ambao ingekuwa vigumu kwetu kuwafikia kwa njia ya kawaida ya kuutetea ukweli. Wakati wasioamini watakapokimbilia katika taasisi iliyojizatiti katika mafanikio ya tiba ya magonjwa, na inayoendeshwa na madaktari watunza Sabato, wanaletwa moja kwa moja na kuwekwa chini ya mvuto wa ukweli. . . . Kwa hiyo, wanapokuwa wamewekwa chini ya ushawishi wa ukweli, wengine hawatapata tu ahueni kutokana na udhaifu wa mwili, lakini pia roho zao zinazougua ugonjwa wa dhambi zitapata dawa ya uponyaji6.

 

Kwa namna fulani, Ellen White alisisitiza uhusiano ambao ulipaswa kuwepo kati ya injili na huduma za afya. Hata hivyo, Yesu alikuwa akizifanya zote kwa pamoja—kufundisha na kuponya—lakini alitumia “muda mwingi kutoa uponyaji” kuliko kuhubiri7.

 

Zaidi ya hayo, matendo Yake ya uponyaji yalipita uponyaji wa mateso ya kimwili tu. Alifanya “kila kazi ya kuponya kuwa tukio kwa ajili ya kupandikiza kanuni za Mungu akilini na rohoni. Hili lilikuwa kusudi la kazi Yake.8” Huduma ya Yesu ya uponyaji ilijumuisha uponyaji wa mtu kikamilifu na Waadventista wa Sabato wanalazimika kufuata kielelezo Chake.

 

Baada ya muda, Waadventista wa Sabato waliitikia maono na miito ya Ellen White na hatimaye dhehebu likawa chombo kikuu cha kukuza afya kamili na maisha yenye afya kote ulimwenguni. Leo hii, Kanisa la Waadventista wa Sabato lina mfumo mkubwa zaidi wa Afya zaidi ya Waprotestanti ulimwenguni na mamia ya hospitali, zahanati, nyumba za uuguzi na wastaafu kote ulimwenguni. Lakini yote hii ilianza tu na ujumbe sahili miaka 160 iliyopita ambapo suala la afya lilipaswa kuwa sehemu ya utambulisho na utume wa Waadventista wa Sabato ulimwenguni.

Kwa ujumla inaaminiwa kwamba Kol. 1:15 – 20 ni wimbo wa Kikristo wa awali unaoonyesha, kwa ufupi, usanifu, kina, na kwa njia ya kishairi, ukuu wa Yesu kuwa ni Muumba na Mkombozi. Ikiwa ni wimbo, una beti mbili: Yesu Muumbaji (f. 15:17); na Yesu Mkombozi (f. 18 – 20).

 

 

1.  WA ULIMWENGU WOTE (F. 15 – 17)

Ubeti wa kwanza unatupatia taswira muhimu katika kazi ya Kristo kwa ulimwengu mzima. Anatambulishwa kwetu kuwa, “ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote” (f. 15; “wa kwanza” kwa maana ya kuwa mwenye mamlaka juu ya viumbe vyote).

 

Umuhimu wa vyeo hivi viwili unakuzwa kwa kusema kwamba vitu vyote viliumbwa “katika Yeye”—Yeye ni Muumba wa ulimwengu mzima ikiwa na maana kwamba Aliumba vitu vyote mbinguni na duniani, vinavyoonekana au visivyoonekana, pamoja na viumbe wa mbinguni (“enzi au milki au tawala au mamlaka”). Vihusishi vitatu vimetumika ili kuelezea tendo la uumbaji: vyote viliumbwa “katika Yeye” (katika umoja na Yeye; kabla ya dhambi kuwepo), “katika [inaonyesha uweza] Yeye,” na “kwa ajili Yake” (ikimwonyesha Kristo kuwa kiini chake). Wimbo unaendelea kudhihirisha kwamba Mwana wa Mungu hakuwa kiumbe kwa sababu “Amekuwepo kabla ya vitu vyote” na kwa sababu vilikuwa “vimeumbwa kwa njia ya (dia) Yeye na kwa ajili (eis) Yake.” Hatimaye fungu linaweka wazi kuwa “vitu vyote hushikana katika Yeye” (f. 17)—Yesu Kristo ndiye anayeushikilia ulimwengu wote pamoja na kuuhifadhi uwepo wake. Ubeti wa kwanza unatuambia Mwana ni nani hasa kuhusiana na uumbaji (Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, Muumbaji, na Mtegemezaji), na ukuu na mamlaka Yake juu ya viumbe vyote (mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote), na Muumba na Mtegemezaji wake.

 

 

2. KRISTO MKOMBOZI (F. 18 – 20)

Ubeti wa pili unamtambulisha Mwana kuwa kichwa cha mwili Wake, kanisa, na kuwa mwanzo wa ubinadamu mpya. Cheo “mzaliwa wa kwanza wa waliokufa” husisitiza Mamlaka Yake miongoni mwa wale watakaofufuliwa, maana pasipo ufufuo Wake hakuna ufufuo kutoka mautini.

 

Dhana ya mamlaka inaelezewa zaidi na kifungu hiki “Atakuwa na nafasi ya kwanza katika kila kitu,” hiyo ni kusema Mwana atarejesha kile kilichokuwa cha Kwake alipokuwa ameumba vitu vyote. Hii inawezekana kwa sababu ya kufanyika mwili Kwake: “Ilimpendeza sana Baba kuwa utimilifu wote ukae Kwake.” Kusudi la kufanyika mwili linaelezewa kuwa ni: Ili kuvipatanisha vitu vyote—mbinguni na duniani—kwa njia ya kifo cha kafara Yake. Kwa namna moja au nyingine, ulimwengu wote utakuwa umepatanishwa kwa Mwana (Fil. 2:9 – 11).

 

 

3. MAONI KUHUSIANA NA WIMBO:

Ubeti wa kwanza unamwasilisha Mwana kuwa Muumbaji ambaye kimsingi hutofautiana na vilivyoumbwa—Yeye ni Mungu. Ukuu Wake juu ya na jukumu Lake la msingi katika uumbaji vimeonyeshwa wazi. Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana ndani ya ulimwengu. Akiwa mwonekano wa Mungu na mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote, wajibu Wake wa msingi ni kufunua kwa ulimwengu wema wa Mungu. Ni wakati huu katika historia ya ulimwengu kwamba Anachukua jukumu hili muhimu. Ubeti wa kwanza unaelezea hali ya ulimwengu pasipo kuwepo kwa pambano la ulimwengu. Ubeti wa pili unaonyesha pambano la ulimwengu na kuelezea kazi ya Mwana kuwa inahusika katika upatanisho wa ulimwengu wote. Ufanisi wa kazi hii sasa unaonekana katika ukuu Wake ndani ya kanisa na utafikia upana wa ulimwengu hata kama ni upatanisho wa ulimwengu.

 

Katika Utafiti wa Ulimwengu wa Washiriki Waadventista wa Sabato iliripotiwa kwamba asilimia 47 ya wale waliohojiwa wanaamini kwamba ufuasi kamili wa ujumbe wa afya hutoa uhakika wa wokovu. Hakuna ushauri wa kibiblia au wa Roho ya Unabii unaounga mkono maoni haya, ambayo ni kinyume kabisa na mafundisho yetu rasmi kama ilivyoelezwa kwa ufupi na mtume Paulo: “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu” (Efe. 2:8, 9). Matendo yetu hayatuhakikishii wokovu: ni zawadi ya neema ya Mungu! Ombi letu ni kwamba kusiwe na mkanganyiko katika siku zijazo juu ya jambo hili.

 

Baadhi ya maelezo ya ziada kutoka kwenye utafiti huo yanaweza kutusaidia. Uchunguzi huo ulithibitisha kwamba zaidi ya asilimia 80 ya wale waliohojiwa walikubali ujumbe wa afya wa Waadventista wote na kwamba ndiyo msingi wa imani za Kanisa la Waadventista. Wanakubali zaidi kwamba inathibitishwa na sayansi ya afya na inaweza kuimarisha ubora na urefu wa maisha. Zaidi ya asilimia 90 ya washiriki wa kanisa wanajiepusha na pombe na asilimia 97 na aina zote za tumbaku. Licha ya pendekezo kali la kanisa la kutumia mlo kamili wa mboga, ni asilimia 19 tu ya waliohojiwa waliripoti kuwa wala mboga au wasiotumia mazao ya wanyama kabisa (vegan).

 

Tangu Uumbaji, Mungu aliweka msisitizo juu ya ustawi kamili kuanzia na wazazi wetu katika Bustani ya Edeni—huduma ya kiroho, mazoezi ya viungo, chakula chenye lishe bora, na vifungo maridhawa vya uhusiano kati ya washiriki katika familia ya kwanza. Baada ya Anguko na Gharika alitoa maagizo juu ya vyakula safi na najisi, elimusiha, na usafi. Yesu alikua kikamilifu katika kimo (mwili), hekima (akili), akimpendeza Mungu (kiroho) pamoja na wanadamu (angalia Luka 2:52). Alisema wazi kwamba alikuja ili tuwe na uzima “kisha tuwe nao tele” (Yohana 10:10).

 

Alipoulizwa kwa nini kanisa hilo changa lilikuwa limepewa ujumbe wa afya, Ellen White alijibu kwamba ni kwa sababu kazi yetu ilikuwa bado haijafanywa.* Afya ni muhimu ili tuweze kutumika, lakini pia tuwe na akili safi na utambuzi wa ukweli wa milele. Hatujaokolewa na ujumbe wa afya. Kuishi kwa afya kunaweza kutusaidia kutupatia usahili wa kiakili ili tuweze kusikia kwa uwazi zaidi sauti ya Roho Mtakatifu na kuimarisha uelewa wetu wa Neno la Mungu. Hilo ni kweli hasa wakati akili zetu zikiwa hazijaharibiwa na pombe, tumbaku, na dawa nyinginezo.

 

Kuuishi ujumbe wa afya kunaweza kuimarisha safari yetu ya kiroho. Hebu tusiukubali tu—bali tuukumbatie! “Mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa” (2 Nyakati 20:20).

Kila siku, baada tu ya wito wa kuchukua barua, Art alishuka hadi kwenye ukumbi wa shule na kutembea taratibu kuelekea ukuta uliokuwa na masanduku ya barua yenye milango ya shaba. Mlango kwenye kila sanduku ulikuwa wa takriban inchi nne za mraba, na ulikuwa na utaratibu changamano wa kufunga ili kuhakikisha kuwa vilivyomo viko salama. Sanduku 231 lilikuwa lake, na lilikuwa tupu kila siku mwezi wa Desemba.

 

Leo ilikuwa Desemba 24, siku moja kabla ya Krismasi. Art alisimama mbele ya masanduku kwa muda mrefu, akikaribia kuamua kuondoka, lakini alikuwa amedhamiria kuangalia sanduku lake, huenda matokeo ya leo yangeweza kuwa tofauti.

 

Hatimaye, alipiga hatua mbele, akanyoosha mkono, na kuzungusha namba maalumu ambazo zingefungua Sanduku 231. Moyo wake ulikuwa na huzuni, lakini wenye matumaini.

 

 

SHAUKU YA KWENDA NYUMBANI

Art alikuwa na umri wa miaka 13, mvulana Mzaliwa wa Marekani kutoka kabila la Mohican, akisoma katika shule ya bweni ya serikali huko Lawrence, Kansas. Angependelea kuishi na wazazi wake, dada zake watatu, na kaka zake wawili, huko nyumbani katika Hifadhi ya Menominee huko Wisconsin, lakini hakukuwa na shule katika eneo lao. Serikali ya Marekani ilikuwa imechagua kufanya mapatano na Haskell, shule ya binafsi huko Lawrence, na viongozi wa Kikabila wa Halmashauri walikubali kwamba watoto hao wangeweza kwenda.

 

Isipokuwa kwa miezi ya joto ya kiangazi, na majuma mawili mafupi wakati wa Krismasi, shule ya Haskell ikawa makazi ya Art. Shule iliendeshwa kwa mkono mkali wa kijeshi. Chakula kilikuwa duni, si kitu kama chakula alichoandaa mama Art nyumbani kwa ajili ya familia. Kila siku ilimbidi avae shati la sare iliyohitajika yenye miraba yenye kung’aa ya rangi nyekundu na nyeusi iliyoashiria kuwa yeye ni “Mhindi,” mtu anayedaiwa kuwa na thamani ndogo kuliko walimu wake au watu wengine mjini.

 

Art alijisikia vibaya na mpweke. Moyo wake ulimuuma sana hata akafikiri huenda umevunjika. Alijaribu kutomtazama mwanafunzi yeyote yule, hakika wangeyaona machozi yaliyokuwa yakimlengalenga. Kila dakika alitamani angekuwa nyumbani pamoja na familia yake katika Hifadhi ya Menominee.

Hasa Krismasi hii.

 

“Nyumbani” kwa kweli hakukuwa Wisconsin, “nyumbani” ilikuwa mbali kueleka Mashariki katika milima ya kule ambako sasa kuliitwa jimbo la New York. Lakini, kwa vile serikali ilitaka eneo hilo, kabila lake lote la Wamohican Wazaliwa wa eneo hilo walikuwa “wameondolewa,” na “kuhamishiwa” kwenye misitu ya ajabu na nyika ya Wisconsin. Walipofika, kila Mmohican alipewa jina jipya, na familia ilipewa ekari 90 za ardhi.

 

Babu yake Art aliposimama mbele ya wakala wa Kihindi kwenye nyumba yake mpya ya hifadhi, mwanamume huyo alisema kwamba majina yote mapya yalikuwa yamechukuliwa. “Kwa hivyo, nitakupa jina langu,” wakala alisema. “Ninatoka Uingereza, na jina langu ni Church. Utakuwa Bwana George Church.”

 

Mtu fulani alipewa jukumu la kuwafundisha Wahindi Wamarekani kuwa wakulima, lakini hilo halikufaulu sana. Badala yake, baba yake Art alichagua kuwa mjenzi, seremala stadi ambaye alitumia miti ya asili na matofali yaliyovunjika yaliyopatikana kwa urahisi ili kuwajengea Wahindi wenzake nyumba imara. Alikuwa mkandarasi makini, lakini ujenzi wa majengo ya mawe ulikuwa kazi ngumu uliohitaji umahiri wa baba yake Art na wanawe wote. Walifanya kazi kwa muda mrefu, taratibu sana wakifanya kazi yenye mafanikio.

 

Alipofikisha umri wa miaka 11, Art aliuliza kama angeweza kwenda shule. Ilikuwa vigumu kwa Mama na Baba kumruhusu aende, lakini hatimaye familia ilikubali kwamba angeweza kupokea tiketi ya gari-moshi kutoka kwa karani wa usafirishaji na kusafiri kuelekea Kansas ya mbali.

 

Art alifurahi kujifunza, lakini aliishi akitazamia kwa hamu wakati wa likizo. Hasa likizo ya Krismasi.

 

 

ZAWADI BORA

Mwaka huu, mwaka wake wa tatu katika shule ya Haskell, hakukuwa na likizo ya Krismasi. Janga kubwa la mafua lilikuwa limeupiga ulimwengu na kusababisha vifo vingi kila pande za Amerika, hususan miongoni mwa Wazaliwa wa Marekani katika makazi yao ya hifadhi. Viongozi wa shule, wakihofia kwamba huenda kuwaruhusu wanafunzi kwenda likizo kungeweza kusababisha kurudi shuleni na ugonjwa huo, walikuwa wamefunga shule, wakawaweka karantini wanafunzi, na kufuta safari zote za likizo.

 

Hakuna mtu aliyeenda nyumbani kwa ajili ya Krismasi.

 

Art alihisi kama vile Krismasi yenyewe imefutwa, na kuwa na wasiwasi kwamba asingeweza kurudi nyumbani tena.

 

Diski ya namba hatimaye iliitika, na mlango wa Sanduku la Posta 231 ukafunguka.

 

Ndani, bahasha ndogo ilisubiri.

 

Art aliona uandishi wa kuparuza wa mama yake juu ya bahasha, akaichomoa haraka kutoka kwenye sanduku lake, akaificha ndani kabisa ya mojawapo ya mfuko wake wa koti, na kukimbia Kansas mchana huo wenye baridi. Moyo wake ulikuwa ukilipuka kwa furaha na miguu yake ilikuwa ikicheza kwa mahadhi ya furaha! Barua kutoka nyumbani! Kutoka kwa Mama!

 

Kwa kitambo kidogo, kila kitu kilionekana kuwa sawa.

 

Alikimbia hadi sehemu yake maalumu tulivu iliyo chini ya ngazi ya bweni, mahali ambapo hakuna mtu angeweza kumwona, akaifungua bahasha hiyo kwa umakini. Ndani yake alikuta kadi ya kawaida sana iliyotengenezwa na Mama.

“Heri ya Krismasi Mwanangu,” Mama alikuwa ameandika kwa penseli nyeusi. Kisha alikuwa amechora moyo mzuri na maneno, “Tunakusubiri kwa hamu nyumbani.” Chini ya moyo Mama alikuwa ameandika maneno mengine mawili, maneno ya familia ambayo yalifanya muhtasari wa kila kitu ambacho Art alijua kuhusu Mungu na Yesu na Krismasi na familia.

 

“Kwa upendo. Mama.”

 

Kulikuwa na jambo jingine zaidi. Mama alikuwa ameunganisha kwa umakini sarafu ya fedha angavu kwenye kadi. Hakumwambia jinsi ya kuitumia au kwa nini alikuwa ameituma au kusema chochote juu ya sarafu hiyo.

 

Aliiunganisha tu vizuri ili isidondoke kutoka kwenye barua. Namna alivyotumia fedha hiyo ni juu yake mwenyewe! Senti kumi zote. Ilikuwa ni bahati (wakati huo) kwa mvulana ambaye alikuwa amevaa nguo nyekundu na nyeusi, akilia kwa furaha chini ya ngazi.

 

Alipapasa kidole gumba chake juu ya sarafu polepole na kusoma maneno tena na tena na tena. Krismasi haikuwa juu ya zawadi pekee; Ilikuwa ni juu ya familia! Walimpenda!

 

Walitamani arudi nyumbani!

 

Kadi iliyotengenezwa na Mama–furaha ya upendo wa familia yake–Art mara nyingi alisema ilikuwa ni zawadi kubwa

Sarah alikuwa binti mzuri, aliyekuwa tayari wakati wote kukusalimu kwa tabasamu na kwa uchangamfu. Lakini siku moja, wingu la giza jeusi lilionekana kuujaza moyo wake, na hakuweza kueleza kwa nini iwe hivyo. Alijihisi mwenye huzuni na mwenye mashaka kila wakati, na rafiki na familia yake walitambua kuwa kuna kitu hakikuwa sawa.

 

Asubuhi moja yenye jua kali, Sarah akiwa ameketi peke yake chini ya kivuli cha mti mkubwa wa mwaloni, bibiye, Bibi Ruth, alimkaribia kwa tabasamu maridhawa. Bibi Ruth alikuwa na njia yake ya kuelewa mambo ambayo hakuna mtu mwingine aliweza kufanya hivyo.

 

“Sarah,” Bibi Ruth alisema, “Naona kwamba umebeba mzigo mzito moyoni mwako. Je, ungependa kuzungumzia?”

 

Machozi yakaanza kumtoka Sarah, akaitikia kwa kichwa. “Sijui, Bibi. Ninahisi tu huzuni na hofu kila wakati. Sijui nina shida gani.”

 

Bibi Ruth alimshika Sarah na kwenda naye mahali pazuri chini ya mwaloni. Alichukua Biblia ndogo kutoka kwenye mfuko wa sketi yake na kufungua mstari ambao alijua ungemfariji mjukuu wake. Alisoma kwa sauti kutoka Wafilipi 4:6–7: “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane kwa Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”

 

Sarah alisikiliza kwa makini maneno hayo na kuyafuta machozi yake. “Lakini nitafanyaje hivyo, Bibi? Je, nitaachaje kuwa na wasiwasi?”

 

Bibi Ruth alitabasamu kwa uchangamfu na kujibu, “Ni safari, mpendwa wangu. Kama safari nyingine yoyote, huanza na hatua moja. Kwanza, tunaomba pamoja na kumkabidhi Mungu mashaka yako yote.

 

Anakujali sana, na anataka kukusaidia.”

 

Kwa hiyo, Sarah na Bibi Ruth walipiga magoti chini ya mti wa mwaloni na kuomba pamoja, wakimimina hofu na wasiwasi wote wa Sarah kwa Mungu. Alihisi mwanga wa matumaini, kama mwanga mdogo unaomulika katika giza la moyo wake.

 

Walipoinuka kutoka magotini, Bibi Ruth alimshika mkono, na wakaanza kutembea kuelekea nyumbani. Walikaa kimya kwa muda kabla ya Bibi kuongea tena. “Unajua Sarah, hauko peke yako. Kuna watu wengine wengi duniani ambao wamekuwa na aina ya hisia kama wewe! Hata mashujaa hodari katika Biblia kama Daudi walikabiliana na nyakati za huzuni na hofu. Katika kitabu cha Zaburi, Daudi alizungumza kuhusu mapambano yake.

 

Katika fungu moja, aliandika, ‘Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao’ (Zaburi 34:17). Tafadhali kumbuka, mpendwa wangu, kamwe hauko peke yako katika mapambano yako. Mungu yuko nawe wakati wote, akiwa tayari kukusikiliza na kukusaidia.”

 

Sarah alisikiliza kwa umakini, macho yake yakijawa na matumaini. Bibi Ruth alimwambia kuhusu mtu mwingine kwenye Biblia, kijana mdogo aitwaye Yusufu. “Sarah, Yusufu alikuwa na nyakati nyingi ngumu maishani mwake pia. Mamake alifariki alipokuwa bado mdogo sana; kakaze walimwonea wivu sana kiasi kwamba waliamua kumuuza kama mtumwa; na akasingiziwa kufanya jambo baya sana ambalo hakulifanya na alitupwa gerezani kwa ajili ya jambo hilo! Lakini katika Mwanzo 50:20, alisema, ‘Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema.’ Kwa namna fulani, Yusufu aliona kwamba hata wakati mambo yanapoonekana kuwa magumu, Mungu anaweza kuyageuza kuwa kitu chema sana.”

 

Sarah alipokuwa akivifikiria visa hivi, alianza kuhisi dalili ya matumaini moyoni mwake. Pengine, huenda Mungu anao mpango kwa ajili ya huzuni yake pia.

 

Zaidi ya juma na miezi iliyofuata, Sarah aliendelea kuomba na kutafuta msaada kutoka kwa wazazi wake na kwa daktari anayejali. Alijifunza kushiriki hisia zake na rafiki zake pia, na walimpatia upendo na msaada wao.

 

Siku moja, wakati Sarah akiwa amesimama kwenye mti uo huo wa mwaloni, aligundua kuwa wingu zito ambalo liliukalia moyo wake lilikuwa limeondoka. Alikumbuka fungu lingine ambalo bibi Ruth alimpatia, kutoka katika Zaburi 34:18: “Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, na waliopondeka roho huwaokoa.”

 

Sarah alitambua kuwa Mungu amekuwa pamoja naye wakati huu wote, akimpitisha kutoka katika giza la wasiwasi na huzuni na kumwongoza kuielekea nuru angavu ya tumaini na uponyaji. Aliwasimulia wengine kisa chake, akiwakumbusha kwamba hata katika nyakati zao za giza kuu, kamwe hawakuwa peke yao. Kwa imani, maombi na kwa msaada wa wapendwa wao, wao pia, wanaweza kupata amani na uponyaji.

Mchapishaji

Jarida la Adventist World, jarida la kimataifa la Kanisa la Waadventista wa Sabato. Konferensi Kuu, Divisheni ya Asia Pasifiki ya Waadventista wa Sabato ndio wachapishaji.

 

Mkurugenzi Mtendaji/ Mkurugenzi wa Huduma za Adventist Review

Justin Kim

 

Meneja wa Uchapishaji wa Kimataifa

Hong, Myung Kwan

 

Kamati ya Uratibu ya Jarida la Adventist World

Yo Han Kim (chair), Tae Seung Kim, Hiroshi

Yamaji, Myung Kwan Hong, Seong Jun Byun,

Dong Jin Lyu

 

Wakurugenzi wenza/ Wakurugenzi, Huduma za Adventist Review

Sikhululekile Daco, John Peckham, Greg Scott

 

Wahariri waliopo Silver Springs, Maryland, Marekani

Enno Müller, Beth Thomas

 

Wahariri waliopo Seoul Korea
Hong, Myung Kwan; Park, Jae Man; Kim, Hyo-Jun

 

Mkurugenzi wa Mambo ya Kidijitali

Gabriel Begle

 

Mkurugenzi wa Muungano wa Mifumo na Uvumbuzi

Daniel Bruneau

 

Meneja wa Shughuli

Merle Poirier

 

Mratibu wa Tathmini ya Uhariri

Marvene Thorpe-Baptiste

 

Wahariri /Washauri wengine

E. Edward Zinke

 

Meneja wa Fedha

Kimberly Brown

 

Mratibu wa Usambazaji

Sharon Tennyson

 

Mratibu wa toleo la Kanda (Adventist World)

Penny Brink

 

Bodi ya Utawala

Yo Han Kim, chair; Justin Kim, secretary; Hong,

Myung Kwan; Karnik Doukmetzian; SeongJun

Byun; Hiroshi Yamaji; Joel Tompkins; Ray Wahlen; Ex-officio: Paul H. Douglas; Erton Köhler; Ted N. C. Wilson

 

Maelekezo ya Usanifu na Muundo

Types & Symbols

 

Kamati ya Adventist World ya Divisheni ya Afrika Mashariki – Kati:

Blasious Ruguri, Musa Gideon Mitekaro, Tom Ogal, Emanuel Pelote.

 

Tafsiri

Ufunuo Publishing House, South Tanzania Union Conference.

 

Msomaji wa prufu

Lilian Mweresa

 

Usanifu wa toleo la Kiswahili

Daniella Batista, Ashleigh Morton, Digital Publications

 

Uchapishaji wa Kidijitali

Charles Burman, Digital Publications (www.digitalpublications.co.za)

 

Muelekeo wa Sanaa na Ubunifu

Mark Cook, Brett Meliti, Ivan Ruiz-Knott

/Types & Symbols

 

Kwa Waandishi: Tunakaribisha miswada huria. Tuma barua zote kwa uhariri kwa 12501 Old Columbia Pike, Silver Spring, MD 20904-6600, U.S.A. Faksi ya ofisi ya Uhariri ni: (301) 680-6638

 

Waraka pepe: worldeditor@gc.adventist.org

Tovuti: www.adventistworld.org

 

Rejea zote za Biblia zimechukuliwa kutoka kwenye Swahili Union Version Bible Toleo la Chama cha Biblia la mwaka 1952.

 

Jarida la Adventist World linachapishwa kila mwezi na kuchapwa kwa wakati huo huo huko Korea, Brazili, Indonesia, Australia, Ujerumani, Austria, Ajentina, Meksiko, Afrika Kusini, na Marekani.

 

Vol. 19, Na. 12

Swipe left

swipe left To move to the next page

Swipe right

swipe right To move to the previous page
Allow Send-it to use cookies?

Send-it uses cookies to track how you use the application. Find out more about what data we collect and how we use the data in our privacy policy.